Maalim Seif: Tunataka Zanzibar yetu!

Seif ni Katibu mkuu wa CUF sasa huu ndio msimamo wa CUF au ni wake mwenyewe? Kama ni wa CUF Lipumba atoke hadharani na kutuweka wazi kuwa CUF ndio sera yake. Kama sio sera ya CUF basi Seif yuko tofauti na Chama chake na hastahili ukatibu mkuu afukuzwe

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Huyu si mswana uamsho? Lazima awawakilishe vyema waarabu wenzake katika kudai koloni lao jipya la zanzibar!

Huvi kuna nini kilichojificha katika Muungano huu ambacho hakitakiwi kijuilikane mpaka inafikia mtu akiamua kuuzungumzia anatiwa hatiani na kuonekana kama anatenda dhambi?! Inawezekana ile Dhana ya Sheikh Ilunga Hassan ya kwamba Zanzibar inatawaliwa na Watanganyika kwa 'MFUMO KRISTO' kupitia mgongo wa Muungano hapa ndio inajidhihirisha! Na ndio maana Wazanzibari hatuipendi CHADEMA, na itakua ni ndoto Chama hichi kua cha Kitaifa mpaka tutakapojitenga na Watanganyika.
 
Kuna mahali nimesema, Uamsho hawawezi kufutwa Zanzibar maana sera zao ndizo sera za kila Mzanzibar.

Kina Shein wanabanwa na "double standards" zao kusikiliza Dodoma, but mioyoni mwao ni Uamsho mtupu!!
 
Huyu ni Mpemba na wapemba hawatakiwi Unguja na hawapendwi hili liko wazi so wauguja ndio hawataki kuvunja muungano ni wapemba tu... na wamanga..

Kumbe Watanganyika ndio wamezuia uchimbaji wa mafuta Zanzibar duh Sijalijua hili!!!!

Kama ni kweli wapemba hawatakiwi Unguja, je unaweza kutwambia ni kwanini hawatakiwi? Wenzako wanazungumza kwa kutumia mdomo wa kawaia lakini wewe nahisi umetumia mdomo wa chini! Yakhee kama unahisi ladha ya pilipili siye wapemba hua twala iyo midomo!
 
Maalim Seif Sharif Hamad ahutubia mkutano mkubwa wa hadhara kisiwani Pemba hii leo na anasema:

"Mimi sitafuni maneno kwamba ni muumini wa Zanzibar yenye mamlaka kamili kitaifa na kimataifa itakayofuatiwa na mashirikiano kati yake na Tanganyika kupitia Muungano wa Mkataba.

Namshangaa leo anakuja kiongozi wa Zanzibar anasema tuna bendera na muhuri na wimbo wa taifa, hayo yanatosha. Hivi huyu anajua anachokisema au anatumikia maslahi ya waliomtuma? Una bendera gani hii ambayo mwisho wake Chumbe? Mimi nataka niione bendera ya Dola ya Zanzibar inapepea Umoja wa Mataifa, New York pale. Nataka tuwe na Paspoti ya Zanzibar, nikisafiri nitoe Paspoti ya nchi yangu. Nataka tuwe na Ofisi za Kibalozi za Zanzibar katika nchi za nje. Leo hata mamlaka ya kiuchumi hatuna.

Tumeamua rasilimali yetu ya mafuta na gesi asilia yasiwe mambo ya Muungano, mpaka leo Tanganyika wamekwamisha, wanatuzuia tusinufaike na rasilimali zetu tukajenga uchumi wetu. Wanasema tuna viwango na mfumo mmoja wa kodi lakini bidhaa zikitoka Zanzibar wanazitoza ushuru tena. Lengo ni kuua uchumi wetu ili hatimaye tudhoofike na tusalimu amri kwao. Yaguju! Wasahau hilo.

Leo hata katika mikutano ya kimataifa, viongozi wetu wa Zanzibar hawapewi heshima ya uwakilishi wa nchi yetu. Inafika mahala hata Naibu Waziri tu wa Bara anaongoza ujumbe wa Tanzania wakati kuna Waziri kamili kutoka Zanzibar lakini haheshimiwi. Tutarejesha mamlaka yetu kamili.

Tuwe na Benki Kuu, tuwe na sarafu yetu ya Zanzibar, tupange uchumi wetu kwa maslahi ya watu wetu. Tunataka tuwe na uanachama katika jumuiya na mashirika yote ya kimataifa. Tuwe na Waziri wa Mambo ya Nje wa Zanzibar. Tuwe na uwezo wa kuingia mikataba na nchi za kigeni.

Hayo ndiyo tunayoyataka. Tukisema hivi hatuna maana tunataka ugomvi na Tanganyika. Hapana! Tunataka tuwe majirani wema na Tanganyika kama tutakavyokuwa na ujirani mwema na Kenya. Hayo yatafikiwa kupitia Muungano wa Mkataba wa Madola mawili huru kamili."


Kama utasoma kwa Umakini Speech hii utaona Dhulma wanayofanyiwa wazanzibar na CCM

ukitazama maana ya kina ya maandishi hayo, ni ufumbuzi wa shortcut juu ya changamoto alizoziainisha.
Na always shortcut can cut you.
Ufumbuzi wa kujitenga ni mbegu ya matatizo aliyoonya hayati mwalimu. Wakishajitenga kabla hawajaenjoy kujitenga kwao ataibu mtu mwingine na kudai unguja iwe taifa huru tofauti na pemba. Ni vizuri wakaatack tatizo kwa right solution.
 
Ukiona Makamu wa Rais anadai uhuru wa nchi anayoiongoza, ujue kuna maswali mengi tu ya kujiuliza. Anadai kwa nani wakati yeye at a certain moment ndiye 'Rais'?
 
Ukiona Makamu wa Rais anadai uhuru wa nchi anayoiongoza, ujue kuna maswali mengi tu ya kujiuliza. Anadai kwa nani wakati yeye at a certain moment ndiye 'Rais'?

Nafikiri hakuna maswali mengi, at least for me. President of U.R of Tanzania must do the necessary, yani ya kwamba aitishe referendum Zanzibar.
Swali ni moja tu.
1. Mnataka muungano ? na majibu ni mawili tu
a) Hapana b) ndiyo.
 
Kwenda kule muongo seif hajawahi kukaa wete kwao mtambwe kasoma huko kenda boarding form one kaRudi kusomesha fidel castro school hajawahi kukaa wete
Wete pale yupo kaka yake
Jambo alilo nalo Seif ni kutaka kukata minyororo ya kanisa kwa waislam Wa znz
Na wale wote wanaOpinga ni mawakala kanisa

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
Wote wanaopambana na makanisa wakishamaliza hawaachi wanaanza kupambana na misikiti
 
Jackbauer
maalim seif kiongozi wa SMZ hata kama kipo nje ya mjadala wa katiba mpya

Mkuu, kwani Maalim Seif aliapishwa kuilinda Katiba ipi? Ya Zanzibar ambayo inatambua Muungano? Kama inautambua Muungano naye ameapa kuilinda Katiba hiyo huoni kwamba anakiuka kiapo chake na anatakiwa kufukuzwa kwenye cheo alicho nacho kwa sababu amekisaliti kiapo chake? Ndiyo maana Rais Kikwete hawezi hata siku moja kuthubutu kuuvunja Muungano. Akifanya hivyo, sasa atakuwa Rais wa nchi gani? Atakuwa Gorbachev na hicho sicho alichoapa. Si uliona yaliyompata Gorbachev na "Perestroika" yake? Ashukuru Marekani waliomtuma walimpa u-lecturer kwenye Vyuo vyao huko Marekani.
 
Amefikiria wapemba kama laki mbili hivi waliopo Bara na biashara zao na mali zao itakuaje?

Excellent analysis. Wataanza kutusumbua tena kuwa wananyanyaswa! Sie wakivunja muungano jambo la kwanza wazanzibar wote watatakiwa kuja kwa VISA na watafanya biashara kama Investors from abroad, sijui kama hawaoni umuhimu wa muungano, sijui.

Badala ya kuomba marekebisho ya muungano wao wanataka uvunjwe wacha uvunjwe then tuwatimue kama mbwa!
 
"Watanganyika waliobaki wameduwaa kwa kuachwa na Wazanzibar, wao WATABAKI SALAMA" Hii ndoa imeisha kuwa ndoana kwa wenzetu bora tutengane, kama yupo kiongozi ndani ya serikali ya umoja ni msaliti kweli muungano uko karibu kufa. NENDENI TU MTAKUWA MMEISHA PATA BWANA MWINGINE MZURI
 
let them go. kwanza wamekuwa mzigo tu, hao wapemba ndo wafanyabiashara wakubwa wa hoteli na vyakula huku tanganyika. hoteli zote kubwa za Zbar zinalishwa na chakula toka bara, kama huamini nenda pale bandarini saa 12 asubuhi ndo utaamini hawa watu wanasema mawazo yao
 
Maalim Seif Sharif Hamad ahutubia mkutano mkubwa wa hadhara kisiwani Pemba hii leo na anasema:

"Mimi sitafuni maneno kwamba ni muumini wa Zanzibar yenye mamlaka kamili kitaifa na kimataifa itakayofuatiwa na mashirikiano kati yake na Tanganyika kupitia Muungano wa Mkataba.

Namshangaa leo anakuja kiongozi wa Zanzibar anasema tuna bendera na muhuri na wimbo wa taifa, hayo yanatosha. Hivi huyu anajua anachokisema au anatumikia maslahi ya waliomtuma? Una bendera gani hii ambayo mwisho wake Chumbe? Mimi nataka niione bendera ya Dola ya Zanzibar inapepea Umoja wa Mataifa, New York pale. Nataka tuwe na Paspoti ya Zanzibar, nikisafiri nitoe Paspoti ya nchi yangu. Nataka tuwe na Ofisi za Kibalozi za Zanzibar katika nchi za nje. Leo hata mamlaka ya kiuchumi hatuna.

Tumeamua rasilimali yetu ya mafuta na gesi asilia yasiwe mambo ya Muungano, mpaka leo Tanganyika wamekwamisha, wanatuzuia tusinufaike na rasilimali zetu tukajenga uchumi wetu. Wanasema tuna viwango na mfumo mmoja wa kodi lakini bidhaa zikitoka Zanzibar wanazitoza ushuru tena. Lengo ni kuua uchumi wetu ili hatimaye tudhoofike na tusalimu amri kwao. Yaguju! Wasahau hilo.

Leo hata katika mikutano ya kimataifa, viongozi wetu wa Zanzibar hawapewi heshima ya uwakilishi wa nchi yetu. Inafika mahala hata Naibu Waziri tu wa Bara anaongoza ujumbe wa Tanzania wakati kuna Waziri kamili kutoka Zanzibar lakini haheshimiwi. Tutarejesha mamlaka yetu kamili.

Tuwe na Benki Kuu, tuwe na sarafu yetu ya Zanzibar, tupange uchumi wetu kwa maslahi ya watu wetu. Tunataka tuwe na uanachama katika jumuiya na mashirika yote ya kimataifa. Tuwe na Waziri wa Mambo ya Nje wa Zanzibar. Tuwe na uwezo wa kuingia mikataba na nchi za kigeni.

Hayo ndiyo tunayoyataka. Tukisema hivi hatuna maana tunataka ugomvi na Tanganyika. Hapana! Tunataka tuwe majirani wema na Tanganyika kama tutakavyokuwa na ujirani mwema na Kenya. Hayo yatafikiwa kupitia Muungano wa Mkataba wa Madola mawili huru kamili."


Kama utasoma kwa Umakini Speech hii utaona Dhulma wanayofanyiwa wazanzibar na CCM

Hivi hilo taifa huru la awali la Zanziba ni lipi? Na hao wazanzibari ni wapi? Labda kwanza tujikumbushe historia.

Inatambulika kuwa pamekuwepo na watu wakiishi Zanziba kwa zaidi ya miaka 50000. Kwa kama miaka 2000 hivi, baadhi yao walikuwa wafanyabiashara kutoka uarabuni na uajemi. Ingawa wazawa wao hawakubali lakini bila shaka walichanganyikana na waafrika weusi. Hata hivyo watu wa kwanza kutangaza himaya yao huko walikuwa kutoka uajemi, al maaruf washiraz. Viongozi wao wa mwanzo walikuwa Hassan bin Ali Sultan, Darhash bin Shah n.k. Hawa walikuja kuzidiwa nguvu na wareno ambao walitawala Zanziba kwa zaidi ya miak 200 hadi waarabu kutoka Oman (wayarubid) walipowashinda nguvu mwaka 1698. Mwaka 1840, mtawala wa Oman Seyyid Said bin Sultan Al Busaida alifanya Zanziba makao makuu baada ya kuipokonya Mombasa (na Pemba) kutoka kwa washirazi. Biashara kubwa ya waarabu ilikuwa viungo, meno ya tembo na watumwa. Viungo vililimwa kwenye mashamba makubwa kwa kutumia watu kutoka sehemu iliyokuja kujilikana kama Tanganyika. Meno ya tembo walichukua kutoka huko huko na waliwabebesha watanganyika hadi Zanziba ambako waliyauza pamoja na watanganyika waliozibeba. Wakati mwingingine walinunua watanganyika kutoka kwa viongozi wao ( ingekuwa leo wangeitwa mafisadi) na kuwaswaga hadi kwenye markiti Zanziba. Kwa hali hiyo utajiri na mafanikio makubwa ya Zanziba ya wakati ule ilitegemea sana nguvu, damu na machozi ya watanganyika. Watanganyika walikuwa watwana wakati washirazi,waarabu na wahindi walijihesabu kuwa waungwana. Baada ya wazungu kuona bishara ya utumwa haina tija, waliwalazimisha watawala wa zanziba kusitisha biashara hiyo. Hii walikataa wakijua thika kuwa kufanya hivyo ni kuua uchumi wao. Hata hivyo walizidiwa nguvu na mwaka 1890 Zanziba iligeuzwa protectorate ya uingereza. Ingawa Zanziba haikuwa koloni lakini mtawala alikuwa muingereza. Kuthibitisha hii, ni pale mwaka 1896 Seyyid Khalid bin Barghash alipotikisa kiberiti, ilipigwa mizinga na baada ya dakika 38 za kutetea uhuru wake kwa nguvu alisalimu amri.

Zanziba ilibakia protektoret hadi Disemba 10 1963 walipopewa uhuru na Sheikh Mohamed Shamte wa ZPPP kutangazwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Zanziba na Pemba na Jamshid ibn Abdulla kuwa mkuu wa nchi. Desemba 16 1963, Shamte alihutubia Umoja wa Taifa kama kiongozi wa taifa huru. Haukupita mwezi serikali yake ilipinduliwa katika mapinduzi ambapo waarabu na washirazi wengi waliuliwa. Jamshid alitoroka na meli yake ambayo baada ya Kenya kukataa kuiruhusu kutia nanga Mombasa, Nyerere aliiruhusu kutia nanga na alimpa hifadhi hadi hapo alipoenda uhamishoni. Waliochukua nchi ya Zanziba na Pemba walianza kufanya juhudi za wazi za kuigeuza nchi yao kutoka kuwa ya kiarabu na kishiraz na kuifanya ya kiafrika nyeusi. Viongozi wengine walichukua nafasi hio kuoa mabinti wa kiarabu, kishiraz au kihindi maana awali wasingeweza.

Tarehe 26 Aprili 1964, takriban miezi minne baada ya mapinduzi, nchi za Tanganyika na Zanziba na pemba ziliungana kuunda Tanzania. Nchi ambayo iko mpaka sasa na ambayo hawa waheshimiwa wanaikana.

Narudia swali langu la awali baada ya yote haya, "ni Zanziba huru gani wanayoizungumzia"? Hiyo ambayo wanawax nostalgic ni ile ya mababu zao wakiarabu, kihindi na kishirazi? Ni ile ya Shamte na Jamshid? Au ile ya wakina Karume?Tukitambua ukweli kuwa wengi wanaoongoza huo uamsho ni wa kutoka koo za kiungwana na kwa wale waliotoka kwenye utwana, waliowatangulia walioa waungwana! Hivi wanaamini kweli kuwa tumesahau waliyowaendea mababu zetu? Hatambui kuwa hizi kelele zao na kejeli zao kwa baadhi yetu ni uthibitisho kuwa uhusiano pekee ambao wataukubali ni ule wa sisi kuwa watwana na wao waungwana? Wamesahau kuwa historically, wao ndio wamekuwa wakitunyonya watanganyika?

Hivi wanaamini kweli sisi tuko retarded kiasi kuwa baada ya kebehi zao, matusi yao bado baada ya kuvunja Muungano tutaona kuwa wanatufanyia fadhila kutaka tuungane nao kwa mkataba chini ya masharti yao! kweli akutukanae hakuchagulii tusi.

Tunachokitaka baadhi yetu ni kuwa waseme wazi kwa maneno na vitendo kuwa hawautaki Muungano. Lakini wajue kuwa ukivunjika hawatakuwa tofauti kwetu na Kenya, Sudan au nchi nyingine. Upendeleo wowote watakaotaka wapewe, itabidi na raia wa Tanganyika wapewe Zanziba. Kama wataruhusiwa kumilki ardhi kwetu basi na watanganyika nao waruhusiwe kumilki ardhi kwao. Wakitaka watanganyika waingie kwa pasi kwao basi wazanzibari nao itabidi waingie kwa pasi Tanganyika! Mnasema sisi ni ndugu lakini mnasahau ugomvi wa ndugu ni mbaya kulikoni.

Amandla.......
 
Ameamua kuonyesha uamusho wake hadharani.!

Hivi uamsho ni nini ??? Kukataa Serikali mbili?? Kama ni hivyo je CHADEMA wote ni muamsho?? Nafikiri tujadili hoja za mtu na si mtu aliyetoa hoja. C'mon guys, I know we are better than that.
 
Wakuu, as Days goes on mie nimekuwa nawashangaa sana wenzetu, Waliberali wa CUF.
Leo Maalim Seif alikuwa Zanzibar kwenye Harakati za Kudai Zanzibar Huru.
Zanzibar yenye Mamlaka Yote, hii ikifanikiwa inamaana kuwa Hakuna Mungano.
Cha ajabu Huyu huyu Mzee, Maalim Seif pamoja na wa Liberali wenzake wa CUF, wanasema Lipumba ndo Rais 2015????????
Haya wameyasemea Morogoro, Tanganyika.
Natatizika hapa, Hawa Jamaa CUF wanataka kutawala Tanganyika na Zanzibara???????
Kuna Sabababu gani ya the Same Maaliim Seif Kudai Mamlaka kamili ya Zanzibar and at the same time Kuja Tanganyika.
Kudai Uuungwaji Mkono na Wa Tanganyika.
Maalim Seif anadai Mamlaka Kamili ya Zanzibar kwa Kofia ya CUF.
Maalim Seif huyu huyu anakuja Tanganyika tena kuomba Wa Tanganyika waunge Mkono CUF????
Jamani Mbona Wa Liberali CUF wamechanganyikiwa hivyo, Mbona Mwana Ndoa mwenzao CCM hafanyi hayo??????
Hivi Wakuu, Liberal Lipumba kwani ni Mzanzibar????


Hebu tujadilini jamani, hawa Wa Liberali wa CUF ni nini hasa wanataka
 
Ttzo unashindwa kutofautisha kati ya cuf na zanzibar,z'br ni ya waz'br c ya cuf,waz'br wanataka nchi yao wamechoka kutawaliwa na mkoloni mweusi.
 
Back
Top Bottom