Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 58
Kwa muda sasa nimekuwa nafuatilia kwa makini sana juhudi za Kikwete za kutengeza mabilionea mia moja tu (100) wa kitanzania katika kipindi chake cha uongozi.
Kwa muda haikuniingia akilini kuwa ni sera gani ya kiuchumi au ni mshauri gani wa kiuchumi ambaye Kikwete anamfuata ili kufanya hili liwe kweli. Swali la nyongeza ni kuwa je ni pesa au vyanzo gani vya pesa vitatumiwa na Kikwete kutengeneza hawa mabilionea watanzania mia moja?
Taarifa ya mkaguzi wa mahesabu ya serikali kwa mwaka 2006 ilionyesha kuwa kuna matumizi zaidi ya bilioni moja ya ikulu ya Kikwete ambayo hayakuwa na ufafanuzi wowote (soma kuwa walitumia kila aina ya wizi na uongo lakini bado wakashindwa kuficha pesa bilioni moja, je ni kiasi gani walifanikiwa?), mwaka 2007 ulijaa report ya matumizi mabaya ya pesa katika miradi mibovu kama ya richmonduli, wizara ya ujenzi, wizara ya ulinzi, nk.
Baada ya report ya wizi wa BOT, nimeanza sasa kutambua maana ya maneno ya Kikwete ya kutengeneza mabilionea mia moja. Taratibu majina ya vijana mafisadi wanaokuja juu kina Lukaza na wengine yameanza kutengeneza list hii. Wakili fisadi na mtetezi wa mafisadi mengi Tanzania ndugu Mkono ameingia moja kwa moja kwenye hii list. Mzee wetu wa Richmonduli - Lowasa naye bado hajachoka na ulaji wa pesa ya bure ya serikali.
Hii ya wizi wa BOT na ushiriki wa kina Rostam Azizi na kampuni yake ya Kagoda imezidi kufunua maana ya maneno ya Kikwete. Kitendo cha mtoto wa Kikwete kuingia kwenye kampuni la kifisadi la wanasheria wa IMMA kinaelezea vizuri mwelekeo wa Kikwete na juhudi zake za kutengeneza mabilionea mia moja.
Swali linalounguza sasa hivi (burning question) ni kuhusu hao wengine ambao watakuwemo kwenye hii list ya aibu. Kwa vile Kikwete anapata 10% ya kila tukio la kifisadi linalotokea nchini (kama huamini muulize karamagi swali kuwa ni kwanini bado yeye ni waziri), basi kuna uwezekano kabisa kuwa Kikwete atakuwa ni number moja kwenye hii list. Katika siku zinazofuatia nitajaribu kutafuta mabilionea wengine ambao Kikwete anatengeneza kwa njia za wizi na kifisadi na ubadhilifu wa mali za watanzania.
Swali binafsi kwako Kikwete, wewe na hao mabilionea 99 wenzako mnategemea kuishi wapi siku ya siku ikifika?