Sasa hawa watoto kuwatoa shule kwa ajili ya siasa hivi kweli ni ubinadamu au ilikuwa jumapili?, hawa wanajua kitu kinachoendelea kweli??!! Hivi hawa watoto wanajua maana halisi ya UFISADI ??!? , hivi hawa watoto wanaweza KUPIGA KURA 2015?!!?? hivi hawa watoto wanajua kuwa mashamba makubwa yanauzwa kwa bei ya kutupwa kwa wawekezaji na wananchi wanahamishwa kupelekwa kuanza upya ulimaji kwenye mapori?!?!?! hivi hawa wanajua kuwa juzi juzi tu nyumba za serikali ziliuzwa kwa bei ya kutupwa na leo hii baadhi ya viongozi wanaishi kwenye mahoteli !?!?!??, hivi wanajua kuwa kuna wanyama pori wanaouzwa nje waziwazi kupitia airport zetu?!!?, Hivi wanajua kuwa hali ya uchumi wa Tanzania inazidi kuwa duni kila kukicha chanzo kikiwa hicho chama wanachokipigia dole gumba??!?!?!, Ebwana Nape wewe mtu mzima, hao hawajui zaidi ya kuwa siku hiyo alikuja mtu sana sana aliwapa mabakuli ya uji na slice za mikate kama walipewa baada ya kupiga picha ya pamoja. Nape ongeza bidii, utafanikiwa tu. Ila angalia kuna Mungu ambaye anaweza kukupa dhambi kwa kuwatumia watoto kwenye mambo yasiyowahusu. CCM juu juu zaidi. Mimi siyo mfuasi wa chama chochote ila ni mwananchi mwenye uchungu na maendeleo ya nchi yangu na ni mpiga kura tangia nilipofikia umri wa kuanza kupiga kura.Duuu inasikitisha kwa kweli, hivi ni kwanini hawasomi alama za nyakati. We nape wewe poteza muda tu huko!!!!!!