Sheikh Juma Mwindadi

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,921
30,265
SHEIKH JUMA MWINDADI

Imenichukua miaka mingi kuitafuta picha ya Sheikh Juma Mwindadi.

Hatimae picha ya Sheikh Jjuma Mwindadi nimeipata kutoka kwa familia yake.

NImefahamishwa kuwa ingawa watu wamezoea kumwita ''Juma,'' yeye jina lake ni ''Jumaa Mwindadi Jumaa.''

Mara ya kwanza kukutana na jina hili ilikuwa katika Nyaraka za Sykes.
Nimemsoma Sheikh Juma Mwindadi katika nyaraka hizi zikimweleza Sheikh Juma Mwindadi kuwa alikuwa Mwafrika wa kwanza kuchaguliwa katika Dar es Salaam Municipal Council na Mwafrika wa pili alikuwa Kleist Sykes.

Ningependa msomaji wangu usome kipande hiki nilichokitoa katika kitabu cha Abdul Sykes ili uwe na uelewa mpana wa hali ya siasa katika miaka ile kuelekea kuundwa kwa TANU:

''Kueleweka kwa nini Abdulwahid alimuunga mkono Nyerere inahitajika uchambuzi kuelewa siasa za mfumo wa kikoloni katika Tanganyika.

Mwaka wa 1951 Abdulwahid na Mwapachu walipokuwa wakishughulika kuifufua TAA, walijiwa na Ivor Bayldon, Brig. Scupham na V.M. Nazerali kuombwa kuunga mkono kuundwa kwa chama cha kisiasa kitakachojumuisha Watanganyika wa rangi zote.

Hawa walikuwa wajumbe wa Baraza la Kutunga Sheria.

Bayldon alikuwa mlowezi tajiri kutoka Nyanda za Juu za Kusini na alikuwa amehamia Tanganyika kutoka Afrika ya Kusini.

Wajumbe wa Kiafrika wa Baraza la Kutunga Sheria walioliunga mkono wazo hili walikuwa Chifu Kidaha Makwaia na Liwali Yustino Mponda wa Newala.

Watu wengine mashuhuri walioshauriwa na kuombwa kuunga mkono chama hiki walikuwa: Dr Joseph Mutahangarwa, Chifu AbdIel Shangali wa Machame, Chifu Mkuu Thomas Marealle wa Marangu, Chifu Adam Sapi Mkwawa, Chifu Haruna Msabila Lugusha, Dr Wilbard Mwanjisi, Abdulkarim Karimjee, Dr Vedasto Kyaruzi, Liwali Juma Mwindadi, H.K. Viran, Stephen Mhando, Ally Sykes na Dossa Aziz.

Huu ulikuwa mchanganyiko wa Wazungu ambao tangu hapo walikuwa raia wa daraja la juu, baadhi yao kama Bayldon walikuwa walowezi; machifu kama vile Marealle, Waafrika wasomi kama Mwapachu; tabaka ya wafanyabiashara wa Kiasia kama Karimjee na watu wa mjini kama Dossa Aziz na Juma Mwindadi.

Wote hawa walikuwa viongozi waliokuwa na wafuasi katika jumuiya zao.

Katika barua Nazerali aliyomtumia Ally Sykes miaka miwili baada ya kudhihiri kuwa chama kile walichokusudia kisingeweza kuundwa, kwenye sehemu moja alikuwa na haya ya kusema: ''Haja kubwa ilikuwa kuandaa kikundi cha watu walio wakweli, waaminifu na wenye imani katika maendeleo ya watu katika nchi yetu, pamoja na fursa sawa kwa wote.''

Nikaja kukutana tena na Juma Mwindadi katika Nyaraka za Rajabu Ibrahim Kirama wakati natafiti maisha yake.

Nyaraka hizi za Rajab Ibrahim Kirama zinakaribia miaka 100.

