Sasa kama wanachagua wenyewe kuwa single moms iweje baadae binti anaanza kukusumbua ww uliempa mimba mtoto akishazaliwa, anakukaba kama luba umuoe, si ajabu akahamia kwa nguvu kwako, wakati mwanzo alijifanya anataka kuwa single mom
Na single moms wengi wakishahudhulia harusi kadhaa za wenzio ofisini roho inaanza kumuuma kwa nn alizalia home ndo hapo sasa ananunua mwanaume Wa kufunga nae ndoa
Mfano hai ni mm, mke wangu alijiona ana elimu na ana kazi nzuri hivyo hahitaji mume akaamua kuzaa awe single mom, kumbe ndo amejifungia milango
Alishangaa kuona kila wiki anahudhuria harusi za wenzie waliojitunza, huku umri ukizidi kumtupa mkono hadi alipokutana na mm nikiwa hoi kimaisha lakini hakujali akasema nachotaka mm ni ndoa, ww usijali mi ntalipa gharama zote za sherehe hadi mahari ntakupa upeleke kwetu
Nilishangaa sana ndo watu wakaniambia huyo alijifanya single mom msaidie tu
Ndo nikamuoa kwa kuniwezesha kimaisha kama sharti langu..
.so hakuna kitu kama single mom ni ile hadithi ya sungura sizitaki mbichi hizi