Maamuzi ya spika makinda juu ya Zitto

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), amegonga mwamba katika hatua yake ya kwanza ya utetezi dhidi ya madai mazito aliyoyatoa dhidi ya Baraza la Mawaziri, kwamba lilirubuniwa ili kutaka kuliua Shirika Hodhi la Mali za Mashirika ya Umma (CHC).

Spika wa Bunge la Tanzania , Anne Makinda jana alimbana Mbunge huyo, akisisitiza kuwa awe amewasilisha kwake vielelezo vya ushahidi kuhusu kauli yake hiyo ifikapo Jumatatu.

Kukwama kwa Zitto kunatokana na Spika Makinda kumgomea Mbunge huyo ambaye pia ni Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, kumwombea serikalini nyaraka alizotaka kuzitumia kutetea hoja yake hiyo, baada ya Spika kusema nyaraka hizo ni za siri.

Akitangaza bungeni mjini Dodoma, Spika Makinda alisema mara baada ya kumtaka Zitto kuwasilisha ushahidi wa kauli yake hiyo aliyoitoa bungeni Juni 23, Zitto alimwandikia barua akimwomba kumwombea serikalini nyaraka mbili ili azitumie katika ushahidi wake.

Spika alizitaja nyaraka alizoomba Zitto kuwa ni Waraka wa Wizara ya Fedha na Uchumi uliowasilishwa kwenye Kamati ya Makatibu Wakuu kuhusu CHC na Waraka uliowasilishwa kwenye Baraza la Mawaziri kuhusu CHC, akitumia kifungu cha 10 cha Kanuni ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.

“Taratibu za Baraza la Mawaziri ni za siri na haziwezi kutolewa hapa bungeni. Spika hawezi kumsaidia Mbunge ili aweze kupewa nyaraka hizi za Baraza la Mawaziri kwa vile ni za siri.

“Mheshimiwa Zitto alitamka hapa ndani ya Bunge, kwamba anao ushahidi wa kauli yake hiyo na hata baada ya mimi kumwonya, Mheshimiwa Zitto aliendelea kuzungumza kwa kurudiarudia kwamba ana ushahidi wa kauli hiyo.

“Kutokana na uhakika aliodai kuwa nao, nilimwagiza awe amewasilisha kwangu uthibitisho wa kauli yake hiyo. Sasa kwa vile yeye aliomba nimpe nyaraka hizo ambazo siwezi kumpa, naomba kumwongeza siku awasilishe ushahidi kwa njia zake mwenyewe hadi ifikapo Jumatatu, Julai 4,” alisema.

Spika alitoa mfano wa suala kama hilo ambalo lilitokea bungeni Julai mosi, 2008, ambapo aliyekuwa Mbunge wa Bukoba Vijijini, Nazir Karamagi (CCM), akiwa tayari amejiuzulu nafasi yake ya Waziri wa Nishati na Madini, alisimama bungeni na kudai kuwa kitendo cha Serikali kuiongeza muda Kampuni ya Upakiaji na Uondoshaji Kontena Bandarini (TICTS) kwa miaka mingine 15, kilifanywa na Baraza la Mawaziri.

Kutokana na kauli hiyo, Spika wa Bunge la 10, Samuel Sitta alimtaka Mbunge huyo kutoa uthibititisho kwamba alijuaje Baraza la Mawaziri ndilo lililoamua kuhusu suala hilo wakati yeye hakuwa Waziri wakati huo na wakati taratibu za uendeshaji wa Baraza la Mawaziri ni za siri, hatua iliyomfanya Karamagi kuonywa na Bunge.

Akiwa mchangiaji wa kwanza wa Azimio hilo lililowasilishwa bungeni Juni 23 na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, Zitto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mashirika ya Umma, alisema Azimio hilo liligeuzwa kutoka vile lilivyokuwa awali baada ya mawaziri kushawishiwa.

Hoja ya msingi ya Waziri Mkulo ilikuwa ni kuliomba Bunge kupitisha Azimio hilo ili CHC iongezwe kipindi cha mpito cha miaka mitatu, ili imalize majukumu yake na baadaye majukumu yake yahamishiwe Ofisi ya Msajili wa Hazina, lakini hoja hiyo ilikumbana na upinzani mkali kutoka kwa wabunge wa CCM na upinzani na hatimaye ikafanyiwa marekebisho.

“Mheshimiwa Spika, ndani ya Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma na hata katika Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, tulikubaliana kwamba CHC wapewe muda wa kutosha kukamilisha kazi na majukumu yao, halafu baada ya hapo Waziri alete Azimio hapa na si kuwapa kipindi cha mpito cha miaka mitatu kama Azimio lilivyowasilishwa leo.

“Nawaombeni wabunge wenzangu wote, tukatae uamuzi huu wa Baraza la Mawaziri kwa kuwa yametokana na kurubuniwa na watu wenye lengo la kuiua CHC kwa ajili ya maslahi yao. Ikumbukwe kuwa chombo hiki kinaangalia mali za umma na mashirika, hivyo kutaka kukiua na kupeleka majukumu haya kwa Msajili wa Hazina ambaye uwezo wake wa kulinda mali za umma ni mdogo sana, ni kutaka kuiba mali za Watanzania,” alisema Zitto.

Alisema Azimio la Serikali la kuipa CHC kukamilisha majukumu yake lililenga kusaidia wafanyabiashara walioiba mali za umma ikiwa ni pamoja na kukopa mabilioni ya fedha kutoka iliyokuwa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambao kesi zao ziko mahakamani, kupata ahueni kwa vile hatua hiyo itapoteza ushahidi.

Baada ya kueleza hayo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), George Mkuchika, aliomba Mwongozo wa Spika akitaka Zitto athibitishe kauli yake kwamba mawaziri walirubuniwa, kwa vile imewadhalilisha mawaziri hao ambao wanafanya kazi kwa maadili na kwa kuzingatia maslahi ya nchi.

Mkuchika alisema kitendo cha kusema uamuzi huo unatokana na kurubuniwa kwa mawaziri kinaleta picha mbaya kwa Watanzania ambao wamewaamini.

Baada ya maelezo ya Mkuchika, Spika alimtaka Zitto kuwa makini na kauli anazotoa anapochangia, ikiwamo ya kudai kwamba mawaziri wanashawishiwa na kurubuniwa; lakini Zitto aliposimama tena ili kuendelea kuchangia alitamka tena kuwa anao ushahidi kwamba mawaziri walikuwa wameshawishiwa na kurubuniwa hadi wakatengeneza Azimio hilo jipya.

“Mheshimiwa Spika, siwezi nikatafuna maneno hapa, nina uhakika na ninachokisema, uamuzi wa Baraza la Mawaziri ni matokeo ya ma-lobbyist (washawishi) na kama Serikali mnabisha, leteni hapa mapendekezo ya awali ambayo yaliwasilishwa katika Kamati ya Makatibu Wakuu na Baraza la Mawaziri ili tuone yalikuwa yanasemaje.”

Kutokana na msimamo huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi alimwomba Spika Makinda kumtaka Zitto awasilishe bungeni ushahidi kutokana na kauli yake hiyo, hatua iliyomfanya Spika kumpa Mbunge huyo muda wa kuandaa ushahidi huo na kuuwasilisha bungeni jana.

Shughuli zinazofanywa na CHC ambazo mpaka sasa hazijakamilika ni pamoja na urekebishaji wa TRL baada ya kampuni ya Rites kuondoka, kushughulikia uuzaji wa hisa za Serikali NBC (T) Limited, uperembaji na uhakiki wa vitendo na mashirika yaliyobinafsishwa, urekebishaji wa mashirika 34 yaliyobaki na kukamilisha ufilisi wa mashirika ya umma 24 yaliyobaki.

