Maamuzi ya Prof Ndalichako yanashangaza

Maamuzi ya Prof Ndalichako yanashangaza

Nilishasema toka awali kua huyu mama anakurupuka sana watu wakapinga vikali. Mpaka hapa sijaona mwelekeo wa mafanikio kwa uwepo wa huyu mama Wizara ya Elimu. Wizara ya ELIMU sio NECTA, sio taasisi ndogo! Hii wizara ndio moyo wa nchi.

Sijui mwaka huu vyuo vikuu vingapi vitakavyopokea wanafunzi wa fani za Sayansi. Utaratibu wa kizamani sana huu.
Nasikia Prof ni mwl. Na kama ni mwalimu, basi apitie notice zake za undergraduate, aone juu ya kitu kinachoitwa multipple intelligent kwa mwanafunzi. maana sio kila mwanafunzi anaweza sayansi au art. lakini pia asisahau juu ya broom taxonomy domains za kujifunza, ndiyo maana ni vigumu Diamond kusoma zaid ya mziki
 
nampongeza kwa maamuzi hayo; dunia ya sasa ni ya sayansi na technology, tutapata wapi wanasayansi kama watoto tokea chekechea wanamezeshewa kuwa sayansi ningumu,mara ooh ! pcm/pcb unakuwa kichaa : ni maamuzi mwafaka ingawa yamechelewa:kumbukeni tuna upungufu wa wataalamu wa sayansi mf. walimu zaidi ya 7816na zaidi pia upungufu wa wauguzi, madaktari , waandisi,
 
pia ni kwanini waalimu wawpangie wanafunzi masomo kwa lazima bila hat wanafunzi kuchagua. wasiwaaribie future watoto na wadogo zetu. ni vyema shule zipewe hiyo oda ya serikari mapema sana
 
Binafsi naona km kuna wakati Serikali hufanya jambo kwa kusudi fulani, kumlazimisha mwanafunzi asome asichokitaka/asichokiweza ni sawa na kumlazimisha afeli kwa upande mwingine ni kuzalisha wajinga toka mashuleni badala ya waerevu. Matamko ya Profesa ni kujitia upofu, anataka kujifanya hajui kuwa masomo ya sayansi kutofanya vizuri ni kutokana na uhaba wa walimu wa masomo hayo pamoja na ubutu wa waliopo, kwanini asishauri Serikali kuandaa kwanza walimu wa Sayanse wenye uwezo wa kutosha na ushawishi kwa wanafunzi? Kingine, baadhi ya walimu wa shule za msingi na sekondary ni wale waliofeli ktk malengo ya elimu waliyoitaka na wakaamua kujitupia/kujiweka ktk Uwalimu kukabiliana na maisha ila nia yao haikuwa hiyo. Kwa dhamira kbs nafikiri kuna sababu za msingi Serikali kuamua kuvurugavuruga elimu kila wakati kwa madhumuni fulani. Ukimwansha alielala utalala wewe.
 
Wewe unadhani changamoto ya idadi ndogo ya wahitimu wa Sayansi itaanza kuondolewa vipi, pamoja na incentive za mikopo kwa wanafunzi wa Science chuoni ila bado vijana wanaogopa Sayansi, lazima serikali itafute njia za kutengeneza nguvu kazi bora ya kizazi kijacho, iwe kwa kuburuzwa baadhi yetu au kwa majadiliano.
Tatizo sio kuwa hakuna wanafunzi wa kusoma ualimu wa sayansi, tatizo vyuo vikuu nyetu ndio havifundishi walimu wa sayansi, hebu tizama tumaini saut cbe ekenford hao ndio wanatoa 80% ya walimu na wote ni walimu wa book keeping history na kiswahili, tuanze hao kuwaambia wadahili na walimu wa sayansi, sasa kumfundisha mtoto somo ambalo halina mwalimu ni kuongeza idadi ya zero tu.
 
