Malafyale
Platinum Member
- Aug 11, 2008
- 13,913
- 11,328
CCM rasmi imeitumbikiza Tanzania kwenye mgogoro wa kikatiba na haya shime watz hasa wana JF tusikubali hali hii dhalili iendelee,na ikiwezekana na sisi tutoe"waraka wetu wenye miongozo mingi" kupinga kutishwa kwa Spika na wabunge wengine wapambanaji wa CCM.
Katiba ya Tanzania inaeleza kwa uwazi kabisa mipaka na mamlaka ya Bunge na kiongozi wake yaani Spika;HAMNA sehemu kwenye katiba inayosema kuwa "Spika akiruhusu wabunge wa chama tawala waeleze ukweli kuhusu MADHARA ya ufisadi basi ashtakiwe ama kwa uhaini au akihurumiwa basi afukuzwe uanachama",hii ni kejeli kubwa kwa demokrasia,na nakiri sijawahi ishuhudia ktk nchi yeyote ile yenye utawala BORA zaidi ya hapa Tanzania!
Sheria mama ya Bunge inaeleza wazi kuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kulishambulia bunge na mamlaka yake akiwa nje ya bunge,sheria inasema kuwa hata mbunge anatakiwa alishambulie bunge akiwa bungeni tu;na ni mwiko kwa mtu yeyote pia kupinga,kujadili na kudharau jambo ambalo tayari bunge limekwisha lipitisha na kulitolea ufafanuzi,na ukifanya hivyo unaweza fungwa jela kwenye mahakama halali za kikatiba;sasa huyu Mwenyekiti wa CCM-Shinyanga mzee Mgeja yeye sio mbunge,hii nguvu ya kulitolea ufafanuzi hata kumsimanga Spika kwa jambo lililojadiliwa na kupitishwa kihalali na wabunge kama hili la ufisadi wa Richmond amepata wapi?
Kauli ya Mzee William Kusila,ambaye ni Mwenyekiti wa CCM-Dodoma na mbunge wa jimbo la Bahi ndiyo limenishangaza zaidi!William Kusila kwa nguvu alizonazo za ubunge alipaswa kulisemea jambo hili kwenye vikao halali vya bunge,lkn akakaa kimywa na hata akakubali Richmond ijadiliwe tena mwezi Novemba,iweje sasa amshambulie Spika?
JF as a great thinker institution;we need to react as soon as possibe on this senseless mayhem,na ikiwezekana na sisi tutoe tamko rasmi na kulipeleka kwenye jumuiya za kimataifa hasa mabalozi wa nchi za Ulaya-Magharibi,Canada na USA; sehemu ambazo kwa utafiti wangu wa haraka haraka CCM huwa wanaogopa sana!
Wamefanya mambo mengi sana mabaya kwa watz,lkn hili la kulishambulia,kulitukana,kulikejeli na kulidhalilisha bunge na Spika wake tusiache lipite hivi hivi,Naam wanazuoni wote wa JF tujipange kwa hili jambo lisilo la kidemokrasia na tukichanganya nguvu na sauti zetu ni dhahili kilio hiki kitasikia nje ya mipaka ya tz na watatetemeka hawa MAFISADI!