Mabomu ya Machozi yatumika kuwasambazi wananchi pamoja na Wanafunzi Mjini Dodoma

Haya bwana, wenye mawzao ya kisasa, wenye akili sana mlonge. Ila debe tupu haliachi kutika, tutasema tu humu na matusi kibao, sijui kama kuna mtu wa kuchukua maoni yetu humu.

kuwafikia mbona yana wafikia sana tu..mambo yamebadilika hata wao wanajua kwamba maoni hayatolewi kwenye midahalo na mkongamano tu hata kupitia mitandao pia watu wanaweza kutoa maoni yao.
 
Haya bwana, wenye mawzao ya kisasa, wenye akili sana mlonge. Ila debe tupu haliachi kutika, tutasema tu humu na matusi kibao, sijui kama kuna mtu wa kuchukua maoni yetu humu.

Remmy, i think i know how you feel. Pole sana. Badala ya kukata tamaa namna hii kudhani kwamba watu wanashindana nani mwenye akili kuliko mwingine, nadhani wewe na wenzio ndani ya chama ni lazima mtafute namna ya kufanya mapinduzi kwenye fikra zenu. Fikra zenu bado zimekwamba kule nyuma miaka kumi iliyopita.

Leo watu wana namna nyingi za kujieleza na kujifunza tofauti na ilivyozoeleka huko nyuma. Kuna blog, SMS, simu, internet, na television. Hatusubiri tena vikao vya vyama ndipo tujue jambo gani lilitokea na sisi kutoa mawazo yetu.

Ni kwa sababu chama chenu hakijazoea mjadala ndio maana mtu yeyote anayetoa mawazo mnamshuhulikia kwa kutumia dola badala ya kumjibu. Ni kwa sababu chama chenu hakijazoea kukosolewa ndio maana mkikosolewa mnadhani watu wanataka kuhatarisha amani. Hamjazoea wananchi kuhoji mnapokosea ndiyo maana mkihojiwa mnatumia mabomu ya machozi badala ya kujirekebisha na kusonga mbele

Usikate tamaa Remmy, you can be force for change within your party, utakuwa umesaidia sana chama chako
 
Sasa kama ukumbi hautoshi,mnataka watu waruhusiwe kuingia ili wakakae wapi?

Public hearing hii inafanyika kwa siku 3 mfululizo,sio lazima kila mtu aingia leo...waweke utaratibu wa wale waliojiandikisha kutoa maoni yao juu ya muswada ndio waingie ndani kwa zamu kulingana na uwezo wa ukumbi kubeba watu. Wakimaliza watoke na kuwapisha wengine wenye maoni yao. Wengi wa waliojazana pale ni mashabiki na washangiliaji-wale hawana haja ya kuwemo ndani,wanaweza kufuatilia proceedings hizo kwa kutumia PA system nje ya ukumbi na kwenye vyombo vya habari-radio ONE wanarusha live.

Kwa wale walioamua kuendesha public hearing yao nje,ni counter-productive kwasababu maoni yao hayatafika yanapotakiwa kufikishwa...sana sana wanapoteza muda wao.

By the way,mjadala wa leo ni kuhusu Muswada wa kuanzisha tume ya Katiba, na sio kujadili Katiba yenyewe...hivyo inputs/ideas/critique inatakiwa ku focus kwenye vifungu vilivyo ndani ya Muswada wenyewe.
Baada ya kusema haya mimi nina wazo moja japo kwa mchakato unaoendelea sasa linaweza kuwa limepitwa na wakati. Kwa nini zisiwepo mechanism nyinginezo za kukusanya maoni juu ya muswada husika kama vile wananchi kuruhusiwa kutoa maoni yao kwa njia ya barua, e-mail,social network platforms etc

Kwa kuruhusu hizo njia nyingine,hata watu wasioweza kufika Dar,Dodoma au Zanzibar physically wataweza kutumia haki yao ya kutoa maoni pasipo kulazimika kuwepo kwenye maeneo yanapofanyika shughuli hiyo

Tutolee ujinga wako hapa wee pumbafu fisadi mkubwa, siku zenu zinahisabika za kukaa hapa Tanzania mmetunyonya sana nyie wajinga. hatukubali mpaka tunawang;oa na ufisadi wenu. Muda wenu unafikia kikomo aaaanzeeeeeni wajinga nyie
 
Nimeshangaaa kusikia TBC 1 na ITV kuwa waliotawanywa ni wananchi wa Dodoma pamoja na wanafunzi wa vyuo vikuu. Je wanafunzi wao si wananchi???????
 
cha ajabu ni kuwa policy forums tangu juzi walitoa ofa ya kulipia ukumbi wowote mkubwa jambo ambalo halikupendwa na waandaaji.nafikiria kufungua kesi ya kukimbizwa na polisi bungeni
 
VIUNGA vya Bunge mjini Dodoma jana viligeuka uwanja wa mapambano baada ya askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), kutumia mabomu na risasi za moto kutawanya mamia ya wanafunzi wa vyuo vikuu waliotaka kuingia katika ukumbi wa Pius Msekwa kushiriki mjadala wa maoni wa Muswada wa Sheria ya Mapitio ya Katiba.Wakati hali hiyo ikiwa hivyo mjini Dodoma, mkutano wa aina hiyo ulifanyika jijini Dar es Salaam uliovurugika baada ya kutokea vurugu.

Mapambano yaliyotokea mjini Dodoma, kati ya wanafunzi wa vyuo vikuu na FFU yalisababisha wakazi wa maeneo ya Makole, Uhindini, Sabasaba na Mtaa wa Railway kukimbia ovyo huku baadhi yao wakifunga maduka na biashara zao kuhofia kujeruhiwa kwa risasi.Hofu hiyo ilitokana na idadi kubwa ya watu, wengi wakiwa ni wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya mjini Dodoma, kulazimisha kuingia kushiriki mjadala huo katika Ukumbi wa Msekwa wenye uwezo wa kuhimili watu 300 ambao tayari ulikuwa umeshajaa.


Katika vurugu hizo, wanafunzi hao walivunja lensi ya kamera ya Mpigapicha wa gazeti hili kwa jiwe walilokuwa wanataka kumpiga nalo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk James Msekela, wakati akizungumza nao.


Msekela aingilia kati

Vurugu hizo ambazo zililazimisha polisi kupiga risasi takribani 19 hewani, zilianzaa saa 5:00 asubuhi na kudumu kwa zaidi ya dakika 45. Hata hivyo, wakati risasi zikirindima wabunge na wadau mbalimbali walikuwa wakiendelea na mjadala huo katika ukumbi huo.

Dalili za kuwapo kwa vurugu hizo zilianza kujionyesha mapema kufuatia baadhi ya wanafunzi kuzuiliwa kuingia katika lango la ukumbi huo licha ya kufika mapema.Kuzuiliwa kwa wanafunzi hao kulisababisha baadhi ya wabunge hasa wa Chadema kulazimika kutoka nje ya ukumbi na kwenda kuwatuliza ili wasilete fujo.


"Nawashauri mtumie hekima na busara katika kuingia ndani ya ukumbi huu kwa kuwa ni haki yenu kikatiba, lakini tulieni tufanye utaratibu,"alisema Mbunge wa Kawe, Halima Mdee.Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini, naye alitumia muda mwingi kuwasihi wanafunzi kuacha kutumia nguvu, badala yake watumie hekima.


Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema, ambaye anabebeshwa zigo hilo la ghasia, naye alitoka ndani ya ukumbi huo wa Msekwa na kuwahutubia wananchi hao waliokuwa wamefunga barabara. Lema anayetajwa kuamsha umma huo kufika viunga hivyo vya Bunge, aliwaambia wanafaunzi hao kuwa ni haki yao kuchangia maoni katika muswada huo kwani unagusa mustakabali wa nchi na alipinga hatua ya muswada huo kujadiliwa na mikoa mitatu (Dodoma, Dar es Salaam na Zanzibar).


Dk Msekela alimlaumu Lema kwamba ndiye chazo cha wanafunzi kujitokeza kwa wingi.

"Matatizo haya yamesababishwa na Lema ambaye jana alikwenda katika vyuo vikuu kuwahamasisha wanafunzi wafike kujadili muswada huo," alisema Dk Msekela.Hata hivyo, Lema aliyekuwa amesimama nyuma ya Dk Msekela, alijitokeza na kukiri kufanya hivyo na kusisitiza kwamba hataacha kufanya hivyo kwa kuwa ni haki yake.

"Mimi Lema ndiye niliyekwenda UDOM kuwahamasisha waje kwa kuwa hawa ni wasomi na muswada umeandikwa kwa lugha ya Kiingereza, hivyo wananchi wa kawaida hawawezi kuujadili tusipowaleta wasomi kama hawa," alisema Lema na kusisitiza:

"Sitaacha kwenda vyuoni kwani Jumamosi (kesho) nitakwenda kufungua tawi huko."
Awali wanafunzi walikuwa wakiimba nyimbo mbalimbali za hamasa zikiwamo nyimbo za Taifa pamoja na wimbo maalumu ambao hutumiwa na wanafunzi wa Vyuo vikuu unaosema, "Kama sio juhudi zako Nyerere, mafisadi wangetoka wapi."Wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali, wanafunzi hao walisema hawatoki katika eneo hilo na wako tayari kwa lolote.

Barabara zilifungwa

Barabara ya Kati Dodoma ilifungwa na wanafunzi hao na kusababisha magari kutumia njia ya Dodoma Inn (Barabara ya kwanza) ambayo ina mzunguko mrefu.Wananchi katika maeneo ya Makole, Uhindini, Sabasaba na Mtaa wa Railway walitaharuki na kukimbia ovyo huku baadhi yao wakifunga maduka na biashara zao kuhofia mirindimo ya risasi.

Tambwe achafua

hali ya hewa Dar
Wakati Dodoma kukiwaka moto, mjadala huo ulifanyika pia katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, lakini haukuisha vizuri baada ya Mkuu wa Kitengo cha Propaganda cha CCM, Tambwe Hizza kuchafua hali ya hewa.
Hizza ambaye alikuwa ni msemaji wa 10 na wa mwisho akiwakilisha CCM , alishindwa kuendelea na mada yake baada ya washiriki wa kongamano hilo kupiga makofi ya bila mpangilio huku wakimzomea.

Akitoa hoja yake, Tambwe alianza kwa kumpongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kile alichokiita kuonyesha nia ya kupatikana kwa Katiba mpya na kwamba kupinga muswada huo ni matokeo ya mfumo wa vyama vingi ambao unaruhusu tofauti ya mawazo.


"Tangu nchi yetu iliporuhusu mfumo wa vyama vingi tulijua kutakuwa na mawazo tofauti," alisema Hizza huku akirushiwa maneno ya kebehi na washiriki wakisema "Jadili muswada"

Lakini Hizza aliendelea kusema, "Wote tunataka Katiba mpya. Kwa mujibu wa Ibara ya 98 ya Katiba ya sasa, mabadiliko ya katiba yanaweza kuwa ni kubadilisha, kufuta au kuirekebisha ,kwa hiyo jina tu marejeo ya katiba katika muswada huu lisiwape tabu."

Washiriki walimzomea Tambwe huku wengine wakipiga makofi, lakini yeye aliendelea kuzungumza bila kujali kelele zao. Wakati washiriki wakiendelea kumzomea Tambwe, Mwenyekiti wa mdahalo huo, Mbunge wa viti Maalumu, Pindi Chana (CCM), aliwataka washiriki wa kongamano hilo kunyamaza na kumsikiliza Tambwe.


Ushauri huo Chana haukuweza kuwatuliza badala yake walizidisha kelele huku wakimzomea wakisema, "Aondoke..., aondoke, aondoke, aondoke…". Hali hiyo ilidumu kwa dakika tano, kisha Chana alitangaza kuahirisha kongamano hilo na Tambwe akarudi kuketi sehemu yake.


Uamuzi wa Tambwe kuketi ulizidi kuwasha moto kwani washiriki walianza kuzozana na nusura ngumi zipigwe, lakini askari polisi waliokuwapo katika ukumbi huo walifanikiwa kutuliza ghasia.


Vijana wazozana

Hali hiyo ilionyesha wazi kuwapo kwa makundi makubwa mawili ya Chadema na CCM, ambayo yalipingana, huku baadhi ya vijana wa chama tawala wakiwashutumu vijana wenzao wa chama pinzani, wakidai kuwa chama hicho kimewapa fedha ili wakafanye fujo.

"Chadema wamewapa fedha mje kufanya fujo, tuna ushahidi hata kijana wetu mmoja naye amepewa," alisema Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kinondoni, Emanuel Makene. Hata hivyo, kauli hiyo ilipingwa na mzee aliyejitambulisha kwa jina la Salim Nyambua Said, akisema CCM wamekosea kuleta watu wasio makini kwenye kongamano hilo,

"Chanzo cha vurugu hizi ni CCM kuleta wahuni.'' Kauli hiyo ilimsababisha kutaka kupigwa na vijana wa chama tawala kabla hajaokolewa na polisi.

Vijana wengi waliokuwapo nje ya ukumbi huo, walisisitiza kuwa hawahusiki na Chadema na kwamba wao hawakuridhishwa na maneno ya Tambwe. "Sisi hatuhusiki na Chadema, ila tumekerwa na Tambwe Hizza, badala ya kujadili muswada anaviponda vyama vya upinzani," alisema kijana mmoja ambaye hakutaka kutaja jina lake.


Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuvunjika kwa kongamano hilo, Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, alisema kuna vijana wameandaliwa kufanya vurugu. "Yanayotokea hapa inaonyesha kuna vijana wameandaliwa, au hawakuandaliwa kuja kufanya fujo, mimi nawashauri kuheshimu mawazo ya watu hata kama hawayataki," alisisitiza Tendwa.


Jaji Warioba

Vurugu katika kongamano hilo zilianza kujionyesha pale aliposimama Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba, ambaye alianza kwa kumsifu Rais Kikwete kwa kuanzisha muswada huo akisema ni hatua nzuri.

"Muswada huu ni hatua ya ya kuelekea kwenye utaratibu wa kupata Katiba mpya…. Nafikiri hii ni hatua kubwa. Tunayo Sheria ya kuunda Tume ambayo Rais angeweza kuitumia, lakini kwa umuhimu wake ameunda tume ambayo atakuwa akipata ushauri, mimi sioni tatizo," alisema Jaji Warioba na kuonekana kuwakasirisha washiriki wa kongamano hilo walioanza kuguna na kupiga makofi mfululizo na kumfanya ashindwe kuendelea kuzungumza.


Hali hiyo ilimfanya Pindi Chana, kuwatuliza washiriki ili Jaji Warioba aweze kuendelea kuzungumza.

Kwa kusoma upepo, Jaji Warioba akabadilisha mwelekeo na kuanza kuukosoa muswada huo hali iliyowafanya washiriki hao kutulia kimya na kumsikiliza.

Jaji Warioba alikikosoa kifungu cha 9 (2) kinachozuia mambo kadhaa kujadiliwa, aliyaita mambo hayo kuwa ni matakatifu. "Kifungu cha 9 (2) kimeweka mambo matakatifu ambayo hayapaswi kuguswa. Haya ndiyo Katiba yenyewe, tunachotaka watu watoe maoni yao," alisema.


Kongamano hilo baada ya kufunguliwa na Waziri wa Nchi Katiba Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Mathias Chikawe, lilikuwa na wasemaji kutoka vyama vya siasa na taasisi mbalimbali.


