Mabinti wa kibongo na Oman

Maamuzi ni ya familia au huyo mwenzie?
Huyo mwenzie hana ndugu wanaosota akawapeleka wakatoke au anampenda zaidi huyo mdogo wako?
Familia kama haijaridhishwa iseme NO! Bint akijifanya haelewi mrudisheni kwa wazazi wake huyo mwenzie amfate huko,amgharamie safari na huyo mdogo wako akishafunzwa na ulimwengu atarudi tu maana mchuma janga hula na wa kwao!!!

binti ni yatima amehamia kwa wazazi wangu mwaka juzi after wazazi wake wote kufariki
 
Umasikini huu tabu sana.

Kumbe Nyerere aliposema wa Mexico wanakimbilia Marekani, North Africans wanakimbilia Ulaya, sisi hatuna pa kukimbilia alikuwa hajaliona chongo la uarabuni!

Habari tunazopata kutoka huko si nzuri.

Ingawa wengine wanaweza kusema "mguu wa msafiri mtume kauombea" na "mgaa gaa na upwa hali wali mkavu".

Kuna kufuata nyuki na kula asali, lakini pia angalieni majuto mjukuu.
 
Achana na hzo mambo mkubwa wala usijiulize mara mbili..mpeleke dogo veta akajifunze kutumia cherehani mpe cherehani uswahilin bugurun kuna dili kibao za kurepair nguo na si huko tu hata masaki pia mafundi cherehani wanahitajika otherwise utakuwa unampoteza dogo
 
Mkuu hakuna haja ya kumruhusu kwenda oman, huku ke hupigwa, hunyimwa chakula, hubakwa na hufingiwa ilhali wakiwa wamenyang'anywa passport.
Kwanza wamekua wakidanganywa kwa kuribuniwa na ainahiyo ya kazi lakini wanapofika huku hufanywa watumishi wandani, na wengine huwekwa kwenye chumba kimoja na kuuzwa kwa wanaume wanaohitaji ngono, huku madalali wakichukua sehemu kubwa ya malipo na wadada wakilipwa kidogo. Na hii ni kwa wadada wakutoka mataifa mbalimbali
 
Kwani mnafikiri uarabuni hamna mabinti ambao hawana kazi au ambao wanajua kuchora hina badilikeni guys huyo bonti mtaenda kumpoteza kwa bei rahisi tu.
 
Habari za asubuhi wanajamvi,wanafamilia tumejikuta katika njia panda baada ya mdogo wangu wa kike(mtoto wa bamdogo) anaishi na wazazi wangu kua rafiki yake ambae alikua Oman anafanya kazi katika salon ya kuchora hina amekuja kumchukua ili waondoke wote wakajiunge katika kazi hiyo.Wanafamilia wote hakuna anayeafiki hilo suala ila yeye ndio amekomaa na huyo rafiki yake anajaribu kutushawishi kua hakuna tatizo atakua katika mikono salama,sisi tunahofia maana binti ndio ana 20 yrs hana professional yoyote ni form four leaver tu.Wanajamvi najua humu kunawenye uzoefu na Oman katika hili naomba mnisaidie kunifunua macho kweli hili jambo liko salama kwa binti huyu?

BIG NO.hii kitu inanikumbusha documentary moja ya kusikitisha niliyo wahi kuitazama.ilikuwa inahusu madhara wanayokumbana nayo wasichana toka wa west africa nchini italy.ni wale waliopolekwa italy na mawakala kama huyo aliyemfata mdogo wako kwa moja ya kisingizio kama hicho-kumpatia kazi.kumbe behind the curtain sio ajira bali nimtiririko wa biashara haramu ya human trafficking.hawa mawakala wanatumia pesa kidogo walizo nazo kumrubuni mzazi wa binti akubari binti yake kwenda ulaya.wakifika huko binti anaporwa document zake zote muhimu na kuanza kutumikishwa kingono kwa malipo ambayo mwisho wa siku anayefaidi ni yule dada/wakala aliyemfata kumtoa kwao africa.na gharama zote za kumsafirisha inabidi azilipe.hapo wengi huishia kuchanganyikiwa na hatimaye hujiingiza ktk matumizi ya dawa za kulevya.mwisho wa siku wakirudi africa wanakuwa kama mazombi hivi.kuweni chonjo sana mdogo wenu hasa huyo mdada anaye mrubuni.ni hayo tu.
 
Asiende kabisa Waarabu wana roho mbayaa mpaka hua najiuliza kwanin sehemu nyingi za waarabu ni takatifu wakati wao sio watakatifu yaan atafanywa kama mbwa ataliwa guchii mpaka akomee,huyo anaemshawishi si achukue ndugu zake awapeleke mpaka mdogo wenu tuu
 
tumejaribu kumshawishi arudie mitihan ili apate crediit ameshindwa mara mbili tumemshaur achague anachotaka kusoma ufundi wowote hataki inshort hatumuelewi kabisa

Kama mnashindwa kumuelewa mpeni mume kwa sababu ataweza hata kutoroka kwa ushawishi atakaopewa na rafikiye
 
Back
Top Bottom