Msome Juma Mwindadi kama nilivyomweleza katika kitabu cha Rajabu Ibrahim Kirama:

''Haukupita muda mrefu uongozi wa Al Jamiatul Islamiyyah Fi Tanganyika ukawatumia barua viongozi wa Muslim Association (Umoja wa Waislamu) Machame kuwataarifu ziara ya Sheikh Hassan bin Ameir lakini barua ilimtaja Sheikh Hassan bin Ameir peke yake.

Inaelekea palitokea mabadiliko na Mwalimu Juma Mwindadi akaongezeka katika safari ile.

Mwaka wa 1945 Sheikh Hassan bin Ameir na Mwalimu Juma Mwindadi aliyekuwa Mwalimu Mkuu wa shule ya Al Jamiatul Islamiyyah fi Tanganyika, Dar es Salaam wakaenda Machame Nkuu kwa nia ya kufanya mkutano wa pamoja na viongozi wa Machame kwa ajili ya kuusukuma mbele Uislamu Kilimanjaro.

Kwa mara ya kwanza viongozi wa Al Jamiatul Islamiyyah fi Tanganyika kutoka Dar es Salaam, Sheikh Hassan bin Ameir na Sheikh Juma Mwindadi walifanya mkutano wa pamoja, Machame Nkuu na viongozi wa Al Jamiatul Islamiyyah fi Tanganyika Machame.

Katika muhtasari wa mkutano huu Sheikh Hassan bin Ameir ametajwa kama Mwangalizi wa Shule za Kiislamu, Mwalimu Juma Mwindadi ametajwa kama Mwalimu Mkubwa wa Muslim School, Dar es Salaam na Muslim Association Machame imetajwa kama tawi la Muslim Association ya Dar es Salaam. Mzee Rajabu Ibrahim Kirama akachaguliwa kuwa President, Makamu wake Ramadhani Marua na Salim Rajabu, Katibu.

Mara baada ya kikao hiki President wa Al Jummiat Islamiyyah “A” Tanganyika Terrritory, Seleman Rajabu akapeleka barua Al Jamiatul Muslim Association, Dar es Salaam kueleza hatua zilizochukuliwa na Machame Nkuu kwa kufika kwa Mkuu wa Wilaya (DC) katika kutafuta kiwanja cha kujenga shule.

Mzee Rajabu alifahamisha kuwa hakuna walichoambulia majibu yakiwa Mkuu wa Wilaya (DC) bado anashughulikia kupeleka habari Dar es Salaam na ikiwa lazima hadi kwa Gavana.''

Nimeelezwa mengi kuhusu Juma Mwindadi In Shaa Allah tutaeleza mchango wake katika siasa za Tanganyika utafiti ukikamilika.

Picha: Sheikh Juma Mwindadi, kitabu cha Rajabu Ibrahim Kirama na picha ya juu ni Paramouny Chief Thomas Marealle na chini ni Chief Abdiel Shangali, Barua ya Salim Rajabu ya tarehe 17/3/45 kwa Chief Abdiel Shangali, Sheikh Hassan bin Ameir.

1693253010848.png
1693253063045.png
1693253161410.png

1693253192504.png

Habari gani Mheshimiwa Muhamed,

Nashauri ongea na idara ya uchapishaji ya Serikali ili vitabu vyako vyote vinunuliwe na Serikali na vipelekwa Maktaba ya Uongozi Istitute na Maktaba Kuu ya Taifa.

Maana naona vina maarifa tele juu ya Historia ya nchi za Tanganyika na Zanzibar.

Historia ambayo naona inapotea siku hadi siku.

Nawasilisha.
 
Che...
Ahsante sana kaka kwa ushauri.
 
Unaitendea haki Tanzania.

Tumepotoshwa sana kuhusu wati waliokuwa nyuma ya nia njema ya uhuru wetu.

