Wapenda shughuli msichanganye Sherehe na Kumbukumbu Rasmi ya Uhuru

Wapenda shughuli msichanganye Sherehe na Kumbukumbu Rasmi ya Uhuru

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
64,554
Reaction score
110,101
Kuelekeza pesa takriban bilioni 1 kasoro kidogo zilizotengwa kwa sherehe kwenda kufanya mambo mengine ya msingi ni jambo sahihi kabisa ila swali kubwa la kujiuliza ni kwa nini zilitengwa kwa hiyo sherehe kwa kuanzia?

Siku ya Uhuru ni muhimu sana kama kumbukumbu ya taifa, hatuwezi kuacha kuadhimisha. Kukosekana kwa sherehe hakumaanishi kutothamini kumbukumbu ya Uhuru kwani kitendo cha kutenga siku maalum na kuifanya ya mapumziko ndilo jambo muhimu zaidi. Sherehe kubwa za mbwembwe nyingi haziongezi urasmi wowote wa siku yenyewe.

Linalopasa sasa ni kuondokana kabisa rasmi na utamaduni wa shughuli kubwa zenye mbwembwe na gharama kubwa kwa siku za Uhuru na Muungaji.

Badala yake maadhimisho yanaweza kufanyika baadhi ya sehemu kama hizi;

1. Viwanja vya Ikulu, kukawepo na gwaride na walikuwa wachache kutoka makundi mbalimbali kama wawakilishi.

2. Rais kutembelea mpakani kwenye kambi mojawapo za jeshi

3. Rais kualikwa bungeni na kuhutubia bunge lililo na wageni mbalimbali kama wawakilishi
 
Mataifa mengine sioni yakifanya sherehe siku ya uhuru, ni sisi tu. Ni muda mwafaka kufuta sherehe hizi, tubaki na kumbukumbu tu ya kwenye vitabu
 
Waswahili ni watu wanaopenda "shughuli" sana, ila utamaduni huu sio wenye afya katika masuala ya kitaifa.
Mataifa mengine sioni yakifanya sherehe siku ya uhuru, ni sisi tu. Ni muda mwafaka kufuta sherehe hizi, tubaki na kumbukumbu tu ya kwenye vitabu
 
Back
Top Bottom