Gily Gru
JF-Expert Member
- Jul 4, 2016
- 7,802
- 20,762
Kuna kipindi wakati niko Rombo nakumbuka nilienda kumuoji mzee mmoja anaitwa mzee Afande kuhusu maswala ya zamani. Yule mzee alinambia kuwa kat ka maisha yake amemwona babu yangu (nami namfahamu), baba yake babu yangu (alifariki 1983 simfahamu) na babu yake baba yake babu yangu (simfahamu). Na alidokozea kuwa wakati baba yake babu yangu alikuwa mdogo sana kwake. Niliongea sana na yule mzee mwishoni nikamnunulia bia mbili za safari nikamuaga niende zangu. .
Huyu mzee Afande alifariki mwaka jana japo umri wake ulikuwa kipengele wengine walidai alikuwa na miaka 120 mpaka 140.Kama mnavyojua mengi husewa na kila mtu husema lake. Ila vitukuu vyake huyu mzee mkubwa ana miaka 40+. Najua kuna watu watabisha ila mkoa wa Kilimanjaro una wazee wenye miaka mingi mno inatakiwa watu walichunguze hili swala.
Kuna wazee kibao ambao nawafahamu wamekufa wakiwa na miaka 100+. Mfano bibi yangu mke mdogo narudia mke mdogo wa babu wa BABA yangu ambaye mimi ni kitukuu wake alifariki akiwa na miaka 119. Ushahidi wa umri wake ulipatiakana mission (kwa wanavyotamka wachaga misheni) kwenye nyaraka za kanisa. Watoto wakizaliwa kipindi hicho walikuwa wanaenda kuwaandikisha mission. .
Kilichofanya niandike huu uzi ni kuwa mzee Afande aliniomba nikamletee ngozi ya mnyama wa mwituni. Kwa uoga wangu sikwenda kwa sababu nilipata wasiwasi usikute huyu mzee anataka kuchukua umri wangu kichawi.
Kilichonifanya niogope ni kwa sababu baba yake mzee Afande alikuwa ana tabia ya kutondokea (neno la kichaga) nikimaanisha anavua nguo zote anazama ardhini kichawi anakaa hata juma moja anarudi. Wanadai wenyewe kuwa anaenda kuzungumza na mizimu huko chini (Kuhusu story za kutondokea nitazileta siku nyingine ni habari ndefu na ni swala la kweli kabisa linatokea). .
Jana kuna mzee mwingine kaniambia maneno haya haya nimletee ngozi ya mnyama wa mwituni. Huyu mzee wala si mzee kivile ana miaka 70+ na hata hana uchawi wowote ni mzee wa kawaida. Nikawaza labda hili neno halina maana mbaya ni maneno tu ya zamani labda kuna kitu yanamaanisha. Sasa ndugu zangu najua JF ni kisima cha maarifa kama kuna mtu anajua maana ya haya maneno anielekeze. .