Simulizi yenye ukweli wa kuumiza juu ya maisha na matukio halisi yanayotokea katika jamii yetu

IamBrianLeeSnr

JF-Expert Member
Nov 10, 2022
2,011
4,164
5C5E6949-4BEB-4622-B9BC-E19C84787200.jpeg


LANGO LA MOTONI



CHAPTER 1



Jumatatu YA TAREHE 26/12/2022



Majira ya saa tisa na dakika arobaini na saba kulionekana dada mmoja ambaye hakuonekana nadhifu kwa mwonekano wa mavazi yake pamoja na nyewe zake zilizoonesha kutimka kama vile alikuwa akikimbizwa na kitu au yupo katika dimbwi la mawazo.



Dada huyu bila hata ya kuangalia upande wa pili yake kama uko salama ili avuke barabara yeye alianza kuvuka na hata kabla hajamaliza alishtushwa na kelele za watu waliokuwa wakimtahadharisha na kufuatiwa na mshindo mkuu uliofanya arushwe upande wa pili wabarabara na gari hilo lililosabasha mshindo huo kusimama mbele kidogo.



Alishuka mama mmoja ambaye kwa mwonekane alionekana kuwa ni mtu mweye uwezo wa kifedha na ndani ya gari kulionekana watoto wawili na dada zao ambao walikuwa na furaha muda mfupi uliopita na furaha hizo zilisitishwa na mshtuko wa kile kilichoteokea mbele yao.



Mama alifika pale alikoangukia binti na wakati huo watu walianza kukusanyika huku wakipiga kelele za kutaka mama huyo apigwe kwa kusababisha ajali hiyo.



Mara wakatoeka wasamaria na kumsaidia mama yule kumbeba binti huyo na kumwingiza kwenye gari la mama na kisha wakaondoka kwenda kumwahisha hospitali.



Walifika hospitali na baada ya kupewa huduma ya kwanza binti huyo alibainika kupatwa na mshtuko na hakuwa ameumia. Hivyo akapewa dawa na kuruhusiwa ili aende akapumzike nyumbani kwa ahadi ya siku ya pili yake arejee ili kwa uchunguzi zaidi.



"pole sana dada, naomba nisamehe na sijui uliingiaje barabarani, kwani nilikuona kwa mbali ukiwa pembeni tena mbali ya barabara, punde si punde nikashangaa uko ubavuni mwangu"



" Mama!! Tafadhali naomba usiseme samahani, nashukuru kwamba niko salama na naomba mimi nikuombe samahani" alimaliza kuongea binti huyo huku akijivuta kuanza kutaka kuondoka eneo hilo.



" Dada naomba nikupeleke nyumbani kwako ili nipafahamu na kesho niweze kuja kukupitia turudi hapa kwa uchunguzi zaidi"



" Hapana sina nyumba"



" Huna nyumba kivipi? mbona sikuelewi dada au bado unamshtuko?"



" Niache tu mama, asante kwa ukarimu niache niondoke"



" hapana, Binti naomba basi hata twende ukapumzike kidogo na baadae utaondoka" Alimalzia kuonge amama huyo huku akimshika mkono na kumsaidia kumpeleka maegesho ya magari na muda mfupi baadae walikondoka na kuwasili nyumbi kwa mama huyo.



Wakati wote huo wale watoto pamoja dada zao wao walikuwa kimya wakimwangalia mama yao aliyeonesha kuchanganyikiwa na tukio la siku hiyo huku wakiwa wamekatishwa furaha yao kwani mtoko wa siku hiyo uliishia kutiwa doa na ajali.



"poleni wanangu tutaenda siku nyingine mungu akitujalia na wakati huu nitawapeleka hoteli nzuri zaidi tuombe uzima baba yenu akiwa karudi salama"



" Sawa mama" aliitikia dada yao mkubwa huku akiwasaidia wadogo zake kushuka garini na muda mfupi familia nzima ilikuwa sebuleni ikitazama tamthliya ya simu ya ajabu na wote walikuwa wakiwa katika furaha hasa wakimwona bibi mmoja aitwaye gusa unate alivyokuwa akitetemeshwa na simu mmoja kutoka kwa mpigaji asiyefahamika.



Lakini binti yule aliyekoswa kugongwa na gari alionekana akiwa na tabasamu lililokosa matumaini huku fikra zake zikionesha kuwa alikuwa dunia ya peke yake tena yenye maumivu na kila aina ya kukataliwa na watu wanaomzunguka.



Machozi yalianza kumtoka dada huyu na baada ya muda alishindwa kujizua na kujikuta akitoa kilio cha chinichini na hii ilizidi baada ya kuona familia ile ikiwa na furaha.



Wenyeji wake walishtushwa na kufadhaishwa na hali ile, kwa busara mama alimwomba amchukue binti yule na kumpeleka chumbani ili ampumzike kwani alihisi kuwa binti huyo ana ana jambo zito na kwa muonekano wa kawaida ni kwamba amefikia kiwango cha mwisho cha kulihimili jambo hilo.



"Dada naomba nikuoneshe sehemu yako ya kupumzikia"



" Nina muda mrefu sijawahi kupata usingizi, ni bora nikae hapa nione mkifurahi itanifariji zaidi na kama waweza naomba maji ya moto kwenye kikombe ninywe"



" yawekwe chochote maji hayo?"



" hapana, ila kama kuna kahawa ningependa"



" ipo" alimjibu mama huyo huku akienda kummwandalia maji hayo na kumletea muda mfupi baadae na wakaendelea na mazungumzo.



Ilikuwa imeshatimia saa tatu za usiku na watoto walikuwa wakisafisha meza baada ya chakula na mama pamoja na mwenyeji wake walibaki pale sebuleni wakiwa wawili huku wakiongea.



" samahani sikujitambulisha mimi naitwa mama ukundi na mimi ni mwalimu ambaye nimeamua kujiajiri na pia mkurugenzi wa taasisi moja ya kina mama hapa mjini, na pale tulikuwa njiani nkwenda na watoto sehemu kwa ajili ya mapumziko na chakula cha jioni"



" Asante dada, mimi naitwa MARIAM..................."



"Samira! Samira! Samira! bado umelala? amka mwanangu jiandae kwenda shule na mimi nataka kuwahi hospitali kumwangalia mtoto ili nawe nikupeleke ukamwone haraka na kisha uwahi shuleni" ilisikika sauti ya mama samira ikimwita ili kumwamsha samira aliyekuwa bado amelala na wakati ni muda wa kujiandaa kwenda shuleni.



Samira alimaka na kusaidiwa na dada wa kazi kujiandaa na muda mfupi baadae alikwa kwenye gari pamoja na wazazi wake na wakati huu walikuwa wameshatoka hospitali kumwangalia mtoto na sasa walikuwa wakimpeleka shuleni na muda mfupi walimwacha shuleni na wao kuondoka kuelekea kazini kwao.



Wakiwa njiani kabla ya kufika kazini ghafla lwalimwona mtoto mmoja mdogo akiwa anasimamisha gari kama alihitaji msaada wa dharula. Bila hiyana baba samira alisimamisha gari lake na kushusha kioo ili aweze kuongea na mtoto huyo.



Mara wakatokea vijana wawili waliokuwa waliokuwa wameshika vitu mkononi na kuwapulizia wawili wale na kisha kutokomea kusikojulikana. baba samira na mama samira walianza kupiga kelele za kuomba msaada kabla ya kujikuta wakiishiwa nguvu na hatimaye gari moja likasimama pembeni na mtu mmoja akashuka na kuwachukua na kuwapeleka mpaka hospitali ambapo muda mfupi baadae walifariki dunia.



Zilipita wiki kadhaa na siku moja walionekana watu kama saba wakiwa kwenye kikao cha familia na mmoja wao alikuwa ni samira akiwa na wanafamilia wengine.



Pamoja na kuwa na umri mdogo tena wa miaka minne tu lakini samira alionekana akilia kwa uchungu baada ya kusikia kauli kuwa " kuanzia sasa samira atatakiwa kuhamishwa shule na kwenye nyumba ili iuzwe na yeye atatafutiwa shule nyingine, na kwa kuwa yeye ni mtoto wa kike hata husika katika mirathi na atasimamiwa masomo tu"



Kauli hiyo iliyotolewa na baba mkuwa wa samira iliungwa mkono na ndungu wengine ingawa shangazi yake hakuridhishwa na maamuzi yale lakini hakuweza kutoa kauli yoyote ya kupinga kwani mfumo dume ulikuwa kazini. alipoonesha kutoridhishwa na maamuzi hayo alifunguliwa mlango wa kutokea huku akisindikizwa na makofi yaliyomwacha na alama mashavuni mwake.



Siku mbili baadae baba mkubwa wa samira alionekana akiwa kasimama nje ya jumba moja kukuuu kukuu akiwa kamshika mkono samira aliyekuwa na begi lake dogo na kumkabidhi samira huku akitoa maelezo ya kuwa ni samira ni mtoto yatima na alimwokota barabrani.



Baada ya kupokelea samira alianza kukaa hapo kwa maisha mapya huku akisahau kabisa kuwa ana familia tena zaidi ya wakati huu kuwa karibu na watoto wenzake.





Miaka mitatu ilipita bila shangazi kujua wapi samira yupo na wakati huo alikuwa amehamia mji mwingine na kila alipojaribu kumpigia kaka yake ili apate taarifa za samira aliambiwa kuwa yuko shule ya bweni na siku mmoja likizo watampeleka.



Shangazi yake samira yeye alijulikana kwa jina la Aunt Amina na alishakaa kwenye ndoa yake kwa muda wa miaka saba bila ya kubahatika kuwa na mtoto. Alibahatika kumpata mme ambaye hakuwa na fedha ila alikuwa na mapenzi ya dhati kiasi kwamba walikubaliana kuwa wasubiri kudra za mwenyezi Mungu ili muda ufike awape watoto.



Lakini ilikuwa imepita miaka mingi na ndugu walishaanza chokochoko ingawa mmewe na Aunt Amina yeye alibaki kuwa na msimamo na ni wakati huu ambapo waliamua kwenda kituo cha watoto yatima ili waweze kumchukua mtoto wampendaye na kumfanya mtoto wao.



Jumatatu moja asubuhi majira ya saa nne Aunt Amina na mmewe walionekana wakiwa kwenye ofisi moja ya kituo cha kulelea watoto yatima huku wakiangalia watoto mbalimbali.



Macho ya aunt amina yaligongana na macho ya Samira na kwa mshtuko wenye usiri ndani yake baada ya kumtambua samira ambaye yeye hakutambua kitu wakati huo, aunt amina alimvuta mmewe pembeni na alimnong'oneza kitu,



" Mpenzi wangu huyu mtoto nimempenda sana, naomba tumchague huyu awe mwanetu"



" haina shida kama umempenda mtoto huyu mie sina neno mpenzi wangu"



" asante kwa kunielewa" alijibu aunt amina huku akielekea ofisini kwa mkuu wakituo na kumwacha mmewe akielekea nje kuipokea simu iliyokuwa ikiita muda huo.



" samahani kaka, hivi jina sahihi la mtoto huyu anaitwa nani?"



" Kulingana na taarifa zake tulizopewa wakati akiletwa msamaria mwema jina lake aliandikishwa Janeth Simon Shikopa"



" ok nashukuru sana" aliongea aunt amina huku akipokea taarifa za samira ambaye katika kituo hicho cha kulelea watoto alitambulika kwa jina la Janeth.



Waliondoka pale na kujerea nyumbani ningawa muda wote huo akili ya aunt amina ilikuwa ikimfikiria janeth na kujiuliza je ni janeth kweli au ni samira? na kama ni samira iwaje wepo kituo cha watoto yatima badala ya kuwepo shule ya bweni? na je ni kwanini apelekwe pale? au kutakuwa na sababu nyuma ya hayo yote?



Walifika nyumbani na maisha yakaendelea huku janeth akiwa mchapakazi na mtoto aliye na bidii na heshima katika kila kazi aliyopewa na shuleni alionekana kujituma pia pamoja na udogo wake.



" mme wangu tumekaa na huyu janeth kwa zaidi ya miezi mitano sasa ila mimi kuna kitu nafikiri zaidi juu ya mtoto huyu"



" unafikiri nini mke wangu"



" huyu mtoto ni mtoto wa marehemu kaka yangu,. hata kama sikubahatika kuonana nae zaidi ya ile siku ya msiba wa kaka lakini naamini ni huyu tuu ingawa sijui kuna nini maana kaka mkubwa anadai yupo shule ya bweni na kila nikitaka amlete ananipa viswahili"



" mmmh kwani mtoto wa kaka yako marehemu alikuwa anaitwa nani?"



"Samira"



" sasa mbona huyu pale kituoni walituambia anaitwa janeth?"



" na mimi ndio nafikiri hapo kuna kitu, sasa mimi leo akirudi toka shuleni nataka nijifanye kumwita samira nione kama ana kumbukumbu"



" Aiseee kweli dunia matata sasa kwa nini kaka yenu afanye hivyo au kuna kitu kuhusiana na utajiri wake?"



" Uko sahihi nafikiri hivyo pia ila ngoja tuone mwisho wake"



Walimaliza kujadili na kila mmoja wao akawa busy na kazi zake mpaka ilipofika mida ya saa moja na nusu usiku wakiwa sebuleni wanaangalia luninga aliingia Janeth akiwa natokea masomo ya jioni na kuwakuta wakiwa pale.



" samira mbona umechelewa leo kurudi?"



