Maamuzi ya spika makinda juu ya Zitto

Sidhani kama nyaraka za serikali huwa zinaombwa kwenye ofisi ya bunge,hii ni mihimili miwili ambayo inajitegemea,nadhani kuna kitu ameomba hapo bungeni kinachousiana na bunge!jaribu kufikiri zaidi,punguza ushabiki!!

Zitto haya mambo anayajua, sasa alitaka kumbabaisha tu huyu mama, sasa na yeye amembana sehemu mbaya , hawezi tena kupumua, hapo inabidi amuombe msamaha tu ! Hizi nyaraka hawezi kuzipata hata kwa mtutu
 
Sidhani kama Zito kupigwa ban ni mara ya kwanza lakini angalia lisijewaumbua kama lile la buzwagi lilivyokuja kuwatokea puani. Logic inaonesha wazi kuwa kuna namna maamuzi hayo yalivyofikiwa. Hata kama vielelezo havitatolewa wenye akili wameshapata ujumbe na mda utatueleza kulikoni.

Mama safari hii hatishiwi nyau, ban kwa zitto safari hii haiepukiki, aende akaandae maandamano vizuri, au ndio anatafuta umaarufu hivyo huyu kijana
 
Kama ni nyaraka kutoka kwenye kikao cha baraza la mawazi, imekula kwake maana huwa wanaapa kabisa kutunza siri za baraza la mawaziri. Hapo kijana ana kazi...
Zikipostiwa hapa JF hizo minits za kikao utasemaje? Usichokonowe wa2
 
Zitto ameingia choo cha kike safari hii, nyaraka alizokuwa anazitaka ni siri, haiwezekani mtu km yeye kuzipata, asubiri rungu tu la Bunge !
when the dove cry......... kweli gin's brain at work, how many times do you want to see public documents online to believe that hakuna siri serikali ya ccm coz it is a system movement??

tic tac...
 
Zitto ameingia choo cha kike safari hii, nyaraka alizokuwa anazitaka ni siri, haiwezekani mtu km yeye kuzipata, asubiri rungu tu la Bunge !

na ikiwa hivyo basi kimbunga cha OPERESHENI SANGARA kwa ajili ya 2015 safari hii ni hapa dodoma, kanda ya kati, lindi, kilwa, mtwara na songea kule kwenye wateja wa CCM..

CCM hata hata mikipewa majibu hamfaulu
 
Hakuna nyaraka za siri,JF iki amuwa zinapatikana na zitawekwa hapa live,cha muhimu ni kujua ni aina gani ya nyaraka zinatakiwa,hii ndio JF bana
 
Kama ni nyaraka kutoka kwenye kikao cha baraza la mawazi, imekula kwake maana huwa wanaapa kabisa kutunza siri za baraza la mawaziri. Hapo kijana ana kazi...

Kwani nyaraka hizo ni za baraza la mawaziri, na hao mawaziri wapo kwa ajili gani. Je serikali nini, na kwa ajili ya nani? kazi ya mbunge ni kufanya nini
kama utajua au utaweza kujibu maswali haya utakujua kuwa kama bunge ni wajibu wao kuhoji hata ikibidi kupewa hati yoyote hata kama ina siri gani.

Kwa kifupi ni kupe ndondo za kufuatilia ni kwamba "seikali imewekwa na wananchi na wabunge wamechanguliwa na wananchi kuidhibiti serikali" ki misingi mmbunge anadhamana kubwa kwa wananchi kuliko kiongozi wa serikali soma maana na chimbuko la serikali. ( Soma social contract ni kitu gani).
 
Kama ni nyaraka kutoka kwenye kikao cha baraza la mawazi, imekula kwake maana huwa wanaapa kabisa kutunza siri za baraza la mawaziri. Hapo kijana ana kazi...

mhh...hilo siamini! cabinet minutes documents zina siri gani unless ni national security matters? Na sehemu ya bunge ni ipi kama haliwezi kufanya kazi yake?
 
Wadau huyu mama kamlazimisha Zitto kuthibitisha kauli yake ya malobbist huku akimnyima nyaraka za serikali alizoomba. Ivi sheria inasemaje juu ya nyaraka za serekali kupatikana pale mbunge anapozihitaji hasa kwanufaa ya nchi??

Hizo nyaraka nadhani Makinda kisha zisoma na anajua zitto akizitia mkononi siku hiyo hiyo zitabandikwa Jf na itakuwa ni muumbuko wa aina yake kuanzia kwa makinda hadi baraza la mawaziri kwa ujumla. mpaka Zitto anaziomba anajua kilichomo ndani yake. Mimi naona ni simple tu kama makinda anazuia kutoa hizo document basi na zitto atatoa pingamizi la kunyimwa uhuru wa kutoa ushahidi. Sidhani report ya mawaziri ktk isue zinazohusu mali za watanzania kama ni siri kiasi kwamba mbunge akiomba kwa utaratibu sahihi eti asipewe. kama wao wanaona hazitokuwa kikwazo kwao kwanini wasizitoe? ni aibu kwa Tanzania chombo nyeti cha kutoa maamuzi kumkabidhi mwanamke. kama zitto angekuwa ameomba nyaraka za jeshi hapo sawa tungeona kweli wasimpatie lakini za mawaziri kuhusu tuhuma? mimi sijamuelewa makinda kama anaongoza bunge kwa hisia au kwa sheria
 
Hiyo ndio kazi aliyotumwa na magamba wenzie lkn ngoja tu mungu yuko nasi na freedom is coming tomorow
 
Back
Top Bottom