TIQO
JF-Expert Member
- Jan 8, 2011
- 13,786
- 2,102
Sikuamini pale nilipomuona RPC akijibu kwa jeuri sana!
Hivi angepigwa mke wake risasi ya ****** angewapongeza hao mapolisi kwa kufanya kazi nzuri?
Sikuamini pale nilipomuona RPC akijibu kwa jeuri sana!
mkuu mawe siyo silaha??polisi kutawanya maandamano kwa madai hawakupewa taarifa sawa ni halali, lakini kwanini watumie risasi za moto waandamanaji walikuwa na silaha gani? Kwanini rpc akimbilie madai waandamanaji wamepiga mawe ofisi za ccm, inaniudhi kauli hii. Kwanini alete siasa? Kwanini waue watu, ria wa nchi hiii?
Hawa askari wetu hasa wakubwa wanatakiwa kuacha kutumia sheria za kikoloni wajue watu wako huru ndani ya nchi yao, sheria za kikoloni hata bungeni waziri mhusika azipeleke zibadilishwe, watu waheshimiwe sio kuku ni watu!!!!!Waheshimiwa wabunge waangalie sheria mbovu zifanyiwe marekebisho kuzuia askari kuuwa raia wasio na silaha, kwa kisingizio eti wanatawanya maandamano!!!! Vinginevyo hata nyinyi wabunge sheria hizo zitawarudi hata kabla ya katiba mpya kupitishwa mziangalie upya kifo hakichagui!!!!!! Iweje maandamano ya amani uyatawanye kwa risasi za moto hao ni al kaida au El shabab ?????Nadhani watakuwa hawana, inasikitisha kwa askari wetu kutumia nguvu mpaka kusababisha mauaji kwa raia.
Ukweli ni kwamba polisi wanatangaza vita na wananchi, ipo siku watapata wanachokitaka. wasijisahau pia kwamba hata wao ni sehemu ya wananchi.
Kwa maana hiyo nani amfuate mwenzie kuanzisha huu ulinzi shirikishi? Waendesha pikipiki wawafuate polisi au polisi wawafuate waendesha pikipiki? Nini kazi ya jeshi la polisi? Usalama wa raia wanaouongelea ni kitu gani hasa?Tuwe wakweli pale inapobidi,polisi sio miungu wa kuota na kuzuia uhalifu ,kazi yao inategemea ushirikiano wa raia,mauaji ya waendesha pikipiki yalikuwa mengi sana kanda ya ziwa miaka btn 2008-2011 na yalimalizwa na waendesha pikipiki wenyewe.Wao ndio wanaokaa mitaani,wanawafahamu vibaka wote na wanawafahamu dealers wa used spare parts za pikipiki etc kitu walichofanya waendesha pikipiki wa kanda ya ziwa ilikuwa ni kuunda umoja wao against wezi wa pikipiki,walikuwa wanapeana taarifa wanapoona sura inayotia mashaka,wanasaidiana kufuatilia nyendo za watu mbalimbali,wanafuatilia pale mwenzao anapokodishwa na mtu asiye eleweka vizuri na pale mwenzao anapochelewa kurudi etc pia wame track na kukamata wezi mbali mbali na kuwakabidhi polisi,sasa kuandamana wakati wao wenyewe hawafanyi ulinzi shirikishi na baadhi yao ndio wanao chora wizi wa pikipiki ni wastage of time na kutafuta scape goats
kujikomba kwa wakuu ili ionekana ni sahihi walichofanya kwa vile walikua wanalinda ofisi za chama zisidhurike!ila angekuwepo julius k nyerere ndio kiongozi wa nchi nafikiri sasa hv wahusika wote wangekua wamewajibishwa na wapo lupango!
Wakati mwingine lazima uwe na maamuzi yanayoweka woga pembeni..vita kwa ajili ya jambo jema ni utukufu mbele za mungu, Hata Yesu(nabii issa) alipoona hekalu la Mungu limegeuzwa pango la wanyang'anyi aliamua kuingilia kati na kumwaga vitu chini ili kurudisha hadhi ya nyumba ya bwana..kazi ni kwetu Watanzania.Haya ndiyo maneno ingawa muda si mrefu utaambiwa unaombea vita ije.
Ndugu zangu, kutokana na jeshi la polisi jana kuua kwa "makusudi" wananchi waliokuwa wanaandamana kupinga mauaji ya wananchi yanayoendelea pasipo jeshi la polisi kuchukua hatua yoyote, huu ndio ukweli na sio maelezo ya RPC-Ruvuma MICHAEL KAMUHANDA alivyodanganya Taifa.
Mosi, RPC anasema kuwa maandamano yale yalichochewa na ushabiki wa kisiasa huku akidai waandamanaji walipiga mawe ofisi ya CCM. Ndugu zangu hapa RPC kadanganya, waandamaji wengi walikuwa madereva wa pikipiki (boda boda) ambao ndio waathirika wakubwa wa mauaji yale na sio CHADEMA, pili, kamanda anadai walifanya maandamano bila kuomba kibali, uzuzu mwingine wa RPC ni huu, hivi polisi ndo wanaolalamikiwa then utoke ukaombe kibali kwao(polisi) ili uende kwa RC kuwalalamikia polisi.
Kituko eee! Halafu RPC asiwe mbumbumbu wa sheria. Polisi hawaombwi kibali cha maandamano bali wanapewa taarifa ya muda, madhumuni na kutakiwa watoe ulinzi kwa waandamanaji. Mwisho RPC anataka ajifiche ili aonekane ameua ili kulinda CCM (watawala) dhidi ya CHADEMA ili asihojiwe na watawala kwa mauaji aliyofanya.
Mbunge wa songea mjini Dr.Emanuel Nchimbi (0754 033388) RPC-Ruvuma (0754 252415) . Said mwema(0754 705557). Je hawa ni watu au miungu wenye haki ya kuua?
Issue ni moja tu!
This has proved that the so called governors of the district and region, representative of the president in that locality are a bunch of mediocre, incompetent gunnery of our time.
kwa nini Watu walivyotaka kuongea na Mkuu wa Mkoa, yeye asingetumia busara kidogo tu, akatoka na kuwatuliza, akayafanya aliyoyafanya baada ya mauaji?
Baada ya mauaji, eti mkuu wa mkoa ndo anaitisha mkutano na viongozi wa mitaa na viongozi wa polisi!!!! My foot.