Wakuu nimepigiwa simu na rafiki'angu toka Songea anasema kumekuwa na mauwaji ya kutisha kwa mda wa wiki sasa na inasemekana watu zaidi ya kumi wamesha uwawa ingawa RPC amedai wananchi wasihofu.
Pia nasikia wananchi waliandamana mpaka kwa mkuu wa Wilaya ila bado uvumbuzi haujapatikana na inasemekana wananchi waliwachoma moto watu wawili kutokana na tuhuma za kuhusika na mauwaji hayo na ndipo wauwaji wakasema sasa wataendeleza mashamulizi.
Mwenye ndugu pande hizo anaweza mpigia simu ili tuweze pata taarifa zaidi ila kuna jamaa yangu mwingine ni polisi nae ameniakikishia kuwa hali si nzuri kwa sasa.
![]()
![]()
![]()
![]()
Ninatoa pole kwa wakwe na shemeji zangu wangoni kwa kadhia kubwa iliyo wakumba,MUNGU AWAPE NGUVU NA KUWAONGOZA KATIKA KILA HERI
Pasco kwa kutufanya tuamini zaidi atasema hata yeye alikuwepo Songea wakati wa tukio hakuna mauaji ila ni polisi ndio walioshambuliwa tunawasingizia. Mmesahau ya Apollo.
Mheshimiwa DCI Manumba hizo ndio taarifa za kufanyia kazi, usingoje kusimuliwa tuma vijana wapate ukweli!!! Vinginevyo squad ya Zombe mpya itatokea au pengine tayari ipo inauwa watu kimya kimya!!!! Fuatilia bwana wacha kujichimbia ofisini ukisubiri eti uletewe!!!!Ushauri wa bure!!!!Wana Songea tumechoshwa na vitendo vya Kamhanda kwa sababu
kwa hiyo sisi songea tumechoka kuonewa ktk mkoa wetu wenyewe, hatuna pa kupeleka kero zetu, tunakufa usiku na mchana kama tupo somalia hivi
- anashirikiana na majambazi
- anajishughulisha na biashala ya meno ya tembo
- hajali wananchi na kukiwa na taarifa ya matukio km hayo wewe uliyepeleka taarifa ndo unawekwa ndani na pengine kuuawa ili kusiwepo na taarifa tena
- anashiriki kufanya mauaji na wahalifu kwa kuwaazima silaha, akijua unataarifa zake anua mtu mwingine nawewe unabambikiwa kesi hiyo. vinginevyo anakuua tu
dunia imefikia mwisho lakini mungu hawaondolee roho mbaya binadamu. hii taarifa ni ya kweli kabisa
Uletaji wa taarifa wa namna hii na unataka watu wajadili sidhani kama unakubalika kwenye jukwaa makini kama hili.Wewe ndio mleta taarifa sasa unataka nani mwingine atoe taarifa? Sisi hatujui wewe ndio unajua sana unauliza kwetu ili iweje?
Kaka mbona wewe unaonekana mzoefu hapa JF ..........wewe kama hunandugu Songea tulia..........acha wenye jamaa songea wapige kisha tutajua kinachoendelea.
Kweli kabisa watu 56 ndio wameshindwa kudhibitiwa na polisi bila kuwafyatulia risasi? kweli wengine tumesema hili jeshi linahitaji kuvunjwa na kuundwa upya bado lina mawazo ya kikoloni sana!
inawezekana kabisa hata hao nane wameuawa na polisi wadoria,ije vita tu nadhani watuwana hamu ya kutumia risasi za motoKwa mujibu wa Wananchi wa mji wa Songea walishatoa taarifa kwa RPC, kuhusu mauaji yanayo fanyika songea kila siku, RPC akasema hakuna kitu kama hicho (kama kawaida dharau), sasa leo asubuhi kuna raia mwingine tena mmoja amefariki kwa kupigwa risasi, wananchi baada ya kuona hali hiyo wakaanza kuandamana kuelekea ofisi ya mkuu wa wilaya, Ndipo wale jamaa wasio kuwa na kazi ya kufanya (FFU) walipopigiwa simu na kuja kutoa kichapo kwa raia ambao wanakufa kama wanyama.