Pia ukusanyaji wa madeni ya iliyokuwa NBC yenye thamani ya Sh. bilioni 15.8 na urekebishaji wa kampuni ya TTCL baada ya hatua ya awali ya ubinafsishaji kushindikana na mwekezaji wa Airtel kuonesha nia ya kutoka kwenye ubia.
 
magamba wanaficha ushahidi kwa kisingizio cha siri, kama ni siri basi hakuna kesi kwa nini kujadili mambo ya siri?
huyu spika bwana yeye asema haya mambo ni ya siri lakini tena anataka yajadiliwe!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Mbona sasa wameishampatia Zitto utetezi?, Kuwa yeye ana ushahidi ila ni siri (Classified information) haziwezi kuwa halali kama zinakiuka sheria ya nchi. Mpeni Zitto adhabu muwaamshe wananchi walio na madukuduku yao kibao kuhusu hali ya maisha, mgao wa umeme. Mbona kila ushahidi ukiletwa mnaupotezea?, Lema hatujasikia kitu, Msigwa vilevile. CCM anayewapa strategy hizi anawamaliza. Kitendo cha kusema ni siri tayari umeshaweka wazi kuwa Zitto ana insider information, na mnataka alete classified information mumjengee hoja ya jinai.
 
Mbona sasa wameishampatia Zitto utetezi?, Kuwa yeye ana ushahidi ila ni siri (Classified information) haziwezi kuwa halali kama zinakiuka sheria ya nchi. Mpeni Zitto adhabu muwaamshe wananchi walio na madukuduku yao kibao kuhusu hali ya maisha, mgao wa umeme. Mbona kila ushahidi ukiletwa mnaupotezea?, Lema hatujasikia kitu, Msigwa vilevile. CCM anayewapa strategy hizi anawamaliza. Kitendo cha kusema ni siri tayari umeshaweka wazi kuwa Zitto ana insider information, na mnataka alete classified information mumjengee hoja ya jinai.

ni kweli zitto naye hakapige hiyo ni classified information wasije mzushia kesi kwa hiyo hawezi kuongelea issue hizo au la spika hatoe kibali kwanza hakito unamuomba tena ushahidi kwa kutumia hicho kibali
 
Mjini shule na hakuna siri katika dunia hii. Pamoja na spika Makinda kukataa kumsaidia Zito kupata hizo nyaraka akisema, "Waheshimiwa wabunge, kwa mujibu wa sheria, nyaraka za Baraza la Mawaziri ni siri; na hili liliwahi kuelezwa na Spika wa Bunge aliyepita Julai 2008 alipokuwa akizungumzia suala la TICS. Hivyo, ofisi yangu haiwezi kumsaidia Zitto kupata nyaraka hizo, ila namwongezea muda hadi Jumatatu Julai 4 mwaka huu, awe amewasilisha utetezi wake," Zito amefanikiwa kupata " photocopies" zote za vielelezo muhimu (ikiwemo waraka wa Baraza la Mawaziri) na kuwakilisha utetezi jioni ya tarehe 29/6/2011. Habari hizi zimethibitishwa na zito mwenyewe.


Chanzo. Gazeti la Tanzania Daima
 
Mjini shule na hakuna siri katika dunia hii. Pamoja na spika Makinda kukataa kumsaidia Zito kupata hizo nyaraka akisema, “Waheshimiwa wabunge, kwa mujibu wa sheria, nyaraka za Baraza la Mawaziri ni siri; na hili liliwahi kuelezwa na Spika wa Bunge aliyepita Julai 2008 alipokuwa akizungumzia suala la TICS. Hivyo, ofisi yangu haiwezi kumsaidia Zitto kupata nyaraka hizo, ila namwongezea muda hadi Jumatatu Julai 4 mwaka huu, awe amewasilisha utetezi wake,” Zito amefanikiwa kupata " photocopies" zote za vielelezo muhimu na kuwakilisha utetezi jioni ya tarehe 29/6/2011. Habari hizi zimethibitishwa na zito mwenyewe.


Chanzo. Gazeti la Tanzania Daima

Hii kama ni kweli poa sana!! Zitto amzidi Kete Mama Magamba
 
Chama cha magamba watasem ni za kugushi . teh teh teh . Hoja itaisha na zitto ataonywa teh teh teh
 
hoja itaisha ama ndo inapaswa kuanza upya? manake zitto akidhibitisha sasa maana yake ni kauli yake ifanyiwe kazi na hao warubuniwa wahusika! kama hoja inaisha ilikuwa haina maana yoyote kudhibitisha!