" Mama umelijuaje hili jina? ni mama na baba yangu tuu walikuwa wananiita kabla hawajafa"



Bila hata kuongea neno aunt amina alinyanyuka na kwenda kumkumbatia Samira na kuanza kulia kwa uchungu jambo lililomfanya na mme wake nae atafute kuitambaa chake na kuufuta uso wake kushairia nae alishikwa na huzuni baada ya kumwona mkewe akiwa analia kwa hisia.



" ilikuaje ukawa pale samira?"



" mwalimu aliniambia nilipelekwa pale na baba mmoja aliyeniokota"



" maskini samira pole sana mwanangu, mimi shangazi yako kabisa ingawa nilikuja siku moja tu ya msiba wa baba yako na nikafukuzwa kwenye kikao na siku chache baadae nilihama kutoka mji niliokuwa ninakaaambao pia ulikuwa mbali na kwenu na kuja hapa na mjomba wako, tutaongea vizuri kesho haya jiandae ule chakula"



Usiku huo haukuwa na maneno ya ziada zaidi ya kila mmoja kuwahi kulala huku nyumba nzima ikiwa imezingirwa na furaha yenye maswali mengi ndani yake.

ITAENDELEA.........
 
56463BD4-D72A-4935-904A-316C8A1A3AE4.jpeg


CHAPTER 2

Ilipoishia

" maskini samira pole sana mwanangu, mimi shangazi yako kabisa ingawa nilikuja siku moja tu ya msiba wa baba yako na nikafukuzwa kwenye kikao na siku chache baadae nilihama kutoka mji niliokuwa ninakaa ambao pia ulikuwa mbali na kwenu na kuja hapa na mjomba wako, tutaongea vizuri kesho haya jiandae ule chakula"


Usiku huo haukuwa na maneno ya ziada zaidi ya kila mmoja kuwahi kulala huku nyumba nzima ikiwa imezingirwa na furaha yenye maswali mengi ndani yake

Endelea


Siku ya pili yake asubuhi Aunt Amina aliwahi kuamka na kila mmoja akaelekea kwenye mihangaiko yake na huku nyuma walimwacha samira akiwa katika dimbwi zito la mawazo na kujiuliza maswali mengi.

" hivi ni kwa nini baba mkubwa aliamua kunifanyia hivyo? na kwa nini aunt alifukuzwa kikaoni?"

Haya ni baadhi tu ya maswali aliyojiuliza samira huku akianza kupatwa na taswira sahihi ya maisha yake na familia yake na ni wakati huu ikamjia picha ya mtoto walikwenda kumwona hospitali ingawa yeye alikuwa mdogo kiasi cha kushindwa kukumbuka kwa usahihi juu ya mtoto huyo uhusiano wake na familia yao.

***

TUKUNYEMA BAR

Ilikuwa ni jioni moja katika bar ya Tukunyema alionekana Mzee Zombo akiwa kwenye meza moja iliyosheheni vinywaji huku ikiwa na mabinti na baadhi ya wapambe waliozunguka meza hiyo na kumfanya Mzee Zombo a.k.a Bilionea la ukubwani kuonekana kwa taabu.

Wapambe wale walikuwa wakimpa mzee zombo kila aina ya sifa na kumfanya ainuke mara kwa mara na kuanza kuwarushia fedha huku wengine akiwamwagia vinywaji nao wakifurahia na baadhi wakiongezewa vinywaji.

Pembeni kuna baadhi ya wateja nao walikuwa wakimshangilia na wengine wakiyatamani maisha yale lakini wachache walishindwa kujizuia na kujikuta wakinong'onezana.

" Huyu mzee alikuwa maskini sana na historia yake ni kuwa hata shule alikimbia......" hata kabla ya kumaliza maongezi yale kijana mmoja ambaye ni shushushu wa Mzee zombo aliyekuwa amekaa pembeni alinyanyuka na kwenda kumnong'oneza mzee zombo.

" Mfalme, nina taarifa za kishushushu, niruhusu kukuambia"

" Sema! sema! kijana nani nataka kuharibu hali ya hewa hapa?"

" Nimesikia wakinong'onezana kuwa wewe ni gaidi namba moja wa kimataifa na kama haitoshi wanamashaka na utajiri wako, kwani wewe boss umeishia darasa la ngapi?"

" pumbavu! pumbavu! wewe wakuniuliza mimi nimeishia darasa la ngapi? do you know what time is it you pig son? kama ningekuwa sijasoma shule ningewezaje kukutukana kiingereza?" alifoka mzee zombo huku akimzaba vibao yule kijana

" sio mimi boss wameongea wale vijana" aliongea kijana yule huku akiwanyooshea kidole wale vijana ambao hata kabla ya mzee kuongea neno walishaanza kutabasamu kutokana na maneno ya mzee zombo

Alinyanyuka kwa haraka mzee zombo pale alipokuwa amekaa na kuwaendea wale vijana, " nyie vijana!!! mnafikiri kila mwenye mvi ni mzee? wengine wanafanya kazi kwenye mashine za kusagia nafaka, habari zenu nimezipata, mnahoji juu ya utajiri wangu? mimi mtoto wa mjini toka kitambo sana.

Kwanza ile nyumba nikaayo ni ya kwangu, maana nimeanza kusikia hapa mjini kuna watu wanadai ile nyumba ni ya mdogo wangu na mimi nimehamia baada ya yeye kufa na mkewe.


Mimi niliijenga nyumba ile na kumpa mdogo wangu ili mimi nikae kwenye kale kanyumba kadogo na kabovu ili nijaribu kuona maskini mnapata taabu kiasi gani, na nimeichukua nyumba yangu na kuanza kukaa baada ya mdogo wangu kufariki lakini nashangaa mnaanza kuleta majungu yasiyo na msingi.

Ni upendo wa aina gani mpaka niamue hata kumpeleka mtoto wa pekee wa mdogo wangu kusoma nje tena ulaya na sio ulaya vijijini bali ulaya mjini city center.....Wengine hapa hata kukaa na paka tuu mnashindwa upendo kama huu mtaupata wapi? ilitakiwa mnisifie na kunifanya mfano wa kuigwa

Sasa nyie vidudu ambao tena hamna mbele wa nyuma mnaanza maneno au hamkupitiwa na ofa wakati nimesema bar nzima mnywe kwa bili yangu?

Mhudumu wape hawa kreti moja kila mmoja" alimaliza mzee zombo huku akianza kuondoka kwa madaha


" mzee sisi hatutaki bia zako na ukweli ni kwamba wewe shule huna na mjini waishi kwa mipango feki na kama ungekuwa na uchungu wa fedha hizo kamwe usingetumia kipuuzi hivyo" aliongea mmoja wa vijana wale na kuondoka eneo hilo

Mzee zombo alirejea kukaa kwenye nafasi yake huku akionesha tabasamu la hasira, " kunyweni!, kunyweni! hapa ni burudani tuu achaneni na vijana wenye hila zao"

Hazikupita dakika nyingi mzee zombo a.k.a bilionea la ukubwani alinyanyuka na kuondoka akiwaacha vijakazi wake kwa ahadi za kurudi baadae huku akionekana mwenye mawazo mengi na aliendesha gari kwa umbali fulani na kisha akasimama.

" hivi binadamu wakoje? mbona wanapenda sana kufuatilia mambo yasiyowahusu? hivi hela za mdogo wako si za kwako? na elimu inahusiana vipi na matumizi tena bar? au natakiwa ninywe kwa calculator? wameniudhi sana wale vijana na nikionana nao naweza hata wagonga na gari"

Akiwa katika dimbwi hilo la mawazo yasiyo na msingi wowote mara dirisha la gari lake liligongwa na alipolifungu alikutana uso kwa uso na..............................

Je nini kitamsibu mzee zombo a.k.a bilionea la ukubwani?
 
837DE7DB-5E7B-41E6-8A6E-53FC96408E29.jpeg

Chapter 3

Ilipoishia

" hivi binadamu wakoje? mbona wanapenda sana kufuatilia mambo yasiyowahusu? hivi hela za mdogo wako si za kwako? na elimu inahusiana vipi na matumizi tena bar? au natakiwa ninywe kwa calculator? wameniudhi sana wale vijana na nikionana nao naweza hata wagonga na gari"

Akiwa katika dimbwi hilo la mawazo yasiyo na msingi wowote mara dirisha la gari lake liligongwa na alipolifungu alikutana uso kwa uso na..............................

Endelea

Akiwa katika dimbwi hilo la mawazo yasiyo na msingi wowote mara dirisha la gari lake liligongwa na alipolifungua alikutana uso kwa uso na askari wa usalama barabarani aliyekuwa akimtaka mzee zombo aliondoe gari kwani alilipaki sehemu isiyo sahihi.

Mzee zombo aliondoka na kujikuta aikishia kwenda bar nyingine na kuendelea kunywa lakini muda mwingi alionekana kutawaliwa na mawazo na hakuwa zombo aliyezoeleka.

Jioni ya siku hiyo aunt amina alionekana akiwa na mawazo mengi na uso wake ulikuwa uligubikwa na machozi hasa baada ya kumkumbuka kaka yake aliyekufa katika mazingira ya kutatanisha huku polisi wakishindwa kuwapata wahusika na mbaya zaidi akakumbuka jinsi alivyoahidiwa kupewa mtaji wa biashara siku chache kabla ya kifo cha marehemu

Aliumia pia kuona jinsi mtoto samira mapito aliyopitia na kujikuta akitokwa na machozi zaidi na alipogeuka nyuma macho yake yaligongana ya yale ya samira ambaye nae alianza kutokwa na machozi baada ya kuona shangazi yake akiwa katika hali ile, na muda mfupi baadae nyumba hiyo iligubikwa na huzuni na majonzi mpaka pale mmewe na aunt amina alivyoingia akiwa na mahitaji ya chakula cha usiku na wote wakaingia jikoni kuanza kuandaa chakula hicho.

Ilipofika mida ya saa nne mme wa aunt amina akiwa amelala na samira amelala pia, aunt amina aliamka na kwenda nje kisha akaichukua simu yake na kumpigia mtu.

" weee malaya mkubwa nimekuambia usinipigie simu tena na ukome kama hela nilishakulipa wataka nini tena? mzee zombo siibiwi kirahisi na kama huamini uliza mabinti wa mji huu, mimi ndio bilionea wa ukubwani" aliongea mzee zombo kwa sauti ya kilevi huku sauti za mziki na kelele za baadhi ya wanywaji zikisikika

" samahani kaka, mimi ni amina, mdogo wako"

" Bado tuu unamawazo yako ya kutetea upumbavu, si nakuuliza?"

" hapana mimi sipo huko ila nauliza juu ya samira kama amerudi likizo kutoka huko shule ya bweni maana nilitamani aje kunitembea"

" mbona unajifanya kama mwalimu mkuu vile? unajua mimi ni kaka yako? habari za likizo niachie mimi, na akirudi utaambiwa... kwani nani analipa ada yake??

tulishakuja kukuomba???? tena kwa kukukomesha yule mtoto juzi nimeongea nae zaidi ya nusu saa na anaongea kiingereza sana unajua gharama zake wewe?????

unaanza kuulizia uliza kuhusu likizo na siku utauliza risiti.... sasa kwa kifupi na kwa kumalizia utapewa taarifa akirudi na mwambie na huyo mjinga mwenzako tena ashukuru tangu muoane sijawahi onana nae, maana ningempiga kelebu, mtu gani hawezi hata kuleta wajomba.... yaani anazidiwa na kuku bwana.. maana kila siku tunakula mayai na kuku wapya?"

" sawa kaka asante na usiku mwema" alikata simu aunt amina na kurudi sebuleni ambako aliyasahau kabisa masuala ya samira na sasa akaanza kulia kwa uchungu baada ya kuitafakari kauli ya kaka yake juu ya yeye kutopata mtoto.

Alilia kwa muda mpaka pale mmewe aliposhtushwa na sauti ya kilio na kwenda sebuleni na akajaribu kumuuliza mkewe na baada ya kusimuliwa kisa kizima alimpa mkewe maneno yenye kumpa nguvu,

" mke wangu, Mungu ana neno ambalo anataka kututumia mimi na wewe kama mfano kwa wengine, sijawahi kukusaliti na kuwa na mtu mwingine, nami hujawahi kunifanyia hivyo..

pengine kwanza tuamini kuwa hii ni bahati kwetu kwani kuna wenzetu wana watoto lakini ndoa zao zinawaka moto na wengine wanafikia kushindwa kuvumilia na kwenda nje ya ndoa na kuzaa huko..

lakini wengine wana watoto na kwa kuwa walishindwa kuwatunza leo hii ni majambazi, mashoga, changudoa na wanajutia kuzaa hata kufa kwa presha.... Muda wa Mungu huja kwa wakati na ukija huja na furaha zaidi... amka mpenzi wangu tukalale" alimazima kuongea huku akimsaidia mkewe kunywa maji na kisha wakaelekea chumbani

Asubuhi na mapema mzee zombo bila hata ya kuaga alimka na kulitia mafuta gari lake na kisha kwenda kwenye kile kituo cha watoto yatima kilichopo umbali mrefu kidogo ili akadadisi kama samira yupo ingawa ilikuwa imepita miaka kadhaa bila ya yeye kwenda hapo.

Alipofika pale kituoni alionana na uongozi na muda mfupi baadae alioneka mzee zombo akiwa anatoka nje ya kituo hicho huku mikono ikiwa kichwani kuashiria hali haiko shwari na akawasha gari lake na kuanza safari ya kurudi mjini haraka.

Akiwa njiani alionekana kuwapigia simu baadhi ya watu na hazikupita dakika nyingi alionekana akiingiza gari katika hotel moja iliyotulia na kukutana na baadhi ya watu waliokuwa wametangulia eneo hilo.

