Sikilizeni nyie wanawake mnaochezea ndoa zenu

Sikilizeni nyie wanawake mnaochezea ndoa zenu

The redemeer

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2025
Posts
4,778
Reaction score
8,209
Mwanamke asikudanganye mtu, nisikilize Mimi

Maisha ya kulea watoto peke yako (Single motherhood) yanakuja na changamoto nyingi sana. Hata kama kuna mtu anakuambia ni mazuri unakuwa na uhuru lakini kumbuka uhuru usio na mipaka hugeuka kuwa utumwa kwako mwenyewe.

Kuna baadhi ya wanawake walioko kwenye ndoa huwashauri wanawake wenzao kuvunja ndoa zao kwa sababu ya mambo madogo yanayozungumzika (petty disputes) huku wao wakisuluhisha tofauti zao na kushikilia ndoa zao kama lulu. Usikubali wakakuingiza mkenge huu.

Lakini pia kuna baadhi ya wanawake walioharibu ndoa zao wamekuwa vinara wa kushawishi wanawake wengine walioko kwenye ndoa wawe jeuri, wapiganie HAKI sawa ili nao ndoa zao zivunjike wafanane.

Wewe mwanamke aliyeko kwenye ndoa yake anakuambia vunja ndoa yako kwa sababu ya changamoto X, lakini yeye bado anaishikilia ndoa yake licha ya changamoto X,Y,Z.

Ni kweli kuwa single mother sio ulemavu ila sio jambo rahisi. Ingekuwa rahisi ndoa zisingekuwa na umuhimu. Usidanganyike maisha ya single mother yakupate katika mazingira yasiyoepukika lakini isiwe kwa kujitakia nakuambia utajuta. Usipojuta hadharani lakini utakuwa na majuto moyoni. Na usisahau, majuto ni mjukuu.

My dear akili za kuambiwa changanya na zako usiwe kama mbayuwayu. Usisahau kuwa adui wa mwanamke ni mwanamke na wengi wameharibu ndoa na mahusiano yao kutokana na ushauri mbovu kutoka kwa marafiki wabaya (adui).

Maisha huku nje ya ndoa sio marahisi sana na hakuna aliyesema maisha ndani ya ndoa ni mteremko tu kuna milima, mabonde na tambarare pia. Somo ni mbaya huku nje kumejaa na wateja hakuna kila mwanaume anapambana na familia yake au watoto wake wale, wasome, watibiwe. Jichanganye utajuta.

Chagua washauri wako wa ndoa na mahusiano kwa makini na hekima. Na kabla hujapokea ushauri wowote kuhusu ndoa au mahusiano yako kumbuka kuwa chochote ulicho nacho hata kama huoni thamani yake, kuna mtu anakitamani na anakitaka au anataka ukipoteze ili mfanane.
 
Chagua washauri wako wa ndoa na mahusiano kwa makini na hekima. Na kabla hujapokea ushauri wowote kuhusu ndoa au mahusiano yako kumbuka kuwa chochote ulicho nacho hata kama huoni thamani yake, kuna mtu anakitamani na anakitaka au anataka ukipoteze ili mfanane.📌📌📌📌🔨🔨🔨🔨💪🏿
 
Back
Top Bottom