Maandamano yaendelea kushika kazi Afrika Kusini kufuatia kukamatwa kwa Jacob Zuma

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,558
1626068320022.png

Mamia ya watu wamekamatwa nchini Afrika Kusini huku ghasia zikienea kufuatia kufungwa jela kwa rais wa zamani Jacob Zuma.

Waandamanaji wanaomuunga mkono Zuma kwanza waliingia mitaani baada ya kiongozi huyo wa zamani (79) kujisalimisha kwa mamlaka Jumatano ili kuanza kifungo cha miezi 15.

Lakini polisi sasa wanasema wahalifu wanachukua fursa ya machafuko, ambayo yalisambaa kutoka mkoa wake wa KwaZulu-Natal hadi Johannesburg, huko Gauteng.

1626068381058.png

Picha zimeonesha majengo na magari yakiwaka moto.

Idara ya intelijensia, imesema watu 300 waliandamana barabara kuu mjini Johannesburg nchini humo.

Watu takribani 800 walihusika kwenye tukio ambalo afisa wa polisi alipigwa risasi huko Alexandra. Maafisa wawili walijeruhiwa.

Polisi pia walijibu ripoti za unyang'anyi jijini Johannesburg na KwaZulu Natal. Zaidi ya watu 60 wamekamatwa mpaka sasa.

Haijulikani kama wanahusika na maandamano yanayomuunga mkono Zuma, huku msemaji wa polisi wa KwaZulu-Natal Jay Naicker akiliambia shirika la Reuters kuwa wameshuhudia ''wahalifu wakijaribu kutumia hali ya vurugu za maandamano kujitajirisha''.
 
Hao ni wahuni wasiopenda kazi ndo wanaleta shida zote hizo
 
Kiukweli sisi ni tatizo acha tutukanwe na wazungu!

Kwa haya yanayojiri south ni kielelezo kabisa kuwa mwarika ni mjinga na hajitambui .

South Limekua Taifa LA hovyo kuliko CHAD au NIGER!

Rais anadhitakiwa kwa wizi dhidi ya Mali ya Taifa mwananchi masikini analalamika kuwa Rais mstaafu kaonewa hii ni aibu kubwa sana
 
Back
Top Bottom