Chama cha magamba watasem ni za kugushi . teh teh teh . Hoja itaisha na zitto ataonywa teh teh teh
 
WanaJF, hapa kuna watu kuwajibishwa kama itaonekana kuna madudu yalifanyika which is obvious including JK mwenyewe!! ngoja tusubiri kuona lakini kwa vile nchi haina mwenyewe yataisha kimagamba!
 
Zitto, Lissu na Lema huyu bi kiroboto akitaka tu kuupotezea uthibitisho huu, mu mkomalie mpaka abwage manyanga yeye mwenyewe. Sasa hivi ana only one option, either hao mawaziri or yeye mwenyewe wabwage manyanga. Kunkoma nyani giladi.
 
Bibi kiroboto kabla ya kujadili ripoti ya zito atuletee kwanza ripoti ya lema juu ya mizengwe pinda kulidanganya bunge.
 
Why kwanini? Mama huyu jamani anapenda kuiingiza Serikali Matatizoni,Alipata ushauri juu ya kumuomba Zito kudhibitisha ushahidi huo.Du nampa pole sasa ITAKULA KWAKE AU KWA HAO MAWAZIRI husika.Na hii kama kawaida she always expanding the motion,tupo kuona next move.
 
Zitto , akitumia kifungu cha 10 cha Kanuni ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.

Mwenye hicho kifungu atuwekee hapa ili tuone nani anachemsha. HAKI, MAADILI NA MADARAKA
Kama nimemwelewa vizuri Makinda, kifungu hiki kinaruhusu bunge kupewa nyaraka za serikali, lakini kinachomtatiza spika ni kuwa nyaraka hizi ni za siri!
Nimsaidie kidogo: Mbele ya bunge hakuna siri ya serikali isiyoweza kuhojiwa na bunge vinginevyo wabunge hawatakuwa wawakilishi wa wananchi. Ikumbukwe kuwa wananchi ndio wenye mamlaka ya mwisho juu ya jambo lolote, na wawakilishi wao ni wabunge; hivyo serikali kulificha bunge kitu chochote, ni sawa na serikali kuwaficha wananchi jambo lolote. Je hiyo ni serikali kwa maslahi ya nani?
 
Wakati Spika wa Bunge, Anne Makinda, amemuongezea Mbunge wa Kigoma Kaskazni (Chadema), Zitto Kabwe, muda hadi Jumatatu ijayo, kupeleka uthibitisho kuhusu tuhuma alizozitoa bungeni dhidi ya Baraza la Mawaziri kwamba, lilirubuniwa katika kufikia maamuzi ya kuliongezea muda Shirika Hodhi la Mali za Mashirika ya Umma (CHC), wakati huo huo Spika Makinda alikataa maombi ya Zitto ya kumtaka amuombee kwa Katibu Mkuu Kiongozi nyaraka za siri kutoka Wizara ya Fedha na Baraza la Mawaziri ili aandae utetezi wake.

Zitto alitoa tuhuma hizo Juni 23, mwaka huu wakati akichangia mjadala bungeni kuhusu Azimio la Bunge la kuridhia kuongeza muda wa CHC.
Alisema uamuzi uliofikiwa na Baraza la Mawaziri wa kupendekeza CHC iongezewe muda wa uhai wa miaka mitatu na kisha kuhamishia majukumu yake kwenye Ofisi ya Msajili wa Hazina, ni matokeo ya kurubuniwa na wajanja aliowaita ‘Lobbyists' (washawishi). Kutokana na kauli hiyo, Spika Makinda alimuagiza Zitto kupeleka uthibitisho bungeni ifikapo jana, baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, kumuomba Spika amuagize Zitto kuthibitisha usemi wake, au afute kauli kuwa Baraza la Mawaziri lilirubiniwa.

