Maazimio ya Wanakagera(KYL) kuelekea Kagera mpya

Maazimio ya Wanakagera(KYL) kuelekea Kagera mpya

Kajansi hata mie natokea maeneo ya hapo Bkb V na nikupongeze ulivyoweka initiatives kama hizo.sasa mfano tukidentify kitu ambacho itabidi tukifanye,zaidi navyoona tutaishia kuelewana sisi wa hapahapa jamvini na wakati pale mkoani wapo vijana kibao hawajuhi hili wala lile tutawapataje na kuwafikiaje hawa?ndo maana mie nilionelea kamati iundwe ifike maeneo watu wasaidiwe na nyinyi kama ww ndo mnakuwa case study eneo husika ama vip?
i.e tujumuishe mass isiwe mtu mmoja mmoja ili iwe participatory zaidi

Nimekupata mkuu nadhani inasound practical! Lets move on.
 
Haya tuje hapa tutoe maoni/maazimio yetu juu ya nini tunafanya,tufanyeje,tuanzie wapi n.k ili baada ya hili zoezi kaka yetu Omutwale atuongoze kuelekea kwenye majukumu na utekelezaji

Tunaomba tutumie siku 3 kwanzia leo hadi J2 ili hatua inayofuata ianze,njooni nyote hapa mwambie na yule jirani ilimradi awe mwanakagera na aliye tayari kwa shughuri hii

Kwa mara nyingine tena karibuni sana ..Mnyegere ba tata na ba mawe!!!!

Ushauri!
Wazo ni zuri sana lakini kumekuwepo vikundi au kamati kama hizo nyingi sana zilizoko dar na mara nyingi zimekuwa zikifika Bukoba hasa katika wakati wa sikuu ya xmas na kujadili mambo sawa na unayodai. Kifo cha kamati hizo au hivyo vikundi upotea mara moja baada ya kujiingiza katika masuala ya kisiasa.Wengi wa waanzilishi wa hizi kamati au vikundi malengo yao huwa ni siasa na hili ndilo linalokwamisha maendeleo ya mkoa huu.

Kwa kazi yangu nimekuwa nikishiriki sana katika mikutano ya vikundi kama hivi alkini mwisho vinaishia kwenye masuala ya kujuana,starehe za pombe na michakato ya kisiasa,nani anafaa wap na kwa nini ,wengine kudiriki hata kutangaza nia wakiwa katika mikutno kama hiyo.

kama hiyo kamati au kikundi hakitakuwa katika muktadha huo basi mimi najitolea kusaidia kwa njia moja au nyingine nikiwa kama mwandishi wa habari kwa kuwa hivi sasa nina-host kipindi cha tv kinachoitwa 'barua kutoka kanda ya ziwa' katika channel ten kila jumpili saa 12:30 na kwa kuwa mtalenga katika mambo ya maendeleo (siyo siasa) nitasaidia sana.

Byabato
0282220183
 
Last edited by a moderator:
Kuwapa angalizo wanasiasa na watu wenye nafasi kutoka mkoa wetu kumshauri (kumuonya) rais na wanasiasa wengine wasichochee migogoro na majirani zetu (Rwanda, Uganda, Burundi nk). Kwa maana vijana wetu wanaweza kupata faida ya ziada endapo tutakuwa na mahusiano mazuri na majirani kama ifuatavyo:
1. walimu wenye uwezo kutoka nchi jirani kusaidiana na walimu wetu hata wale wa kata.
2. fursa za kibiashara kama kuuza kahawa maana ina bei nzuri kwa majirani zaidi ya hapa
3. exposure endapo vijana wetu wataenda huko na kuelewa ni jinsi gani wenzetu wanafanya
Mengine mengi tu mnayajua pia
 
Rweye tuanze hivi napendekeza wapatikane watu angalau wawili wawili waliopo kila wilaya za mkoa wa Kagera waliomo humu jf tugharamie kikao chao hapo Bukoba mjini na michango ya gharama za kikao chao ipie hapa Jf. Tuandae Agenda za kikao na wao watuletee feedback ya wayforwad!

Nawakilisha.
 
Naamini tunaweza na tuko kimkakati sasa,vyema kabisa naunga mkono. naombeni tena tuwe beyond siasa,madhehebu yetu na maeneo tunayotoka
Kati ya vitu tulivyovipendekeza kwenye kamati ya wataalamu tumempata mwandishi ndugu yetu M.Byabato karibu twende wote.
Sasa navyojua mpaka sasa walioko hapo Bkb ni wengi ila Omutwale,Byabato,Kanyansi n.k tayari mko hapo jipangeni na wengine toka wilayani mfanye kikao ili ajenda ziwepo tusonge mbele.
 
Ushauri alioutoa ndg Byabato ni wa kuzingatiwa sana.
 
Kwa walioko hapo Bkb basi mpange lini mkutane sie hapa tutawapeni ajenda kama alivyoshauri Kajansi alfu mtwambie na gharama za maandalizi ya kikao ili tutume michango yetu pia.

NB: Mjitahidi kufanya haraka kidogo tunawasubiri ninyi.
 
pambaneni na wahamiaji haramu wa kitusi kwanza, maana watawaharibia tu, kuna mtu mmoja ametoa wazo la kufanya sensitization kwa wananchi , hili liende sawia na mbinu za kuwafichua wahamiaji haramu.
 
Waitu bwakya buta,nimbalamya nywena amoi! ...ndugu zetu mjadala wetu wiki jana ulifikia mahali pazuri na kumbukumbu zinaonesha tuliwaomba hapo mkoani muandae kikao ili sie huku tufanye kuwapa ajenda na kuwawezesha katika gharama za kikao hicho,sasa tuanze kwa kuulizana mmefikia wapi??

Walioko hapo mkoani tafadhari.
 
Inakuwaje, mbona sioni mrejesho?
 
Walio mkoani mbona kimya jamani? mimi nasubiri kuchangia chochote inshallah
 
Mwenyikiti awe Prof Tibaijuka, Makamu wa Mwenyekiti awe Kagasheki, na Katibu awe Karamagi, na ili maendeleo yaje kwa Haraka Rei ijengwe upya tunataka Bujkoba iwe kama Dubai kituo cha Biashara Uganda na Rwanda watakuwa wanakuja kununua vitu, na Hoteli Nyingi zitajengwa na kuwa na wateja kutokana na biashara na nchi jirani, na Meli za Kasi ziwepo pia.
 
Kuwapa angalizo wanasiasa na watu wenye nafasi kutoka mkoa wetu kumshauri (kumuonya) rais na wanasiasa wengine wasichochee migogoro na majirani zetu (Rwanda, Uganda, Burundi nk). Kwa maana vijana wetu wanaweza kupata faida ya ziada endapo tutakuwa na mahusiano mazuri na majirani kama ifuatavyo:
1. walimu wenye uwezo kutoka nchi jirani kusaidiana na walimu wetu hata wale wa kata.
2. fursa za kibiashara kama kuuza kahawa maana ina bei nzuri kwa majirani zaidi ya hapa
3. exposure endapo vijana wetu wataenda huko na kuelewa ni jinsi gani wenzetu wanafanya
Mengine mengi tu mnayajua pia

Nakubaliana nawe,mkoa wetu unapakana na nchi zote za EAC. Kadri ushirikiano baina ya nchi hizi utazidi kuimarika,ndivyo fursa nyingi ktk sekta za.elimu,uchumi na biashara zitafunguka ktk mkoa wetu.

Matatizo ya wahamiaji haramu hayatenganishwi na utawala dhaifu na rushwa! Wana Kagera tuna jukumu la kuwaelimisha wananchi wenzetu walioko vijijini wachague viongozi makini badala ya watoa rushwa! Wanapewa pombe na tshirts baadaye wanalalamika eti serikali ya kijiji,diwani na mbunge hawasikilizi shida zinazo wakabili!!
 
Wakuu nawaomba tusikwepe main isues hasa swala la kahawa!! Kama tunataka kukomboa mkoa wetu tujitoe kwenye utumwa wa kuibiwa na kupangiwa bei za kahawa hili hali ni Mali yetu!!
 
Wakuu msiangaike na mtu kama Karamagi, muulize kwa mara ya mwisho alienda lini home??
The man is not even concerned!!
Ma Tibaijuka na Ta Kagasheki sawa!!
 
Tutafute Namba ya kuondoa viongozi mafisadi na wezi kwenye vyama vya ushirika kuanzia vijiji hadi KCU!!! Hicho ni kikwazo muhimu cha maendeleo!!
 
Tutafute Namba ya kuondoa viongozi mafisadi na wezi kwenye vyama vya ushirika kuanzia vijiji hadi KCU!!! Hicho ni kikwazo muhimu cha maendeleo!!

Mkuu tunataka watu wa hapo mjini mje hapa tuwaone tuwachangie gharam ili haya mambo tuanze kuyaongea kwenye vikao siyo tunaendelea kuonge hapa huku makubaliano hamfanyi, ...ugumu huko wapi mbona hamsemi jamani?
 
Walio mkoani mbona kimya jamani? mimi nasubiri kuchangia chochote inshallah

Mkuu hata mie binafsi sielewi ndugu zetu wa hapo mjini mpaka sasa kusema kweli ndo wanatukwamisha make tayari tumejitoa kuwaghalamia gharama za vikao lakini haonekani hata mmoja hapa tena
Juzi M.Byabato kaja hapa akasema kusaidia na yeye yuko hapo mjini lakini simuoni tena naye ...lakini subiri kwanza ikishindikana kabisa tuna plan B ya hili jambo.
 
Wakuu nawaomba tusikwepe main isues hasa swala la kahawa!! Kama tunataka kukomboa mkoa wetu tujitoe kwenye utumwa wa kuibiwa na kupangiwa bei za kahawa hili hali ni Mali yetu!!

mambo ni mengi hakika mkoa wetu umekuwa marginalised kupita kiasi unaweza ukajiuliza inakuwaje mkoa wenye mapori,tambalale,udongo wa maana,mito na mvua za kutosha haujapewa mradi wowote wa scheme za umwagiliaji ilohari tayari wanaona njaa inavyokuwa tatizo kufuatia nigomba kuharibika???
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom