Maamuzi ya NEC ya CCM na Hatima ya Spika Sitta

Maamuzi ya NEC ya CCM na Hatima ya Spika Sitta

Huyo jamaa wa Dodoma simshangai maana uchaguzi karibu sasa asipo wahi kukampeni kwenye upande unaokamata vyombo vya dola anaweza na anaogopa kupigwa dafrau ,huyo ametunga shabaha ya mbali kabisa 2010 ,hana jingine.

Ila kama Sitta anataka kujibu mapigo hayo anayo fursa ya kumpeleka mahakamani mpumbavu huyo kwa kumchafulia jina na kumuhusisha na kosa kubwa kabisa ambalo hukumu yake ni kuuwawa na zaidi pia amdai fidia ka ya bilioni moja hivi,tuone kama hakupata swine flu ,ila kwanza ampeleke kupimwa akili isije kuwa anapeleka wakichaa mahakamani
 
Kama wale wabunge wanaopambana na ufisadi watasalimu amri mbele ya vitisho vya mafisadi basi utakuwa ndio mwisho wa maisha yao ya kisiasa.

Kusalimu kwao amri watakuwa wamesaliti wananchi na hivyo hawataungwa mkono tena na wananchi na wakati huo huo wao kwa sasa hawakubaliki na kundi la mafisadi. Therefore surrender will be their own political assasination. Therefore the only survival of critical MPs is to carry on their fight against curruption and corrupt leaders
 
Wazo langu ni kwamba, hata kama agenda ni mbovu kama kutafuta ngazi ya kufika mbinguni, bado ufahamu wa mwenyekiti ni kitu muhimu sana! Kama Mwenyekiti ni hoi kikao kitaamua yasiyoeleweka na watu watazungumza kama vichaa na kushangiliwa.

JK ana lawama ZOOTE.

Kwanini unampa lawama JK wakati hao wenyeviti wa mikoa wamechaguliwa na wanachama mikoani?

Katiba ya CCM ibara 108(8) inasema wazi kuwa NEC ina kazi ya kuchunguza lawama kuhusu viongozi na inaweza kuwafukuza uanachama au kurudishia uanachama mtu. Na kama kulikuwa na watu waliotoa malalamiko kuhusu spika, NEC ilikuwa ni chombo muhimu na mwenyekiti anachotakiwa ni kuendesha tu mikutano.
 
Napenda mufahamu kuwa NEC haikuwatisha wabunge wa NEC peke yake bali imewatisha wabunge wa Tanzania nzima na hiyo inamaanisha kauli za wananchi wanazowatuma wabunge wao kuihoji serikali hazitakiwi kuonekana katika maeneo ya anga za bunge ,kwa maana hiyo WaTanzania wote wamenyamazishwa au wamefungwa midomo yao kupitia tiketi za wabunge.
Huu ni udikteta wa aina yake ambao unatumiwa eti vikao vya siri ,siri gani hiyo ,mnakaa mkidanganyana kuwa mnafanya vikao vya siri, niliwahi kusema kuwa siri siku hizi ni biashara kubwa hivyo kila mkijifungia dau linaongezeka na ndio kama mnavyoona kuwa habari zipo nje na nyingine zishaandikwa magazetini ,je mnalo la kulificha ?

CCM msijidanganye wakati wa ukoloni wa kutawaliwa na wazungu na waarabu umepita na ndio hivyo hivyo kutawaliwa kikoloni na rangi nyeusi hakutakubalika ndani ya jamii ya WaTanzania ambao wamechawanyika dunia nzima na sasa wanaelewa ni namna gani mambo yanatakiwa yawe na vipi utawala unatakiwa ufanye na usipofanya wananchi nini wakifanye.

Zama za kuwa na siri za Chama tawala zimepita huu ni mfumo wa vyama vingi kama nyinyi mnavyotumia mashushu kuwasimika ndani ya vyama vya upinzani na kuwalipa donge nono ndivyo hivyo vyama vya upinzani vinavyosimika watu wao ndani ya CCM tena huku upinzani mashushu hata hawataki kiasi kikubwa saa ingine hurusha tu na kusema hiyo ya leo, Hivyoachaneni na msemo wa kusema mnafanya vikao vya siri huko ni kujidanganya,mnadanganyana wenyewe kwa wenyewe,vikao hivyo ndivyo vinavyowapeleka mbali na kufanya vitendo visivyo vya kibinadamu dhidi ya wenzenu au wananchi kama mlivyofanya Pemba 2001.

Ila wale viranja wa vikao hivyo wajue tu siku likilipuka watakuwa hawana tena pa kufanyia vikao vya siri isipo kuwa mahakamani.
 
Tanzania hakuna demokrasia bali kuna ubabe, hakuna amani bali kuna woga na hakuna sababu ya kuwa bunge.
Wabunge wanaingia bungeni kutetea masilahi ya nchi na wananchi walio wachagua hivyo wanapaswa kuwa huru na wala si kutishiwiwa na serikali husika. Na kama wanatishiwa sasa kuna umuhimu gani wa kuwa na bunge ambalo ni mzigo kwa wananchi?. Inaonesha wazi NEC ina nguvu kuliko bunge, kuliko serikali na kuliko mahakama. Hatuna haja ya kuwa bunge kwani ni vichekesho vya hali ya juu.

Ushauri wangu kwa wabunge wa CCM ambao wanaungana na sisi katika kupinga ufisadi ni jambo la busara na hekima kukihama chama hicho haraka ili wawe huru kupinga ufisadi huo.

Kwa sasa kila chama kiwe na bunge lake ili kuweza kujadili maada kwa uhuru na kweli. Maana inaonesha wazi kwamba bunge lilipo litashindwa kujadili baadhi ya maada kwa faida ya CCM na serikali iliyopo madarakani.
 
Ni kweli wabunge ni wawakilishi wa wananchi kule bungeni,lakini ili uwe mbunge ni lazima uwe mwanachama wa chama fulani kutoka na katiba ya jamhuri ya muungano.

Unapokuwa Mwanachama maana yake umekubali kwa dhati imani, malengo na katiba ya hicho chama ulichojiunga nacho,na kuilinda kwa moyo wako wote na lazima uape kufanya hivyo.

Kwa CCM, Chombo kama CC,NEC na mkutano mkuu ,kamati za siasa ndiyo vyombo vinavyosimamia utekelezaji wa kanuni na katiba yake,na nidhamu ya chama na mwanachama.

Hivyo kama wewe ni mwakilishi wa wananchi kupitia CCM unabudi kutekeleza katiba na maazimio ya vyombo hivyo vya juu vya CCM.
kama huwezi unajiengua, unaweza kwenda chama chochote halali cha siasa na kufichua uozo wa chama tawala ukiwa uhuru kabisa.

Ndani ya CCM au chama chochote Maadili na nidhamu ya chama lazima zifuatwe,kwani chama si kundi au genge la wahuni.

Hata kwenye familia zetu mtu ambaye hafuati nidhamu na maadili ya familia,binafsi anipishe kwenye nyumba yangu niendele kusimamia nidhamu na maadili ya familia yangu.

Napenda kushauri ni jambo jema kuwawakilisha wananchi kwenye maendeleo kama mwakilishi wao lakini nidhamu na maadili ya chama kilichopewa au kukupa ridhaa ya kuwawakilisha ni vyema ikalindwa kwa nguvu zote na kuheshimiwa.

Huu ndio utaratibu uliyobora kabisa.

Taratibu za kuwachuluia mafisadi,watendaji wa serikali waovu zipo tumejiwekea wenyewe ni vyema zikafuatwa.

Kama chama Tawala kinashindwa kutuleta maendeleo uamuzi tunao sisi wananchi wa kuona ni chama kipi kitaleta maendeleo ya kweli kwetu sisi.