The Boss na katika hii global village tunahitaji watu watakao weza ku communicate effectively kwa Kiingereza tukiwa kama moja ya nchi za jumuiya ya madola, tunahitaji malawyer wazuri wakuweza kusimimia mikataba ya rasilimali zetu, sasa kama nguvu zote zikitupwa kwenye physics na chemistry huko kwingine tutaendelea kuumizwa.
Hivi aliyekuambia kwenye sayansi hakuna sheria ni nani? Serikali imesema wanafunzi wasome masomo yote; sayansi na Sanaa hadi kidato cha 4. Baada ya hapo michepuo itaendelea. Lengo la serikali ni kubadili hadhi ya sasa ambapo wanafunzi wanaomaliza kidato cha 4 wengi wao wanakuwa wamesoma masomo ya sanaa na lugha na wachache wao wanakuwa wamesoma sayansi.
Sheria siyo taaluma inayojitegemea, It is simply cross-cutting course of knowledge/discipline/faculty. Kama inavyotakiwa kwa uandishi wa habari, Mwanasheria anatakiwa asome kwanza basic course/faculty katika ngazi ya shahada ya kwanza, halafu asome sheria katika masters level. Baada ya kupata uhuru nchi ilitaka wanasheria (administrative lawyers/criminal justice kwa ajili ya administration of justice. Hiyo ndiyo sababu kuanzisha degree ya sheria. Ni bahati mbaya kwamba licha ya mambo mengi yamebadilika, mfumo huu wa kufundisha framework badala ya sheria, umeendelea kuwepo bila mabadiiko. Na hii ndio maana kila wakati tumekuwa tukiambiwa nchi haina wanasheria wa kuchambua mikataba ya madini, mafuta, gesi na kadhalika. Inatakiwa mtu asome shahada kuhusiana na core faculty (madini/gasi/mafuta/misitu nk) aelewe content husika kisha baadaye a-specialise na kubobea katika sheria inayohusu discipline fulani. Vivyo hivyo kwa uandishi wa habari. Wanasheria na waandishi wa habari wetu wako watupu hasa (content paucity) kutokana na mfumo wetu wa university training of lawyers/journalist. Katika nchi zilizoendelea huwezi kukuta mtu anasoma eti shahada ya kwanza sheria au uandishi wa habari. Inatakiwa kwanza mtu apate content (faculty) mahsusi halafu baadaye asome skills za sheria/unadishi wa habari katika competent knowledge yake. Nadhani hili limeeleweka.
 
Wengi mmeona habari ya leo kuwa sasa ni lazima wanafunzi wote wasome Sayansi kabla ya hiii zimekuwepo habari nyingi za kushangaza za wizara hii ya elimu. Siku Magufuli aliposema anashangaa fimbo kupigwa marufuku mashuleni, kesho yake tu Wizara hii ikatangaza 'fimbo kurudishwa mashuleni'
yaani halikuwa na mjadala wala kutolewa maelezo labda why fimbo zilizuiwa mwanzo au kuna watalaam gani walihusika kufikia maamuzi.

Halafu yakaja maamuzi ya kuongeza ufaulu ili kujiunga na vyuo, hili nalo limechukuliwa kama Tanzania ni kisiwa vile mpaka sasa wala hakuna maelezo iwapo mwanafunzi wa kitanzania akipata nafasi kusoma nje ya nchi kwa ufaulu ambao hapa nchini haumruhusu, vyeti vyake vitakuwa na 'status' gani hapa nchini mradi maamuzi ya wizara hii sasa ni kama vile Tanzania ndo 'The world'
na kila atakachoamua yeye ndo 'final'

Huyu mama na Mabosi zake wanasahau kuwa tuko katika 'global village' Maamuzi ya ajabu ajabu sanasana yatawaathiri watoto wa masikini tu
wengine wenye options za kusoma nchi jirani na nchi za mbali hayatawagusa na mwishowe watakao 'umizwa na maamuzi' haya ni watoto wa masikini.Sasa hili la lu kulazimisha Sayansi nalo unajiuliza nchi ngapi duniani linatumika?

Je mtoto wa kitanzania akisoma Kenya au Uganda au kwingineko
ambako hakuna 'maamuzi ya aina hii' huyu mama atafanyaje? Hivi why 'tuna invest kwenye kuongeza kero na vizingiti' vya kila aina kwa watanzania? Kwani Tanzania ni kisiwa? Si masuala ya elimu yanapaswa kuwa 'Universally acceptable'? Sasa huyu mama ndo mifano wa maprofessa wetu?
adhabu ya viboko haikuwahi kuondolewa mashuleni.kilichofanyika ni kuitolea maelekezo juu ya namna bora ya kumshughulikia mwanafunzi kwa viboko kuepuka madhara yasiyo na msingi.
 
Mpaka miaka mitano iishe tuombe uhai tu tutashuhudia maamuza ya ajabu zaid ya haya
 
Wengi mmeona habari ya leo kuwa sasa ni lazima wanafunzi wote wasome Sayansi kabla ya hiii zimekuwepo habari nyingi za kushangaza za wizara hii ya elimu. Siku Magufuli aliposema anashangaa fimbo kupigwa marufuku mashuleni, kesho yake tu Wizara hii ikatangaza 'fimbo kurudishwa mashuleni'
yaani halikuwa na mjadala wala kutolewa maelezo labda why fimbo zilizuiwa mwanzo au kuna watalaam gani walihusika kufikia maamuzi.

Halafu yakaja maamuzi ya kuongeza ufaulu ili kujiunga na vyuo, hili nalo limechukuliwa kama Tanzania ni kisiwa vile mpaka sasa wala hakuna maelezo iwapo mwanafunzi wa kitanzania akipata nafasi kusoma nje ya nchi kwa ufaulu ambao hapa nchini haumruhusu, vyeti vyake vitakuwa na 'status' gani hapa nchini mradi maamuzi ya wizara hii sasa ni kama vile Tanzania ndo 'The world'
na kila atakachoamua yeye ndo 'final'

Huyu mama na Mabosi zake wanasahau kuwa tuko katika 'global village' Maamuzi ya ajabu ajabu sanasana yatawaathiri watoto wa masikini tu
wengine wenye options za kusoma nchi jirani na nchi za mbali hayatawagusa na mwishowe watakao 'umizwa na maamuzi' haya ni watoto wa masikini.Sasa hili la lu kulazimisha Sayansi nalo unajiuliza nchi ngapi duniani linatumika?

Je mtoto wa kitanzania akisoma Kenya au Uganda au kwingineko
ambako hakuna 'maamuzi ya aina hii' huyu mama atafanyaje? Hivi why 'tuna invest kwenye kuongeza kero na vizingiti' vya kila aina kwa watanzania? Kwani Tanzania ni kisiwa? Si masuala ya elimu yanapaswa kuwa 'Universally acceptable'? Sasa huyu mama ndo mifano wa maprofessa wetu?
Nitakujibu kuhusu fimbo mashuleni, Corporal Punishment Act ya mwaka 1972 inayoruhusu mtoto kuadhibiwa kwa viboko hajawahi kufutwa wala kurekebishwa ili kuondoa adhabu ya viboko. Kama liliwahi kutokea naomba kurekebishwa.
 
Anasema eti kuelekea Tanzania ya viwanda Sayansi ni lazima
nimejiuliza USA na China huko kote walilazimisha wanafunzi wote kusomea Sayansi?
au hii yetu ni 'ubunifu mpya'?
Kwa walimu wanajua fika kwamba si kila mwanfunzi anaweza kusoma sayansi kama mitaala ilivyo. labda tubuni mitaala mingine na kuboresha huduma ya elimu vinginevyo ni ndoto na ni shida kwa walimu
 
Lakini pia, jambo hili lilihitaji wadau toka sekta ya elimu kulijadili, naona ameamua tu na bosi wake na inakuwa amri, upuuzi mtupu.

Serikali ya awamu ya tano haina muda wa kujadili kitu. Atakachosema rais kinakuwa sheria hapohapo.
 
The Boss

Nchi hii hatuhitaji wanasiasa pekee ili kusonga mbele... Vipi kuhusu Wanasheria, vipi kuhusu Waalimu wa masomo ya Sanaa..


Nafikiri serikali ingeangalia namna ya kumpunguzia mwanafunzi mzigo.. Kuna umuhimu gani wa mwanafunzi kusoma masomo ya Sayansi kisha kidato cha tano anaenda Sanaa???


Hiyo ni mfano michache hapo sijagusia upatikanaji wa rasilimali za kuwezesha hao watoto.

SERIKALI imetangaza mwongozo mpya kuwa kuanzia sasa masomo ya sayansi ni lazima kusomwa na wanafunzi wote wanaosoma elimu ya sekondari kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne.
 
Nchi imepandikizwa uoga hakuna awezae kuhoji
Wafanya kazi wanaishi kwa hofu
Wananchi wanaishi kwa hofu
Wanafunzi wanaishi kwa hofu
Utazan tuko utumwani nani atahoji na ni nani atamtetea mwenzie
Inaumakuona kura za wananchi zinawatesa wenyewe
 
Huyu mama mwanzoni niliona kama anaweza kuwa msaada ktk hii sekta ya Elimu lkn naona anaelekea kule kule kwa kina Mungai


Mimi mwanangu namuandaa kuwa Mwanasheria. Kwanini nimsumbue na Physics na Chemistry,?


Kwanini asikomae na masomo yake.
 
Back
Top Bottom