By the way, huwa hakunaga kukosea kuoa ama kuolewa BAADA YA TUKIO HUSIKA. Palatability ya chakula ambacho mtu ameagiza mwenyewe hutegemea sana mindset yake. You will always get what you put in. Ndoa siyo tunda la kimuujiza la kuangua mtini siku hiyohiyo na kulila, bali ni mbegu ya mche kwa ajili ya kupanda, then kupandikizwa, kupaliliwa, kumwagiliwa maji na dawa, kuachanisha, kupogolea, kutengenezewa kivuli, kuhamia ndege na wanyama waharibifu, kukagua magonjwa na kudhibiti, then kuvuna tayari kwa kuliwa. Wengine wanakimbilia kutafuta tunda la kuvuna wakati ndiyo kwanza stage ni mche. Wakikosa matunda wanalalamika na kukasirika na kutishia kuvunja ndoa. Very disappointing!