Nisaidieni ushauri kuhusu pesa ya kujikidhi(boom) niliyokuwa naitunza

professional ethics

Senior Member
Dec 24, 2023
108
352
Wakuu mdogo wenu nipo njia panda, naomba ushauri wenu. Mimi ni wanafunzi wa mwaka wa tatu hapa Duce nachukua bachelor of science with education biology na geography. (Umri wangu ni miaka 23)

Wakuu nimetunza boom toka nipo mwaka wa kwanza hadi sasa na milioni nne na laki Saba kama reserve yangu ( nimeishi kwa kujibana na Kwa shida sana).

Lakini wakuu hapa natamani sana pindi nitakapomaliza shahada hii mwezi wa Saba, naendelea kuendelea na Master of education hapa hapa UDSM kwa kutumia hii pesa niliyoitunza.

Lakini, pia Wakati nitakapokuwa naendelea na master nime plan niwe nafanya shughuli mbalimbali hasa za ujasiriamali ili niweze ku-mudu maisha hapa jijini.

Wakuu wangu, naomba ushauri mimi mdogo wenu je nipo sahihi kwa mawazo haya niliyo nayo.

Goals za elimu kwangu, natamani sana kuwa mkufunzi, Pia katika maamuzi hasa katika eneo la elimu.

Status ya uchumi wa familia yangu ni duni sana, lakini naamini katika elimu, licha ya kuwa wengi wanaona elimu ni scam.
 
Ngoja waje na wengine, lakini Ukufunzi unamaanisha Ualimu wa Vyuo? Ule hausomewi mkuu, na pia unaweza pata kazi popote kisha ukahamia kufanya kazi Vyuoni kama wanauhitaji na taaluma yako.

Pili, umejibana umefikisha Mil 4 afu unataka ukasome tena. Ebu itendee haki familia yako mzee. Degree iyo inatosha kabisa sasa hivi fanya iyo Mil 4 izaliane atleast hadi unamaliza mwaka 2024 iwe Mil 10+

Kusoma jipe break, utaanza ata 2025 au mbele uko, kwa kutafuta scholarship ambayo itakua na hela ila kujisomesha Masters sikushauri.

Ngoja waje wataalamu zaidi.
 
Kama unaamin katika elimu ndo itakutoa sw endelea na ndoto zako ila ka unataka utoke kimaisha itumie iyo hela kupiga biashara utatoka tu kimaisha achana na masuala ya kusoma iyo shahada inatosha sn
 
Achana na master degree ya education,fanya field tofauti au fanya mishe zingine,unless unataka kuwa lecturer
Soko la ajira halihitaji sana watu wenye master ya same field,utapoteza muda na hela zako bure
 
Ngoja waje na wengine, lakini Ukufunzi unamaanisha Ualimu wa Vyuo? Ule hausomewi mkuu, na pia unaweza pata kazi popote kisha ukahamia kufanya kazi Vyuoni kama wanauhitaji na taaluma yako.

Pili, umejibana umefikisha Mil 4 afu unataka ukasome tena. Ebu itendee haki familia yako mzee. Degree iyo inatosha kabisa sasa hivi fanya iyo Mil 4 izaliane atleast hadi unamaliza mwaka 2024 iwe Mil 10+

Kusoma jipe break, utaanza ata 2025 au mbele uko, kwa kutafuta scholarship ambayo itakua na hela ila kujisomesha Masters sikushauri.

Ngoja waje wataalamu zaidi.
Asanteh mkuu
 
Achana na master's degree kwa Sasa. Ifanye mipango ya baadaye.
Tumia hiyo pesa kutafuta pesa zaidi, Kama umeweza kujibana wakati wenzako wanalimbuka na wadada na pombe za Dar, wewe utafika mbali. Kumbuka hakuna atakayekuajiri ukimaliza degree yako ya pili.
 
Sikushauri uendelee na master, jibane sana mpk unamaliza walau uwe na 6m alafu ingia kitaa, tafuta mishe komaa sana !

Pombe na mademu visikie tu kwa jirani hakika utatoboa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom