Responded Maandamano ya Wananchi wa Buza - Dar es Salaam "Tumechoka tunamhitaji mkuu wa mkoa aje tunateseka"

Responded Maandamano ya Wananchi wa Buza - Dar es Salaam "Tumechoka tunamhitaji mkuu wa mkoa aje tunateseka"

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
4,783
Reaction score
14,975

Wananchi wa Kata ya Buza Wilaya ya Temeke wameandamana kutoka Buza Kanisani hadi Ofisi za Chama cha Mapinduzi Kata ya Buza wakiitaka Serikali kurejesha magari ya Daladala Kutoka stendi mpya iliyopo kwa Mama Kibonge hadi Stendi ya Buza kanisani kutokanana kupata changamoto kubwa ya usafiri.

Wakizungumza na waandishi wa Habari katika ofisi hiyo wamesema wamekuwa wakipata shida ya usafiri wa kwenda mjini kutokanana na Daladala kushindwa kufika mwisho wa gari Buza kanisani na badala yake gari hizo kuishia Stendi mpya ya Mama kibonge jambo ambalo linapelekea kutumia gharama nyingi za usafiri kuelekea mjini hivyo wakimtaka Mkuu wa Mkoa Albert Chalamila kufika eneo hilo na kuwatatulia kilio chao.

Video: ICON TV TZ

Pia soma
~ Kituo kipya Buza kwa Mama Kibonge ni mradi wa nani? Mnatesa Wananchi kwa maslahi ya nani?
~ TAKUKURU: Tunafanya uchunguzi Kituo cha Buza Kanisani kuhamishwa, tunashauri kwa sasa utaratibu wa zamani urejee
 
Back
Top Bottom