Mimi naona tamko la Askofu ni sawa kabisa, na hakuna mahali anakoishutumu CDM. Ujumbe hapa ni uwa vikundi hivi havitajenga amani. Na CCM wakiwa waasisi, ambao wameamua kuvitumia sambamba na polisi kudhuru wananchi wasio na hatia, pale wanapohisi kuwa wamevutiwa na hoja za vyama vya upinzani ndio walengwa namba moja katika hili. Ingekuwa ccm hawatumii Green gurds kuuwa, kuteka, kumwagia tidikai, kuiba kura, kupiga n.k kungekuwa na haja gani ya kuwa na Red brigade? Ingekuwa polisi wanatoa ulinzi na kuhakikisha haki inapatikana kwa wote, kungekuwa wapi na haja ya brigadia hizi?
Saanane usishangae, MWEMA (IGP) Aliwaambia maaskofu na wachungaji waanzishe vikundi vya ulinzi kwenye mihadhara na ibada zao ili kujilinda na wa magaidi. Sembuse CDM yenye malengo mahususi kuchukua madaraka ya nchi? Hii ni kujisahau tu