Maandamano makubwa Songea!

Maandamano makubwa Songea!

These are very SAD News! RIP for all who lost their life fighting for their basic RIGHTS!
 
Matunda ya kushabikia ccm baada ya kulishwa pilau na pombe za kienyeji kila baada ya miaka mitano ndo hayo.
 
Tutaendelea kuimba TZ ni kisiwa cha amani wakati roho za watu wasio na hatia zinateketea, jamani tuiombee hii nchi.
 
Hivi mtu ukiambiwa wajibika ni kosa? Polisi hawataki kuwajibika, wakiambiwa kwa nia njema kabisa wanachojua ni kupiga na kuua tu basi.
 
Wana Songea tumechoshwa na vitendo vya Kamhanda kwa sababu
  • anashirikiana na majambazi
  • anajishughulisha na biashala ya meno ya tembo
  • hajali wananchi na kukiwa na taarifa ya matukio km hayo wewe uliyepeleka taarifa ndo unawekwa ndani na pengine kuuawa ili kusiwepo na taarifa tena
  • anashiriki kufanya mauaji na wahalifu kwa kuwaazima silaha, akijua unataarifa zake anua mtu mwingine nawewe unabambikiwa kesi hiyo. vinginevyo anakuua tu
kwa hiyo sisi songea tumechoka kuonewa ktk mkoa wetu wenyewe, hatuna pa kupeleka kero zetu, tunakufa usiku na mchana kama tupo somalia hivi
 
hadi sasa wameuawa raia 2 kwa kupingwa risasi na askari.raia walio na uchungu kwa kuuwawa ndugu zao na watu wanaosadikiwa kutoka msumbiji kuja chukua viungo vya binadamu.mmoja wa majambazi aliuwawa kati ya wawili waliochomwa moto.na kabla hajafa aliteswa na kurekodiwa na raia hadi akataja sehemu walipo lizaboni.lakini polisi wapo kimya.

Ninatoa pole kwa wakwe na shemeji zangu wangoni kwa kadhia kubwa iliyo wakumba,MUNGU AWAPE NGUVU NA KUWAONGOZA KATIKA KILA HERI
 
Hakuna asiyejua,alieidhinisha mauaji haya nchi nzima ni Amiri Jeshi Mkuu,Mh Jakaya Mrisho Kikwete...

Kuna wakati ilitoka post katika thread ya JF kwamba kikao kilifanyika wakati wa vurugu za Arusha, na Mkuu aliridhia kwamba kama ikibidi watu wauwawe na iwe hivyo. Nadhani jeshi la Polisi toka wakati huo wamekuwa wakifanya kazi kwa mentality hiyo...kama ikibidi raia wauwawe na iwe hivyo. Mie nadhani hatuko mbali sana na critical mass, ambapo hali inaweza kubadilika siku moja na nchi yote ikaingia katika maandamano. Sintashangaa kama JW wanasubiri hilo kwa hamu sana, wapate sababu ya kuingilia kati ili kulinda raia kama ulivyo wajibu wao. Ila tatizo ni kwamba JK aliliona hili siku nyingi, akabadili Mkuu wa Majeshi siku nyingi na kumweka ambaye ana maslahi yake (refer WikiLeaks na ubadishwaji wa Mkuu wa Majeshi Tanzania kipindi cha JK). Inaonekana JK alishajifunza kipindi cha Mwinyi, ambapo ni Nyerere tu aliyeweza kuwaambia Wanajeshi watulie kambini wakati wakisema "huyu raisi wananchi wameraramika wamechoka na yeye anabeba wahindi na waarabu tu!" Kiaro alimfungia safari Mwinyi kwenda Ikulu na convoy ya maofisa wakuu wa Jeshi, ikabidi Mwinyi abanwe kigugumizi (kisa kikiwa kimeanzia mtoto wa Kiaro kugongwa na gari la Mhindi huko Mbeya na Mhindi huyo kuachiwa huru wakati mtoto wa Kiaro yuko mahututi hospitali). Nyerere leo hayupo bwana.
 
Tumethubutu Tumeweza na Tunasongea mbele kwa Ari zaidi Nguvu zaidi na Kasi zaidi ya risasi.

Sikio la kufa huwa halisikii dawa kesho Komba akipita naTOT plus....watasahau.

Wana Songea Tieni, Tieni Tieni...kwa moyo mmoja, nambari wani eee... nambari wani ni Sisiyemu.

CCM Oyeeee!!!!!
 
si mnamwona mwandishi wa YBC alivyo lala hapo chini,lakini kwa roho ngumu atatangaza kuwa hakukuwa na risasi za moto na hakuna aliye uwawa kulikuwa na usalama wa hali ya juu,wakati nalala chini nilikuwa na kwepa mawe kutoka kwa waandamanaji kutoka hapa songea ni mimi ,, wa TBC ,hawataki kusema ukweli kabisaaaaaaaa,NADHANI POLISI WANGE mpiga risasi mtangazi ndio ujumbe ungefika kwa wahusika,lakini kwa wananchi ujumbe haufiki kabisaaa,ni maonezi hadi lini jamani?

TBC wote ni wale wale hawana tofauti wanatangaza wanachoambiwa na wakubwa wao. Huwa hawasemi ukweli kabisa utadhani nao wamekunywa maji ya bendera.

NASUBIRI BBC JIONI.


ACHENI NISEME, HATA MKINI.............. ACHENI NISEME, HIVI SERIKALI YA KIKWETE INASUBIRI NINI KUJIUZULU, KWANI IMESHINDWA KUONGOZA KILA MWEZI NI MAUAJI YA WATUA WASIO NA HATIA. NA KILA SIKU NI TAARIFA ZA POLISI WAMEUA RAIA KISINGIZIO JAMBAZI KUMBE ILI WAMUIBIE.

MAKAMANDA WA POLISI NA SERIKALI WOTE WAPO KIMYA WANAFANYA UCHUNGUZI!!!!!

TUMECHOKA KWANINI MSIJIUZULU KWA AMANI KULINDA HESHIMA YENU!!!!

ACHENI NISEME NIMECHOKA........................ HATA MKINI.................... UKWELI NIMESHASEMA.................



MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
si mnamwona mwandishi wa YBC alivyo lala hapo chini,lakini kwa roho ngumu atatangaza kuwa hakukuwa na risasi za moto na hakuna aliye uwawa kulikuwa na usalama wa hali ya juu,wakati nalala chini nilikuwa na kwepa mawe kutoka kwa waandamanaji kutoka hapa songea ni mimi ,, wa TBC ,hawataki kusema ukweli kabisaaaaaaaa,NADHANI POLISI WANGE mpiga risasi mtangazi ndio ujumbe ungefika kwa wahusika,lakini kwa wananchi ujumbe haufiki kabisaaa,ni maonezi hadi lini jamani?
Pasco kwa kutufanya tuamini zaidi atasema hata yeye alikuwepo Songea wakati wa tukio hakuna mauaji ila ni polisi ndio walioshambuliwa tunawasingizia. Mmesahau ya Apollo.
 
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma (Kamuhanda) analalamikiwa kwa kulea majambazi ambao wanaua Raia kila kukicha na kuwaibia,wanachi wakienda kumlalamikia anawambia hakuna kitu kama hicho sasa wanasongea wanasema liwalo na liwe hadi kieleweke.

Haya ndiyo matatizo ya kupeana vyeo kwa hisani bila kuangalia uwezo. Public management ni kazi ngumu sana. Nafikiri jeshi la polisi linahitaji mafunzo ya hali ya juu hasa katika ku-manage watu. Polisi wamejitwisha kazi ya kulinda masilahi ya CCM haya ndiyo matokeo yake. Kama wangekuwa wanafanya kwa manufaa ya wananchi, asingekuwa anatoa kauli za 'hakuna kitu kama hicho' baada ya kulalamikiwa, kitu ambacho angefanya ni kutumia ushawishi wa kushirikisha wananchi kukabiliana na hali hiyo. Kama vile kuanzisha ulinzi shirikishi, kutoa polisi wa kutosha kufanya doria na kuweka mitego. Ila unapo-dismiss malalamiko ya wananchi unawafanya waone kuwa 'They are on their own' na madhara yake ndiyo haya.

Nina uhakika kama angepelekwa taarifa na viongozi wa CCM kuwa CDM wanapanga kuandamana angekurupuka na kupiga marufuku na kuwasha defenders kuzunguuka mji. Sooner or later Tanzania will be not safe place to live, Its not too late, tunaweza kuokoa gari hili lisitumbukie shimoni kwa kuacha siasa katika masuala ya usalama wa raia.
 
Hivi mtu ukiambiwa wajibika ni kosa? Polisi hawataki kuwajibika, wakiambiwa kwa nia njema kabisa wanachojua ni kupiga na kuua tu basi.

Tanzania tumezidi na nidhamu za uoga. Inapaswa kuwajibika kwa kujiuzulu kuanzia Raisi na Serikali yote. lakini kwa jinsi wanavyotufanya wananchi hatuna akili utashangaa majibu watakayotoa kama Jeshi la polisi......... ni maudhi tupu ndiyo yatakuja......

NA WATASEMA WANAFANYA UCHUNGUZI NA KUUNDA TUME KUCHUNGUZA MAUAJI YA SONGEA.

heheheheheheh TUMEWAZOEA CHAMA CHA MAJAMBAZI;

Naona kwa hao waliokufa leo ni wengi hivyo hiyo Biashara yao ya kunyofoa Nyeti leo wamepata maiti wengi kweli!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

ACHENI NISEME................... HATA MKINI....................ACHENI NISEME KUWA SERIKALI YOTE INAPASWA KUJIUZULU.


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Kutokana na mauaji ya kila siku yaliyodumu kwa wiki mbili mfululizo kwa kila siku mwananchi mmoja au wawili kuuawa kwa kuchinjwa bila ya sababu yoyote katika manispaa ya Songea wananchi sasa tumechoka na uozo wa serikali isiyokuwa na meno (toothless bull dog) uongozi wa serikali ya magamba katika mkoa wa Ruvuma ni uozo mtupu kuanzia Regional Commissioner Mwambungu sijui kwanini wamekuleta kama RC ungeendelea tu kuwa DC maana kiatu ulichokivaa hakikutoshi, ukiwa kama Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa umeshindwa kuchukua hatua yoyote kwa mauaji yanayokithiri kila siku? umeoza we mzee! kwa RPC ndio kabisaa takataka sijui IGP Mwema anatumia vigezo gani kuteua Ma RPC maana wa mkoa wa Ruvuma hana sifa hata ya kuwa mgambo (labda awe green guard) huyu takataka ananuka rushwa na anafadhili magenge mengi sana ya ujambazi, kuna kipindi kuna bunduki mbili ziliibiwa na tunajua yeye ndio aliyehusika na ule mchezo na kipindi cha utafiti wa kuzipata alikuwa akitusaliti na kuvujisha taarifa kwa watu wake mbinu tulizopanga kuzipata zile bunduki, hadi pale ile task force iliyotoka HQ kuja kubaini hizo bunduki bt baada ya kuzuia kupitisha habari za upelelezi kwa RPC maana walijua anavujisha taarifa. Leo asubuhi watu wengine wawili wameuawa na bado polisi mmelala watu wamechoka! na nawapongeza sana wananchi wa Songea mjini kwa kuandamana leo asubuhi hiyo ndio nguvu ya umma tunataka muamke ili kuishtua hii serikali ya magamba iliyo lala isiyojali maslahi ya wanachi wake. Polisi kwa kuwapiga risasi watu wawili leo maaeneo ya ofisi ya mkuu wa mkoa haitazima uchungu na hisia za wananchi wa Songea waacheni wapige mabomu ya machozi na kupiga risasi za moto lakini lazima polisi wajue wajibu wa kulinda raia wao, na mnabahati leo mission ilikuwa ni kuchoma moto kituo kikuu cha polisi pamoja na nyumba ya huyo kenge RPC na bado harakati zitaendelea tu! ukiwa kama RPC hauwezi ukaletewa madai ya mauaji na ukasema unataka uletewe ushahidi..... ushahidi wakati watu wanakufa! kazi yako ni nini kuomba ushahidi au kutafuta ushahidi? Sasa watu wameamua kukupelekea maiti Nashukuru kweli Tanzania sasa inamebadika watu wanataka haki na wamechoka kuendeshwa na serikali ilijaa kila aina ya rushwa na uozo! Kama JK na timu yake iliyooza imeshindwa kuwawajibisha sisi tutawafunza adabu!

"Without revolution we can't develop"​
Congratulation! Very well spoken!
 
Back
Top Bottom