Maaskofu waipinga CHADEMA...

Maaskofu waipinga CHADEMA...

askofu kkkt atahadharisha uanzishwaji vikundi vya ulinzi

askofu wa kanisa la kiinjili la kilutheri tanzania (kkkt) dayosisi ya dodoma, amon kinyunyu, amesema kitendo cha viongozi wa vyama vya siasa ya kuamua kujianzishia vikundi vya ulinzi wa kujilinda kwenye vyama vyao, ni ishara tosha ya kuhatarisha amani ya taifa.

Askofu kinyunyu amesema viongozi wa siasa wanaoanzisha vikundi vya namna hiyo ni kuashiria jinsi gani walivyokosa heshima kwa mungu na kwa mamlaka ya serikali ambayo ina ulinzi na usalama unaolinda nchi kwa ujumla.

Alitoa kauli hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa miradi ya mifumo ya miundombinu ya watoto ikiwamo ya maji, madarasa na vyoo vya kisasa iliyodhaminiwa na shirika la compassion international tanzania kwa kushirikiana na washirika wenza kutoka kwenye makanisa ya huduma ya mtoto iliyofanyika katika viwanja vya kanisa la tag miyuji mjini hapa.

Askofu kinyunyu alisema kitendo cha vyama hivyo kuanzisha vikundi vya kujilinda, ni ishara ya kuleta machafuko ya amani ya nchi.

Pia alisema kitendo hicho kitawafanya vijana waliopo katika vyama hivyo kuendelea kuchukiana badala ya kupendana.

Alisema viongozi wa kisiasa hawana budi kutambua kuwa kwa kuanzisha vikundi hivyo ni kuzidi kujenga uhasama mkubwa utakaoiumiza jamii isiyohusika wakiwamo watoto, wanawake, wazee na walemavu.

“hapa wanatakiwa kujua kuwa kitendo hicho ni ishara tosha inayoashiria kuanzisha vita ambayo washirika wakubwa ni vijana tunaowategemea kushika madaraka mbalimbali ya kiserikali na ya kisiasa,” alisema.

Askofu kinyunyu amewataka viongozi wa vyama vya siasa kuheshimu amani iliyopo iliyobarikiwa na mungu tangu kuumbwa kwa ulimwengu.

Kwa upande wake, mkurugenzi wa compassion intenrational tanzania (cit) hapa nchini, mchungaji joseph mayala, alisema kitendo hicho ni sasa na uwekezaji kwa vijana wawe na roho ya ukatili badala ya upendo na amani.


source: home

nb:

..askofu mkuu wa kkkt malasusa naye ametoa kauli inayoelekea kuwananga cdm.

..soma hapa chini:home
baba kemea kabisa hili pepo la green guard
 
Maaskofu wanakurupukaga na matamko bila utafiti,baadae wanashindwa kutengua kwa waumini,
hawa ndio waliosema Kikwete chaguo la Mungu lakini leo hii wanajuta kwa sababu walisukumwa na
msisimko badala ya ukweli halisi'
 
Maaskofu wanaoheshimika ni
1 catholic
2 Luther
3 Anglican.....
Hao wengine ni wa kimarekani!
Mtu ana elimu ya 4m4 nae anajiita Askofu

acha ujinga wewe kasome maamdiko kama Kuna cha degree katika kipawa cha Mungu,biblia haitaji sifa ya degree katika uaskofu labda biblia ya chadema
 
kazi nzuri viongozi wetu wa kiroho endeleeni kuwakumbusha na kuwathadhalisha hivyo hivyo nina amini na wao ndani yao wana hofu ya mungu, kwa kuwakumbusha na kuwakataza mabaya wataona haya kwa watu wanaowaongoza, hivi hebu tutafakari watanzania tukichukiana wao kama viongozi wanapata faida gani? maana moja ya kazi ya kiongozi ni kuhakikisha watu wanakuwa umoja na upendo.
 
Hicho kikundi kipo.kwenye katiba ya CHADEMA. Viongozi wa dini wafanye tafiti badala ya kupotosha waumini wao

Ben umefanyika upotoshaji mkubwa sana kwenye hili kiasi watu wamesimamia kucha utadhani ni jambo jipya!ieleweke Red brigade ilikuwepo na hoja hapa ni kuifanyia marekebisho tu na si kuianzisha kama kitu kipya.yeyote anaetaka kusimama jukwaani kulaani red brigade aanze na Green Guard pia.Kwa nini tunaishi kwa double standards kiasi hicho!!!!
 