Nakuombea kwa Yesu wangu upate ulinzi na afya tele
 
Habari gani Mheshimiwa Muhamed,

Nashauri ongea na idara ya uchapishaji ya Serikali ili vitabu vyako vyote vinunuliwe na Serikali na vipelekwa Maktaba ya Uongozi Istitute na Maktaba Kuu ya Taifa.

Maana naona vina maarifa tele juu ya Historia ya nchi za Tanganyika na Zanzibar.

Historia ambayo naona inapotea siku hadi siku.

Nawasilisha.
Sheikh Shikamoo,nakusalimia nimefurahi pia kupata historia nyingine ,mimi najiona kama mmoja wa wanafunzi wako,kuna ushauri hapo juu kweli kabisa,kukiwa na vitabu toka kwako itapendeza Sana...wewe ni hazina...
 
SHEIKH JUMA MWINDADI

Imenichukua miaka mingi kuitafuta picha ya Sheikh Juma Mwindadi.

Hatimae picha ya Sheikh Jjuma Mwindadi nimeipata kutoka kwa familia yake.

NImefahamishwa kuwa ingawa watu wamezoea kumwita ''Juma,'' yeye jina lake ni ''Jumaa Mwindadi Jumaa.''

Mara ya kwanza kukutana na jina hili ilikuwa katika Nyaraka za Sykes.
Nimemsoma Sheikh Juma Mwindadi katika nyaraka hizi zikimweleza Sheikh Juma Mwindadi kuwa alikuwa Mwafrika wa kwanza kuchaguliwa katika Dar es Salaam Municipal Council na Mwafrika wa pili alikuwa Kleist Sykes.

Ningependa msomaji wangu usome kipande hiki nilichokitoa katika kitabu cha Abdul Sykes ili uwe na uelewa mpana wa hali ya siasa katika miaka ile kuelekea kuundwa kwa TANU:

''Kueleweka kwa nini Abdulwahid alimuunga mkono Nyerere inahitajika uchambuzi kuelewa siasa za mfumo wa kikoloni katika Tanganyika.

Mwaka wa 1951 Abdulwahid na Mwapachu walipokuwa wakishughulika kuifufua TAA, walijiwa na Ivor Bayldon, Brig. Scupham na V.M. Nazerali kuombwa kuunga mkono kuundwa kwa chama cha kisiasa kitakachojumuisha Watanganyika wa rangi zote.

Hawa walikuwa wajumbe wa Baraza la Kutunga Sheria.

Bayldon alikuwa mlowezi tajiri kutoka Nyanda za Juu za Kusini na alikuwa amehamia Tanganyika kutoka Afrika ya Kusini.

Wajumbe wa Kiafrika wa Baraza la Kutunga Sheria walioliunga mkono wazo hili walikuwa Chifu Kidaha Makwaia na Liwali Yustino Mponda wa Newala.

Watu wengine mashuhuri walioshauriwa na kuombwa kuunga mkono chama hiki walikuwa: Dr Joseph Mutahangarwa, Chifu AbdIel Shangali wa Machame, Chifu Mkuu Thomas Marealle wa Marangu, Chifu Adam Sapi Mkwawa, Chifu Haruna Msabila Lugusha, Dr Wilbard Mwanjisi, Abdulkarim Karimjee, Dr Vedasto Kyaruzi, Liwali Juma Mwindadi, H.K. Viran, Stephen Mhando, Ally Sykes na Dossa Aziz.

Huu ulikuwa mchanganyiko wa Wazungu ambao tangu hapo walikuwa raia wa daraja la juu, baadhi yao kama Bayldon walikuwa walowezi; machifu kama vile Marealle, Waafrika wasomi kama Mwapachu; tabaka ya wafanyabiashara wa Kiasia kama Karimjee na watu wa mjini kama Dossa Aziz na Juma Mwindadi.

Wote hawa walikuwa viongozi waliokuwa na wafuasi katika jumuiya zao.

Katika barua Nazerali aliyomtumia Ally Sykes miaka miwili baada ya kudhihiri kuwa chama kile walichokusudia kisingeweza kuundwa, kwenye sehemu moja alikuwa na haya ya kusema: ''Haja kubwa ilikuwa kuandaa kikundi cha watu walio wakweli, waaminifu na wenye imani katika maendeleo ya watu katika nchi yetu, pamoja na fursa sawa kwa wote.''

Nikaja kukutana tena na Juma Mwindadi katika Nyaraka za Rajabu Ibrahim Kirama wakati natafiti maisha yake.

Nyaraka hizi za Rajab Ibrahim Kirama zinakaribia miaka 100.

Msome Juma Mwindadi kama nilivyomweleza katika kitabu cha Rajabu Ibrahim Kirama:

''Haukupita muda mrefu uongozi wa Al Jamiatul Islamiyyah Fi Tanganyika ukawatumia barua viongozi wa Muslim Association (Umoja wa Waislamu) Machame kuwataarifu ziara ya Sheikh Hassan bin Ameir lakini barua ilimtaja Sheikh Hassan bin Ameir peke yake.

Inaelekea palitokea mabadiliko na Mwalimu Juma Mwindadi akaongezeka katika safari ile.

Mwaka wa 1945 Sheikh Hassan bin Ameir na Mwalimu Juma Mwindadi aliyekuwa Mwalimu Mkuu wa shule ya Al Jamiatul Islamiyyah fi Tanganyika, Dar es Salaam wakaenda Machame Nkuu kwa nia ya kufanya mkutano wa pamoja na viongozi wa Machame kwa ajili ya kuusukuma mbele Uislamu Kilimanjaro.

Kwa mara ya kwanza viongozi wa Al Jamiatul Islamiyyah fi Tanganyika kutoka Dar es Salaam, Sheikh Hassan bin Ameir na Sheikh Juma Mwindadi walifanya mkutano wa pamoja, Machame Nkuu na viongozi wa Al Jamiatul Islamiyyah fi Tanganyika Machame.

Katika muhtasari wa mkutano huu Sheikh Hassan bin Ameir ametajwa kama Mwangalizi wa Shule za Kiislamu, Mwalimu Juma Mwindadi ametajwa kama Mwalimu Mkubwa wa Muslim School, Dar es Salaam na Muslim Association Machame imetajwa kama tawi la Muslim Association ya Dar es Salaam. Mzee Rajabu Ibrahim Kirama akachaguliwa kuwa President, Makamu wake Ramadhani Marua na Salim Rajabu, Katibu.

Mara baada ya kikao hiki President wa Al Jummiat Islamiyyah “A” Tanganyika Terrritory, Seleman Rajabu akapeleka barua Al Jamiatul Muslim Association, Dar es Salaam kueleza hatua zilizochukuliwa na Machame Nkuu kwa kufika kwa Mkuu wa Wilaya (DC) katika kutafuta kiwanja cha kujenga shule.

Mzee Rajabu alifahamisha kuwa hakuna walichoambulia majibu yakiwa Mkuu wa Wilaya (DC) bado anashughulikia kupeleka habari Dar es Salaam na ikiwa lazima hadi kwa Gavana.''

Nimeelezwa mengi kuhusu Juma Mwindadi In Shaa Allah tutaeleza mchango wake katika siasa za Tanganyika utafiti ukikamilika.

Picha: Sheikh Juma Mwindadi, kitabu cha Rajabu Ibrahim Kirama na picha ya juu ni Paramouny Chief Thomas Marealle na chini ni Chief Abdiel Shangali, Barua ya Salim Rajabu ya tarehe 17/3/45 kwa Chief Abdiel Shangali, Sheikh Hassan bin Ameir.

Upendo ulioje. Mzee Kirama haoni shida kutaka Chief Shangali awepo kwenye mkutano wakutangaza dini ya Islam Kilimanjaro. Tuna mengi ya kujifunza sisi tuliojo leo toka kwa hawa wazee wetu. I am so proud of Mzee Kirama.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom