muhosni
JF-Expert Member
- Feb 12, 2011
- 1,108
- 152
Ni kuhusu kuhudhuria public hearing ya mswaada wa katiba
Wanaharakati wafunga barabara na kuendesha public hearing kuhusu mswada wa kuandika katiba mpya baada ya kukataliwa kuingia ukumbi wa msekwa
Bunge baadaye latangaza kwamba public hearing kundi la pili litaingia ukumbi wa msekwa leo saa tisa kutoa fursa kwa waliokosa nafasi asubuhi
Bunge latangaza kwamba Public hearing sasa itafanyika siku tatu mfululizo ukumbi wa Msekwa
Vyombo vya habari vyashindwa kurusha matangazo live kutoka Dodoma
Wanafunzi wamewazomea Chenge na Lukuvi na kuwaita mafisadi, haikuchukua muda wakaja FFU na kuanza kutembeza mabomu ya machozi
Baada ya kupigwa mabomu Wanaharakati, Wananchi, na Wanafunzi wamehamia Nyerere Square kuendelea na "Citizen Public Hearing"
Maoni yangu:
Serikali imewakosea wananchi waliotumia muda na gharama zao kufika dodoma na kuwakataza wasiingie ukumbini. Katazo halikuwa la kistaarabu bali ubabe na amri kama vile wananchi hao walikuwa wafungwa. Ilikuwa ni jukumu la serikali kuhakikisha inawapatia wananchi hao ukumbi mbadala kwa haraka na kuwabembeleza na kuwapeleka huko kwenye ukumbi mbadala. Serikali haikutenda haki kuwapiga mabomu.
Ni kama kusema kwamba serikali haikutaka maoni ya wananchi bali wananchi ndio wanaolazimisha kutoa maoni yao! Hii inatia shaka kama maoni ya wananchi kweli yatafanyiwa kazi, au ni kutimiza tu mchakato kwamba kabla ya sheria kupitishwa maoni ya wananchi yalikusanywa, bila kujali kama yaliingizwa kwenye mswada.