Mabango ya kitabu cha Sheikh Ponda kwenye kuta za nyumba mitaani Dar es Salaam

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,920
30,261
MABANGO YA KITABU CHA SHEIKH PONDA KWENYE KUTA ZA NYUMBA MITAANI DAR ES SALAAM

Nakumbuka siku ya kwanza nilipokutana na Sheikh Ponda ilikuwa mwaka wa 1988 kwenye semina ya vijana Kiislam Iliyofanyika Chuo Cha Biashara Dodoma (CBE).

Sheikh Ponda na kijana mmoja kutoka Zanzibar, Sheikh Salum Abdallah walikuwa kati ya maimamu wadogo zaidi kwa umri waliokuwa wakitusalisha.
Nilikipenda kiraa cha Sheikh Ponda kuanzia siku ile.

Kuanzia siku ile pale Dodoma Sheikh Ponda akawa rafiki yangu na wala sikujua kama Sheikh Ponda atakuja kuacha alama kubwa katika historia ya Waislam wa Tanzania.

Wala haikunipitikia hata kwa mbali sana kuwa jina la Sheikh Ponda litakuwa kielelezo cha matatizo wanayokabili Waislam toka EAMWS ilipopigwa marufuku na serikali mwaka wa 1968.

Wengi katika wale tuliohudhuria mkutano ule wa Dodoma ni vijana waliokuwa wanajitahidi kubeba bendera ya Uislam Tanzania.

Baadhi wametangulia mbele ya haki - Burhani Mtengwa, Mussa Mdidi, Ilunga Hassan Kapungu, Hassan Mnjeja kwa kuwataja wachache.

Vijana hawa wengi wao walikuwa wanafunzi wa Dr. Hussein Malik wakipita na mwalimu wao katika shule za sekondari Dar es Salaam na katika misikiti wakisomesha Uislam.

Sheikh Ponda alipokuwa Segerea rumande nilikwenda kumtembelea kiasi cha mara mbili hivi nikiongozana na mmoja wa vijana wake aliyekuwa kiongozi wa vijana wa Kiislam mashuleni.

Taarifa nilizokuwa nikizipata kutoka Segerea zilikuwa zikinijaza simanzi lau kama walionipatia hizo taarifa walikuwa wakiniambia kuwa sheikh hajambo.
Nilishangaa siku nilipokwenda kumuona Segerea.

Sheikh Ponda alinitokea akiwa na tabasamu tukasalimiana vizuri na tukazungumza hili na lile.

Hivi ndivyo ilivyokuwa nilipokwenda tena kumtazama na hata tulipokutana Mahakamani Morogoro.

Muda wote mimi nikiwa na Sheikh Ponda Segerea nikitafuta dalili za mtu aliyekuwa katika fadhaa na majuto.

Sikuona.

Nilishuhudia kwa macho yangu heshima aliyokuwa akipewa na askari na wafungwa wenzake mle ndani ya jela.

Ikawa Sheikh Ponda ananitania mimi na kunichekesha kwa mambo yetu ambayo alipokuwa uraiani hutiana moto kila tukipigiana simu au tukikutana.

Niliondoka Segerea nimefarijika sana huku akinirushia maneno akinikumbusha mrembo mmoja ambaye sote tunamgombea - Bi. Bilkis.

''Najua Mmanyema unatamani wasinitoe humu ndani ili umuoe wewe Bilkis!''
Huyu Bilkis ni mjukuu wake.

Nami humrudishia nikasema, ''Alhamdulilah.''

Sheikh Ponda anazidi kucheka kwani hajui kama ile, ''Alhamdulilah,'' nashukuru kuwa mpinzani wangu kadhibitiwa rumande hatoki au ''Alhamdulilah,'' yangu nashukuru ndugu yangu yuko katika hali nzuri.

Hii Semina ya Vijana wa Kiislam inanikumbusha mbali sana enzi ya chama kimoja.

Tulimuomba kiongozi mmoja wa CCM aje atufungulie semina yetu.
Akatuuliza nia ya semina ilikuwa kitu gani na maswali mengine.

Akatukubalia.

Baadae akatuletea taarifa kuwa hatoweza kuja kufungua semina yetu.
Hatukushangaa kwa kuwa sote tukijuana na palikuwa na pazia jepesi sana baina yetu.

Tukawa tumepwelewa.