Ben umefanyika upotoshaji mkubwa sana kwenye hili kiasi watu wamesimamia kucha utadhani ni jambo jipya!ieleweke Red brigade ilikuwepo na hoja hapa ni kuifanyia marekebisho tu na si kuianzisha kama kitu kipya.yeyote anaetaka kusimama jukwaani kulaani red brigade aanze na Green Guard pia.Kwa nini tunaishi kwa double standards kiasi hicho!!!!

kweli ilikuwepo ila sasa inaboreshwa kwa kupewa mafunzo ya kivita kumiliki slaa,kuteka watu na kuwa tayari kama kundi la waasi ili chadema ikishindwa 2015 waanzishe vita,
 
Maaskofu wanakurupukaga na matamko bila utafiti,baadae wanashindwa kutengua kwa waumini,
hawa ndio waliosema Kikwete chaguo la Mungu lakini leo hii wanajuta kwa sababu walisukumwa na
msisimko badala ya ukweli halisi'

nani aliyejuta au wewe ndiyo umejuta kwa sababu mzee wako alikosa?
 
teh teh wananikumbusha yule mfuga nyoka wa kijijini kwetu sikimbi na yule aliyetaka kuanza kufuga nae bidhaa hii hadimu du wakaanza ooh sheria za kijiji haziruhusu kufuga nyoka nyumbani mara oohh sasa yule mfugaji mpya pamoja na majirani zake mbona yule mfugaji wa zamani anlifu na anaendelea kufuga nyoka? au sheria hii imeanza tuu mara baada ya ya mfugaji mpya kujitokeza? amini amini nawaambia si mwenyekiti wala uyeyote aliyeweza kujibu mikono nyuma kikao cha dharura kikaishia hapo teh teh Green guard= to red guard so what is the problem
 
Mbona hapo CCT Dodoma wamejenga Ukuta kuzunguka na wakaweka Walinzi? Huyu Jamaa vipi tena?

Kaka Askofu, VUA Gauni na uvae GAMBA. Mbona hajaona vyama vingine? Tangu mauwaji yameanza alishasema kitu?

Ndiyo maana nawalaani sana hawa wala vya bure, *&#^$@@ zao wezi wakubwa, waongo wakubwa na wanafiki wakubwa.

AGAIN: (Simwiti wala Baba Askofu) Kaka Askofu, Vua gauni na uvae Gamba.

news.2012.12.001.01.jpg
tortoise_shell_hide_2.jpg
 
...haya maaskofu ya KKKT nilishawahi sana kuandika humu na kuhoji kuhusu unafiki wao.....kwa kujiingiza kwenye masuala ya siasa za maji taka za nchi hii.....ni haya haya maaskofu ya KKKT yaliwahi kubariki kikombe cha babu wa loliondo.....kilichopelekea maelfu ya wagonjwa kupoteza maisha kwa kuacha dawa zao za hospitali na kukimbilia kikombe cha babu wa loliondo yalichobariki......yaani siku hizi TZ imefika mahali hata unashindwa kutofautisha dini na siasa.....maana kila mtu nchi hii amekua mpiga siasa......ndio maana hata wana siasa feki wanakimbilia makanisani siku hizi kutafta sympathy.....maana makanisa yamekua vijiwe vya wanasiasa .....na kanisa la KKKT ndio linaongoza.......
 
TATIZO NI MODERATORs wetu

wanaona Kichwa Cha habari kimejaa minyoo wanakiacha, wangekibadili au kukirekebisha..!
 
Hivi kuna tofauti kati ya Red Brigade na lile kundi hatari la mumiyani?

Tofauti ni kuwa kundi hatari la MUMIYANI(GREEN GUARDS) kazi yao ni kupiga watu, kung'oa kucha watu, kuua watu, kupora mali za watu. RB kazi Tao kuwa ni kulinda Viongozi wao na kuweka usalama kwenye Mikutano yetu
 
Mbona hapo CCT Dodoma wamejenga Ukuta kuzunguka na wakaweka Walinzi? Huyu Jamaa vipi tena?

Kaka Askofu, VUA Gauni na uvae GAMBA. Mbona hajaona vyama vingine? Tangu mauwaji yameanza alishasema kitu?

Ndiyo maana nawalaani sana hawa wala vya bure, *&#^$@@ zao wezi wakubwa, waongo wakubwa na wanafiki wakubwa.

AGAIN: (Simwiti wala Baba Askofu) Kaka Askofu, Vua gauni na uvae Gamba.

news.2012.12.001.01.jpg
tortoise_shell_hide_2.jpg

Ndugu umemdhalilisha sana kiongozi wa kiroho.
 
Alitakiwa kwenda mbali zaidi ya hapo kama ameamua kuacha altare na kujiingiza kwenye siasa.
Alitakiwa avitaje vikundi kwa majina, vilianza lini, na vinayemtumikia ni nani!.

Ni ukosefu wa umakini kulaumu vikundi vya ulinzi huku akiacha vacuum ya ulinzi katika vyama, wakati anajua wazi yanayotendeka na walinzi rasmi-Polisi.
Huyu alitakiwa aombwe aongelee suala la Mwangosi kwanza, ndipo athubutu kulaani vikundi vya ulinzi.
Hapa ndiyo utajua mipaka ya kazi hizi inamaanisha nini!

