Inakuwaje wananchi wanasababu ya kufanya mkutano halafu wanazuwiwa na kupigwa mabomu ya machozi na kutawanywa?

wemamzuri

Member
Jan 27, 2019
75
70
NCHI ni wananchi. Uwepo utaratibu unaodumu WA kuwapa wananchi Uhuru WA kutoa maoni na malalamiko na kuchukua hatua pale inapofika mambo kutochukuliwa hatua, haki kutotendeka, kuchelewesha mambo, uonevu, ubaguzi, nk. Sura ya kwanza ya katiba ibainishe NCHI na mamlaka ya wananchi yaliyojuu ya MTU au kiongozi yeyote hata RAIS.

Mfano
1. Inakuwaje wananchi wanasababu ya kufanya mkutano halafu wanazuwiwa na kupigwa mabomu ya machozi na kutawanywa?

2. Inakuwaje wananchi wanasababu ya kufanya maandamano ya AMANI halafu wanazuiwa na kupigwa mabomu ya machozi!

3. Viongozi WA wananchi ktk kuanzisha mikutano na maandamamo ya AMANI wapaswa kuwekewa kinga ya kutoshitakiwa au kukamatwa ovyo na kuteswa. Hii ndiyo mamlaka ya wananchi.

4. Wananchi watakuwa huru kutoa maoni na kupiga kura kubadili jambo lolote linalohatarisha ustawi wao.

Mfano kuboresha au kubadili katiba, kuboresha bunge, kuboresha SERIKALI, kuboresha mahakama, kuboresha polisi, magereza, jeshi, sheria za NCHI na kanuni zake n.k kwa njia ya MTU binafsi, mkutano, CHAMA, n.k BILA bughuza yoyote. Na MTU yoyote hatakamatwa BILA NDUGU na SERIKALI ya mtaa wake kujulishwa.
 
Back
Top Bottom