Mimi natoka.
Nawaachia usia.
Sisitizeni watu kufanya kazi kwa bidii.
Umasikini wote wa watanzania msiwadanganye kuwa unatokana na serikali.
Kufeli kwa form four msiwadanganye kuwa kumesababishwa na serikali.
Waambieni ukweli, bidii unashinda changamoto nyingi. Ndio maana katika umasikini uliopo kuna wanaofanikiwa.
Ndio maana katika matokeo mabaya ya form four kuna wanaofaulu.
Waambieni ukweli, kuwa bila kufanya bidii hata ikiingia Chadema madarakani wataendelea kuwa masikini.
Waambieni ukweli kama mnajali taifa hili.
Msipofanya hivyo mtakuwa mnapoteza muda wenu na wa wale mnaowadanganya, kwa sababu HUTUTAWARUHUSU kushika dola.