Baadhi ya ya watu waliokuwa hapo ni pamoja na wadogo zake watatu pamoja na mjomba wao ambao kwa pamoja walionekana kushtushwa na taarifa hizo ingawa sio kwa kumwonea huruma bali walianza kuona madhambi yao yanaanza kufichuka.

" Duuuh, sasa na huyu amina na mmewe wana wazimu? walijuaje? dada yetu yule anaweza kuibua kesi na hapo mipango yetu yoote itafichuka..... mimi naona tuamue kitu ndugu zangu" aliongea mjomba

" hapa hakuna kudiscuss sana mimi naona na familia yao iwafuate baba na mama samira maana meno hayajachoka kabisa kutafuna kuku na mtu anataka kukunyan'anya kipande mdomoni... au nyie mnaonaje?" aliongea zombo

"Hilo ndio suala zima kaka, maaana mimi sitaki tena kurudia yale maisha ya zamani maana hata hapa si waona nimekuja nikiwa nimekaa sasa nani arudi kulima viazi" aliongea mdogo wa zombo

"Sasa mimi natoa oda, wewe bwana mdogo KIWI unatakiwa usafiri mpaka mji anaokaa amina na uone mazingira kisha uje tukae na kujadili kitu" aliongea mzee zombo kwa msisitizo huku akimkabidhi kitita cha fedha bwana kiwi.

Kesho yake Kiwi alishuka katika kituo cha magari cha paranga'anda majira ya saa kumi na nusu na moja kwa moja akatafuta hotel na kuweka mizigo yake na kuanza kuzunguka mitaani. Asubuhi yake majira ya saa kumi na moja kasoro alimng'aza samira akiwa anatoka shule na akamtambua ingawa ulipita muda mrefu tangu aonane na samira.

Alianza kumfuatilia kwa ukaribu mpaka akaona nyumba aliyoingia na kuona nje akiwa kakaa aunt amina na baadhi ya marafiki wakiongea neno.Akaondoka zake na kurejea hotelini na siku ya pili alikuwa njiani akirudi mjini ili kutoa ripoti ya utafiti wake.

Asubuhi iliyofuata nyumbani kwa zombo alionekana mzee zombo na kiwi wakinena jambo na baadae mzee zombo alisimama na kupiga simu na dakika ishirini baadae gari moja dogo liliingia na vijana wawili wakashuka na kuungana na mzee zombo na kiwi pale sebuleni.

" Asante sana kwa kuwahi, sasa kuna kazi moja ndogo sana nataka kuwapa,naona kuna vinyang'au vinataka kunisumbua nataka msaada wenu, si mnajua TV ikiwa inapiga sana kelele inatakiwa kuzimwa au kui-mute kupitia rimoti? sasa nyie kama rimoti nataka mtumike vyema."

"Sawa sawa mzee ila unakumbuka kazi ile ya kwanza kuna malipo hukutumalizia?"

"Msijali hii itakuwa na malipo safi, sasa nataka msafiri mpaka paranga'anda kuna nyumba moja iko jirani sana na eden bar mtaona watu hawa hapa pichani, nataka mhakikishe mnawaliza sawa?

kwani nataka yabaki makochi tu mle ndani, kila kitembeacho hakikisha kinapotezewa uhai na mikikuta hata ubwabwa nyie kuleni" alimaliza mzee zombo huku akitoa bahasha na kuwapa wale vijana na kuahidi kuwapa ndonge nono zaidi.


Saa mbili na nusu za usiku aunt amina alianza kuangahika baada ya vidonda vya tumbo kumshika, akamtuma samira aende mtaa wa tatu akanunue maziwa kutoka kwa mfugaji mmoja wa ng'ombe na wakati huo mmewe aunt amina alikuwa ndio anaingia kutoka kazini.

Dakika chache baadae baada ya samira kuondoka mlango uligongwa na baada ya aunt amina kuufungua mlango alikutana uso kwa uso na sura zilizovalia mavazi ya kininja na kuficha nyuso zao na wakampulizia kitu usoni.

wakati akipiga kelele mara mmewe aliyekuwa ndani akaja ili kutoa msaada na kukutana na gongo moja la utosini na kuanguka kisha wakampulizia kitu fulani puani na kuondoka na mmoja wa watu wale aliiona picha ya samira ikiwa ukutani na akaipenda na kuondoka nayo pia.

wakati samira akiwa anarudi alipishana na gari moja lililotokea eneo hilo kwa kasi na kumfanya ajifiche na alipoingia ndani alishtuka kuona mjomba wake akiwa kalala huku damu nyingi zikimtoka na aunt amina akiwa analia kuomba msaada .

Akatoka mbio na kwenda kwa majirani huku akipiga kelele za kuomba msaada na majirani wakaanza kukusanyikana na muda mfupi baadae walikuwa hospitali...............

SAFARI NDIO INAANZA
 
237CE029-D110-4BE3-8AB8-3D2DA30BA4A8.jpeg

Chapter 4

Ilipoishia

wakati samira akiwa anarudi alipishana na gari moja lililotokea eneo hilo kwa kasi na kumfanya ajifiche na alipoingia ndani alishtuka kuona mjomba wake akiwa kalala huku damu nyingi zikimtoka na aunt amina akiwa analia kuomba msaada .

Akatoka mbio na kwenda kwa majirani huku akipiga kelele za kuomba msaada na majirani wakaanza kukusanyikana na muda mfupi baadae walikuwa hospitali.

Endelea

Hospitalini walionekana baadhi ya watu wakiwa wamekaa na kusimama eneo la mapokezi huku wakiwa na hofu na kwa mbali daktari alionekana akitoka kwenye moja ya chumba cha wagonjwa wa dharura na kuwafuata na kuongea nao kisha vilio vikaitawala hospitali hiyo.

Vilio hivyo vilikolezwa zaidi baada ya kuambiwa kuwa mmewe na aunt amina alikuwa kashafariki hata kabla ya kufikishwa katika hospitali hiyo. Mbaya zaidi hali ya aunt amina ilikuwa bado ni mbaya kwani alikuwa akilalamika maumivu ya macho na kichwa kwa ujumla hivyo samira na majirani wengine wakaondoka eneo hilo na kurudi nyumbani kwa ajili ya taratibu nyingine za mazishi ya mjomba wake.

Zilipita siku saba baada ya mazishi ya mjomba wa samira huku aunt amina akiwa bado yuko hospitali, na siku hii samira alionekana akiteta jambo na daktari na baada ya maongezi hayo samira akaondoka mpaka wodini.

Alifika karibu na kitanda cha aunt amina na kukaa pembeni huku akimwangalia aunt yake ambaye alikuwa kafungwa kitambaa cheupe machoni mwake ili kuzuia mwanga usimuumize zaidi macho yake yaliyokuwa yameathiriwa na sumu aliyopuliziwa usoni siku ya tukio.

" nesi, nesi nesi" aliita aunt amina

"hapana sio nesi ni mimi samira, pole sana aunt yangu, unaendeleaje leo?"

" Bado nina maumivu makali, niliogopa nilivyosikia mtu akiufungua mlango na kisha akakaa kimya nikadhani labda watu wale wanakuja kunimaliza, naogopa sana mwanangu samira, sijui wananitakia nini watu hawa,mjomba wako anaendeleaje?"

Zilipita sekunde kadhaa samira akiwa kimya ingawa machoni alikuwa akitokwa na machozi mfululizo na kilio cha chini kilichomfanya ashindwe kujizuia na kulia kwa sauti kubwa na dakika moja baadae daktari alikuja na kumtoa nje jambo lililompa wasiwasi zaidi aunt amina.

" jamani naomba mniambie ukweli mme wangu yuko wapi?"

"tulia dada, mmeo yuko salama wewe pumzika nafikiri mwanao samira ameshindwa kujizuia kukuona bado unaumwa ila wewe jikaze ili apate nguvu ya kukuhudumia" alimaliza kuongea nesi wa zamu aliyekuwa pale wodini.

Samira aliondoka pale wodini na kurudi mpaka nyumbani na wakati huu alikuwa katika dimbwi zito la mawazo juu ya hatma yake na shangazi yake ambaye alihitaji fedha nyingi ili aweze kupelekwa hospitali nzuri nje ya nchi na kufanyiwa upasuaji mdogo na macho yake yaweze kuona tena.

***

MojaMOja Bar

Zilikuwa zimepita takribani wiki mbili tangu kitokee kifo cha mme wa aunt amina na mbaya zaidi ni kwamba hakuna ndugu yoyote wa aunt amina aliyehudhuria msibani wala kumtakia pole pamoja na taarifa kuzagaa kuwa walipatwa na majanga.

Katika bar hiyo ya mojamoja walionekana mabinti sita wakiingia kwa mbwembwe na madaha na kwenda kuizunguka moja kwa moja sehemu ambayo bilionea wa ukubwani mzee zombo alikuwa ameketi huku akijitamba kama kawaida yake.

"kuna watu duniani hawana akili, hivi mtu unatoka bafuni unaenda kushika nyaya ya umeme bila hata ya kandambili? inabidi ifike pahala watu tuheshimiane kabisa, sasa vijana wangu wamefanya kazi nzuri na jinsi nilivyofurahi nitawapa na bonasi" aliongea maneno hayo mzee zombo huku akiwatizama vijana wake wa kazi waliotekeleza amri ya kuimaliza familia ya aunt amina na wakati huo walikuwa wana imani kuwa familia yote ipo ahera.

Akiwa katikati ya maongezi ghafla simu yake iliita na akatoka nje kwenda kuipokea na aliporudi alikuwa kabadilika yaani sio yule mzee zombo wa majigambo.

" inawezekana kuwa kweli? mbona niliambiwa kuwa kazi imefanyika kwa ufanisi? hapana lazima kitu kifanyike haraka sana" alijisemesha mzee zombo kiasi cha kuwafanya wapambe wake waingiwe na wasiwasi.

" Mzee kuna nini tena?" alihoji mmoja wa wapambe wale

" acha upumbavu wako, kwani hujui kilichotokea au wajifanyisha tu hapa? tena toka kabisa usikae karibu yangu" alimaliza mzee zombo huku akimwacha mpambe huyo katika tafakari nzito na kuanza kuingiwa na hofu kwani mzee zombo tangu aupate utajiri huo wa ukubwani amekuwa mtu wa kuropoka mambo yasiyo na tafsiri sahihi.

Mpambe yule alisimama kwa muda eneo lile na kumwangalia mzee zombo aliyekuwa akiondoka taratibu huku akijisemesha kama vile mtu aliyekuwa akiandamwa na madeni.

Songambele

Samira alionekana akiingia nyumbani kwa mwalimu Jack ambaye alimkaribisha samira na wakakaa sebuleni ingawa samira alionekana kutokwa na machozi kama vile alihitaji msaada wa haraka kuirejesha furaha yake.

" Pole sana mwanangu samira, aunt amina anaendeleaje?"

" wamesema natakiwa kuwa na fedha kiasi cha shilingi millioni 10 ili tumsafirishe mpaka india na aweze kutolewa sumu machoni mwake kwa upasuaji na ndipo atapata ahueni na kuona tena, nimechanganyikiwa mwalimu, wajua yeye ndio mama, baba na ndugu yangu sijui maisha haya yana siri gani kwangu"

"sikia mwanangu, kitu cha msingi ni kumuomba Mungu amtunze na kutupa sisi nguvu ya kuweza kutafuta njia maalumu ya kumsaidia, ukizidi kulia na kukumbuka maisha yako na maswahiba haya, utazidi kujitesa mwanangu"

" Asante, ila mapito yangu na umri wangu haviendani, natamani kuishi kama wasichana wengine kwa kuwa na furaha katika maisha"

" Yatapita na utakuwa na furaha zaidi, sasa mimi nitajaribu kuongea na kina mama wenzangu katika kikundi chetu ambacho aunt amina ni katibu ili tuone tunafanya nini kuokoa maisha ya rafiki, dada na mmdogo wetu aunt amina ni hela kubwa ila naamini Mungu atafungua njia"

"Asante sana mwalimu mimi naomba niondoke na kwenda kumwandalia chakula cha jioni" samira alimaliza kuongea maneno hayo huku akijifuta machozi na kuondoka nyumbani kwa mwalimu jack

Samira alikuwa ameshatembea umbali wa mita kadhaa kutoka nyumbani kwa mwalimu jack na wakati huo alikuwa akijiandaa kuvuka barabara. Lilikuja gari moja dogo kwa kasi ya ajabu na kusimama mbele yake na ghafla mlango ukafunguliwa.
 
CHAPTER 5

Ilipoishia

" Yatapita na utakuwa na furaha zaidi, sasa mimi nitajaribu kuongea na kina mama wenzangu katika kikundi chetu ambacho aunt amina ni katibu ili tuone tunafanya nini kuokoa maisha ya rafiki, dada na mmdogo wetu aunt amina ni hela kubwa ila naamini Mungu atafungua njia"

"Asante sana mwalimu mimi naomba niondoke na kwenda kumwandalia chakula cha jioni" samira alimaliza kuongea maneno hayo huku akijifuta machozi na kuondoka nyumbani kwa mwalimu jack

Endelea


Samira alikuwa ameshatembea umbali wa mita kadhaa kutoka nyumbani kwa mwalimu jack na wakati huo alikuwa akijiandaa kuvuka barabara. Lilikuja gari moja dogo kwa kasi ya ajabu na kusimama mbele yake na ghafla mlango ukafunguliwa.

Alishuka kijana mmoja mwenye umbo la miraba minne na mwenye sura ya upole na kama ungepata nafasi ya kumtazama kwa ukaribu ungekubali mwenyewe kuwa kaka huyu kweli alikuwa mtanashati, mtu mwenye kila sifa za mwanaume wa kisasa ambaye kamwe asingeliweza kukaa sehemu pasipo jicho la dada yoyote yule kumpa maksi zake za utanashati.

" wewe kaka vipi? yaani na barabara yote hiyo wewe uamue kuja kunifuata hapa nilipo? au ni hako ka Mark X kako ka mkopo kanakupa wazimu?" alitweta samira kwa hasira iliyoambatana na mawazo juu ya aunt amina.

" Samahani dada yangu, na mimi nina mawazo mengi sana hapa"

"wewe una mawazo wewe???? acha dharau, hebu tuache wenye mawazo tukapumzike"

"Tafadhali nishirikishe mawazo yako kwani naweza kuwa msaada, na kama hutojali naomba nikupe lifti kwenda uendako" alisisitiza kaka huyo huku akimvuta samira na kumfungulia mlango.

Samira hakuwa na jinsi zaidi ya kuingia kwenye gari hilo na safari ikaanza ya kwenda nyumbani kwa samira. Walipofika pale kaka yule alishuka na kumfungulia mlango ingawa samira alihoji amepajuaje mahali pale.

" napafahamu sana hapa kwani mjomba wako alikuwa rafiki yangu sana na kama haitoshi alinisaidia sana kutafuta kiwanja kipindi nahamia hapa."

"Ok basi sawa" alimaliza samira na kuingia jikoni kuanza kumwandalia chakula aunt samira na muda mfupi baadae walikuwa njiani wakielekea hospitali.

" pole sana kwa msiba wa mjomba wako na nimefurahi kuona kuwa wewe umesimama kidete kumsaidia shangazi yako,kwani tatizo ni nini linalomfanya shangazi yako aendelee kubaki hospitali?"

" asante, wanadai anatakiwa kupelekwa india na gharama zake ni milioni kumi za kitanzania, naona kama haitawezekana kamwe" alijibu swali hilo samira na kuanza kulia jambo lililomfanya kaka yule asimamishe gari na kwenda kumnunulia maji samira ili yamsaidie.


Walifika hospitali na kijana yule akabaki nje na baada ya samira kumlisha shangazi muda wa kuondoka ulifika na moja kwa moja wakaondoka zao na kurudi nyumbani na kaka yule akaondoka lakini alikuwa amemwachia namba ya simu ili ampe maendeleo ya aunt amina .

***

Jumanne tarehe 27/12/2022

kikao cha dharula kiliitishwa nyumbani kwa mwalimu jack na ajenda kuu ilkuwa ni suala la aunt amina na uchangishaji wa fedha kwa ajili ya matibabu yake.Samira nae alialikwa pale kikaoni ili aweze kuchangia jambo na kwa pamoja wapate utatuzi.


Kikako kile kilikuwa kigumu sana kwani wiki tatu kabla ya kifo cha mmewe na aunt amina kutokea, aunt amina alichukua mkopo kwa ajili ya kuanzisha biuashara ya mazao ambayo mmewe alikuwa akiisimamia.

Mkopo huo bado ulikuwa haujarejeshwa na kwa kuwa mmewe na aunt amina ndio alikuwa msimamizi mradi huo na mpaka kifo kinamkuta bado walikuwa hawajakaa vizuri na mkewe kujadili walipofikia hivyo hata aunt amina asingeweza kuwa na neno lolote.

Nguvu za ziada ilibidi zitumike ingawa nazo hazikuzaa matunda yoyote zaidi ya kupatikana shilingi laki saba na sitini elfu ambazo nazo kwa mazungumzo ya chini kwa chini zilitakiwa kulipa gharama za madeni ya msibani na pia kuongeza katika kulipia bili ya hospitali.


Samira alipokea zile hela na kuanza kuondoka kurudi nyumbani kwake mida ya saa nne kasoro za usiku. Akiwa njiani alivamiwa na kundi la vijana wajulikanao kwa jina la SOMBA SOMBA ambao walimdaka na kumpora fedha na wakiwa wanajiandaa kumbaka wasamaria wema walijitokeza na kumsaidia na wale vibaka wakakimbia.


Hali ilizidi kuwa ngumu kwa samira kwani asubuhi tuu alipoamka akiwa na majeraha ya jana yake usiku alipigiwa simu kuwa alitakiwa kwenda kulipa bili hospitali.

Ni wakati huu ambapo samira hakuwa na jinsi zaidi ya kuipekua simu yake na kukutana na namba ya kijana ambaye walikutana jana yake. Hakuwa na jinsi akauweka moyo wake kuwa mgumu na wenye ujasiri na kisha akampigia simu.

" Hallo kaka, "

"niambie samira"

"salama kiasi,tafadhali naweza kuonana na wewe muda huu? kwani nina jambo la muhimu sana"

" Ok usijali, niambie ulipo nitakuja mara moja"


" Naomba tukutane nje ya geti la hospitali"

" sawa usijali, nipe dakika 15" alimaliza kuongea kaka huyo na kukata simu kisha akanyanyuka kulifuta gari lake na kuondoka.


Samira alionekana akiwa nje ya geti kuu la kuingilia hospitali na hazikupita dakika nyingi kaka yule ajulikanaye kwa jina la BENITO SONGOMBO aliwasili pale na kwa haraka akashuka na kumfuta samira ambaye alikuwa amekaa kwa huzuni.

" pole samaira nini kimetokea?"

" jana nilipewa laki saba na elfu sitini kwa ajili ya malipo ya aunt amina na kumalizia deni la msiba wa mjomba, nikiwa narudi nyumbani nikavamiwa na kuumizwa na wakataka kunibaka nawashukuru majirani walitoka na kuniokoa na asubuhi nimepigiwa simu kuwa natakiwa kulipa bili ya hospitali na sijui nini nifanye"

Ok, usijali hebu nifuate kwenye gari," aliongea ben huku akimsaidia samira kuingia kwenye gari na kuondoka nae mpaka benki moja na kumtolea fedha taslimu shilingi laki nane na kumwambia samira akalipe bili na abakiwe na elfu arobaini kwa ajili ya matumizi madogo huku akifanya mchakato wa kutafuta fedha nyingine za matibabu zaidi ya aunt amina.

kw amara ya kwanza samira alionekana kuwa na uso wenye matumanini kwa haraka alimwangukia ben miguuni na kumshukuru huku akisema, " kweli nimeamini hata malaika wa heri anatembelea motoni, maana nilikuwa katika moto.

Waliachana pale na samira kaondoka huku akimwacha ben akimwangalia kwa makini samira mabye alikuwa ni chotara aliyechakaa kutokana na matatizo mpaka ikafikia kipindi zile nywele zake zilizopendwa na wengi zikafifia kutokana na shida.


***

Mzee zombo alionekana akiwa ndani ya gari akiongea na mtu kwa maneno makali yenye kuonesha kuwa amekatishwa tamaa na utendaji kazi wao.

" hivi wewe si ni mbwa? hela zote zile halafu eti leo nasikia samira bado yupo mtaani na huyo aunt yake? hivi nyie mnanitafutia nini mimi? au na nyie niwakodie watu waje kuwapa shughuli?"


"Samahani mkuu"

"Mkuu pua yako, sasa nawapa hii mara ya mwisho tu, ikishindikanika inahamia kwenu nataka mpaka ifikapo kesho kutwa nione majeneza mawili yanapita hapa? sawa?


"Sawa mkuu"

" haya toa makalio yako hapa, unaona raha kukalia magari ya kifahari , pumbavu zako... escape verocity wewe"

Mzee unamaaisha nini?" alihoji kijana yule kwa uoga ulioambatana na kicheko cha tumboni maana alijua fika mzee zombo hana elimu zaidi ya ujanja ujanja.


Maanada yake nini??? huoni kama huo ni msisitizo wa kwenda kujituma? tatizo lenu hamtembei nchi za mbali, kwanz ahata ukienda utafanya nini? bakini tuu hapa tuwape kazi ngumu, haya logout"

Kijana yule aliondoka na kuingia kwenye gari lake na kutokomea kusikojulikana akiwa na kicheko mwaka.


Saa saba za usiku nyumbani kwa samira kulionekna vijana kama sita waliokuwa wamevalia magwanda ya kujikinga na baridi na mmoja wao alikuwa ameshika........................
 
CEDE208A-3DA4-41C6-BB2B-C1C831D2A1C8.jpeg

CHAPTER 6

Ilipoishia

Mzee unamaaisha nini?" alihoji kijana yule kwa uoga ulioambatana na kicheko cha tumboni maana alijua fika mzee zombo hana elimu zaidi ya ujanja ujanja.


Maanada yake nini??? huoni kama huo ni msisitizo wa kwenda kujituma? tatizo lenu hamtembei nchi za mbali, kwanz ahata ukienda utafanya nini? bakini tuu hapa tuwape kazi ngumu, haya logout"

Kijana yule aliondoka na kuingia kwenye gari lake na kutokomea kusikojulikana akiwa na kicheko mwaka.

Endelea

Saa saba za usiku nyumbani kwa samira kulionekana vijana kama sita waliokuwa wamevalia magwanda ya kujikinga na baridi na mmoja wao alikuwa ameshika panga na wengine walikuwa wakiranda randa na kuchungulia ndani na kugundua hakuna mtu na kiongozi wao akatoa simu yake na kumpigia mtu.

"Boss mbona kunaonekana hakuna mtu ndani maana tumecheki kila sehemu hakuna dalili za mtu?"

" Nyie msinitanie naomba msinifanye kichaa kabisa mbona kiongozi wenu hapo amenipigia na kunihakikishia hata jioni alimwona akirudi nyumbani? hebu fanyeni kazi na acheni longolongo" alimaliza kuongea boss huyo na kukata simu.

Jambo hilo lilionekana kummaliza nguvu kijana huyo aliyekuwa kashika panga na kuwaamuru wenzake waondoke eneo hilo mara moja kwani walihisi kama majirani walianza kuamka.

Robo saa baada ya vijana wale kuondoka gari moja dogo lililokuwa likiendeshwa na ben na upande wa kushoto akiwa kakaa samira lilisimamaa na kumshusha samira ambaye alisikika akisema, " asante kwa surprise Ben, sikutegema kama leo ningetoka na kula chakula kizuri, nakushukuru umekuwa kaka yangu na asante kwa kumsaidia aunt amina"

"usijali Samira, sisi binadamu ni ndugu, na tunatakiwa kusaidiana bila kutegemea malipo yoyote..na wala usiwe na wasiwasi na mimi juu ya malipo au labda nataka kitu kwako, hapana nami kuna watu waliwahi nisaidia bila hata kudai, naamini na mimi nina deni kwa watu wenye shida pia na asante kwa kuwa dada na mungu atakupigania" alimaliza kuongea maneno hayo bwana ben na kuondoka eneo hilo.


Siku ya pili asubuhi samira alionekana akiwa hospitali kwa furaha akiongea na shangazi yake na akautumia mwanya huo kumsimulia juu ya mkasa aliokutana nao wa kuporwa na jinsi kijana ben alivyomsaidia na kumwahidi kuwa angemsaidia matibabu ya yake.


Akiwa pale hospitali mara alipigiwa simu na ben na alipotoka alikutana na ben akiwa daktari wa hospitali hiyo ambaye alimsuprise baada ya kumwonesha document zote za aunt amina kupelekwa nchini india kwa ajili ya matibabu.

Furaha ilimshika samira na kwa mshtuko ule ghafla alijikuta akianguka na kupoteza fahamu.Nusu saa baadae aliamka na kujikuta yuko pale hospitali kwenye kitanda akiwa kapumzishwa.

" Nesi nilikuwa naota au ukweli kuwa aunt yangu ataenda kupatiwa matibabu nje?"

" sio ndoto samira, ni ukweli mtupu na hivi sasa taratibu zimeshaanza kufuatwa kwani baada ya siku mbili atatakiwa kuwa ameshafika huko ili kuanza matibabu"

"Mungu wangu nakushukuru kwa kunikumbuka kipindi hiki ambapo dunia imenitenga" aliongea samira maneno yale na kutoka nje kwani ulikuwa ni muda wa daktari wa zamu kupita kwa wagonjwa.

Alirudi nyumbani na kuendelea na maandalizi ya chakula cha mgonjwa na jioni ya siku hiyo ben alikuja kumchukua na wakaongozana pamoja kwwenda hospital.Waliporudi ben alimshusha nyumbani na kuondoka zake.

Majira ya saa mbili na nusu za usiku samira akiwa anatoka nyumbani kwa rafiki wa aunt amina kumpa taarifa ya aunt amina kufanikiwa kupata ufadhili wa matibabu ghafla gari moja moja lilisimama na kumchukua kwa kumteka na kumpeleka kusikojulikana.

Hakuna aliyejua wapi alikuwa samira kwani hata majirani walishangaa mpaka inafika mida ya saa sita za usiku hakuwako nyumbani jambo ambalo halikuwa la kawaida kwa samira.

Baadhi ya majirani wakaanza kujipanga kumtafuta kwa kuanza hospitali ili kujua kama alirudi huko baada ya kutoka uko alikokuwa lakini bado hakukuwa na taarifa sahihi za kuweza kumpata.


Samira alikuwa kafungwa kitambaa cheusi usoni mwake pamoja na ule mwanga wa mbalamwezi lakini kamwe usingeweza kumgundua na watu wale walikuwa wamemzingira kana kwamba walitarajia kumshambulia kwa zile silaha za jadi walizokuwa wamezishika mikononi mwao.


" haya wewe binti sali sala yako ya mwisho, haiwezekani mtoto mdogo kama wewe utusumbue kiasi kwamba tunaonekana hatufai katika kazi tuliyotumwa" alifoka kijana mmoja ambaye kwa sauti yake ya ubabe ungehisi kuwa alikuwa ni kiongozi wa wenzake au la alitaka kuonesha kuwa anafanya kazi sana pengine kuwazidi wenzake.


Wakati huo Samira alishapoteza matumaini ya kuishi hapa dunia akisubiri kufa tu ghafla wakashtushwa na kishindo kikuu kilichoambatana na watu wawili kulalamika maumivu ya kichwa na kuanguka chini huku wengine wakikimbia na akiwa katika taharuki alishangaa kuona akibebwa jujuu kama beseni la ndizi na alipojaribu kujitoa mask alikutana na uso wenye mask pia.


Alingizwa kwenye bari moja bila ya kutambua wapi anaelekea kutokana na giza nene wala bila kupata nafasi ya kumtazama dereva huyo kutokana na ile mask aliyofungwa zaidi.Dakika chache baadae gari lilismama na akashusha na kutupwa chini kisha gari nikaondoka.


Akiwa hajui ni wapi katupwa na anahangaika kujitoa mask mara alisikia sauti ya mtu akimuuliza mwenzake

"Jamani huyu sio mtu huyu?"

" mzee majaliwa huyu ni mtu hebu washa tochi ya simu yako tumwangalie aliongea mzee mangi ambaye alikuwa akitoka kilabuni akiwa na rafiki yake mzee majaliwa..

" walifanikiwa kumfikia samira na kumsaidia na kuanza kuondoka naaye bila hata ya kumuuliza kitu kwani muda huo alikuwa akitokwa na machozi na kutoamini kama huyo hai na kujiuliza maswali mengi juu ya mambo hayo yanayomtokea na kuishia kusema kwa sauti kubwa " ASANTE MUNGU"

Mzee majaliwa na mzee mangi walifanikiwa kuonana na majirani wengine waliokuwa wakimtafuta samira na wakakubaliana wote waende kutoa taarifa kituoni ili nae apate nafasi ya kutoa maaelezo ya nini kilichomsibu.

walifika pale kituoni na samira akaeleza mkasa mzima na baada ya hapo wakarudi nyumbani na kila mmoja akaenda kwake na kumwacha samira akiingia nyumbani kwake na kulala.

Asubuhi na mapema samira aliamka na kwenda hospitali kumwangalia shangazi na kuona maendeleo yako ingawa hakutaka kumsimulia mkasa huo na baada ya kuongea na daktari juu ya maandalizi ya siku ya pili yake ambayo aunt amina alitakiwa kusafiri.

Aliporudi nyumbani alienda kwa jirani na kuazima simu ili ampigie ben na muda mfupi baadae samira aliondoka kwenda ambako ben alimwambia wakutane. Alipofika pale alimsumulia mkasa mzima.

Ben alimpa pole na baada ya hapo akaenda kumnunulia simu mpya na kumkabidhi na wakaachana kwa ahadi ya kukutana siku ya pili yake saa kumi na mbi jioni ili kumchukua aunt amina na kumpeleka uwanja wa ndege kwa ajili ya safari ya kwenda india.

Aunt amina alikuwa mwenye uso wa matumaini muda wote na akamshukuru sana ben ingawa hakuweza kumwona usoni na kumtania kuwa " asante sana mwanangu, naamingi kwa kudra za mwenyezi mungu nikirudi nitakuja kukuona vizuri. Asante"

"karibu sana aunt amina na nakutakia safari njema na matibabu mema"

Aunt amina apelekwa kwenye ndege na waliruka saa 08:45 za usiku kueleka india kwa ajili ya matibabu. Baada ya kuaagana ben na samira wakaondoka na kumwacha samira kituo cha daladala kwani ben alitakiwa kuwahi sehemu kwenye kikao cha biashara.



Mzee zombo alisikika akiongea na vijana wake na wakati huu alikuwa akitoa maelekezo kwa ukali zaidi.

" Pumbavu sana nyinyi, tena sio wanaume ni wanawake, yaani mnapiga simu na kusema kuwa mlipigwa? yaani kazi ndogo hiyo inawashinda? hamjui hata kutumia natural security?"

'mkuu alituzidi nguvu huyo mtu na hatujui amejuaje mkakati wetu

"nyambafu sana wewe tena usiongee kitu, nataka jioni hii mfanye kitu mbaya nitakutumia ujumbe haraka saa nimekaa sehemu mbaya"


Samira alikaa kituoni kwa muda mrefu kidogo na hatimaye daladala ikaja na akapanda kuelekea nyumbani. Alipofika karibu na nyumbani kwake alishangaa kuona moto mkubwa ukiwaka juu ya paa la nyumba yake na alipotazama kwa ukaribu akaona ............
 
6E46BA25-F7D6-465B-890E-58A66673FF89.jpeg

Chapter 7

Ilipoishia

" Pumbavu sana nyinyi, tena sio wanaume ni wanawake, yaani mnapiga simu na kusema kuwa mlipigwa? yaani kazi ndogo hiyo inawashinda? hamjui hata kutumia natural security?"

'mkuu alituzidi nguvu huyo mtu na hatujui amejuaje mkakati wetu

"nyambafu sana wewe tena usiongee kitu, nataka jioni hii mfanye kitu mbaya nitakutumia ujumbe haraka saa nimekaa sehemu mbaya"

Endelea

Samira alikaa kituoni kwa muda mrefu kidogo na hatimaye daladala ikaja na akapanda kuelekea nyumbani. Alipofika karibu na nyumbani kwake alishangaa kuona moto mkubwa ukiwaka juu ya paa la nyumba yake na alipotazama kwa ukaribu akaona kuwa moto umepamba na majirani wakijaribu kuuzima.

Majirani walipomuona samira walishikwa na mshangao ulioambatana na kumrukia kwa furaha kwani walihisi yuko ndani na wakashangazwa kuona jinsi watu hao waliochoma nyumba moto walivyoweza kuufunga mlango na kufuli kubwa nje ili kuhakikisha jitihada zozote za kuwaokoa waliomo ndani zinakwama.

Wakati huu samira hakutokwa hata na chembe ya chozi ila uso wake ulionesha kuwa ni mtu aliyekata tamaa na hakuongea neno zaidi ya kuangalia nyumba ile ikiteketea na juhudi za watu zikigonga mwamba kuokoa chochote kile kutokana na kushindwa kupata njia ya kuingia ndani.

Basi kikao chaa dharula kikafanyika nyumbani kwa mwenyekiti wa mtaa na mwalimu jack akaomba amchukue samira iili aweze kumtunza mpaka hapo aunt amina atakaporudi ili taratibu nyingine ziendelee..

Samira alipokelewa vizuri na familia ya mwalimu jack ambaye yeye alikuwa ameolewea na anaishi na mmewe pamoja na mtoto wao mdogo kwani ndoa yao ilikuwa bado changa.


Maisha yaliendelea na sasa samira akawa na jukumu pia la kumsaidia mwalimu jack kukaa na mtoto wakati mwalimu jack akiwa kazini na mmewe akiwa dukani kwake ambako ni jirai sana na makazi yao.

Siku moja majira ya saa nne za asubuhi mwalimu jack akiwa kazini na samira akiwa anafanya usafi sebuleni baada ya kumlisha na kumlaza mtoto, mara mmewe na mwalimu jack aliingia na kunza kuongea na samira.

"unajua wewe mtoto ni mzuri sana?"

"asante anko"

"naona chakula changu sasa kinakufanya unawiri sawa sawa"

" ha ha ha asante mjomba sio chakula tu, ila hata ukarimu wenu umenifanyanisahau kote nilikopitia nawashukuru sana"

"ok, sasa si unajua hii ni jamii?"

" ndio anko"

" sasa unaonaje tukijamiana kabisa?"

" anko unamaanisha nini tafadhali sijakuelewa?"

"ninachomaanisha nipe kidogo nichangamshe damu, si wajua huwezi kukaa hapa hivi hivi? hata kama ni mpangaji si lazima alipe kodi?" mjomba alimaliza kuongea maneno hayo na kuanza kumshikashika samira na kumlazimisha kuingia chumbani.

Samira alifanikiwa kumponyoka na kutoka nje akiwa analia kwa uchungu kwani alibanwa sana kooni na kuparuliwa usoni wakati wa tafrani hiyo. Mmewe na mwalimu jack akatoka nje kwa haraka na kuongea maneno ya chinichini yenye kuogofya ndani yake.

" Sasa wewe si kabambe? basi nitakuonesha na kama unadhani wewe mjanja basi msimulie na huyo mama mundu uone, hata pombe inaonjwa sasa wewe ni nani upitishe togwa na kuiweka kabatini kwangu na niiache?" alimaliza maneno hayo na kuondoka zake kurudi dukani kwake.

Usiku wakati wakiwa mezani kwa chakula cha usiku mwalimmu jack alishangaa kumwona samira akiwa na kovu usoni hivyo akaona amuulize.

" Samira vipi tena mbona una mikwaruzo usoni"


" aunt jack niliumia wakati naanika nguo ila usijli naendelea vyema"

" jamani kuwa makini usije pata majeraha na aunt amina akija aumie"

"Usijali aunt jack" alimaliza neno hilo na kunyanyuka kuelekea jikoni akimwacha mwalimu jack akiwa na mmewe mezani ambaye wakati huo alijifanya kuwa busy na kijiko chake huku mkono mwingine akiigusa gusa simu yake.

Siku ya pili asubuhi mmewe na mwalimu jack aliamka akiwa na hasira kama mbogo na kudai kuwa kaibiwa hela yake aliyoiweka juu ya kabati ingawa hakuna aliyedai kazichukua.

Hapo ndipo baba wa watu akapandisha hasira na kuanza kupekuwa chumba baada ya chumba mpaka akafanikiwa kuikuta bahasha yenye fedha hizo ikiwa kwenye kabati la nguo za samira tena katikati ya dira lake.

Samira alipokea kipigo cha mbwa mwizi kutoka kwa mmewe na mwalimu jack na kibao kimoja kilichomfanya aangukie sakafuni na kumpa nafasi mwalimu jack kumuuliza

" samira umeanza na tabia ya kuiba? humu ndani tupo watu wazima watatu tuu na mtoto mdogo asiyejua hata nini maana ya fedha, unafikiri utasema nini ueleweke na wakati wewe ndio unabaki hapa?"

" samahani aunt, kamwe sitakuja kuiba na sijawahi kuiba, labda wakati nafanya usafi nilichua bila kuona ila naombeni mnisamehe" aliomba samira kwa sauti ya chini huku akizidi kuomba msamaha.

Wakati huo mmewe na jack alishapiga simu polisi na hazikupita dakika nyingi polisi wawili walifika pale na kumchukua samira wakiambatana na mwalimu jack na mmewe kwenda kituoni kutoa maelezo. Baada ya kufika pale na kutoa maelezo samira alichukuliwa na kuweka mahabusu na kwa hasira mwalimu jack na mmewe wakaondoka.

Wakiwa njiani waliachana mwalimu jack akaelekea kazini na mmewe akanyoosha kuelekea dukani kwake na alopokuwa peke yake akaanza kujisemesha,

" pumbavu sana, yaani wewe umepewa bure na uko nyumbani kwa mtu bure unakula jasho lake lakini bado unaleta kiburi?

sasa kiburi chake kimemponza, yaani mchezo mdogo tuu nimemchezesha nae kaingia kati na nafikiri sasa huko atajamiana na mbu, na nitakapoenda kumtoa hapo baadae lazima alegeee tuu mtoto mdogo sana yule, ngoma yangu ile"


Pale polisi baada ya masaa kama mawili vile, polisi walikuwa wanakabidhiana zamu na polisi aliyekuwa akiingia muda huo alipofungua mlango wa mahabusu akashagaa kumwona samira.

" samira mdogo wangu kuna nini tena mpaka uko humu ndani? si ni jana tu nimekuona hapo mtaa wa pili ukiwa huru, vipi kuna nini?"

" dada nimetuhumiwa kuwa nimeiba fedha lakini ukweli sijaiba fedha yoyote ile"

" Kwa hiyo umefanya utaratibu gani? maana hapa sio pazuri"

"yaani sijui lolote dada"


"huna ndugu yoyote wa kuja kukuwekea dhamana?"

" Yupo kaka ben, ila sina namba yake kichwani"

"ook yule ben mwenye ile gari mark X?"

"Ndio"

Polisi yule wa kike baada ya kujibiwa hivyo na kwa kuwa anamfahamu ben alimpigia na muda mfupi baadae ben alikuja na akafanikiwa kumwekea dhamana na kumtoa kisha akaondoka mpaka nyumbani kwa mwalimu jack na kuomba msamaha kwa niaba ya samira na akaomba pia amchukue samira ili amtunze mpaka aunt yake atakaporudi jambo ambalo mwalimu jack alilipokea kwa furaha ili kuepusha kuendelea kuibiwa.


Ben na samira wakaondoka mpaka hostel moja ya wanafunzi ambapo ben akampangia chumba samira na kumwekea mahitaji yote ya msingi, kisha wakaachana.

Huku nyuma nyumbani kwa mwalimu jack mmewe na mwalimu jack aliishiwa nguvu kwani aliona kuwa njama zake zimegonga mwamba na akaanza kukaa kwa hofu akihisi kuwa samira angetoa siri muda wowote.