Swali najiuliza kwani wawakilishi wetu wamekuwa wakali kipindi kuelekea uchaguzi mkuu mwakani,misije ikawa ' old wine in a new bottle'
 
- Wakuu tupo pamoja sana, simu zote za wale wanaoshukiwa kunipa dataz inmefahamika kwamba zinasikilizwa, kwa hiyo nina-work on another way ya ku-receive dataz,

- Lakini as soon as nikiiweka sawa ninazimwaga hapa, nia na madhumuni ni kuweka wazi majina ya viongozi wote waliowasaliti wananchi kwenye hiki kikao na walischokisema, subira yavuta heri wakuu!

Respect and Later!

Field Marshall Es!
 
- Wakuu tupo pamoja sana, simu zote za wale wanaoshukiwa kunipa dataz inmefahamika kwamba zinasikilizwa, kwa hiyo nina-work on another way ya ku-receive dataz,

- Lakini as soon as nikiiweka sawa ninazimwaga hapa, nia na madhumuni ni kuweka wazi majina ya viongozi wote waliowasaliti wananchi kwenye hiki kikao na walischokisema, subira yavuta heri wakuu!

Respect and Later!

Field Marshall Es!

FMES!!!

This is what Tanzanians needs, brave hearts to address what they believe and fight for....

Usichoke kwani nia ni kusaidia wale ndugu zetu wasio na watetezi ilhali keki ya Tanzania ni yetu sote na si ya wachache wanaofaidi kwa niaba!
 
- Wakuu tupo pamoja sana, simu zote za wale wanaoshukiwa kunipa dataz inmefahamika kwamba zinasikilizwa, kwa hiyo nina-work on another way ya ku-receive dataz,

- Lakini as soon as nikiiweka sawa ninazimwaga hapa, nia na madhumuni ni kuweka wazi majina ya viongozi wote waliowasaliti wananchi kwenye hiki kikao na walischokisema, subira yavuta heri wakuu!

Respect and Later!

Field Marshall Es!


Kwa jambo la siri hutakiwi kabisa kutumia namba yako and your usual handset!!! Kinachofanyika uwe na handset separate na hiyo ya kwako na namba tofauti tofauti, angalao kwa sasa ambako bado mchakato wa kuziandikisha unafanyika, it works out. Baadaye kidogo itakuwa ngumu kwa simu but angalao njia mbadala zipo!!!

I hope wahusika hawatawashughulikia watoa habari, easy to trace kama wamerecord mawasiliano!!!
 
bora sasa wanafki ambao mlifikiri kikwete anachukia ufisadi..sasa mmeona akipambana na wanaoutokomeza ufisadi..
 
Magazeti yetu bwana! Yanafanana kabisa na wale waliomfungulia mashtaka ya MAUAJI ACP Zombe na wenzake huku hawana ushahidi. Hizo milioni 50 aligawiwa nani?


Waligawiwa kina Kusila, Mgeja, Guninita na wenzao ndio maana waliongea utumbo mtupu!
 
- The message kwa wapiganaji iko wazi kabisa na hiki kikao, kwamba waache ile tabia yao ya kujichekesha chekesha na mafisadi, yale mambo ya kualikana nao kwenye sherehe zao, they should stop now,

- Kwa sababu Kusila anawakilisha ideas za mabosi wake, kwamba wakipata their way watawafunga wapiganaji wote kwa kesi ya uhaini, sasa eti unataka kualikana kwenye sherehe na watu wa namna hii ambao wako radhi kukufunga maisha kwa kesi ya uhani, just because unasema aginst ufisadi wao wka wananchi?

- Ninyi wapiganaji, just think about this for a minute!

Respect.

FMEs!
 
Kwanini unampa lawama JK wakati hao wenyeviti wa mikoa wamechaguliwa na wanachama mikoani?

Katiba ya CCM ibara 108(8) inasema wazi kuwa NEC ina kazi ya kuchunguza lawama kuhusu viongozi na inaweza kuwafukuza uanachama au kurudishia uanachama mtu. Na kama kulikuwa na watu waliotoa malalamiko kuhusu spika, NEC ilikuwa ni chombo muhimu na mwenyekiti anachotakiwa ni kuendesha tu mikutano.

Je, mwenyekiti anapocheka hovyo wakati hoja za kipumbavu zinapotolewa nalo ni juumu lake!
 
- Wakuu tupo pamoja sana, simu zote za wale wanaoshukiwa kunipa dataz inmefahamika kwamba zinasikilizwa, kwa hiyo nina-work on another way ya ku-receive dataz,

- Lakini as soon as nikiiweka sawa ninazimwaga hapa, nia na madhumuni ni kuweka wazi majina ya viongozi wote waliowasaliti wananchi kwenye hiki kikao na walischokisema, subira yavuta heri wakuu!

Respect and Later!

Field Marshall Es!

Naheshimu sana juhudi zako na kukupongeza za kupambana na na ufisadi uliokithiri ndani ya nchi yetu na chama tawala. Fuatilia hizo data na ukishakuwa na uhakika zako basi tuwekee bandiko hapa. Hawa mafisadi ndani ya CCM na Serikali walidhani watatunyamazisha Watanzania pamoja na ushahidi wa kutosha kwamba nchi inayumba kutokana na kutokuwa na uongozi sasa watajuta kwa juhudi zao za kutaka kuwakumbatia mafisadi.
 
- Wakuu tupo pamoja sana, simu zote za wale wanaoshukiwa kunipa dataz inmefahamika kwamba zinasikilizwa, kwa hiyo nina-work on another way ya ku-receive dataz,

- Lakini as soon as nikiiweka sawa ninazimwaga hapa, nia na madhumuni ni kuweka wazi majina ya viongozi wote waliowasaliti wananchi kwenye hiki kikao na walischokisema, subira yavuta heri wakuu!

Respect and Later!

Field Marshall Es!

haya baba!tunasubiri.
ubarikiwe sana!
 
Nothing last ever , mwandishi mmoja alisema yana "mwisho haya" na sasa dalili za mwisho wake ndio zinaanza kujitokeza. Viongozi wa hicho chama kilichobatiza na kuubariki umaskini wa watanzania walio wengi wakati wao wakila "maziwa na asali" wameshindwa kusoma harama za nyakati. Bado wanafikiria watanzania ni walewale wa enzi za ujima, mimi naamini asilimia kubwa ya watanzania wanapata hizi taarifa ambazo zinawaumiza sanaaa!!! na kuzipima.
 
Mkuu FMES

Heshima Mbele ...

Yaani maneno yako yamenipa ugonjwa tayari na nimeshachangayikiwa na nimeogopa sana.

Tuawaachie watawale na wanaweza amua watakavyo kila wakitaka..

Wameshaamua...mie nilishakata tamaa!

inanikumbusha kisa cha nchi ya mandondocha iiliyoongozwa na watu wabinafsi wenye mtandao mkubwa zaidi ya ule wa majambazi..inafanana na hii
 
nimemwona chiligati asubuhi tbc anabwabwaja!Lol!nimesikia kutapika
 
kweli ukombozi unakaribia sana, nikizingatia maneno na msimamo wa Kada Mpinzani, FMES na sasa Gembe ninaambini hata Kibunango, Nnauye, Mwawando nk hawa ni CCM wa hapa JF, au kwa maneno mengine ni watetezi wa CCM. Sasa tutafakari kwa pamoja je kunauwezekano wa kuisafisha CCM? bora tuunge mkono chama mbadala.

Natoa wito kwenu akina Sikonge, Mtanzania na CCM wote hapa JF, ni vigumu almost impossible kutenganisha CCM na ufisadi. Come on guys, tuikomboe nchi yetu. Tambua kuwa CC na NEC wameshatoa azimio kwamba Kinana na wenzake wakutane na wabunge wote na kuwaambia shhhh!!! so, nothing will come from either Mwakyembe or Kilango which is critic to our dictatorship like government.
 
Hii CCM sasa naona imeshageuka kuwa jamvi la wasusi,coz kila ujinga unaoongewa unatukuzwa without kujali kuwa unapoteza dira ya chama,watu kama hawa hawapo real sisi tunawaita vimbaumbau,na hizi ndio zile sampuli za wanaotegwa kwa mchele,hawatofautiani na kuku!!
"Hypocrites are every where,but being hypocrite is what creates hatre"
 
Back
Top Bottom