Maandamano makubwa Songea!

Maandamano makubwa Songea!

Nawapa pole sana waliofiwa, naamini jeshi letu la polisi litakuwa makini na kuomba radhi kwa mauaji ya raia wasio na hatia. Mungu azilaze roho za marehemu mahala pema peponi, amina.
 
wanasiasa wanafanya tunauana....... sisi kwa sisi.... Mola uwasamehe.
Source: Bushoke
 
libya maandamano yalianza mtu moja tu jamaa serekali jipangeni mtakuja kukimbia office zenu na suti zenu tz inawatu wengi kushinda hao polis wenu hamuoni mifano kuna mtu alifikiria kama gaddafi atakimbia kama panya kwenye mitaro msizarau kikiwaka hakuna na igp wala Nani kila mtu atakimbia

Sio kwa dizaini ya hawa watanzania wa sasa, wenzetu tayari wameuawa huko bado tunaogopa kuingia barabarani nchi nzima kupinga utawala huu wa kifedhuli wa ccm ya jakaya
 
Tunaangamia kwa kukosa Maarifa, kwani kwa hili sidhani kama kuna mwenye haki ya kufanya hivyo ktk maana si police wala wananchi waliochukua hatua stahili. kumbuka hayo ni matokeo ya teuzi zisizozingatia merits ukiaanza na mkoa wenyewe plus RPC kwani tumeshuhudia rpc anatoa taarifa ya ajali mbaya iliyogharimu idadi kubwa ya maisha ya watu huku akicheka, na wakati mwingine akitikisa funguo zake, kana kwamba si issue
 
JAMANI TANZANIA INAELEKEA WAPI? VASCO DAGAMA ATAKUMBUKWA MILELE
PICT0021-1.jpg
PICT0024-2.jpg
PICT0020.jpg
PICT0024-1.jpg
[/QUOTE]
 
Unyama walio ufanya FFU songea leo unatisha
kwa uwoga wao walinizuia nisipige picha wkt wanafanya uovu wao
 
Unyama walio ufanya FFU songea leo unatisha
kwa uwoga wao walinizuia nisipige picha wkt wanafanya uovu wao
Kupiga picha siku hizi mpaka upeleke maombi polisi?..au uoga wako tu kaka!
 
Polisi wakiwa katika gari lao wakati wa kutuliza vurugu mjini songea baada ya wakazi wa manispaa hiyo kuandamana kupinga mauaji ya raia wasio na hatia yanayofanywa na watu wasiojulikana.
Picture+009.jpg
 
Polisi wakiwatawanya na kuwakamata baadhi ya waandamanaji hao katika manispaa ya Songea baada ya wakazi wa manispaa hiyo wengi wao wakiwa madereva wa pikipiki kuandamana hadi ofisi ya kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma kupinga mauaji ya watu yanayoendelea kwa kasi mjini humo ambao hadi sasa jeshi la polisi halijafanikiwa kuwakamata wauaji: http://latestnewstz.blogspot.com/

Picture+007+(1).jpg


Picture+011.jpg
 
Madereva pikipiki wakiwa wamefunga barabara ya songea kwewnda tunduru karibu na mlango wa kuingilia ofisi ya mkuu wa mkoa wa Ruvuma, wakilitaka jeshi la polisi mkoa huo kuchukua hatua dhidi ya mauaji ya watu yanayoendelea mjini songea ambapo hadi sasa zaidi ya watu 8 wameuawa na watu wasiojulikana wengi wao wakiwa ni madereva wa pikpiki.

Picture+002+%281%29.jpg
 
Ona nchi hii ilivyopendelewa, ukiangalia matukio makubwa ambayo yanatoa uhalali kabisa kwa umma kutafakari kama ni sahihi kuendelea na utawala huu au ujitwalie mamlaka yake, ila mara zote we take for grant these golden opportunity na tumeendelea kuwa mabingwa wa kuimba nyimbo za kipuuzi oh Mungu anajua, oh ipo siku yataisha ****** tu acha tuendelee kusubiri huruma ya mnyonyaji....!
Tunaozidi kulaaniwa ni sisi na ardhi yetu kwa kuruhusu damu za wapendwa wetu kuwa zimepotea for nothing!
 
Hili ndilo tatizo hasa la kuingia mkataba na Ibilisi, anakumiriki mwili na roho, pia kujitwalia uwezo wa kukufanya chochotea kile atakacho.
Mwili wako ni mali ya ibilisi
Roho yako ni mali ya Ibilisi.
Mbele ya Ibilisi huyu hakuna tofauti kati ya tofari na Roho yako

Tumetumia nafasi zetu, haki zetu na akili zetu zote kufanikisha kuiweka CCM madarakani na kuipa nguvu ya kikatiba.

Tumeiweka CCM madarakani kwa;

kuchelea maovu ya utawala wa CCM,
kukubali wito wa CCM wa Kuogopa mabadiliko ya kisiasa,
Kuwaachia wezi wa kura wa genge la kiCCM kutimiza matakwa yao binafsi
Kuhongwa vijikanga na vijiTshirts ili kuuza utu na haki,
Kuyakataa maendeleo kwa nguvu zetu zote na kukubali mfumo wa uliotuweka tena katika utumwa kikoloni ndani ya nchi yetu wenyewe.
Kukumbati mahabithi kwa ujira mduchu huku wao CCM wakifaidika na Kuiza ncho yetu kwa Makampuni ya Kimataifa kama Barick Gold Mines na mengineyo yanayo miriki ardhi yetu kwa nguvu,
Kuhifadhi wala rushwa na mafisadi ili kuendelea kulinda himaya yao watoto wao wajukuu zao na ukoloni mambo leo ulioturudisha tulipokuwa kabla ya Dember, 9 1961.


Ili kuwaondoa CCM madarakani,Tunahitaji zaidi ya mara mbili ya juhudi zilizotumika kuwaweka madarakani.
Sisi Wananchi ndiyo tumewaweka madarakani CCM, ni sisi wananchi tutakao watoa CCM madarakani.
Wananchi tusitegemee shujaa au nabii kutoka juu kuj kuiondoa CCM.
Kuiondoa CCM madarakani ni kazi yetu Namba 1 na muhimu kuliko hata milo yote mitatu ya siku,
CCM wapo madarakani kwa sababu wanachi tunaridhia kuwepo kwao madarani.
Bila ridhaa yetu wananchi CCM hawawezi kuwepo madarakani.
Bila wananchi kuafiki kwa namna moja au nyingine CCM hawawezi kuwa madarakani.
Yawezekana kabisa nia mioyoni mwetu haiafiki CCM kuwepo madarakani,hata hivyo vitendo vyetu,tabia zetu, mienendo yetu na mazoea yetu ya kuamini kila lisemwalo TBC au kutoka kwa viongozi wa serikali yanaafiki CCM kuwepo madarakani.
Ni Pale tu Nia zetu zitapoendena na Vitendo vyetu, zitakapoendena na mienendo na tabia zetu ndipo CCM itapoondoka madarakani na kubaki katika vitabu vya Historia kama Utawala haramu wa Vizuka Makaburu weusi wa Tanzania.
Wananchi tuna uwezo wa kufanya lolote kuleta haki usawa na fursa ya maendeleo kwa wote lakini uwezo huo umekuwa ukigubikwa na woga, unyonge,utengano na hali ya kukata tamaa.
Mnyonge na Mnyonge ni sawa na wenye nguvu kumi.
 
Hakuna njia nyingine za kusimamisha maandamano ila kwa kutumia silaha na kuua watu. Poleni wafiwa na majeruhi inasikitisha sana kwa nchi inayojitangaza kisima cha amani
 
Also, President Kikwete has been blamed for choosing his friends to the cabinet, a result of which he has no power to condemn them for their irresponsibility. The example of two consecutive bomb blasts at Mbagala and Gongo la Mboto arm base respectively in 2009 and 2011 where General Mwamunyange as well as the defense minister, Mwinyi, were in charge, but they insisted that it was not their fault for the blast and denied to brief the country about the reason for the blasts. The President himself kept praising to the two officials that they are working to secure a country something that raised anger among the victims of blasts.
 
Also, President Kikwete has been blamed for choosing his friends to the cabinet, a result of which he has no power to condemn them for their irresponsibility. The example of two consecutive bomb blasts at Mbagala and Gongo la Mboto arm base respectively in 2009 and 2011 where General Mwamunyange as well as the defense minister, Mwinyi, were in charge, but they insisted that it was not their fault for the blast and denied to brief the country about the reason for the blasts. The President himself kept praising to the two officials that they are working to secure a country something that raised anger among the victims of blasts.
I don't know what Mr. president JK will tell us about these situations, as to why he didn't take a proper measure on those irresponsible personel? In addition to Medical doctors strike throughout the country which led to lose of lives! JK and his Co will end up will end up in jail if we are to build a strong national which respects our land laws and principles of living.
 
Back
Top Bottom