Sikiliza usia wa baba/mzee wako

mimiamadiwenani

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
5,411
7,016
Kwema ndugu!

Usiache wala kudharau mausia ya mzee wako ukisema sasa umekuwa mtu mzima na hivyo unajiongoza mwenyewe. DON'T.

Wazee wetu hasa akina baba wana baraka mno. Na kuna baraka mno kwenye kuyashika na kuyafuata mausia ya mzee wako. Mimi ni miongoni mwa watu waliofanikiwa kwa 99% kwa kufuata mausia ya mzee wangu.

Kumuheshimu mzee wako ni kumuheshimu Mungu. Ndipo riziki na baraka zako vilipo. Leo nimeamka vizuri nimewiwa kuandika uzi huu.

Wengi utotoni mnasikiliza mno wazee, mkishafika 35+ mnaona mnaweza kujiongoza, mnaacha na kuyapuuza mausia ya wazee wenu. Ni makosa makubwa sana.

Mnaitikia tu ila mioyoni mna mawazo yenu. Hakuna mzazi anayemtakiwa mabaya mtoto wake. Na Mungu mara nyingi anapitisha baraka kwa mtoto wa kiume hasa kupitia kwenye mausia ya mzee wake.

Yasikilize mausia ya mzee, na uyafanyie kazi. Usiishie kutikisa kichwa tu kinafiki ili akuone unamsikiliza. Yafanye na kazi pia.

Mzee wako amekuambia acha hiki fanya kile kwa sababu A, B, C. Acha usiwe mbishi, ukijua hakuna mzee anayemtakia mabaya kijana wake.

Nimefaidi vingi mno kwa kugundua hili. Na naendelea kufaidi vingi mno.

Usiyadharau mausia yake ukisema now mzee kazeeka sana na ameshaanza kupoteza kumbukumbu pamoja na uwezo wa kufikiri. Hakuna umri ambao hutakiwi kuacha hata nukta moja ya neno la mzee wako lianguke, kama wakati ambao ameshazeeka sana.

Uwe mtiifu. Kumtii mzee wako siyo kuendeshwa wala kupelekeshwa, bali unaongozwa kwenye nuru ya mafanikio yako. Usije kuona umekua! Usipuuze maneno yake hata herufi moja.

Mheshimu mno mzee wako!
 
Back
Top Bottom