Mabinti siku hizi wanazaa zaa bila mpango

Mabinti siku hizi wanazaa zaa bila mpango

Molembe

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2012
Posts
9,933
Reaction score
11,864
Kwa kweli siku hizi sijui nini kimewapata hawa mabinti wetu, wanazaa tu bila ndoa yaani siku hizi binti kumbebea mimba mpenzi/mchumba wanaona kawaida wengi wao wakiwa wanachuo.

Ukitembea mtaani unakutana na wasichana wana mimba kana kwamba wameolewa kumbe wako kwao ukienda vyuoni huko ndiko kuna balaa, mimba zimekuwa kama fasheni. Ni nani aliewaroga wale na sijui wamekula maharage ya wapi wale matokeo wanaishia kuachwa wale na kulea watoto wenyewe wakiwa na stress.

Hivi mmeshindwa kutunza usichana wenu mpaka mtakapofunga ndoa ndo mzae yaani unakuta mtu hata hujui historia yake kwao hupajui kisa kakwambia anakupenda na uongo mwingi unabeba mimba mkishazaa mnaishia kuachwa .

Kazi inabaki kupiga picha na kuweka FB na Instargram "I am single mother" kama kwamba kuna mtu anapenda kulea mtoto mwenyewe hivi mkikituliza mpaka mkaolewa mtapungukiwa nini. Kwanini umtie mzazi wako aibu kwa kuzaa kabla ya ndoa, mnasababisha watoto wa mitaani waongezeke.
 
Dusherere tamu pili wanahisi ukimzalia mwanaume unashow love ili ashawishike kukuoa
 
Molembe

ndoa kitu gani, mtu akitaka kuwa na mtoto kwani lazma asubiri ndoa.
 
Last edited by a moderator:
ndoa kitu gani, mtu akitaka kuwa na mtoto kwani lazma asubiri ndoa.

Kuwa na mtoto ni jambo jema na lazima ujipange wewe upo chuo unasoma unabeba mimba huku ukijua huna uwezo wa kumhudumia huyo mtoto.
 
aliyekudanganya binti anashika mimba hovyo ni nani? siku iz tunapanga tu kiroho safi kuwa single moms. No stress.
Alaf unawalaumu wanawake sababu wao ndo wanabeba matumbo, vipi kuhusu hao waliowasababishia? mnakua mmekula mchele gani? au mmelogwa?
 
Acha tu wabebe ila wajue hao walio wapa kama hawatawaoa basi hakuna atae waoa ...nashangazwa na wanaume wenzangu wanao oa binti mwenye mtoto daaaaaaaah i cant believe wanajitoa ufahamu au!?
 
Molembe

Tatizo na nyie wanaume mnawapa mimba mabinti bila mpango, oeni acheni ujanjaujanja!! Hebu acheni kuwapa hizo mimba muone kama watazipata....!!
 
Last edited by a moderator:
Mambo yanabadilika sana siku hizi. Mambo ya ndoa hayaingii akilini mwa wengi.
 
Back
Top Bottom