Maamuzi ya NEC ya CCM na Hatima ya Spika Sitta

Maamuzi ya NEC ya CCM na Hatima ya Spika Sitta

Jamani ......huyu KUSILA si ndio yule MLEVI ambaye hata familia yake imemshinda...sasa atawezaje kutoa hoja ya maana...anachosubiri yeye ni huruma tu na kujipendekeza ili aweze kubebwa ukizingatia kwa sasa KAFULIA. Huyu ni machafu sana na hafai kabisa katika kusaidia taifa hili. Ni bora apoteleee huko aliko. WAPIGA KURA WAKE NINAWAHURUMIA...ZERO hamna kitu.

Wadau twaomba data zake huyo....
 
Hakika hii game ni ngumu sio mchezo....Hivi Watanzania tutaendelea kuhujumiwa na viongozi wa namna hii hadi lini? mtu ukitetea maslahi ya wananchi wako unaonekana ni Muhaini?
 
- Wakuu wote JF, heshima iwarudie ninasema hivi tuna silaha moja tu hapa JF nayo ni keyboards zetu, ninajaribu kila njia tena arround the clock kuyaanika wazi majina ya viongozi wetu wote waliozungumza ndani ya hiki kikao na pumba zao against wananchi, soon tutakuwa na more pumbas!

- Kuna watu wa Muungwana wanaonitumia ujumbe kwa pembeni toka niiweke hii, kwamba eti Rais alikuwa anapima upepo na kutaka kujua nani ni nani katika safu ya mafisadi kwa hiyo I am being unfair kumshambulia, ninasema hivi that is the most political nonsense I ever heard, Rais anatakiwa kufahamishwa na Usalama Wa Taifa in advance kinachoendelea ndani ya hili taifa. Hapa pia nina ujumbe kwa wapiganaji, na hasa Mzee Mengi yale maneno yenu ya kila wakati kwamba eti Rais anajitahidi sana kupigana na mafisadi mnahitaji kuyaacha maramoja, tena ninasema now!

Wakuu baadaye, tuna dataz zaidi zinazohitaji kwanza uthibitisho and then zitamwagwa hapa JF kumkoma nyani kama kawa!, maana I mad as a hell!

Respect.


Field Marshall Es!
 
Hii ni Ilani/taarifa ya chama tawala CCM kwa wananchi wa Taifa linalokumbatia vyama vingi vya siasa.

Nadhani umefikia muda mwafaka kurudisha rasmi mfumo wa chama kimoja. Maana karibia taarifa yote hiyo ni maoni executive ya kijamaa pale nchi inapokuwa kwenye crisis. Hakuna consensus baina yake na vyama vingine kisiasa.
 
Wajumbe wengi wa kikao hicho wanajiuliza swali moja muhimu, kwamba kwa nini Rais aliruhusu kutokea kwa yote yaliyojiri kwenye hiki kikao?
[/U] [/COLOR]

1. If a wrong man uses a right means, then the right means work in the wrong directions.
-Chinese proverb.
2. Mtu mwenye akili akikupa mawazo ya kipumbavu huku akijua kuwa wewe una akili na ukayakubali, basi atakudharau.
-J.K. Nyerere
3. Ukimuona mtu anakimbilia kwenda Ikulu tena kwa kutumia vijipesa kidogo, huyo ni wa kumuogopa kama ukoma.
-J.K. Nyerere
4. Every man's work is a portrait of himself.
-Jose Ortega Gasset
5. The Presidents hardest task is not to do what is right but to know what is right.
-Lyndon Johnson
6. The trouble with the rat race is that even if you win you are still a rat.
-Lily Tomlin
7. You can be sincere and still be stupid.
-Charles F.Kettering
8. People who know the very least seem to know the loudest.
-20th Century proverb
9. Nearly all men can stand adversity, but if you want to test a man's character, give him power.
-Abraham Lincoln
10. The way the wind blows, that's the way the grass bends.
-Confucius
Nachukia siasa kwa sababu inaleta hasira........!Maanake unaweza kumchapa mtu vibao....!
 
Last edited:
CCM rasmi imeitumbikiza Tanzania kwenye mgogoro wa kikatiba na haya shime watz hasa wana JF tusikubali hali hii dhalili iendelee,na ikiwezekana na sisi tutoe"waraka wetu wenye miongozo mingi" kupinga kutishwa kwa Spika na wabunge wote wa CCM.

Katiba ya Tanzania inaeleza kwa uwazi kabisa mipaka na mamlaka ya Bunge na kiongozi wake yaani Spika;HAMNA sehemu kwenye katiba inayosema kuwa "Spika akiruhusu wabunge wa chama tawala waeleze ukweli kuhusu MADHARA ya ufisadi basi ashtakiwe ama kwa uhaini au akihurumiwa basi afukuzwe uanachama",hii ni kejeli kubwa kwa demokrasia,na nakiri sijawahi ishuhudia ktk nchi yeyote ile yenye utawala BORA zaidi ya hapa Tanzania!

Sheria mama ya Bunge inaeleza wazi kuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kulishambulia bunge na mamlaka yake akiwa nje ya bunge,sheria inasema kuwa hata mbunge anatakiwa alishambulie bunge akiwa bungeni tu;na ni mwiko kwa mtu yeyote pia kupinga,kujadili na kudharau jambo ambalo tayari bunge limekwisha lipitisha na kulitolea ufafanuzi,na ukifanya hivyo unaweza fungwa jela kwenye mahakama halali za kikatiba;sasa huyu Mwenyekiti wa CCM-Shinyanga mzee Mgeja yeye sio mbunge,hii nguvu ya kulitolea ufafanuzi hata kumsimanga Spika kwa jambo lililojadiliwa na kupitishwa kihalali na wabunge kama hili la ufisadi wa Richmond amepata wapi?

Kauli ya Mzee William Kusila,ambaye ni Mwenyekiti wa CCM-Dodoma na mbunge wa jimbo la Bahi ndiyo limenishangaza zaidi!Kusila kwa nguvu alizonazo za ubunge alipaswa kulisemea jambo hili kwenye vikao halali vya bunge,lkn akakaa kimywa na hata akakubali Richmond ijadiliwe tena mwezi Novemba,iweje sasa amshambulie Spika?

JF as a great thinker institution;we need to react as soon as possibe on this senseless mayhem,na ikiwezekana na sisi tutoe tamko rasmi na kulipeleka kwenye jumuiya za kimataifa hasa mabalozi wa nchi za Ulaya-Magharibi,Canada na USA; sehemu ambazo kwa utafiti wangu wa haraka haraka CCM huwa wanaogopa sana!

Wamefanya mambo mengi sana mabaya kwa watz,lkn hili la kulishambulia,kulitukana,kulikejeli na kulidhalilisha bunge na Spika wake tusiache lipite hivi hivi,Naam wanazuoni wote wa JF tujipange kwa hili jambo lisilo la kidemokrasia !
 
Taarifa Rasmi: Kuhusu Kikao Cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM

Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imefanya Mkutano wa kawaida tarehe 16-17 Agosti, 2009 chini ya Uenyekiti wa Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

Katika mkutano huu Halmashauri Kuu imejadili masuala mbali mbali kuhusu hali ya kisiasa nchini, maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa, zoezi la uboreshaji wa daftari la wapiga kura, pia imefanya uteuzi wa wagombea katika nafasi mbalimbali.

Baada ya kujadili masuala hayo, Halmashauri Kuu ya Taifa imefanya maamuzi yafuatayo:-

1. MAANDALIZI YA UCHAGUZI
(a) Serikali za Mitaa
Halmashauri Kuu ya Taifa imepitisha ratiba ya CCM kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa; kwa mujibu wa ratiba hiyo muda wa kuchukua na kurudisha fomu kwa wagombea wa CCM kwa uongozi wa Vitongoji, Serikali za Vijiji na Mitaa ni toka tarehe 10/8/2009 hadi 20/8/2009.
Halmashauri Kuu ya Taifa imetoa wito kwa wana CCM na wapenzi wa CCM katika ngazi ya Vitongoji, Vijiji na Mitaa wajiandae kushiriki kwa ukamilifu katika mchakato wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu kwa kuzingatia ratiba ya CCM na pia ratiba ya wasimamizi wa Uchaguzi huu (TAMISEMI).

Aidha, Halmashauri Kuu ya Taifa imewahimiza wana CCM na wapenzi wa CCM wajitokeze kujiandikisha katika orodha ya wapiga kura kuanzia tarehe 4/9/2009 hadi 25/9/2009 na kwamba muda ukiwadia wajitokeze kuwapigia kura wagombea wa Chama Cha Mapinduzi hapo tarehe 25/10/2009.

(b) Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura - Pemba

Halmashauri Kuu ya Taifa baada ya kupokea taarifa kuhusu zoezi la uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura Kisiwani Pemba, imetoa wito kwamba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ihakikishe zoezi hilo linasimamiwa kwa makini, na liendeshwe kwa haki na kwa utulivu; na kwamba Serikali ya Mapinduzi ihakikishe kwamba kila mwenye haki na sifa ya kujiandikisha anapata haki hiyo, na wale wasio na sifa wasiruhusiwe kujiandikisha.

Kimsingi zoezi hili sharti liendeshwe kwa kuzingatia sheria ya Uchaguzi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na sio vinginevyo.

2. KUONGEZA IDADI YA WANAWAKE KATIKA VYOMBO VYA UWAKILISHI

Halmashauri Kuu ya Taifa imetafakari upya mapendekezo yake ya awali kuhusu utaratibu wa kuongeza idadi ya wanawake katika Bunge la Muungano na katika Baraza la Wawakilishi. Mapendekezo mapya ni kama ifuatavyo:-

<!--[if !supportLists]-->(a) <!--[endif]-->Kwamba kwa kuwa idadi ya Wabunge wote kwa mujibu wa Katiba Ibara ya 66(1)(b) ni 249, viti asilimia arobaini (40%) itengwe kwa ajili ya wanawake, yaani viti 100.

<!--[if !supportLists]-->(b) <!--[endif]-->Kwamba ukomo wa viti Bungeni ubaki 360, hivyo pendekezo hili litaongeza idadi ya viti kutoka 323 vya sasa hadi 349, na vitabaki viti 11 kufikia ukomo wa viti (360) Bungeni. Hali hii inawezesha Tume ya Uchaguzi kuongeza idadi ya majimbo mapya 11.

(c) Utaratibu wa asilimia 40 utakapotumika utawezesha kupatikana kwa Wabunge Wanawake 100 kwa viti maalum pekee, idadi ambayo ikijumulishwa na wa kuchaguliwa ambao kwa sasa ni 18, watano wa kuteuliwa na wawili kutoka Baraza la Wawakilishi, tutapata Wabunge wanawake 125. Kiwango hiki ni sawa na asilimia 50 ya Wabunge wote waliotajwa kwenye Ibara ya 66(1) (b) ya Katiba.

(d) Ili kufikia lengo la kupata wabunge wanawake 50%, wanawake hawana budi kushindana kwa bidii katika majimbo. Kwa hali hii Halmashauri Kuu ya Taifa imeagiza CCM katika ngazi zote zifanye uhamasishaji wa Wanawake wengi kwenda kugombea katika majimbo ya uchaguzi mwaka 2010 ili kuongeza Wabunge zaidi ya 18 waliopo hivi sasa.

3. UTEUZI WA WAGOMBEA UENYEKITI WA WILAYA

Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, imepitisha wana CCM walioomba kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CCM katika Wilaya za Rorya, Tarime na Arumeru.

Nafasi za Tarime na Rorya zimetokana na kugawanywa kwa wilaya ya Tarime na kuwa wilaya mbili na ile ya wilaya ya Arumeru imetokana na kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Wilaya hiyo, Ndugu Lucas Lobulu aliyefariki Mei 6, 2009.

Waliopitishwa kugombea nafasi hizo ni:-

Wilaya ya Arumeru
Ndugu Jeremiah Saruni Kaaya
Ndugu Gabriel Kilale Nnko
Ndugu Joseph Ole Loning’o Saivoiye

Wilaya ya Tarime
Ndugu George Mkama Chacha
Ndugu Bogomba Rashid Chichake
Ndugu Peter Keba Wangwe

Wilaya ya Rorya
Ndugu Leonard Yodal Ambonya
Ndugu Jomoko Mjee Kateti
Nyanganira

Wilaya husika zitafanya uchaguzi kwa ratiba itakayoandaliwa baadaye.

4. CHAGUZI NDOGO BUSANDA, MAGOGONI NA BIHARAMULO

Baada ya Halmashauri Kuu ya Taifa kujadili tathmini ya chaguzi ndogo katika majimbo ya Busanda, Magogoni na Biharamulo, imewashukuru na kuwapongeza wale wote waliofaikisha ushindi wa CCM katika Uchaguzi mdogo wa Majimbo ya Ubunge ya Busanda (Mwanza) na Biharamulo Magharibi (Kagera) pamoja na Uchaguzi mdogo wa Uwakilishi wa Jimbo la Magogoni, Zanzibar.

Aidha, Halmashari Kuu pia imetoa pongezi za dhati kwa wana-CCM, wapenzi wa CCM na wananchi kwa ujumla kwa ushindi waliokipatia Chama Cha Mapinduzi katika chaguzi hizo ndogo za Ubunge, Uwakilishi na za Udiwani katika Kata 10 za Tanzania Bara.

Kutokana na ushindi huo, kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa kiliwaomba wana-CCM, wapenzi wa CCM, wakereketwa na wananchi kwa ujumla kuendelea kukipa ushindi Chama Cha Mapinduzi ili kiendelee na majukumu ya kumkomboa Mtanzania na kudumisha amani na utulivu.

5. MAHAKAMA YA KADHI

Halmashauri Kuu ya Taifa imeridhika na hatua zinazochukuliwa na Serikali za kulipatia ufumbuzi suala la Mahakama ya Kadhi Tanzania Bara. Moja ya hatua hizo ni uundaji wa Kamati ya mazungumzo baina ya viongozi wa dini ya Kiislam na Serikali kuhusu mchakato wa uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi nje ya mfumo wa Serikali.

Aidha, Halmashauri Kuu imesisitiza kwamba iwapo wapo Waislam wanaona haki zao hazikamiliki bila ya kuwa na chombo cha aina hiyo, wasizuiliwe. Waruhusiwe kuanzisha Mahakama ya Kadhi wao wenyewe na Serikali isijihusishe kuiendesha mahakama hiyo kwani kwa kufanya hivyo itakuwa imejiingiza katika shughuli za kidini; na kwamba Mahakama hiyo isihusike na kesi za jinai wala madai, bali ihusike na masuala ya ndoa, talaka na mirathi.

6. WARAKA WA BARAZA LA MAASKOFU (RC)

Baada ya Halmashauri Kuu ya Taifa kuzingatia waraka wa Maaskofu, na hasa malumbano na hisia tofauti zilizojitokeza kuhusu waraka huo, imeelekeza kwamba viongozi wakuu wa nchi wafanye mazungumzo na viongozi wa dini zote ili kutafuta njia tulivu ya kusafisha hali ya hewa na kujenga umoja na utengamano katika jamii yetu.

7. MALUMBANO YA VIONGOZI

Kuhusu tabia iliyozuka hivi karibuni ya baadhi ya Wabunge, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Viongozi wa Chama kutoa matamshi hadharani yenye mwelekeo wa kuchafuana majina, na yanayoashiria kuvunjika kwa umoja na mshikamano ndani ya CCM na Serikali zetu, na pia yenye mwelekeo ya kudhoofisha muungano wetu, Halmashauri Kuu ya Taifa pamoja na kukemea vikali tabia hii, imetoa maagizo yafuatayo:-

i. Kwamba kuanzia sasa viongozi wote wa CCM warejee katika nidhamu ya Chama ya kuzungumzia masuala ya Chama katika vikao rasmi vya Chama na sio vinginevyo.

ii. Kamati za Wabunge wa CCM, na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa CCM zitumike kujadili masuala yahusuyo CCM ndani ya vyombo hivyo.

iii. Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar watumie taratibu zilizopo katika kushughulikia kero za Muungano badala ya kufanya kwa suala la mafuta kwa upande wa Zanzibar.

iv. Viongozi watakao vunja maadili haya watakuwa wamejibainisha kwamba hawana nia njema na CCM, na watahesabiwa ni wasaliti wa CCM hivyo Chama hakitasita kuwapa adhabu kali, ikiwa ni pamoja ya kuvuliwa uongozi na hata kufukuzwa katika Chama.

v. Halmashauri Kuu ya Taifa imetoa wito kwamba mapambano dhidi ya rushwa na maovu mengine ni jukumu la wana CCM wote na raia wema wote kwa mujibu wa Katiba ya CCM Ahadi 4 ya WanaCCM. Halmashauri Kuu ya Taifa imeonya kuhusu dhana inayojengeka kwamba vita dhidi ya rushwa na ufisadi inahusu kikundi kidogo tu cha wana CCM, usahihi ni kwamba vita hii ni ya wana CCM wote kwa mujibu wa Katiba ya CCM vita hivi lazima iendelee kuhusisha wana CCM wote na wananchi wote wenye mapenzi mema na nchi yetu.

vi. Kwa kutambua kuwepo matatizo ya matamshi na vitendo visivyoridhisha katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi, Halmashauri Kuu ya Taifa imeamua kuunda Kamati Ndogo ya kutafuta undani wa matatizo hayo na kupendekeza kwa Kamati Kuu njia za kuyatatua. Aidha, Kamati hiyo pia itaangalia utendaji kazi wa Kamati za Chama katika Bunge na Baraza la Wawakilishi kwa nia ya kubaini upungufu uliopo ili kupendekeza kwa Kamati Kuu kuhusu njia za kurekebisha. Pia, Kamati itaangalia masuala ya uendeshaji wa shughuli za Bunge na Baraza la Wawakilishi na kushauri namna ya kuimarisha, pale panapostahili.

vii. Kamati hiyo itaongozwa na Mzee Alli Hassan Mwinyi Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Wajumbe wengine ni Mzee Pius Msekwa Makamu Mwenyekiti CCM (Bara) na Ndugu Abdulhaman Kinana.

8. KUHESHIMU VIONGOZI WASTAAFU

Halmashauri Kuu ya Taifa imewakumbusha wana CCM, Viongozi na Watanzania kwa jumla kuhusu umuhimu wa kudumisha utamaduni wa kuwaheshimu na kuwaenzi viongozi wastaafu, hususan Marais wastaafu.

Aidha, Halmashauri Kuu ya Taifa imesikitishwa sana na hali iliyojitokeza Bungeni ya kutoa maneno ya kejeli dhidi ya Mzee Benjamin W. Mkapa, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu.

Halmashauri Kuu ya Taifa imesisitiza kwamba Mzee Mkapa katika kipindi chake ameliongoza Taifa letu kwa ufanisi mkubwa, aliinua hali ya uchumi, aliendeleza miundombinu, aliendeleza huduma za kijamii hasa elimu, afya, maji na kwa jumla alilijengea heshima kubwa Taifa letu.

Mzee Mkapa anastahili pongezi sio kejeli, anastahili heshima na sio dharau, anastahili kuenziwa na sio matusi.

Kwa kuzingatia hayo, Halmashauri Kuu ya Taifa inatoa wito kwa wana CCM na Watanzania wote wenye nia njema na nchi yetu waache mara moja kumchafua na kumkejeli Mzee Mkapa na badala yake apewe heshima anayostahili na aachwe apumzike kwa amani.

UTEUZI WA MAKATIBU WAPYA WA MIKOA

Halmashauri Kuu ya Taifa imewateua wafuatao kuwa Makatibu wa Mikoa:-

Ndugu Sauda Mpembalyoto (Katibu wa Wilaya ya Hai)
Capt. (Mst) Frarten Kiwango (Katibu wa Wilaya ya Kibaha Mjini)

Hawa wanajaza nafasi zilizoachwa wazi na Ndugu Amina Makilai aliyekuwa Katibu wa Mkoa wa Pwani na sasa ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa UWT, pia Ndugu Salum Msabah aliyekuwa Katibu wa Mkoa wa Kigoma na sasa amerejeshwa Makao Makuu ya CCM kuongoza Kitengo cha Propaganda.

UCHAGUZI WA MJUMBE WA NEC KUPITIA JUMUIYA YA WAZAZI

Nafasi hii iliachwa wazi na marehemu Richard Nyaulawa na ilikuwa inawaniwa na wagombea watatu.

Kutokana na kura za wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa aliyechaguliwa ni Ndugu Jasson Rweikiza aliyepata kura 88.

Wengine waliogombea nafasi hii ni Ndugu Ramadhani Maneno kura 85 na Ndugu Sifa Swai kura 46.

Imetayarishwa..(CCM Website)
11:50:20 17.08.2009


Ripoti ya vikao vya CCM haitoagi kila kitu kwa vile wao kila kitu ni siri tu kwa sababu ya ufisadi.
 
8. KUHESHIMU VIONGOZI WASTAAFU

Halmashauri Kuu ya Taifa imewakumbusha wana CCM, Viongozi na Watanzania kwa jumla kuhusu umuhimu wa kudumisha utamaduni wa kuwaheshimu na kuwaenzi viongozi wastaafu, hususan Marais wastaafu.

Aidha, Halmashauri Kuu ya Taifa imesikitishwa sana na hali iliyojitokeza Bungeni ya kutoa maneno ya kejeli dhidi ya Mzee Benjamin W. Mkapa, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu.

Halmashauri Kuu ya Taifa imesisitiza kwamba Mzee Mkapa katika kipindi chake ameliongoza Taifa letu kwa ufanisi mkubwa, aliinua hali ya uchumi, aliendeleza miundombinu, aliendeleza huduma za kijamii hasa elimu, afya, maji na kwa jumla alilijengea heshima kubwa Taifa letu na kuandika Ilani kama hapo juu kama mwongozo wa Taifa.

Mzee Mkapa anastahili pongezi sio kejeli, anastahili heshima na sio dharau, anastahili kuenziwa na sio matusi.

Kwa kuzingatia hayo, Halmashauri Kuu ya Taifa inatoa wito kwa wana CCM na Watanzania wote wenye nia njema na nchi yetu waache mara moja kumchafua na kumkejeli Mzee Mkapa na badala yake apewe heshima anayostahili na aachwe apumzike kwa amani.

Kuna kesi kadhaa za wala rushwa na watumiaji wabaya ya madaraka. Watuhumiwa hawa wote ni viongozi au walikuwa viongozi wa ngazi za juu kabisa katika Taifa letu. Karibia kesi zote zinapigwa danadana tu ndani ya Taifa linalosema linajali utawala wa sheria. Madhambi waliyofanya wengine wanastahili kifungo cha maisha kwa uhujumu wa Taifa letu.

Viongozi hawa, baadhi yao walistaafu tu baada ya madudu yao kuanza kuanikwa wazi, lasivyo wangeendelea kuwa viongozi wetu. Kweli mnakaa chini na kuweka maoni kama haya kwa vile tu tuna utamaduni wa kuheshimiana na kujaliana kama Watanzania, basi kiongozi automatically anakuwa anaheshimika?! Mtu/Kiongozi anaheshimika kutokana na utu wake na heshima yake kwa Taifa. Kulazimisha watu wawaheshimu viongozi/binadamu kwa vile tu walikuwa viongozi itatufanya tufike kwenye wakati ambapo tutakuwa tunawapigia magoti wakina-Hitler na akina Milo&#353;evi&#263; wa Kibongo. Haya mambo ya kulindana-lindana pale watu wanapofanya madudu na kumbumbuluka yamejengeka vichwani mwetu na tumeyafanya miongoni mwa fikra zetu kuu, na ndiyo haya yanatufikisha kwenye kupiga kwata nyuma-mbele bila mwelekeo ndani ya bonde la kashfa na kuandika miongozo kama hii kwa Taifa.
 
Hivi vikao vya level ya juu kiasi hicho ni uswahili au ni nini?? Tunategemea hawa ndiyo watoe dira ya Chama kutupeleka mbele kuhakikisha maisha bora kwa kila mtanzania??? Wabadilishe waandike maisha bora zaidi kwa mafisadi!!!! Hata hivyo sishangai sana kutegemea mambo ya kutumia brain kwa usanii unaojulikana!!! Si mnapenda sura eehhhh!!! Inayouzika kwa porojo za kishwahili uswazi ehhhh!!!!! Kwa kawaida kila mkulima atavuna alichopanda!!! Ndicho tulichovuna 2005!!!! Sasa tumlaumu nani??? Jibu ni rahisi, wapiga kura katika level zote, uteuzi na mwishowe kura kwa viongozi wenyewe na wananchi!!! |Je 2010 angalao kwa upande wa wananchi wameshahamasishwa vya kutosha??? Hapana!!!! Tutaendelea kurudia makosa hadi pale tutakapoamua kuamka usingizi wa pono!!! Ni lini?? Sina jibu!!!

Who is/was serios there!??? Inatisha!!
 
Haki itatendeka au itaonekana imetendeka pale tutakaposikia kauli ya Mh Spika mwenyewe. Akinyamaza hivi anatukatisha tamaa. Najua yeye ni JASIRI sana hasa katika kuongea lile analoliamini. Nisichokijua kwake ni mapenzi yake kwenye CHEO na MADARAKA aliyonayo sasa.
 
Wakuu lakini inabidi tupime maneno ya Kusila. Ni nani walioshindwa kwenye uchaguzi wa kutafuta mgombea urais kwa tikiti ya CCM? Kigoda(chaguo la Ben), Mwandosya, au Salim. Which words and what actions constitutes treason? Does fighting corruption or exposing corruption constitutes treason? or Kusila is lost.

Usipoteze muda wako mwingi kufikila sana kwani hivi vikao vya CCM hao wanao ingia wenig ni watu kama kusila wasio na mawazo endelevu hivyo kufikilia kama wanaopinga ufisadi au makosa yoyote ya kizembe kuwa ni treason wala usisumbuke kwani pale kuna watu wamepangwa thats why wengine hawakupewa nafasi.
 
Kwenye hili la Sitta's sagga na NEC, nimejifunza two important lessons, kwamba:-

1. Tanzania tutaendelea kulipia laana ya dhambi ya kumkataa Mrema, kwenye urais kwa sababu so far ana-stand tall kwa kuwa kiongozi pekee wa juu wa bara, aliyeweza kurudisha kadi ya CCM bila kufikiria mara mbili.

2. Utawala wa sasa umeanza kukubali kushindwa, kwa sababu Diria na Mwinyi walipoingia Ikulu, walijaribu sana mwanzoni kumrushia vijembe Mwalimu, lakini within time wakakwama kwa sababu hawakuwa na uwezo wa kuongoza, ndipo Mwalimu akaanza kuwachapa bakora akianzia kwenye sikuu ya wakulima Mbeya,

- Hawa Membe na Muungwana, walipoingia na wao walianza na zile zile za kumrushia vijembe Mkapa, lakini recently wamenza kunyoosha taulo la kushindwa, now Mkapa is on his way back sio siri soon na yeye ataanza kuwachapa bakora kama zile zile za Mwalimu,

Masikini ya Mungu wananchi wa Tanzania, tutawachagua tena anyways!

Respect.

Field Marshall Es

Kuna watu humu huwa wanakesha kumsema Mkapa wee, wamesema mpaka wamechoka hamna jipya kuhusu huyu 'mbaba' wako waliopiga kelele na kumsifia Mwakyembe na kilango kna kwamba hao ni alama ya ukombozi

If we are real serious, if we real mean it-HAKUNA MSAFI CCM, maana wangekuwa wasfi wangeondoka, if and only if the real mean kuwaongoza watu na wala si kwa matumbo yao!

Kweli uchafu huu unaoendelea kama hawa wabunge wenu mnaowasifia kila kukicha wasiporudisha kadi kama Mrema wawekwe kundi gani?

Haya JK na Mkapa wanagonga cheers huku mkiamini JK anatakiwa amkamate mkapa, huku Mkapa ndiye aliyemweka madarakani!

Naomba glass ya maji na panadol hapo tafadhali!
 
Tatizo ninaloliona mimi ni kwamba ndani ya vikao vingi vya CCM wanaingia wazee ambao wengi hawataki mabadiliko na wanashindwa kusoma nyakati. Wanashindwa kujua kwamba watanzania wa sasa wako yofauti na wamechoshwa na ufisadi. Wako tayari kutafuta taarifa sahihi na kuzipata na kuzikubali. Ni wakati muafaka wa UVCCM kusoma upepo na kutoa ushauri sahihi kwa babu zao.
 
iv. Viongozi watakao vunja maadili haya watakuwa wamejibainisha kwamba hawana nia njema na CCM, na watahesabiwa ni wasaliti wa CCM hivyo Chama hakitasita kuwapa adhabu kali, ikiwa ni pamoja ya kuvuliwa uongozi na hata kufukuzwa katika Chama.

Iwapo hili swala ndiyo tu limejulikana juzi na lilikuwa halijaainishwa wazi kwa wanaCCM tangu 1977, basi hiki chama chetu tawala kinatatizo kubwa sana la msingi.

Kwa upande mwingine, maoni kama hayo juu yanaeleza ni kwanini nchi yetu imegubikwa kwenye kashfa juu ya kashfa. Iwapo chama tawala kilikuwa hakina mwongozo kama huo juu mpaka hiyo juzi, siye kama Taifa tulitegemea nini kiwatokee wale waliotuhujumu mpaka hivi sasa?!

Lakini hapa nakumbuka pia lile sakata la ndugu Nape Nnauye. Ilikuwa kuwaje wakati huo waliweza kumshurutisha huyu jamaa kwa mambo ya maadili n.k.?! Maadili ni maadili, CCM kingelikuwa kinafatilia maadili ya wanachama wake wote nchi yetu ingekuwa miongoni mwa nchi zenye uchumi wa kati. Miaka thelathini naa ya CCM ingelikuwa imetumikiwa ipasavyo.
 
JK wake up man? achana na mambo ya hesheem now mzee,u have a lot to do for ur countrymen!! Kuwa diktecta kwa subordinates wako, wnanchi tupo nyuma yako, now why are u not saying anything?usidhani mzaha sasa,wananchi tunajua Kila kitu hakuna siri mkuu,ushauri wa bure huu lakini!act act act its the time now!!
 
- Wakuu wote JF, heshima iwarudie ninasema hivi tuna silaha moja tu hapa JF nayo ni keyboards zetu, ninajaribu kila njia tena arround the clock kuyaanika wazi majina ya viongozi wetu wote waliozungumza ndani ya hiki kikao na pumba zao against wananchi, soon tutakuwa na more pumbas!

- Kuna watu wa Muungwana wanaonitumia ujumbe kwa pembeni toka niiweke hii, kwamba eti Rais alikuwa anapima upepo na kutaka kujua nani ni nani katika safu ya mafisadi kwa hiyo I am being unfair kumshambulia, ninasema hivi that is the most political nonsense I ever heard, Rais anatakiwa kufahamishwa na Usalama Wa Taifa in advance kinachoendelea ndani ya hili taifa. Hapa pia nina ujumbe kwa wapiganaji, na hasa Mzee Mengi yale maneno yenu ya kila wakati kwamba eti Rais anajitahidi sana kupigana na mafisadi mnahitaji kuyaacha maramoja, tena ninasema now!

Wakuu baadaye, tuna dataz zaidi zinazohitaji kwanza uthibitisho and then zitamwagwa hapa JF kumkoma nyani kama kawa!, maana I mad as a hell!

Respect.

Field Marshall Es!

Rais ana sauti kubwa mno kwa tanzania kuzidi hata mahakama ya rufaa.Kama kweli angekuwa anapigana na ufisadi hili neno ufisadi lingekuwa historia.

