Mabinti wa kibongo na Oman

Mabinti wengi wanaokwenda oman kazi yao kubwa ni uchangudoa, housegirl na kusuka kwa wale wenye ufundi huo. Na wengine huwa wanaishia kuolewa na vibabu vya huko.
 
mkuu hiko kitu ndio hata sisi kinatutia wasiwasi ila rafiki yake anapinga vikali sana kauli hiyo
nyie ndo wasemaji wa mwisho wa familia ni jukumu lenu kutoa maamuzi, mtu baki hawezi kuwalazimisha! kwanza bado mdogo sana wakaanze kumla 0713 waarabu wasivyo na utani na 0713!
 
Human trafficking, imeshamiri duniani pindi ufikapo kwa waliokununua huna maamuzi yyt utafanya wanalotaka. Be vigilant
 
Habari za asubuhi wanajamvi,wanafamilia tumejikuta katika njia panda baada ya mdogo wangu wa kike(mtoto wa bamdogo) anaishi na wazazi wangu kua rafiki yake ambae alikua Oman anafanya kazi katika salon ya kuchora hina amekuja kumchukua ili waondoke wote wakajiunge katika kazi hiyo.Wanafamilia wote hakuna anayeafiki hilo suala ila yeye ndio amekomaa na huyo rafiki yake anajaribu kutushawishi kua hakuna tatizo atakua katika mikono salama,sisi tunahofia maana binti ndio ana 20 yrs hana professional yoyote ni form four leaver tu.Wanajamvi najua humu kunawenye uzoefu na Oman katika hili naomba mnisaidie kunifunua macho kweli hili jambo liko salama kwa binti huyu?
Uarabuni kuna format moja tu ya ajira kwa wageni na hasa wafrika nayo ni utumwa. Kama unajali utu na heshima asiende kama unajali fedha tu anaweza kwenda.
 
inaonekana huyo binti mmemchoka, miaka 20 alitakiwa awe busy na masomo au na kitu chochote chenye future ya maisha yake. inaonekana hana mwelekeo huyo binti.
 
Muangalie huo rafiki yke tabia yke na familia hapa tanzania yukoje. Wengi sana wanaenda kwa ajili ya hinna kwan inalipa na wanaonekana mafanikio yao hasa wanaochukuliwa wanatoka znz ss km hatak kusoma na kipaji anacho mwache akiendeleze km uchangudoa ht hapa anaweza kufanya bila ya kushurutishwa. Achen ujinga kama ni kuhofia weng wasingepeleka watoto wao nje kusoma kuhofia kuwa ma.la.ya
 
Mkuu omani kuna mtoto wa dada yangu alipelekwa kama mfanyakazi wa kuuza duka alipofikishwa kaambiwa kuwa duka limeibiwa na hatimae kawa mfanyakazi wa ndani kateswa kama nini ikabidi siku moja kapiga simu kwa kuiba ndipo dada kaenda kumchukua kuna wengine wanateswa sana na kufukuzwa na waishia kuwa watu wa kujiuza na nauli hana ya kurudi
ni hayo tu mwambie asiende huyo hajui yaliyoko huko anaona sifa kuwa kafika sifa lakini maisha yake siyo salama mijitu ya huko bado inaamini kuwa utumwa duniani hauwezi kuisha kwa waafrika
hivi kwa nini achukuliwe akafanye kazi huko wakati na huko kuna watu kama huku ujue kuwa huyo anapelekwa kwa matumizi yasiyo halali
Habari za asubuhi wanajamvi,wanafamilia tumejikuta katika njia panda baada ya mdogo wangu wa kike(mtoto wa bamdogo) anaishi na wazazi wangu kua rafiki yake ambae alikua Oman anafanya kazi katika salon ya kuchora hina amekuja kumchukua ili waondoke wote wakajiunge katika kazi hiyo.Wanafamilia wote hakuna anayeafiki hilo suala ila yeye ndio amekomaa na huyo rafiki yake anajaribu kutushawishi kua hakuna tatizo atakua katika mikono salama,sisi tunahofia maana binti ndio ana 20 yrs hana professional yoyote ni form four leaver tu.Wanajamvi najua humu kunawenye uzoefu na Oman katika hili naomba mnisaidie kunifunua macho kweli hili jambo liko salama kwa binti huyu?
 
inaonekana huyo binti mmemchoka, miaka 20 alitakiwa awe busy na masomo au na kitu chochote chenye future ya maisha yake. inaonekana hana mwelekeo huyo binti.

tumejaribu kumshawishi arudie mitihan ili apate crediit ameshindwa mara mbili tumemshaur achague anachotaka kusoma ufundi wowote hataki inshort hatumuelewi kabisa
 
Muangalie huo rafiki yke tabia yke na familia hapa tanzania yukoje. Wengi sana wanaenda kwa ajili ya hinna kwan inalipa na wanaonekana mafanikio yao hasa wanaochukuliwa wanatoka znz ss km hatak kusoma na kipaji anacho mwache akiendeleze km uchangudoa ht hapa anaweza kufanya bila ya kushurutishwa. Achen ujinga kama ni kuhofia weng wasingepeleka watoto wao nje kusoma kuhofia kuwa ma.la.ya
ushauri wako mzuri sana ila umetumia matusi kuuwasilisha,mjinga ni yule anayejifanya anajua kitu na kumbe hajui ,anyways point taken
 
Ni hivi Tabrett, msilete mchezo kabisa na hiyo kitu, aisee muwe wakali kabisa.Kataeni kwa nguvu zote na huyo rafiki yake piga marufuku asionekane hapo.Huko hakuna kingine zaidi ya kujiuza katika umri huo.Watu wanalia kila siku,hata humu kuna ushahidi.Kazi kwenu.
 
Last edited by a moderator:
We jiulize, huko Oman yakuna vijana? Na kwa nini hiyo kaz ambayo haiitaji ujuzi wa shule isifanywe na waOman wenyewe? Katika kipindi hiki cha karibuni Tanzania imetajwa na UN kama njia mama ya Human Trafficking, sawa wanafamilia kuweni makini na mmoja wenu asije akawa ni mhanga wa hili janga katika siku za usoni!:confused:
 
Wanafamilia mnabidi mtoe msimamo kama wazazi....form 4 leaver...kwanini msiweke mkazo aendelee na masomo.Maana ana safari ndefu,ama hata shule hataki?

Mkuu ukiona hivyo ujue kashafeli huko shuleni na bila shaka hajiwezi kabisaaaa yaani 'bongo lala'...

Mtu anayependa elimu hawezi kukubali kwenda nje ya nchi kwa kazi ya kupaka watu wengine hina...

Pia nina wasiwasi huyu binti kachekecha akili kagundua pia familia yake haina msaada wowote kwake...
 
Back
Top Bottom