Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Hili ni tatizo kubwa sana Tanzania, na huwa naliona katika mihimili mitatu ya usimamizi wa nchi, kuanzia Raisi, Spika, Mwanasheria Mkuu na hata mahakimu katika mahakama zetu!
Viongoi wetu wamefika mahali wanavunja Katiba, Sheria au Taratibu zinazokubalika kwa ulevi tu wa hisia zao binafsi.
Na ni tatizo limekubuhu sana katika siasa, lakini labda huko tunaweza kuwapuuza, kwa kuwa wanasiasa kutumia hisia kufanya maamuzi ni bora kuliko kile ambacho husemwa kuwa tabia yao, uongo!
Lakini sasa, tunapukuwa na Taasisi ya uraisi nchini, ikifanya maamuzi kwa hisia, Bunge likitoa matamko na maamuzi kwa hisia, mahakimu katika maamuzi ya kesi, wakitoa hukumu kwa hisia, tunakuwa tunaenda wapi?
Baada ya wanasiasa, kundi la pili linaloambukizwa kirahisi sana na kirusi cha kufanya mambo na maamuzi kwa hisia ni Polisi. Na hakika nawaambieni, Polisi wetu hapa nchini kirusi cha hisia kilishawakumba siku nyingi sana.
Ni lini Tanzania tutaondokana na kuamua mambo, kutoa matamko au kutenda mambo kwa kuongozwa na hisia? Tmeingiliwa na ugonjwa mbaya sana!