Lakini ukirudi nyuma atamfunga je? Lowasa ama RA wakati pesa zilizochukuliwa ni yeye ndiye kanufaika nazo kuliko RA na Lowasa? yani ya kwamba yeye ni prezda.
 
- Wakuu wote JF, heshima iwarudie ninasema hivi tuna silaha moja tu hapa JF nayo ni keyboards zetu,
Bila shaka mkuu na tunaweza fanya hata zaidi ya hapo! tuko pamoja
- Kuna watu wa Muungwana wanaonitumia ujumbe kwa pembeni toka niiweke hii, kwamba eti Rais alikuwa anapima upepo na kutaka kujua nani ni nani katika safu ya mafisadi kwa hiyo I am being unfair kumshambulia, ninasema hivi that is the most political nonsense I ever heard, Rais anatakiwa kufahamishwa na Usalama Wa Taifa in advance kinachoendelea ndani ya hili taifa.
Pengine alikua anataka kuwaonyesha yuko upande wao halafu badae awakaange kama alivomkaanga lowasa halafu akajifanya anamlilia karimjee kwenye kikao na wazee wa Dar es salaam.Kumbuka muungwana ni mswahili..!

- Hapa pia nina ujumbe kwa wapiganaji, na hasa Mzee Mengi yale maneno yenu ya kila wakati kwamba eti Rais anajitahidi sana kupigana na mafisadi mnahitaji kuyaacha maramoja, tena ninasema now!,
Hawawezi kumpinga rais wa nchi moja kwa moja wanajalibu kupigana vita hii kwa akili kumbuka huwa unatutahadhalisha nguvu za ajabu alizo nazo mkuu wa nchi na hapa watu kama Mengi wanalinda biashara zao kwa kumuhifadhi mkuu wa nchi ila nna imani akimaliza muda wake watamrukia kama kawa..!


- Wakuu baadaye, tuna dataz zaidi zinazohitaji kwanza uthibitisho and then zitamwagwa hapa JF kumkoma nyani kama kawa!, maana I mad as a hell!!
Ndicho ninachokufurahia na kujivunia mkuu, kwenye maslahi ya taifa hauangalii makunyanzi..!
 
Tunako elekea tutakuwa na CCM 2 tutakuwa na CCM ya matajiri ambao ni wachache na CCM ya maskini ambao ni wengi.

Umenakili utabiri wa mwalimu? na kweli very soon tutamuita Nyerere mnajimu
 
Iwapo hili swala ndiyo tu limejulikana juzi na lilikuwa halijaainishwa wazi kwa wanaCCM tangu 1977, basi hiki chama chetu tawala kinatatizo kubwa sana la msingi.

Kwa upande mwingine, maoni kama hayo juu yanaeleza ni kwanini nchi yetu imegubikwa kwenye kashfa juu ya kashfa. Iwapo chama tawala kilikuwa hakina mwongozo kama huo juu mpaka hiyo juzi, siye kama Taifa tulitegemea nini kiwatokee wale waliotuhujumu mpaka hivi sasa?!

Lakini hapa nakumbuka pia lile sakata la ndugu Nape Nnauye. Ilikuwa kuwaje wakati huo waliweza kumshurutisha huyu jamaa kwa mambo ya maadili n.k.?! Maadili ni maadili, CCM kingelikuwa kinafatilia maadili ya wanachama wake wote kwa walau 90% tu, nchi yetu ingekuwa miongoni mwa nchi zenye uchumi wa kati. Miaka thelathini naa ya CCM ingelikuwa imetumikiwa ipasavyo.
Mkuu chama chako peke yako,sio chetu.. kwa uoza huu wa ccm,Tz tutakuwa nyuma milele,kwani ccm haipo tayari kwa lolote,ilobaki tutatiana vidole machoni sisi wenyewe wapinzani huku ccm wakila biriani ktk meza ya ikulu,la sivyo ni wananchi wenyewe kusema sasa basi na sio tu kwa kupiga kura bali kuhakikisha ccm wanaondoka kwa njia yoyote,na upanga uwe umetangulia mbele hapo tutajua wakati umefika.. HAYA BWANA
 
-
Hapa pia nina ujumbe kwa wapiganaji, na hasa Mzee Mengi yale maneno yenu ya kila wakati kwamba eti Rais anajitahidi sana kupigana na mafisadi mnahitaji kuyaacha maramoja, tena ninasema now!
Respect.


Field Marshall Es![/QUO

Hapo tupo wote mkuu. Lakini wengine tulishasema hayo toka siku nyingi lakini kuna watu wakaita kuwa huo ni mkakati wa kupambana na ufisadi.
 
Back
Top Bottom