Maandamano ya amani kwa wanafunzi wote wa vyuo nchini

Mimi Nashauri kabla ya Wanachuo ku-sign boom,na pia kabla ya kuandamana,Wawakilishi wa Wanachuo waende wakutane na UONGOZI wa bodi ya mikopo.Mungu atawasimamia mtafikia muafaka kwa amani.Mimi Nashauri Hiyo bodi ya mkopo IWALIPE FEDHA YOTE WALIYOKUWA Wameahidiwa..Maana(1) pamoja na cku za masomo kupungua,BADO pesa yenyewe hata hivyo ilikuwa haitoshi(2)Ili mradi pesa yenyewe Ni ya mkopo,na budgeti ilishapitishwa na lishatengwa,Wapewe tuu YOTE Maana mwisho wa cku,si itarudishwa YOTE wakati wa kulipa mkopo? Kwa bodi hakuna inachopoteza kwa kulipa boom lote.Hakuna sababu ya msingi kwa bodi kuanzisha mkorogano wote hUU.Walipeni tuu boom la semister nzima.Wakati vyuo vilipofungwa,Wanachuo WALIYOKUWA wamepanga uraiani waliendelea kulipa Kodi ya pango,Vinginevyo wenye nyumba wangepangisha vyumba vyao kwa wapangaji wengine wa uraiani.
 
Ilakumbukeni mnadai mkopo ambao mtaurejesha kwa riba isiyoisha

Nashauri mwaka watatu msipunguze honour zenu
 
Huna adabu tunahangaika kukusanya hiyo fedha unayopewa, bado unasema haitoshi si ukae nyumbani, wapo wazazi wanalipia elimu ya juu %100 wasiandamane uandamane wewe, acha upuuzi. Si lazima ukopeshwe, usituudhi tuna majonzi yetu.
 
Serikali ya JPM haichezewi, waambie hawa vijana wanafikiri Tanzania iliota kama uyoga.
 
hawa vijana wanapambania maslai yao ila kuna watu wapumbavu kwenye hili jukwaa ambao wapo ktk system pendwa wanawatisha.
Kurithishana uoga kizazi Hadi ndio huku mkuu.... Ingekuwa ni kenya wasingezubutu huu upuuzi.... vyovyote vile ...ila serikali haijafanya jambo la kiungwana sana kwenye hili. Uongozi nchi za kiafrika ni changamoto sana katika maamuzi yanayohusu ustawi wa jamii....mistake ndogo ndogo hizi huwa zinajikusanya kwenye jamii na kutengeneza picha mbaya dhidi ya serikali.
 
 
 
Wale wakuandama HESLB siku hizi wamehamia Tazara and not sinza. Sasa sijui wanafunzi wa udsm mtatembea Hadi Tazara au mtapanda magari 😁.
Haya wa kuandamana kazi kwenu.
 
Maandamano pekee mtakayofanikiwa ni kuhakikisha hii seriakli dhalimu hairudi madarakani kwa kupiga kura na kampeni madhubuti ndani ya vyuo, majumbani kwenu na mitaani. Kuhakikisha Mpensa maendeleo ya watu Tundu Lissu anatuongoza Licha ya hapo mtapigwa mpaka mchakae. Maana hawaamini ktk maandamano ya amani wala haki ya kujieleza dukuduku zenu.
 
Kwahiyo kukiwa na msiba ndio watu wasifanye mambo yao?? Huo msiba wataomboleza ndugu na mjamaa. Sio kila mtu.
 
Hizo laki mbili zitawatokea puani!

Be humble. Ni ushauri tu lakini.

Unaweza kuwa upande wa haki na ukaumia vile vile!

La kuambiwa........
Akili za woga usipandikize kwa vijana.

Kwa nini uwe upande wa haki afu uonewe. Nini hukumu ya hao waonevu unayoweza ipendekeza.. ama ndiyo kumuachia Mungu.?
 
Rejea mkataba unasemaje...mengine ni huruma ya mtoaji..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…