Basi tukafanya shura na kuamua kumwendea Sheikh Khamis Khalfan kumuomba aje awe Mgeni wa Heshima na kutufungulia semina yetu.
Sheikh Khamis Khalfani alikuwa mwanazuoni mkubwa Dodoma toka miaka ya 1950.

Sheikh Khamis ni mmoja wa viongozi wa TANU Dodoma pale TANU Western Province ilipofanya uchaguzi wake wa kwanza 1955.

Katika uchaguzi ule Alexander Kanyamara alichaguliwa Rais, Haruna Taratibu Makamu wa Rais, Abdu Mohamed Mwamba, Katibu na Omari Suleiman Mweka Hazina.

Miongoni mwa hawa waasisi wa TANU alikuwa Binti Maftah Karenga, Bakari Yenga na Sheikh Khamis Khalfan kama wanakamati.

Mwaka wa 1968 Sheikh Khamis Khalfan na Bilal Rehani Waikela walikuwa wajumbe wa Kamati ya Mussa Kwikima katika mgogoro maarufu wa EAMWS.

Khutba ya ufunguzi aliyotoa Sheikh Khalfan katika ufunguzi wa Semina ya Vijana ilitutia moyo vijana wote.

PICHA:
Picha ya mwisho kushoto wa tatu ni Sheikh Issa Ponda kama alivyokuwa mwaka wa 1988 miaka 34 iliyopita.

Ponda Issa Ponda aliyekuwa kijana sana wakati ule sasa ni mtu mzima.

Sheikh Hamid Jongo, Imam Mkuu wa Msikiti wa Manyema anaonekana hapo kwenye picha iliyokuwa na bango la semina ya vijana.

Picha ya juu kulia hapo yupo Sheikh Ilunga Hassan Kapungu pamoja na Mwandishi.

1662007831352.png
1662007894595.png
1662007944579.png

Shaikh Mohamed Said.

Shukran sana kwa kumbukumbu hii adhimu ya Mkutano wa vijana wa Kiislamu Dodoma
Allah Subhaanahu wa Taala akulipe kheri za dunia na akhera kwa kutujuza historia hii ambayo inatupa kumjua Shaikh Issa Ponda.

Nikuombe pia utupe walau kwa uchache kuhusu maudhui ya kitabu hicho cha Shaikh Ponda ambacho umekitaja katika Heading
 
Averos,
Angalia hapa kuna makala kama nimekieleza kitabu.
 
Daaah!

Allah akuhifadhi pamoja na Sheikh wetu Sheikh Ponda ambae hajakubali Asali ilowanishe imani yake hata siku moja

kuna siku aliwahi kuniambia hakuna mtihani mkubwa katika zama zetu kama kama mtihani wa njaa kuhamisha makazi kutoka tumboni hadi kichwani
 
@Mohamed Said
Sijaona akhui
Kama waweza nitag
Au nikija Magomeni Masjid Nuur utanifahamisha kwa urefu
''...katika kitabu hiki Sheikh Ponda ameeleza tatizo la udini linalokabili Tanzania, tatizo ambalo serikali inaliogopa kukubali kuwa lipo na waathirika ni Waislam.

Serikali inajua hatari ya dhulma lakini wanaamini tatizo hili litajiondoa lenyewe.

Hofu ya kutaka tatizo litambulike fikra hii linatisha serikali yenyewe kwani athari yake itafika mbali sana iwapo itakubalika kuwa lipo tatizo na linahitaji ufumbuzi.

Kupitia matukio tofauti na kupitia maisha yake mwenyewe Sheikh Ponda, msomaji atasoma na kuiona kwa ushahidi dhulma iloyojijenga dhidi ya Waislam nchini bila kificho toka uhuru wa Tanganyika upatikane mwaka wa 1961.

Katika kitabu hiki, ''Juhudi na Changamoto,'' Sheikh Ponda anamchukua msomaji kutoka tatizo moja hadi lingine kwa ushahidi wa nyaraka na picha.

Sheikh Ponda hakika kaifanyia nchi yetu hisani kubwa kwa kuandika kitabu hiki.''
 
Shukran sana sheikh Mohamed Said kwa ufafanuzi mzuri
Hakika ni kitabu chenye maudhui muhimu kwa msomaji
Jazakalllahu khayran
 
Hivi kipindi anapigwa risasi morogoro ulikua utawala wa upi pale ndio nilimfaham huyu maalim
 
Hawa akina sheikh ponda ukiniambia niwapigania haki nitakuelewa.
Sio akina ndugai.
 
Back
Top Bottom