skendo
JF-Expert Member
- Apr 9, 2011
- 212
- 101
Wakuu nimepigiwa simu na rafiki'angu toka Songea anasema kumekuwa na mauwaji ya kutisha kwa mda wa wiki sasa na inasemekana watu zaidi ya kumi wamesha uwawa ingawa RPC amedai wananchi wasihofu.
Pia nasikia wananchi waliandamana mpaka kwa mkuu wa Wilaya ila bado uvumbuzi haujapatikana na inasemekana wananchi waliwachoma moto watu wawili kutokana na tuhuma za kuhusika na mauwaji hayo na ndipo wauwaji wakasema sasa wataendeleza mashamulizi.
Mwenye ndugu pande hizo anaweza mpigia simu ili tuweze pata taarifa zaidi ila kuna jamaa yangu mwingine ni polisi nae ameniakikishia kuwa hali si nzuri kwa sasa.
Pia nasikia wananchi waliandamana mpaka kwa mkuu wa Wilaya ila bado uvumbuzi haujapatikana na inasemekana wananchi waliwachoma moto watu wawili kutokana na tuhuma za kuhusika na mauwaji hayo na ndipo wauwaji wakasema sasa wataendeleza mashamulizi.
Mwenye ndugu pande hizo anaweza mpigia simu ili tuweze pata taarifa zaidi ila kuna jamaa yangu mwingine ni polisi nae ameniakikishia kuwa hali si nzuri kwa sasa.
Kwa mliosikiliza radio na kuangalia ITV mmejulishwa kinachojiri songea asubuhi hii ni mapambano ya askari na raia
CHANZO CHA MAPAMBANO
Kuna raia wanauawa tangu juzi na matukio yanaripotiwa ila askari hawachukui hatua yeyote ile zaidi wanasema ushahidi hawajauona,usiku wa kuamkia leo limekua tukia la 5 raia kuuliwa na askari kama kawaida yao hawatoi ulinzi kwa raia wao.
Asubuhi raia (Watoto, vijana, wazee) wakaamua kuwatolea uvivu askari na kuandamana hadi kituo cha polisi kudai haki ya kulindwa na kuishi raia walikua wengi kuliko uwezo wa askari wa kile kituo hivyo waliona hapa wakiwa wakali kituo kitachomwa moto maaana walikuja na jazba raia wakawaambia taarifa ziko kwa mkuu wa wilaya raia bila simile wakaanza maandamano hadi kwa mkuu wa wilaya kufika huko naye akanawa mikono kama pilato akasema mkuu wa mkoa ndo liko mikononi mwake.
Raia hawakuishia hapo wakalianzisha hadi kwa mkuu wa mkoa huku wakiimba "TUMECHOKA KUUWAWA" hadi kwa mkuu wa mkoa, hapo ndo movie ilpoanzia kumbe raia wakati wanaenda kwa mkuu wa mkoa inaaminika simu zilipigwa kwa mkuu wa mkoa na askari wanaolinda (FFU) wakafunga geti hapo ndo ikawa vuta nikuvute raia wakaweka kambi nje huku wanaimba nyimbo "MKUU WA MKOA UNAWAOGOPA RAIA WAKO JIUZURU", muda si mrefu gari ya FFU likawasiri likiwa na askari wa kutosha kwa vile raia hawakua na silaha wala ugomvi wakaamua kubaki huku wanaimba.
Askari kama kawaida yao wakawa wanazidi kusogelea huku wakitoa ishara wananchi watawanyike huku wananchi wakigoma hawatoki hadi mkuu wa mkoa naye atoke nje hapo ndo askari wakaanza kufyatua risasi za moto na raia wawili wakafa.habari zikafika mjini raia wameuliwa na askari hapo ndo mji ukazizima raia wakaingia mitaani askari waliokua mitaani walianza kupata upinzani mkali hd askari wawili wamekufa hadi hivi sasa, imebidi jeshi liingilie kati na mji wote kufungwa hivi ss mjini ni makundi ya wanajeshi na askari ndo yametawala hakuna maduka wala mabenki yanayofanya kazi
VIFO
Nimeshuhudia raia wawili na askari mmoja tu kwa macho yangu kwa sehem niliyokuwepo,kiujumla inasadikiwa raia zaidi ya wa4 na askari 2 ndo wamekufa,mji umepoa kabisa na mm ndo niko nyumbani ila ntarudi later mjini kuchukua news zaidi ili niwajulishe
Nawakilisha
Kwa mujibu wa Wananchi wa mji wa Songea walishatoa taarifa kwa RPC, kuhusu mauaji yanayo fanyika songea kila siku, RPC akasema hakuna kitu kama hicho (kama kawaida dharau), sasa leo asubuhi kuna raia mwingine tena mmoja amefariki kwa kupigwa risasi, wananchi baada ya kuona hali hiyo wakaanza kuandamana kuelekea ofisi ya mkuu wa wilaya, Ndipo wale jamaa wasio kuwa na kazi ya kufanya (FFU) walipopigiwa simu na kuja kutoa kichapo kwa raia ambao wanakufa kama wanyama.