Maamuzi ya Prof Ndalichako yanashangaza

Maamuzi ya Prof Ndalichako yanashangaza

Ingawa bandiko lako umelijaza Kiingereza bila ya sababu za msingi kuna hoja hapa umeianzisha naona na mimi nichangie. Kwenye mfumo wetu wa kufundishia darasani kuna tatizo kidogo. Mwalimu inaaminika anajua kila kitu wakati mwanafunzi anachukuliwa ana ubongo ulio wazi wa kujazwa kila kitu toka kwa mwalimu. Aina hii ya ufundishaji iko mpaka kwenye vyuo vyetu vikuu.

Wanafunzi wengi wanaosoma masomo ya mchepuo wa sanaa wanafeli zaidi kuliko wale wanaosoma masomo ya mchepuo wa sayansi, na sababu yake ni rahisi kueleweka. Masomo ya Mchepuo wa Sanaa ni rahisi lakini mitihani yake ni migumu wakati masomo ya sayansi ni magumu lakini mitihani yake ni rahisi. Na ndiyo maana mara nyingi wanaoshika nafasi kumi za kwanza kitaifa kwa Mitihani ya Kidato cha Nne na cha Sita huwa wanatoka kwenye mchepuo wa Sayansi.

..Miaka niliyosoma mimi "top cream" walikuwa wanakwenda kusoma science.

..hawa walikuwa wanafaulu masomo yote hata ya biashara, lakini kwasababu wanajiweza kimasomo walikuwa wanakwenda mkondo wa science.

..wanafunzi waliokuwa hawajiweza ndiyo walikuwa wanajaza mkondo wa biashara.

..siku zote wanafunzi wa mkondo wa science ndiyo walikuwa wakiongoza ktk matokeo ya kidato cha 4. Na walikuwa wanafanya vizuri hata ktk masomo kama history n geography kuwazidi wenzao wa mkondo wa biashara.

..ila tulipokwenda high school wanafunzi wa biashara na arts walikuwa na matokeo mazuri ya form 6 kulinganisha na wanafunzi wa science.

..miaka yetu mwanafunzi mwenye div
2 ya arts ilikuwa hawezi kujiunga Udsm kwa shahada ya sheria. Lakini div 2 wa science alikuwa anaweza kujiunga na shahada ya uhandisi.
 
walimu wengi ni wa jiografia na historia sasa hiyo physics atafundisha nani? Tungeanza kwanza kuviambia vyuo vikuu vyetu vidahili walimu wa sayansi zaidi ili uamuzi utakapofanyika pawepo walimu wa kufundisha.
Ni kweli kuna upungufu wa walimu na upungufu wa facilities, ila je hii ndio sababu ya kutofanya uamuzi sahihi. Kulazimisha wanafunzi wasome basic Sayansi baada ya muda itaongeza idadi ya wahitimu wa Sayansi. Kama nchi tuna upungufu mkubwa wa madaktari, wahandisi na walimu wa Sayansi, tusitegemee bila ya jitahida za maksudi tutatatua matatizo yetu.
 
Hivi kuna mtaala unaoeleweka unaotumika????

Vile vitabu vinavyotumika siku hizi mashuleni walishapitia kuona maajabu yake?

Hizo maabara zipo za kutosha?????

Walimu wapo wa kutosha?????


Vitabu na vitendea kazi vingine???




Kazi ipo aisee.......


Kazi sio ndogo
Tanzania yetu mtu akishaitwa tu Proffesa au Waziri tunamuacha afanye anavyotaka
ndo huyu mama sasa....
 
Tena mwenyewe kakili hata walimu hawapo. Sioni mantiki ya uamuzi huu. Utaratibu uliokuwepo uendelee. Unaweza kumpeleka ngombe mtoni lakini siyo kumlazimisha kunywa maji.
 
Itakuwa imesaidia nini kama wataacha baada ya kidato cha NNE????
Sio wote wataacha, idadi ya wanafunzi wataoendelea na michepuo ya Sayansi itaongezeka, hicho ndio cha muhimu. Hivi tunategemea kweli kama nchi kuendelea tukiwa na idadi ndogo ya wahitimu wa Sayansi, ni jukumu letu wazazi kuwashauri au kuwashawishi vijana wachukua michepuo ya Sayansi zaidi pale tunapoona wana uwezo huo.
 
Hayo ni maono yako kuwa itaongezeka,mimi naona haitongezeka na zaidi sifuri zitazidi.
 
Tena mwenyewe kakili hata walimu hawapo. Sioni mantiki ya uamuzi huu. Utaratibu uliokuwepo uendelee. Unaweza kumpeleka ngombe mtoni lakini siyo kumlazimisha kunywa maji.
Unadhani bila kulazimishana ni lini tutakuwa na walimu wa kutosha wa Sayansi, acheni vijana wasome basic Science, baada ya kipindi kirefu tutaweza kuanza kutoa wahitimu wengi wa Sayansi, changamoto zipo ila kila kitu kina mwanzo.
 
Hayo ni maono yako kuwa itaongezeka,mimi naona haitongezeka na zaidi sifuri zitazidi.
Ndugu, binafsi nimekutana na wanafunzi wengi tu wanaoacha masomo ya Sayansi kidato cha pili kwa kuwa tu kuna kuchagua ila bado wana uwezo wa kuendelea na kuyamudu masomo ya Sayansi, hawa ukiwalazimisha hadi kidato cha nne ni kitu kizuri. Ingawaje kuna ambao Sayansi ni baba mkwe tangu kidato cha kwanza, hawa wataishia kupata F za Physics tu, hii itakuwa collateral damage tu.
 
Tunahitaji mwanzo mzuri,uliondaliwa.
Wewe unadhani changamoto ya idadi ndogo ya wahitimu wa Sayansi itaanza kuondolewa vipi, pamoja na incentive za mikopo kwa wanafunzi wa Science chuoni ila bado vijana wanaogopa Sayansi, lazima serikali itafute njia za kutengeneza nguvu kazi bora ya kizazi kijacho, iwe kwa kuburuzwa baadhi yetu au kwa majadiliano.
 
kuhusu wanafunzi wote kusoma sayansi naunga mkono
 
Inamaana hatuhitaji tena wachumi, wanasheria, wanahabari etc, wote sayansi?
 
1470595305097.jpg
 
Back
Top Bottom