Je, ilikuwa sahihi kwa Rais kuiasa hadharani familia ya Mzee Mwinyi isigombane?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,771
699,153
Maslahi ya mada,

1. Mzee Mwinyi alikuwa Mzee sana kiasi cha kutegemewa kufanya maamuzi yoyote! Kwa umri wake alikuwa kama mtoto akifanyiwa kila kitu.

2. Mzee Mwinyi alikuwa na wake wawili. Kama kuna familia za baba na mama mmoja watoto wanatofautiana na kugombana kabisa wazazi wanapofariki si jambo la ajabu kwa watoto wa familia za mitala.

Kwahiyo shida si migogoro bali chanzo chake, wahusika na namna ya kuitatua kupitia sheria ama watu wanaoaminika na kuheshimika.

Mzee Mwinyi alikuwa na wake wawili na watoto kwa kila mke. Kusema hakuna migororo ni kujidanganya kulikopitiliza. Inahitaji akili kubwa ufahamu wa kutosha na hekima kubwa sana mke mkubwa kuwapenda na kuwasaidia watoto wa mke mdogo na hapa hawezi kulaumiwa hata kidogo.

Migogoro mara nyingi huanzia kwenye vipaumbele kwa watoto na mgawanyo wa mali na majukumu ndani ya familia.

Migororo hii huwa ya wazi ama ya kimyakimya ndani ya familia kulingana na weledi, utashi na nafasi ya wazazi kwenye Jamii. Kuna watu kwa kujua ama kutojua huwa wa kwanza kuchochea migogoro hiyo.Wakidhani wanarekebisha kumbe ndio kwanza wanachochea moto.

Rais ni binadamu kama wengine si mkamilifu kama mimi na wewe lakini kuna vitu anapaswa kuwa navyo kuwazidi wengine wengi ili aweze kuimudu vema nafasi aliyonayo kijamii. Kwenye msiba wa Mzee Mwinyi kwenye hotuba yake rais kachochora kidogo na kuzua mijadala isiyokuwa na lazima.

Rais katuambia kwamba kwenye familia ya Mzee Mwinyi kuna migogoro na hataki kuisikia ikichachamaa huku akimtaka Hussein Mwinyi rais wa Zanzibar na mtoto mkubwa wa Mzee Mwinyi kwa mke mkubwa alisimamie hilo
Nje ya urais wa Hussein ni mtoto wa marehemu Mzee Mwinyi mwenye ndugu wa kuzaliwa na ndugu kwa mama mdogo.

Je, kwa nafasi yake ya pili ataweza kulimudu hilo? Je, Rais alipaswa kuliongelea hilo mbele ya kadamnasi?
 
Kwenye misiba, ndugu au viongozi wa ukoo wakipewa nafasi huwa wanaamua kutema nyongo hapo hapo, maana baada ya msiba kumalizika, kuwapata wahusika wote kwa pamoja huwa inakuwa ngumu kidogo maana unakuta wengine ni wakaidi, wakiitwa kwenye vikao hawaendi.
 
Hii sio mara ya kwanza ilishawahi kutokea siku za nyuma kwa familia ya Masaburi kuaswa the same. Sio vibaya kama kuna dalili za mgawanyiko wakiaswa live waliokuwa na nia mbaya ni rahisi kujirekebisha kwani issue iko public kuliko kuaswa kifamilia ukizingatia ni public family.
 
Kaka mkuu Jana nimenyewa kwangu na kupaua kinyes ukutan ni dalili gan iyo mkuu ama ndo nimechafuliwa nyota??
Na ndege gani au mnyama gani?
 
Back
Top Bottom