***

Ulikuwa umepita mwezi mmoja tangu mzee zombo afanikiwe kuteketeza nyumba ya aunt amina ambaye ni dada yake wa damu ili tu kuhakikisha anatumia nafasi hiyo kupoteza kabisa utambulisho wa samira na kwa habari alizokuwa nazo ilikuwa ni kwamba samira alikufa katika moto huo mkubwa ulioteketeza kila kitu.

Mzee zombo alikuwa akisherehekea ushindi wa kumtoa duniani samira nawatu walikuwa wakinywa kwa furaha na katikati ya tafrija hiyo mara gari la polisi likaizingira nyumba hiyo.
 
076B2A9C-A205-4BF5-ABB5-44FFB621650E.jpeg

Chapter 8

Ilipoishia

Ulikuwa umepita mwezi mmoja tangu mzee zombo afanikiwe kuteketeza nyumba ya aunt amina ambaye ni dada yake wa damu ili tu kuhakikisha anatumia nafasi hiyo kupoteza kabisa utambulisho wa samira na kwa habari alizokuwa nazo ilikuwa ni kwamba samira alikufa katika moto huo mkubwa ulioteketeza kila kitu.

Endelea

Mzee zombo alikuwa akisherehekea ushindi wa kumtoa duniani samira na watu walikuwa wakinywa kwa furaha na katikati ya tafrija hiyo mara gari la polisi likaizingira nyumba hiyo.

Polisi walishuka kwa mwendo wa haraka na kulizingira eneo hilo kwa kubana kila upenyo na ndipo mkuu wao akingia ndani na kumwita mzee zombo. Wakati huo mzee zombo yeye wala hakuwa hata na dalili ya hofu zaidi ya kutabasamu.

"karibuni wakuu, polisi ni sehemu ya usalama na najua mpaka muda hu nipo chini ya ulinzi yani kila idara iko salama"


"Ndugu hatujaja kwa utani hapa, uko chini ya ulinzi na tunakuhitaki uje kituo cha kati hapa kwani kuna maelezo tunayahitaji kutoka kwako" alitoa amri hiyo kamanda ambaye hata kwa sura yake kamwe usingelimwingia kwa neno lolote.

" tuliza munkari kamanda, kwani kuna nini la haraka hivyo ambalo sitakiwi kupata hata dondoo kabla ya kwenda huko kituoni? hebu tukae chemba tuongee sie watu wazima bwana" aliongea maneno hayo bilionea wa ukubwani mze zombo huku akiacha amri ya kupewa vinywaji wale polisi wengine waliokuwepo pale ndani nae akaingia chemba na kamanda mkuu.

" sikia mzee zombo, kijana wako mmoja alionekana katika tukio la moto lililotokea hivi karibuni na kuiteketeza nyumba, hivyo unahitajika kituoni kwa ajili ya malelezo"

" ha ha ha kumbe ndio hilo tuu kamanda? kwani nani mwingine anajua suala hili?"

" Limenifikia mimi pale na upelelezi wa kwanza umeonesha ni nyie mnaohusika kwani inasemekana pia hamna maelewano mazuri na nduguyo"


" hatuishi vizuri na nani? labda wao hawaishi vizuri na mimi, mimi ni mtu wa watu bwana na kama hauamini kuwa mimi ni mtu wa watu basi leo nitakuonesha kuwa mimi ni mtu wa watu" aliongea mzee zombo huku akiingia katika chumba kimoja na aliporudi alirudi akiwa na bahasha ya kaki iliyoonekana kuwa nzito.

" sasa kamanda, naomba ni kukabidhi hii bahasha na kila kitu ili hii kitu ishie si unajua tena masuala ya heshima maana ni watu tu wanataka kunichafua na si unajua nataka kugombea ubunge?"

" hilo nalielewa mzee mwenzangu hebu niachie mimi na kwa advertise utaona nikitoka hapo nje, kwanza ngoja niumalizie huu mvinyo kabla sijatoka" aliongea kamanda huyo huku akiificha vyema bahasha ile na kisha akaunyanyua mvinyo uliokuwa kwenye chupa akaugigida na kutoka nje kwa haraka


" haya afande tangulieni nitawakuta kituoni kuna jambo la kiitelejensia nataka kulishughulikia" alimaiza kamanda huyo akiwaacha wale vijana wakiondoka na yeye akarudi ndani na kuendelea kupata mvinyo katika chumba hicho walichokuwa wamekaa wawili tuu.

" sasa kamanda mimi nitaomba sana nikutumie kuanzia sasa, maana kuna watu wananipiga vita sana hivyo nitaomba msaada wako?

"hiyo haina shida mzee zombo wewe muda wowote ukiwa na jambo nishtue" alimaliza maneno hayo kamanda na wakaendelea na maongezi kwa muda na kisha wakaangana.


***
Ijumaa tarehe 26.07.2002

"Mama ulisema utanisimulia mkasa mmoja na nisiumie na mkasa huo, kwani unahusu maisha yangu, sasa nimekuwa mkubwa nina miaka 15 na leo ndio siku yangu ya kuzaliwa naomba unisimulie"

"Ni hadithi ndefu sana mwanangu na sikupenda uifahamu ila nafikiri ni vyema uifahamu na naamini pia haitakufanya upoteze mapenzi yako kwangu"


"mama unajua wanitisha sana? niambie basi tafadhali mama yangu"


" silikiliza mwanangu Salha, Kama ujuavyo kuwa mimi kazi yangu ni muuguzi mkunga, miaka kumi na tano iliyopita nikiwa kazini alikuja mama mmoja ambaye alikuwa kazidiwa na uchungu na uchungu huo ulitokana na mshtuko alioupata.

Alipokelewa na mimi nikawa msaidizi wake pale na akajifungua mtoto kabla ya muda wake na mtoto huyo alizaliwa akiwa na miezi saba. Ikabidi abaki pale hospitali hata baada ya mama yake kuruhusiwa ili aweze kuhudumiwa na mitambo maalumu ya kulelea watoto wa namna hiyo.


Kila siku asubuhi, mchana na jioni mama yule alikuja kumtembelea mwanae akiwa na baba na mtoto wao mwingine wa kike. Mama yule pamoja na familia yake walikuwa wazuri na walipendana sana.

Siku moja majira ya asubuhi alikuja kama kawaida na alipotoka muda mfupi baadae taarifa zilizagaa na kusemekana kuwa baba na mama wa mtoto yule walikufa walipokuwa wakitoka kumpeleka mtoto wao shuleni baada ya kutoka pale hospitali.

Basi baba na mama yule walizikwa na baada ya hapo familia yao ikaingia katika mgogoro mkubwa sana.Na kwa kuwa mimi nilikuwa nikimsimamia mtoto yule pale hospitali, basi alipofikia muda wa kutoka kwenye zile mashine nilimpeleka kituo chakulelea watoto na baada ya kuanza kutembea niliamua kumchukua na kukaa nae kwa siri kwani sikutaka ndugu zake wajue baada ya kupata kisa cha kumficha mtoto wa yule mama aliyebaki hai na ndugu walikuwa hawajui lolote juu ya mtoto aliyeachwa hospitali.

Mtoto huyu nikamtunza kwa mapenzi ya dhati na mpaka hivi leo ni binti mkubwa na anayesoma kidato cha tatu na jina lake anaitwa SALHA yaani wewe mwanangu. Kwa hiyo ukweli ni kwamba wewe ndio mtoto yule niliyekuwa nikimtunza pale hospitali."


Salha alipatwa mshtuko na ku...
 
E1798BB7-E339-42DA-8DF0-0466D35A6009.jpeg

CHAPTER 9

Ilipoishia

Mtoto huyu nikamtunza kwa mapenzi ya dhati na mpaka hivi leo ni binti mkubwa na anayesoma kidato cha tatu na jina lake anaitwa SALHA yaani wewe mwanangu. Kwa hiyo ukweli ni kwamba wewe ndio mtoto yule niliyekuwa nikimtunza pale hospitali."

Salha alipatwa mshtuko na ku....

Endelea

Salha alipatwa mshtuko na kuanza kulia kwa mfululizo kilio ambacho kilimfanya na mama yake aanze kulia ingawa yeye hakuwa akilia kwa yaliyomsibu Salha la hasha ila yeye sasa akakumbuka jinsi amilvyompoteza mmewe mtarajia asubuhi ya siku ya harusi yao.

Siku hiyo asubuhi mmewe mtarajiwa alikuwa kwenye bodaboda akiwahi kwenda salon kwa ajili ya maandalizi ndipo akakutana ana ajali hiyo iliyomfanya mama salha kuzirai zaidi ya siku nne akiwa mahututi na aliopoamka akapewa habari ya mimba yake ya miezi minne kutoka kwa sababu ya mshtuko.

Waliendelea kulia kwa muda mpaka pale salha aliponyanyuka na kumwendea mama yake na kumwambia, "

"mama, tambua sijalia kwa sababu ya kuwapoteza ndugu ila nalia kwa furaha kwani pamoja na dunia kuwa na watu wa ajabu wenye matukio ya kutisha na kusikitisha ila bado kuna watu kama wewe wenye kutetea uhai wa watu... Nitakuita mama daima na utakuwa mama daima naamini hata mama na baba watafurahi kuona nikifanya hivyo katika ulimwangu wao wa roho, ila nina hamu ya kumfahamu dada"

"Utamfahamu tu mwanangu muda ukifika, ila kwa sasa hata mimi naumiza kichwa kujua yuko wapi maana ndugu zako hawajaweka bayana yuko wapi na ni wagumu sana kuingilika, ila nitajaribu kutafuta mawasiliano ya shangazi yenu mmoja mbaye yeye hakuwa akikaa sana pale wazazi wako na baadhi ya ndugu zako walipokuwa wakiishi"

"Asante sana mama, nakupenda na amini nipo kwa ajili yako" Alinyanyuka Salha na kwenda chumbani kwake ambako mawazo yalimsonga juu ya dada yake na vifo vya baba na mama na baadae usingizi ukamnyemelea na kulala.

**********
Ben na Samira walionekana wakiwa kwenye gari wakitoka hostel na baada ya kutembea umbali wa kilomita kama 25 hatimaye wakawasili kwenye mji mmoja uliofahamika kwa jina la Moshono na moja kwa moja gari likanyoosha na kwenda kusimama katika mtaa mmoja wa watu waliostaarabika uitwao Ichenga na kupaki mbele ya nyumba moja ya kifahari.

"tumefika sasa Samira" aliongea ben huku akimsaidia samira kushuka kwenye gari kisha wakaisogelea hiyo nyumba na kuingia ndani.

" Kaka Ben hii nyumba ni nzuri sana ila mbona inaonesha hakuna watu" alihoji samira huku wakiingia chumba baada ya chumba katika nyumba hiyo ambayo hata kama ilionesha kuwa imetoka kufanyiwa marekebisho lakini bado ile hali ya uzamani iliifanya nyumba hiyo kuwa bora na ya kuvutia tofauti na baadhi ya nyumba pale mtaani.

"samira unajua ninahofia sana na usalama wa Aunt amina na wewe kwani pale nyumba yenu ilishaharibiwa na pia sina uhakika kama hiyo jumamosi akirudi itakuwa busara kumpeleka pale asije patwa na mshtuko, hivyo mtakaa kwa muda katika hii nyumba ili nimsikie nae atakuwa na lipi la kusema"

"Sijui nikuambie nini ili uuje furaha niliyonayo hapa moyoni mwangu, lakini nina imani baba na mama kokote waliko watakuwa wanakuona na kubfurahi pia, Mungu akupe mafanikio mara mia ya sasa.. asante sana kaka" alihitimisha maneno hayo Samira na kuanza kuangua kilio cha chini chini huku wakielekea kwenye gari..

Ni wakati huu ambapo samira akaanza kurudiwa na picha ya udogo wake akiwa na mama yake kwenye gari akipelekwa shule na sehemu mbalimbali na mara mambo ya hatari yakaanza kumsakama mara baada ya baba na mama kufa katika kisa cha ajabu na hatimaye alivyokuja kuokolewa na aunt amina ambaye sasa kuja kwa samira kumekuwa kama mkosi kwa maisha ya familia hiyo.

Akiwa katika msongo huo wa mawazo alishtushwa na sauti ya Ben ikimwambia " samira, tumeshafika hostel yaani ulikuwa na mawazo sana kwenye gari kuna nini kinakusibu kwani nimekusemesha zaidi ya mara tatu unaonekana kama upo haupo vile"

"kaka nilipitiwa na furaha ya nyumba sasa najua nitapumzika salama na kuisubiri siku ya aunt kurudi, zimebaki siku tatu ila naona ni kama miaka nimemkumbuka sana na nina furaha zaidi kuwa sasa kapona"

"Ok, basi mie nakuacha nafikiri zile hela bado unazo hivyo hakuna shida upande wako, nitakucheki kwa simu mida mida" Alihitimisha Ben na kisha wakaachana na samira yeye akaingia hostel.

Wakati anakaribia mlango wa hostel samira kuna kitu kilimfanya asite kuingia na kuamua kurudi nyuma na kujibana sehemu kwani muda huo giza lilikuwa limeanza kuwa la kumfanya mtu asione vyema.

Akajisogeza hatua kama nne na ku...................
 
997DA7A9-2770-4ED6-A591-DFEC921B7E2C.jpeg

CHAPTER 10

Ilipoishia



"Ok, basi mie nakuacha nafikiri zile hela bado unazo hivyo hakuna shida upande wako, nitakucheki kwa simu mida mida" Alihitimisha Ben na kisha wakaachana na samira yeye akaingia hostel.

Wakati anakaribia mlango wa hostel samira kuna kitu kilimfanya asite kuingia na kuamua kurudi nyuma na kujibana sehemu kwani muda huo giza lilikuwa limeanza kuwa la kumfanya mtu asione vyema.

Akajisogeza hatua kama nne na ku...................

Endelea

Akajisogeza hatua kama nne na kukijibanja pembeni ya ukuta wa hostel hiyo, sehemu ambapo hakuna mtu ambaye angefanikiwa kumwona kwa urahisi ingawa yeye aliweza kuona na kusikia vyema kila kilichoendelea.

" Oya huyu mtoto inaonekana hayupo na kama haitoshi muda huu bado kweupe kweupe na kuna wapangaji wengine wanaweza kuja na kuharibu deal, kama vipi wewe zima simu ili boss asitupate muda huu na ikifika mida ya saa sita tuje tufanye kazi hawa ngedere wakiwa wamelala"

Alimaliza kuongea mtu mmoja ambaye kwa mbali alionesha kama alikuwa akitaka kurudi lango kuu kutokea dirishani mwa chumba cha kulala samira alipokuwa kasimama huku mwenzie akimfuata taratibu.

Hazikupita hata sekunde kadhaa, samira alishtuka kuona akiwa kashikwa na mtu aliyembana kwa kitambaaa fulani kwenye mdomo wake na pia kilichoifunika pua yake jambo lililomfanya alishindwe kupiga kelele hata ile ya kurusha mguu na hatimaye taratibu alijikuta akiishiwa nguvu na kupoteza fahamu.

Saa tano na dakika 45 za asubuhi mlango wa chumba uligongwa na kisha dada mmoja aliingia na kukaa kitanda alichokuwa kalala samira ambaye nae ndio alikuwa akianza kurudiwa na fahamu.

" Umeamkaje dada?"

"salama kiasi kwani nipo wapi hapa na nimekujaje hapa?" Alihoji samira ambaye kwa uchovu alikuwa akijiweka sawa pale kitandani.

" Dada, hii inaitwa PLEASE REST IN PEACE GUEST HOUSE," aliongea dada huyo ingawa ilimbidi atulie kuongea baada ya samira kushtuka kulisikia jina hilo.

"Rest in peace!!!!!! yani kama ile ya R.I.P? oooh maskini mimi!!!, MUNGU wangu kwani nini tena?"

"samahani dada, sio rest in peace kama maana ya ile ya kumwambia marehemu hapana,hii ni maana nyingine" aliongea dada huyo huku akimsaidia kumpa tishu ya kufutia machozi samira na kisha akaendelea kuongea

" jana nilikuwa zamu ya usiku ambayo huishia asubuhi ya leo saa mbili, na wakati nikiwa mapokezi nilisikia kishindo hapo nje na nilipoenda haraka nikaona ukiwa umeanguka pale sakafuni.

Ulikuwa haujielewi na kama umelewa vile maana hukuweza kuongea wala kusema lolote. Nikakupekua na kuona mfukoni una shilingi laki 2 na simu yako, vyote nikakuwekea na kuamua kukupa chumba ili upumzike kwani nilihisi utakuwa uliwekewa madawa ya kulevya ili wakuibie na sasa ulifanikiwa kufika mpaka hapa na unahitaji msaada"

Wakati wote huo samira alikuwa kashikwa na bumbuazi iliyomfanya hata yale machozi yakauke na sasa akabaki kushangaa kwani kumbukumbu pia zilianza kumrejea na akakumbuka kuwa jana yake hakuwa na fedha nyingi hivyo bali alikuwa na shilingi elfu kumi na mbili na tena hakuwa ametembea nayo.

Mawazo yakaanza kumrudia tena na wakati huu akafikiria suala la mtu kumwekea fedha na kumpeleka katika hoteli hiyo ambayo hajawai kuisikia na haraka akamuuliza yule dada,

" Samahani dada kwani mtaa huu unaitwaje? na je ni mbali sana na stand kuu?"

" hapana ni umbali mdogo kwani unapanda daladala moja tuu au hata kwa bodaboda ni shilingi elfu tatu tuu."

" ok, asante naomba simu na hela" Samira alimwomba dada huyo na kisha akapokea fedha hizo na baada ya kumlipa akaondoka haraka na kuchukua bodaboda mpaka stand kuu.

Alipofika stand kuu akaenda moja kwa moja kwenye kibanda kimoja cha simu na kuweka zile fedha kwenye simu yake na baada ya hapo akampigia simu Ben na baada ya ben kumwambia sehemu aliyoko. Samira alichukua tena bodaboda na kumfuata.

Walionana na baada ya kumsimulia ben, ben akamhakikishia usalama na kumwambia sasa atahakikisha anamwamisha pale na kupeleka hoteli nyingine ambako atalala kwa siku mbili na siku ya tatu yake wakishampokea aunt amina basi watahama eneo hilo na kwenda kuishi kule Moshono ambako hakuna atakayepajua.

Na kuhusu suala la pesa ile laki mbili ben akamwambia umefanya vyema kuiweka kwenye simu ili tusubiri tuone kama kuna mtu atapatikana ili tumchukulie hatua za kisheria, maana nafikiri kuna kitu kinasukwa na hatujui ni nani maana unakutana na mambo makubwa sana dada samira.

Samira alimshukuru sana na wakaachana na ben kwa miadi ya kuwa aende mpaka hostel akaweke mizigo yake sawa ili dereva aende kumchukua na kumpeleka hoteli mpya.


Samira alifika mpaka pale hostel na kabla ya kuufungua mlango wake akaona aende pale alikojificha usiku kwani kumbukumbu ilimrudia na kukumbuka kila kilichofanyika pale jana yake usiku na wale watu waliokuwa dirishani kwake.

Alipolikaribia dirisha lake kwa chini samira aliona.......................
 
4940B1DF-D522-4897-9496-E6F111D59366.jpeg

CHAPTER 11

Ilipoishia


Samira alimshukuru sana na wakaachana na ben kwa miadi ya kuwa aende mpaka hostel akaweke mizigo yake sawa ili dereva aende kumchukua na kumpeleka hoteli mpya.


Samira alifika mpaka pale hostel na kabla ya kuufungua mlango wake akaona aende pale alikojificha usiku kwani kumbukumbu ilimrudia na kukumbuka kila kilichofanyika pale jana yake usiku na wale watu waliokuwa dirishani kwake.

Alipolikaribia dirisha lake kwa chini samira aliona.......................


Endelea


Alipolikaribia dirisha lake kwa chini samira aliona kuna pakiti ya sigara iliyotumika na kilichimfanya asimame na kuokota ilikuwa ni business card moja iliyokuwa na jina la h zombo ambaye alionesha kuwa ni mmiliki wa kampuni moja ya usindikaji vyakula na matunda.

Kilichomshutua zaidi ni nyuma ya business card hiyo kuwa na jina lake na la aunt amina. Moyo ulimruka na ghafla jasho la uoga likaanza kumtoka bila hta ya kutarajia akajikuta akitamka " Mungu wangu, ina maana watu hawa bado wananitafuta mimi na aunt amina, na je huyu mzee kombo ni nani?"

Hata kabla ya kujipa jibu akasikia muungurumo wa gari likija alipochungulia akaona ni dereva aliyetumwa na Ben, akaificha ile business card na kisha kaingia kuchukua mizigo na kuondoka kuelekea hoteli.

Hoteli hiyo ilikuwa nzuri na aliufurahia ulinzi wa eneo hilo na kwa hakika akijesemesha " Asante Mungu naamini kwa muda hapa nitakuwa salama na naomba umrejeshe salama aunt amina na hakika tuweke mikononi mwako ili tuwe salama"

Kwa upande mwingine mapambano huko mtaani yalipamba moto sana kwani samira alipotea kutoka mikononi mwa vijana wa mzee zombo. Walijaribu kufuatilia kila kona lakini hawakupata dalili yoyote juu ya wapi aliko samira ikabidi wampigie simu bosi wao.

" Pumbavu sana nyie yaani mnakuwa kwama landline crocodilelicious, yaani katoto kadogo kanwashinda... Sasa nasema nitamtuma mtu aje awalete hapa muone moto au mpaka jioni mnipe jibu zuri"

Kijana aliyekuwa anapiga simu akajikuta akishindwa kuvumilia na kucheka na kumuuliza, "mzee kwani hiyo landline crocodilelicious ni nini?"

" acha ujinga, hilo swali muulize baba yako ambaye hakukupeleka high education institute of centre, hapo nimekutukana sana kwa kiingereza, haya sina muda wa kuongea na mapuuzi sasa nasema rudini kazini"

Kijana yule aliishiwa nguvu na kujikuta akikaa chini na kucheka hasa akikumbuka kiingereza cha mzee zombo ambaye hakuwa na historia ya kuhudhuria shule kama alivyokuwa akijitamba na maneno ya kiingereza kisichoeleweka na muda mfupi baadae waliondoka eneo hilo kuendelea kumsaka samira.


Siku hiyo samira aliwahi kuamka na tayari alikuwa ameshajiandaa akimsubiri Ben ili waende airport kumpokea aunt amina ambaye akikuwa akirudi siku hiyo. Ben alifika pale hotelini akiwa analalamika njaa hivyo akaona ni boda aagize chakula kwa kuwa muda ulikuwa bado unaruhusu hivyo wakajumuika pamoja na samira.

Muda mfupi baadae ben na samira walikuwa sehemu ya kupokelea wageni pale airport. Samira alikuwa kavaa sketi yake fupi na top moja iliyomfanya aonekane vizuri hasa chuchu zake zilizokuwa zimechomoza pale kifuani mithili ya vichuguu uchungu viwili huku sketi ikiuacha mguu wake uliojazia nao upate kuonekana kiurahisi.

Lakini hips, nywele ndefu za kimanga na jicho la samira ndio vitu vilivyowafanya baadhi ya wanaume wakware wenye nia binafsi na samira wamkodolee macho huku wengine nao wakimchukia ben kwa kuwa karibu na binti huyu ingawa nae ben mara moja au tatu alidakwa na jicho la samira akiwa anamkodolea macho na akapotezea kwa kumsifia au kumfariji juu ya aunt amina.

Aunt amina aliwasili pale baada ya ndege yake kushuka samira alipong'aza aunt amina alirukwa na furaha na kujikuta akimkumbatia na kulia kwa furaha na hakuamini kama kweli alikuwa kapona na anaona tena.Walingia garini na ben akawachukua moja kwa moja mpaka moshono na kwenda kupaki mtaa wa ichenga na kisha wakashuka garini.

Aunt amina alisita kungia ndani na akajikuta akitokwa na machozi na .................
 
6FB74144-AB66-4B3C-B02A-53E112858C12.jpeg

CHAPTER 12

Ilipoishia

Aunt amina aliwasili pale baada ya ndege yake kushuka samira alipong'aza aunt amina alirukwa na furaha na kujikuta akimkumbatia na kulia kwa furaha na hakuamini kama kweli alikuwa kapona na anaona tena.Walingia garini na ben akawachukua moja kwa moja mpaka moshono na kwenda kupaki mtaa wa ichenga na kisha wakashuka garini.

Aunt amina alisita kungia ndani na akajikuta akitokwa na machozi na.................


Endelea

Aunt amina alisita kungia ndani na akajikuta akitokwa na machozi na ghafla akawa kama mtu aliyepandwa na kichaa na kuanza kupiga kelele huku akikimbia kuifuata barabara kuu ili arudi mjini.

Iliwachukua zaidi ya saa moja na nusu Ben na Samira kuweza kumtuliza na kumwambia ukweli aunt amina juu ya mmewe kuuawa katika tukio lile, nyumba kuchomwa moto na kila njia aliyoipitia samira mpaka kukutana na ben aliyemsaidia na kuhakikisha kuwa aunt anatibiwa na kurudi salama.

Samira pia akamweleza aunt amina kuwa hajawahi kuona mtu mwenye moyo wa kusaidia kama wa ben na imemshangaza na kuona kumbe kuna binadamu bado wa chembe ya utu hata kama dunia na watu wake wanazidi kuwa vichaa na wanyama wasio wajali wenzao na mapito yao.

" Asante sana mwanangu Ben, Mungu akupe baraka tele na pia awe mlinzi wako katika kila njia ya mafanikio mbele yako. Mimi nitaomba jambo moja tuu"


"Asante, sema tu aunt amina"

"Nitaomba kesho kwenda kuliona kaburi la mme wangu na kuwashukuru majirani na kisha nije kuishi hapa kwa muda kama ulivyosema" Aliongea aunt amina kwa sauti ya unyonge na maumivu.

" usiseme kwa muda aunt amina, mimi naomba ukae tuu na pia nitajitahidi kujaribu kuangalia nini nikupe ukifanye ili uweze pata kipato na Samira arudi shule aendelee maana mwaka huu ni kama hajasoma kutokana ma shida hizi"

" asante sana kaka ben, mungu akubariki" alidakia samira na kumfuta ben na kumnyanyua aunt amina ambaye alimkumbatia ben kama ishara kuonesha kuukubali na kuuthamini mchango wake na kisha akamali
zia kwa kusema " mwanangu ni wanaume wachache sana wanaoweza kumsaidia mtu bila ya kutarajia malipo, nakushurukuru kwa kunifanya nione tena"

Ben aliwaacha na kuliwasha gari lake na kisha akaondoka kwenda mjini ambako aliishia kwenye hotel moja na kujipatia chakula cha usiku huku akiwa na fikra nyingi juu ya aunt amina ambaye kiukweli hata kama ungekuwa ni wewe msomaji ungetokwa na machozi kwa jinsi alivyoumia kuona mmewe kaondoka katika tukio la kikatili.

Usiku ule aunt amina aliongea mengi sana na samira na walijadili mengi na kila halipoongea aliishia kulia kwani aliamini kuwa furaha yake na faraja pekee imetoweka, " hebu fikiria unakaa na mwanaume kwa miaka nenda rudi hujabahatika kupata mtoto lakini bado anakupenda kwa dhati na hana hata dalili za kutoka nje ya ndoa au kukusaliti, na hata ndugu wanapojaribu kuwagombanisha bado yuko upande wako, Kweli nimeamini kuwa watu wazuri huwa hawadumu"

Maneno hayo aliyatoa aunt amina bila hata kutarajia na kumfanya samira agundue jambo ambalo alikuwa halijui kwa undani.Samira na aunt amina walikuwa na jambo moja ambalo kwa pamoja walibarikiwa nalo lilikuwa ni kuimba nyimbo kila walipokuwa katika wakati mgumu, muda huu walijikuta wakianza kuimba wimbo wao waupendao ambao taratibu uliwateka na usingizi ukatumia mwanya huo kuwabeba.


Ben alikaa pale hotelini na kuendelea kuagiza vinywaji huku sasa akijikuta kuanza kumfikiria samira kwa mtazamo tofauti na kila alipoongeza funda jipya la kinywaji chake akajikuta akipata ujasiri wa kumpigia samira na kumwambia neno ingawa ujasiri huo kuna wakati ulitoweka na kuamua kuacha.

Alikaa pale kwa muda na akaitoa simu yake na kuiangalia kwa umakini picha ya samira na kila alipotaka kumwambia kitu samira alishindwa akaamua kuandika sms hii, " Nimevumilia kwa muda lakini najikuta nashindwa kuendelea kujifanya sina hisia nawe, naomba kama ikiwa ni kwa mapenzi yako pia bila kuathiri uhusiano wetu basi tufungue ukurasa mpya"

Alishikilia kitufe cha kutumia ujumbe huu kwa muda akitafakari kama atume au asitume. Akiwa katika hali hiyo kuna rafiki yake mmoja alifika pale na kama ilivyo kwa taratibu zao za kusalimiana alimgonga bega ben kwa nyuma na kumsalimia jambo lililomshtua ben kwani alikuwa kwenye dimbwi la mawazo.

Alipokuja kupata fahamu akagundua kumbe ile meseji ilijipekeka alipogongwa bega na yule rafiki, ben alijikuta akitamka kwa sauti kubwa NOOO!!!! NOOO!!! na kutoka nje ili ampigie samira kumwambie sio ujumbe wake.


Alipiga simu ya samira kwa muda ingawa haikupokelewa alipoiangalia saa yake akagundua kuwa ni saa nane kasoro za usiku. akaishiwa nguvu na kuingia hotel kulipa bili yake na kisha kurudi kwenye gari na muda mfupi baadae akawa barabarani.


Wakati anatokeza barabara kuu kuna magari mawili yalikuja kwa kasi moja likitokea nyuma na jingine mbele na kumzingira ben na..........................
 
5C51AF0E-DD23-47B8-AF21-EB78490F08E4.jpeg

CHAPTER 13

Ilipoishia

Alipiga simu ya samira kwa muda ingawa haikupokelewa alipoiangalia saa yake akagundua kuwa ni saa nane kasoro za usiku. akaishiwa nguvu na kuingia hotel kulipa bili yake na kisha kurudi kwenye gari na muda mfupi baadae akawa barabarani.

Wakati anatokeza barabara kuu kuna magari mawili yalikuja kwa kasi moja likitokea nyuma na jingine mbele na kumzingira ben na..........................


Endelea

Wakati anatokeza barabara kuu kuna magari mawili yalikuja kwa kasi moja likitokea nyuma na jingine mbele na kumzingira ben na watu wale wakalivamia gari la lake na kumtoa nje kwa kurupushani huku mmoja wao akiutumia mwanya huo kumchoma sindano moja iliyomfanya ben alegee taratibu na kisha kutupwa kwenye moja kati ya magari yale siti ya nyuma na safari ikaanza huku ben akiwa sasa kalala na hajitambui.

Watu wale walikuwa wamevaa mask ambazo hazikuweza kuruhusu kuzifahamu sauti wala sura zao kutokana na aina ya mask hizo, hivyo ule muda wa purukushani ingekuwa ni ngumu kwa ben kuwatambua .

Mgari yale yalitembea kwa muda wa takribani dakika kama 30 na baadae yaliingia katika jumba moja pembeni ya mji lililoonekana kuwa ni kubwa na pengine mmiliki wake kuwa na kipato cha kutosha. Walimshusha ben aliyekuwa kalala kutokana na ile sindano na kisha watu wale wakamfungia kwenye chumba kimoja na kumwacha.

" Mkuu tumempata mtu uliyetutuma tukamchukue na tumeshamfungia kwenye chumba ulichotuamuru, kuna jingine la kufanya kwa sasa?" alihoji mmoja wa watu wale ambaye kutokana na amri zake kwa wenzake ni dhahiri kuwa alikuwa ndio kiongozi

" Hapana nafikiri mwacheni kama nusu saa kwani kuna kitu nakifanya kisha nitakuja nyie mwongezeni ile sindano ili asizinduke sasa" " Sawa mkuu" alimalizia kijana huyo na kisha kwenda kutekeleza amri.

Saa tisa kasoro za usiku samira alishtuka kutoka usingizini na akawa anajisikia kiu ya maji hivyo akanyanyuka na kwenda jikoni akachukue maji. Baada ya kunywa maji akaona sio mbaya aangalie simu, alishtuka kuona kuna missed calls pamoja na sms kutoka kwa Ben.

" Nimevumilia kwa muda lakini najikuta nashindwa kuendelea kujifanya sina hisia nawe, naomba kama ikiwa ni kwa mapenzi yako pia bila kuathiri uhusiano wetu basi tufungue ukurasa mpya"

Sms hii ilimfanya samira apoteze usingizi wake wote na kujitupa kwenye sofa pale sebuleni na kuanza kuitafakari, " maskini!!!! kumbe muda wote huu ben ana hisia na mimi na akaogopa kuniambia. Au ndio maana kamsaidia aunt amina? Na je nikimkataa inamaana ndio utakuwa mwisho wa msaada wake kwetu au hata kututoa kwenye nyumba?

Je nimwambie aunt amina au nitulie, na je nikimwambia atanichukuliaje? Hapana liwalo na liwe kwa sasa mapenzi hapana, ila nafikiri ni bora nimpigie na kujaribu kumwambia kuwa kutokana na yote yaliyonisibu kwa sasa sina fikra na mambo hayo, ili anipe muda kisha nikihitimu shule tulijadili, je ataelewa lakini?

Hapana nafikiri ngoja nimpigie simu sasa, mmmh!! ila nahisi kama ni usiku sana, nitampigia asubuhi, lakini kwa mtu mwenye kujitoa kama huyu katika maisha yetu, si na mimi natakiwa kumfikiria nae afurahi na kuona pia kuna watu wanamjali?"Samira alijiuliza na kujijibu bila ya jibu sahihi na hatimaye usingizi ukamchukua pale kwenye sofa na kulala usingizi mzito.

Saa tisa na nusu ikielekea saa kumi kasoro za alfajiri mlango wa chumba alichowekwa ben ulifunguliwa na boss wa vijana wale akaanza kuwakaripia wale vijana wake, " jamani mmefanya nini tena? huyu mliyemleta ni nani, mbona simfahamu? Huyu siye angalieni vyema ile picha ya gari niliyowapa"

" samahani boss basi magari yanafanana sana tukajua ndio hili kwani lilikuwa sehemu uliyotuambia tukatege na ni kama lile"

" haya sasa haraka mfungueni na nendeni mkarudishe pale mlikomchukua na hakikisheni hakuna anayewafuatilia, na mara nyingine kuweni makini makosa kama haya hayahitajiki na ni hatari"

"Sawa boss" Aliongea kijana huyo kwa uoga huku akimchukua ben ambaye bado alikuwa hajaamka kutokana na sindano ile.

Muda mfupi baadae vijana wale walifika pale njia panda walikomchukua ben na kumwingiza kwenye gari lake na kisha wao wakatokomea kusikojulikana wakimwacha ben akiwa pale ndani ya gari lake na wakati huo ilikuwa inakaribia kumi na moja kasoro za alfajiri.


Saa moja kasoro za asubuhi ben ali............................................................
 
View attachment 2458947
CHAPTER 13

Ilipoishia

Alipiga simu ya samira kwa muda ingawa haikupokelewa alipoiangalia saa yake akagundua kuwa ni saa nane kasoro za usiku. akaishiwa nguvu na kuingia hotel kulipa bili yake na kisha kurudi kwenye gari na muda mfupi baadae akawa barabarani.

Wakati anatokeza barabara kuu kuna magari mawili yalikuja kwa kasi moja likitokea nyuma na jingine mbele na kumzingira ben na..........................


Endelea

Wakati anatokeza barabara kuu kuna magari mawili yalikuja kwa kasi moja likitokea nyuma na jingine mbele na kumzingira ben na watu wale wakalivamia gari la lake na kumtoa nje kwa kurupushani huku mmoja wao akiutumia mwanya huo kumchoma sindano moja iliyomfanya ben alegee taratibu na kisha kutupwa kwenye moja kati ya magari yale siti ya nyuma na safari ikaanza huku ben akiwa sasa kalala na hajitambui.

Watu wale walikuwa wamevaa mask ambazo hazikuweza kuruhusu kuzifahamu sauti wala sura zao kutokana na aina ya mask hizo, hivyo ule muda wa purukushani ingekuwa ni ngumu kwa ben kuwatambua .

Mgari yale yalitembea kwa muda wa takribani dakika kama 30 na baadae yaliingia katika jumba moja pembeni ya mji lililoonekana kuwa ni kubwa na pengine mmiliki wake kuwa na kipato cha kutosha. Walimshusha ben aliyekuwa kalala kutokana na ile sindano na kisha watu wale wakamfungia kwenye chumba kimoja na kumwacha.

" Mkuu tumempata mtu uliyetutuma tukamchukue na tumeshamfungia kwenye chumba ulichotuamuru, kuna jingine la kufanya kwa sasa?" alihoji mmoja wa watu wale ambaye kutokana na amri zake kwa wenzake ni dhahiri kuwa alikuwa ndio kiongozi

" Hapana nafikiri mwacheni kama nusu saa kwani kuna kitu nakifanya kisha nitakuja nyie mwongezeni ile sindano ili asizinduke sasa" " Sawa mkuu" alimalizia kijana huyo na kisha kwenda kutekeleza amri.

Saa tisa kasoro za usiku samira alishtuka kutoka usingizini na akawa anajisikia kiu ya maji hivyo akanyanyuka na kwenda jikoni akachukue maji. Baada ya kunywa maji akaona sio mbaya aangalie simu, alishtuka kuona kuna missed calls pamoja na sms kutoka kwa Ben.

" Nimevumilia kwa muda lakini najikuta nashindwa kuendelea kujifanya sina hisia nawe, naomba kama ikiwa ni kwa mapenzi yako pia bila kuathiri uhusiano wetu basi tufungue ukurasa mpya"

Sms hii ilimfanya samira apoteze usingizi wake wote na kujitupa kwenye sofa pale sebuleni na kuanza kuitafakari, " maskini!!!! kumbe muda wote huu ben ana hisia na mimi na akaogopa kuniambia. Au ndio maana kamsaidia aunt amina? Na je nikimkataa inamaana ndio utakuwa mwisho wa msaada wake kwetu au hata kututoa kwenye nyumba?

Je nimwambie aunt amina au nitulie, na je nikimwambia atanichukuliaje? Hapana liwalo na liwe kwa sasa mapenzi hapana, ila nafikiri ni bora nimpigie na kujaribu kumwambia kuwa kutokana na yote yaliyonisibu kwa sasa sina fikra na mambo hayo, ili anipe muda kisha nikihitimu shule tulijadili, je ataelewa lakini?

Hapana nafikiri ngoja nimpigie simu sasa, mmmh!! ila nahisi kama ni usiku sana, nitampigia asubuhi, lakini kwa mtu mwenye kujitoa kama huyu katika maisha yetu, si na mimi natakiwa kumfikiria nae afurahi na kuona pia kuna watu wanamjali?"Samira alijiuliza na kujijibu bila ya jibu sahihi na hatimaye usingizi ukamchukua pale kwenye sofa na kulala usingizi mzito.

Saa tisa na nusu ikielekea saa kumi kasoro za alfajiri mlango wa chumba alichowekwa ben ulifunguliwa na boss wa vijana wale akaanza kuwakaripia wale vijana wake, " jamani mmefanya nini tena? huyu mliyemleta ni nani, mbona simfahamu? Huyu siye angalieni vyema ile picha ya gari niliyowapa"

" samahani boss basi magari yanafanana sana tukajua ndio hili kwani lilikuwa sehemu uliyotuambia tukatege na ni kama lile"

" haya sasa haraka mfungueni na nendeni mkarudishe pale mlikomchukua na hakikisheni hakuna anayewafuatilia, na mara nyingine kuweni makini makosa kama haya hayahitajiki na ni hatari"

"Sawa boss" Aliongea kijana huyo kwa uoga huku akimchukua ben ambaye bado alikuwa hajaamka kutokana na sindano ile.

Muda mfupi baadae vijana wale walifika pale njia panda walikomchukua ben na kumwingiza kwenye gari lake na kisha wao wakatokomea kusikojulikana wakimwacha ben akiwa pale ndani ya gari lake na wakati huo ilikuwa inakaribia kumi na moja kasoro za alfajiri.


Saa moja kasoro za asubuhi ben ali............................................................
Muendelezo ukiweka nitag
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom