Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,602
- 22,707
Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Steven Kimondo, amesema haiwezekani taifa likapata amani ya kudumu ikiwa haki za kikatiba za wananchi na vyama vya upinzani zinaendelea kukandamizwa. Amesema viongozi wa serikali na vyombo vya dola wanapaswa kutambua kuwa amani ya kweli hujengwa kwa kuheshimu sheria na haki za raia.
Akizungumza jijini Mbeya, Kimondo alikosoa marufuku ya mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, akidai hatua hiyo inalenga kudhoofisha shughuli za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Aidha, alisema hoja ya "tishio la kiusalama" inayotolewa kuhalalisha zuio hilo haina msingi wa kisheria, akieleza kuwa mikusanyiko mingine ya kijamii na michezo inaendelea kufanyika na kulindwa na Jeshi la Polisi bila kuzuiwa.