Baba Kinyunyi,

Sikudhani kama askofu wa dhehebu kubwa kama KKKT anaweza kutoa mawazo butu kama haya. Baba askofu tunakuomba usiwe kengeza, tazama hali ya nchi kwa macho yalionyoofu. Ilikuwepo Green Guard mbona hukutoa onyo? Ikaanzishwa Blue Guard nayo hukuisikia, Sasa kuna Red brigrade na wewe umeibuka na tamko lako.

Hivi kuna wakati watumishi wa Mungu nao huongea kisiasa?
 
Ntafurahi zaidi kama atakuja kuusoma huu ujumbe. Ndiyo hawa kutwa nzima wanaota kuja kupokea mahela ya Viongozi wa Vyama vya SIASA ambao wote tunajua wana hela za wizi, ila hawa wavaa Magauni wanawapokea kwa furaha na kuwakenulia meno na huku wakipokea fedha zao kwa furaha kabisa.

church.jpg
images

Ndugu umemdhalilisha sana kiongozi wa kiroho.
 
Askofu KKKT atahadharisha uanzishwaji vikundi vya ulinzi

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Dodoma, Amon Kinyunyu, amesema kitendo cha viongozi wa vyama vya siasa ya kuamua kujianzishia vikundi vya ulinzi wa kujilinda kwenye vyama vyao, ni ishara tosha ya kuhatarisha amani ya Taifa.

Askofu Kinyunyu amesema viongozi wa siasa wanaoanzisha vikundi vya namna hiyo ni kuashiria jinsi gani walivyokosa heshima kwa Mungu na kwa mamlaka ya serikali ambayo ina ulinzi na usalama unaolinda nchi kwa ujumla.

Alitoa kauli hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa miradi ya mifumo ya miundombinu ya watoto ikiwamo ya maji, madarasa na vyoo vya kisasa iliyodhaminiwa na shirika la Compassion International Tanzania kwa kushirikiana na washirika wenza kutoka kwenye Makanisa ya Huduma ya Mtoto iliyofanyika katika viwanja vya Kanisa la Tag Miyuji mjini hapa.

Askofu Kinyunyu alisema kitendo cha vyama hivyo kuanzisha vikundi vya kujilinda, ni ishara ya kuleta machafuko ya amani ya nchi.

Pia alisema kitendo hicho kitawafanya vijana waliopo katika vyama hivyo kuendelea kuchukiana badala ya kupendana.

Alisema viongozi wa kisiasa hawana budi kutambua kuwa kwa kuanzisha vikundi hivyo ni kuzidi kujenga uhasama mkubwa utakaoiumiza jamii isiyohusika wakiwamo watoto, wanawake, wazee na walemavu.

"Hapa wanatakiwa kujua kuwa kitendo hicho ni ishara tosha inayoashiria kuanzisha vita ambayo washirika wakubwa ni vijana tunaowategemea kushika madaraka mbalimbali ya kiserikali na ya kisiasa," alisema.

Askofu Kinyunyu amewataka viongozi wa vyama vya siasa kuheshimu amani iliyopo iliyobarikiwa na Mungu tangu kuumbwa kwa ulimwengu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Compassion Intenrational Tanzania (CIT) hapa nchini, Mchungaji Joseph Mayala, alisema kitendo hicho ni sasa na uwekezaji kwa vijana wawe na roho ya ukatili badala ya upendo na amani.


Source: Home

NB:

..Askofu Mkuu wa KKKT Malasusa naye ametoa kauli inayoelekea kuwananga CDM.

..soma hapa chini:Home

-ukiona Askofu yeyote anayeongelea hili la vikundi vya ulinzi kwenye vyama vya siasa kwa kuegemea upande mmoja either CDM,CCM -au CUF..hana maadili ya UASKOFU .MWOGOPENI,MKIMBIENI,HAFAI KUONGOZA WAUMINI.

MY TAKE.
Askofu mwenye hekima ,busara na mtauwa lazima aangalie mirengo yote ccm,cdm cuf n.k,hawa wote wana vikundi na ccm ndo muasisi.
 
kwa ushauri tuu..
wafuasi wa CHADEMA mngechagua maneno ya kuwaongelea vingozi wa DINI(HUSUSANA MAASKOFU)..
mkianza kejeli mtakuwa mnaonyesha ''THE REAL YOU" kwani ni kwa muda mrefu sana hawa viongozi wa dini wamekuwa wapiga debe wenu wakubwa na mlikuwa mnawashangilia humu kama manabii.
vipi,leo manabii wamegeuka maharamia??????
 
Back
Top Bottom