Hata hivyo, Spika Makinda jana aliliambia Bunge kuwa Juni 23, mwaka huu, Zitto alimuandikia barua akimueleza kuwa ili aandae utetezi wake, anaomba amuombee kwa Katibu Mkuu Kiongozi nyaraka mbili. Nyaraka hizo ni waraka kutoka Wizara ya Fedha na kujadiliwa na Kamati ya Kiufundi ya Makatibu Wakuu (IMTC) kuhusu CHC na waraka wa Baraza la Mawaziri kuhusu shirika hilo. "Mheshimiwa Kabwe Zitto alinieleza kuwa anafanya hivyo kwa kutumia kifungu cha 10 cha Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge sura ya 296," alisema Spika Makinda. Hata hivyo, alisema kwa uelewa wake ni kuwa nyaraka zilizoombwa na Zitto ni za siri na kwamba, haziwezi kutolewa.

Spika Makinda alisema Bunge pia liliwahi kuarifiwa hivyo na Spika wa Bunge la Tisa, Samuel Sitta, Julai Mosi, 2008. Alisema Bunge liliarifiwa hivyo wakati Sitta alipokuwa akitoa uamuzi kuhusu suala la aliyekuwa Mbunge wa Bukoba Vijijini (CCM), Nazir Karamagi, kuhusu madai yake kuwa uamuzi wa kuongeza muda wa mkataba wa Kampuni ya Kupakia na Kupakua Mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam (TICTS) ulifanywa na Baraza la Mawaziri. "Hivyo, ofisi yangu haiwezi kumsaidia Mheshimiwa Kabwe Zitto kupata nyaraka alizoomba," alisema Spika Makinda.

Hata hivyo, Spika Makinda alisema kwa kuwa Zitto wakati anachangia mjadala huo bungeni siku hiyo, aliongea kwa kurudia na kusisitiza kuwa ana uhakika na alichokuwa anakisema, anaamini kuwa anaweza kuleta uthibitisho kwa njia anazozijua yeye. "Hivyo, uamuzi wangu wa kumtaka alete uthibitisho upo palepale, isipokuwa nimemuongezea siku hadi Jumatatu tarehe 4 Julai afanye hivyo," alisema Spika Makinda. Aliongeza: "Kwa hiyo maelezo haya yametolewa leo tarehe 29 na Mheshimiwa amepewa barua inayohusika."

Huu utakuwa ni uamuzi wa pili wa Spika Makinda kutaka mbunge awasilishe ushahidi wa anayozungumza bungeni tangu ashike wadhifa huo mwaka jana baada ya uchaguzi mkuu. Mbunge mwingine ambaye alitakiwa kuwasilisha ushahidi ni wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, ambaye alitakiwa kuthibitisha kwamba Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema uongo bungeni katika mkutano wa tatu wa Bunge uliofanyika Aprili. Lema alitakiwa kuwasilisha ushahidi huo baada ya kuwa ameomba mwongozo wa Spika hatua anazoweza kuchukua mbunge atagundua kuwa kiongozi mkubwa kama Waziri Mkuu analidanganya Bunge.

Kutokana na kauli hiyo, Makinda alikuwa mbogo na kumkaripia Lema, akionyesha kukerwa na kauli yake, kisha akamtaka kuwasilisha ushahidi kuwa Waziri Mkuu Mizengo alikuwa amelidanganya Bunge alipokuwa akijibu maswali ya papo kwa papo juu ya kadhia ya mauaji ya Arusha ya Januari 5, mwaka huu. Lema alikwisha kuwasilisha ushahidi wake kwa Spika Makinda, lakini hadi leo (Spika) tangu Aprili hajataka kuuwasilisha bungeni ili ukweli ujulikane.

ZITTO AWASILISHA MAELEZO KWA SPIKA

Katika hatua nyingine, Zitto jana alithibitisha kuwasilisha kwa maandishi maelezo yake kwa Spika Makinda kuthibitisha kuwa Baraza la Mawaziri lilishawishiwa wakati wa kufanya maamuzi hayo. Aliliambia NIPASHE jana jioni kuwa aliwasilisha maelezo hayo ya kurasa nne pamoja na vielelezo kuthibitisha kauli yake na kwamba anasubiri maamuzi ya Spika.

Chanzo: Nipashe
 
Back
Top Bottom