Maaskofu waipinga CHADEMA...

Maaskofu waipinga CHADEMA...

Alitakiwa kwenda mbali zaidi ya hapo kama ameamua kuacha altare na kujiingiza kwenye siasa.
Alitakiwa avitaje vikundi kwa majina, vilianza lini, na vinayemtumikia ni nani!.

Ni ukosefu wa umakini kulaumu vikundi vya ulinzi huku akiacha vacuum ya ulinzi katika vyama, wakati anajua wazi yanayotendeka na walinzi rasmi-Polisi.
Huyu alitakiwa aombwe aongelee suala la Mwangosi kwanza, ndipo athubutu kulaani vikundi vya ulinzi.
Hapa ndiyo utajua mipaka ya kazi hizi inamaanisha nini!

Mkuu njaa haina dini huyu ni njaa tu!!!! Mwangosi aliuwawa kikatili na polisi huyu askofu alikuwa wapi!!! ..njaa noma...
 
Mhasham Askofu Kanyunyu,
Ulisoma kitabu gani katika biblia yako? Mwache Mh. Malasusa aseme, yeye ndiye anakula hilo fingu la kumi la Lowasa. Wewee kama unataka akija Dodoma aingie kanisani kwako tuambie tu. Usishabikie mambo haya ya siasa yatakutoa nje. Fundisha biblia yako, watakuelewa tu wala hakutakuwa na vurugu. Ukihubiri siasa watasema unapiga kelele, hubiri biblia tu mzee tutakusikia.
 
...

....Kama hamjuwi Mwangosi...Huyu askofu nawasiawasi na sadaka......
 
comments za hii thread zinadhihirisha wazi kuwa chadema sio chama cha kidini.
Ingekuwa arusha hili kanisa lake lingekosa sadaka wikiendi hii mpaka askofu aachane na kauli za kimagamba


gazeti la CDM TANZANIA DAIMA linathibitisha CDM ni chama cha kidini
 
Nashukuru huyo askofu amesema hayo maana ukimiya wao ungehusishwa na CDM kuwa chama cha kidini.........yote ya yote CDM wanatakiwa kutoa maelezo zaidi na ufafanuzi makini juu ya hili suala maana naona maadui wanatafuta pa kushikia.


Na CCM je, hawatakiwi kutoa maelezo???
 
Askofu ametoa ushauri mzuri sana kwa chama kinachokua but yasivyo na haya yanamtukana.
 
Hivi kuna tofauti kati ya Red Brigade na lile kundi hatari la mumiyani?
 
KKKT sasa hivi si wanaelemewa na uzito wa EL..El si ndio mfadhili na mfilisi wa miradi ya KKKT.
 
Hivi wewe mleta mada unafahamu tofauti kati ya askofu vs maaskofu?mods tafadhali msaidieni kuibadilisha heading.

Kusema maaskofu wakati habari ni ya askofu ni upotoshaji.
 
Leo ndo hao maaskofu wamezinduka?! Napata mashaka sana na jinsi walivyogutuka. Wanalamikia kikosi kinachoboreshwa wakati vilivyokomaa hawavizungumzii? Makubwa!!!

hana lolote huyo. Waumini wake wamesha mpuuza zamani na hapo alipo anakaa kimkandamkanda tu. hao si ndio walisema dhaifu ni CHAGUO LA MUNGU? Toka lini MUNGU kachagua kilicho dhaifu? SISI NA CHADEMA CHADEMA NA SISI, NA MUNGU YULE TUMJUAE YU PAMOJA NASI.
 
Nyie maaskofu acheni unafiki.
Mbona hamjaikemea CCM KWAkuanzisha Kundi lakigaidi???
Mbona sikuwasikia mkilaani matumizi ya mabomu na bunduki dhidi ya cdm?
Nyingi makofu ni waganga njaa na mbewa wala kondoo.
Ni wanafiki wakubwa muishio kwa kujikweza huku mkiwatafuna kondoo WA bwana.
Dini imewashinda, mmejaza dhambi za uznzi uongo na wizi mpaka madhabahuni, kwa akili zenu za dhambi mnajiingiza kichwa kichwa kwenye siasa kwa kushabikia mafisadi.
Mshindwe na kulegea kwa uongo na uzandiki wenu kwa jina la Yesu.
 
Umesema maaskofu afu habari inasema askofu ok.soma habari za mtu aliyepigwa na majambazi ila akapita kuhani bila kumsaidia akaja msamaria kumwokoa,tutaikomboa hi nchi hata kama makuhani watatusaliti
 
Back
Top Bottom