Viongozi wa vyama vya siasa walikuwa ni Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa APT Maendeleo, Peter Kuga Mziray, Mwenyekiti wa NCCR- Mageuzi, James Mbatia na Katibu wake, Sam Ruhuza.


Pia walikuwapo wawakilishi wa taasisi zisizo za kiserikali kama Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kilichowakilishwa na Imelda Urio.Wengine ni Dk Modesta Opiyo kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe, Gideon Mandes kutoka vyama vya walemavu na Dk Francis Michael. Kwa ujumla, wachangiaji wote waliukosoa muswada huo na kutaka ufanyiwe marekebisho.


Imeandaliwa na Habel Chidawali na Israel Mgussi,
Dodoma, Elias Msuya, Dar

Mabomu yatawala mjadala wa katiba
 
cha ajabu ni kuwa policy forums tangu juzi walitoa ofa ya kulipia ukumbi wowote mkubwa jambo ambalo halikupendwa na waandaaji.nafikiria kufungua kesi ya kukimbizwa na polisi bungeni

Kumbe mkuu unaweza kushitaki polisi kwa kuhatarisha amani ya wananchi wanaojieleza kwa amani?
 
iwe wanaichi, sijui wanafunzi, wanawake au mtu ni mtu poa tu.
JK haendi bila kusukumwa i like this move ya watu kushupalia uondolewe uozo kwenye limswaada la katiba.
 
What is msekwa hall and what is public hearing, i dont understand. It sounds a bit fun. Are we failing to think?:hug:
 
What is Msekwa hall and what is jammii ya watanzania. It sounds fun, may be we are failing to think.:redfaces:
 
Tatizo kubwa la serikali ni kutojipanga ktk mambo yake either kwa makusud au kwa kutokua makini.
Jambo moja lililoendeleza hasira kwa wananch wa kawaida wa dodoma hasa wanavyuo ni wakat sisi tulifika tangu saa 1 asubuh na kuzuiliwa et 2onyeshe vtambulisho vya uraia nk getin lakin Mbunge wa Dodoma mjini ambae pia ni mmiliki wa shule ya City Secondary wanafunz wake walikuja na basi na wakapita bila ya kizuiz getin hapo. Je hapa we unafikir ni fair?
 
Remmy, i think i know how you feel. Pole sana. Badala ya kukata tamaa namna hii kudhani kwamba watu wanashindana nani mwenye akili kuliko mwingine, nadhani wewe na wenzio ndani ya chama ni lazima mtafute namna ya kufanya mapinduzi kwenye fikra zenu. Fikra zenu bado zimekwamba kule nyuma miaka kumi iliyopita.

Leo watu wana namna nyingi za kujieleza na kujifunza tofauti na ilivyozoeleka huko nyuma. Kuna blog, SMS, simu, internet, na television. Hatusubiri tena vikao vya vyama ndipo tujue jambo gani lilitokea na sisi kutoa mawazo yetu.


Ni kwa sababu chama chenu hakijazoea mjadala ndio maana mtu yeyote anayetoa mawazo mnamshuhulikia kwa kutumia dola badala ya kumjibu. Ni kwa sababu chama chenu hakijazoea kukosolewa ndio maana mkikosolewa mnadhani watu wanataka kuhatarisha amani. Hamjazoea wananchi kuhoji mnapokosea ndiyo maana mkihojiwa mnatumia mabomu ya machozi badala ya kujirekebisha na kusonga mbele



Usikate tamaa Remmy, you can be force for change within your party, utakuwa umesaidia sana chama chako

Pole sana if u think mi natetea chama. Ndo shida ya mtazamo wa watz, mtu akitoa mawazo yake what he/ she feels akiwa kinyume basi ni mpinzani tu, na akiwa amesimama kwenye ukweli au yupo sawa na hoja basi ni ccm, wengine je tusio na vyama tutasema nini? tutachangia wapi? mawazo yetu yaweje? la muhimu sijasimamia ccm, na wala cdm, wala serikali, nimesimama kwenye hisia zangu kama mtz na shuhuda wa yale yaliyotokea bungeni jana, thats all. All in all nimezoea sana ushabiki wa humu ndani ni wa chama zaidi kuliko the truth and reality, anyway Mungu ndo anajua yaujazayo moyo wa mtu, wengine tutawasikia midomoni tu, ndo maana kesho anahama chama hiki anasema vile na vile.
 
Tutolee ujinga wako hapa wee pumbafu fisadi mkubwa, siku zenu zinahisabika za kukaa hapa Tanzania mmetunyonya sana nyie wajinga. hatukubali mpaka tunawang;oa na ufisadi wenu. Muda wenu unafikia kikomo aaaanzeeeeeni wajinga nyie

If i were CCM or president, ningewapa madaraka just littlebit tuone. Sijaona uzuri wa Kibaki hata kidogo, mambo ni yaleyale. Yote kwa yote wote ni binadamu tunaofanana kwa hulka, SELF CENTERED.
 
Tatizo kubwa la serikali ni kutojipanga ktk mambo yake either kwa makusud au kwa kutokua makini.
Jambo moja lililoendeleza hasira kwa wananch wa kawaida wa dodoma hasa wanavyuo ni wakat sisi tulifika tangu saa 1 asubuh na kuzuiliwa et 2onyeshe vtambulisho vya uraia nk getin lakin Mbunge wa Dodoma mjini ambae pia ni mmiliki wa shule ya City Secondary wanafunz wake walikuja na basi na wakapita bila ya kizuiz getin hapo. Je hapa we unafikir ni fair?
Wakuu poleni sana na maboom lakini ukombozi wa nchii hii utaletwa na sisi wenyewe! Kila kitu kwa msaada wa japani, msaada wa Marekani au China ila kwa hili la katiba itakuwa kwa msaada wa WATANZANIA WENYEWE!
 
Excellent,.......Vizuri kabisa ,CCM na serikali yake kama ya Augustino Pinocheti (Dikteta) wa Chille ....namfananisha sana G.Lema na Che Guevara, ccm walizoea Slopes sasa hapa ni Hills ...mpaka kamba yao ikatike tu,adha wanayoipata CCM ni chungu zaidi ya anayekunywa dawa ya SHUBIRI
 
Huu ni mswada tu, sasa itakapofika wakati wa wananchi kutoa maoni ya katiba mpya, si ndio itafanyikia kwenye sebule/nyumba za watendaji wa vijiji halafu watasema, nafasi hakuna.
 
kweli ndugu yangu hiyo dawa ni shubiriiii,lazima ccm wakione cha mtemakuni. Muda wakuwachezea watu umekwishaya
 
Pole sana if u think mi natetea chama. Ndo shida ya mtazamo wa watz, mtu akitoa mawazo yake what he/ she feels akiwa kinyume basi ni mpinzani tu, na akiwa amesimama kwenye ukweli au yupo sawa na hoja basi ni ccm, wengine je tusio na vyama tutasema nini? tutachangia wapi? mawazo yetu yaweje? la muhimu sijasimamia ccm, na wala cdm, wala serikali, nimesimama kwenye hisia zangu kama mtz na shuhuda wa yale yaliyotokea bungeni jana, thats all. All in all nimezoea sana ushabiki wa humu ndani ni wa chama zaidi kuliko the truth and reality, anyway Mungu ndo anajua yaujazayo moyo wa mtu, wengine tutawasikia midomoni tu, ndo maana kesho anahama chama hiki anasema vile na vile.

Sorry rafiki, umepata mistaken identity baada ya kuandika kwamba wanaodai haki ya kuingia ndani ya bunge kutoa maoni yao wanataka kuleta fujo katika viwanja vya bunge ambavyo umedai vinaheshimika. Badala ya kujiuliza sababu waandaaji hawakujiandaa kikamilifu na kisha baada ya watu kuzidi watumie akili zaidi kuwahudumia badala ya kuwafungia nje na kuwapiga mabomu. Hata hivyo sasa nimekuelewa.
 
Back
Top Bottom