Mabinti ambao hamjaingia kwenye ndoa

mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
19,763
35,205
Wanaume makini wapo..... tena wengi tuu. Kabla ya kufanya maamuzi piga goti umshirikishe Mungu, sikiliza moyo wako huku ukishirikisha ubongo wako.

Kumekua na maneno mengi ya kuwakatisha tamaa lakini za kuambiwa changanya na zako
 
Wanaume makini wapo..... tena wengi tuu. Kabla ya kufanya maamuzi piga goti umshirikishe Mungu, sikiliza moyo wako huku ukishirikisha ubongo wako.
View attachment 1658928
Kumekua na maneno mengi ya kuwakatisha tamaa lakini za kuambiwa changanya na zako
Huyu dada Shusho ana Roho wa Mungu

Wenye masikio wamesikia.

Wanaume wazuri wapo kama ilivyo kwa wanawake wazuri ambao pia wapo,wengi sana wanao faa.

Bahati mbaya vigezo ndiyo huharibu kila kitu
 
Huyu dada Shusho ana Roho wa Mungu

Wenye masikio wamesikia.

Wanaume wazuri wapo kama ilivyo kwa wanawake wazuri ambao pia wapo,wengi sana wanao faa.

Bahati mbaya vigezo ndiyo huharibu kila kitu
Sasa unategemea angekuwa bora bila kuwa na vigezo hivyo??? Nashauri tena wazidi kuvipandisha juu hadi mbinguni ili vicholechole vishindwe kuvifikia, au vikipanda vinakutana na Malaika Gabrieli angani, mpaka waokoke ndipo mengine yaendeleee.
 
Huyu dada Shusho ana Roho wa Mungu

Wenye masikio wamesikia.

Wanaume wazuri wapo kama ilivyo kwa wanawake wazuri ambao pia wapo,wengi sana wanao faa.

Bahati mbaya vigezo ndiyo huharibu kila kitu
Hakika Shusho ana roho wa Mungu
Na uhakika zaidi ni kwamba Shusho ana mume anayemkamilisha ambaye anamfanya kuwa bora kama tunavyomuona. Na huyo ndio kichwa na kiongozi wa familia yake
 
Wapo wanaume wenye mapesa mengi lakini ndoa bado zimekua ngumu. Pesa ni muhimu ili maisha yaende lakini kupata mke sahihi ni muhimu zaidi
Takwimu zinaonesha wazi kati ya mambo 8 makuu yanayosababisha kukosa furaha ndoani, michepuko, mahusiano hafifu, ugomvi & talaka --- namba moja ni uchumi duni wa wanandoa. Likelihood ya ndoa kudumu penye pesa ni kubwa sana. Yaani, kwa mfano halisi, hakuna mtu mwenye anaamini Zari & Diamond wameachana. It is as though yuko anafanya business tu huko ila wangali mtu na mzazi mwenzie.
 
Takwimu zinaonesha wazi kati ya mambo 8 makuu yanayosababisha kukosa furaha ndoani, michepuko, mahusiano hafifu, ugomvi & talaka --- namba moja ni uchumi duni wa wanandoa. Likelihood ya ndoa kudumu penye pesa ni kubwa sana. Yaani, kwa mfano halisi, hakuna mtu mwenye anaamini Zari & Diamond wameachana. It is a though yuko anafanya business tu huko ila wangali mtu na mzazi mwenzie.
Utandawazi unatupeleka kasi lakini tujue tuu kuna vitu havitabadilika..... Kwa asili na kwa imani zetu mwanamke ndio mwangalizi wa nyumba na mwanaume ndio mpangaji na mtafutaji mkuu.
Mwanamke akipata mume ana kila kitu atapumzika ila mwanaume ukipata mke mwenye kila kitu usilale, tumia nafasi hiyo kufanya mambo yakayokuwezesha kusimama kama baba na ukaweza kuisimamia familia. Diamond angekua mzembe hajishughulishi Leo hii zari angekua hata hamuongelei. Wanawake akili zetu anazijua aliyetuumba tuu hahahaaa
 
Back
Top Bottom