Maalim Seif: Tunataka Zanzibar yetu!

Ndulungu

Member
Oct 22, 2011
87
49
Maalim Seif Sharif Hamad ahutubia mkutano mkubwa wa hadhara kisiwani Pemba hii leo na anasema:

"Mimi sitafuni maneno kwamba ni muumini wa Zanzibar yenye mamlaka kamili kitaifa na kimataifa itakayofuatiwa na mashirikiano kati yake na Tanganyika kupitia Muungano wa Mkataba.

Namshangaa leo anakuja kiongozi wa Zanzibar anasema tuna bendera na muhuri na wimbo wa taifa, hayo yanatosha. Hivi huyu anajua anachokisema au anatumikia maslahi ya waliomtuma? Una bendera gani hii ambayo mwisho wake Chumbe? Mimi nataka niione bendera ya Dola ya Zanzibar inapepea Umoja wa Mataifa, New York pale. Nataka tuwe na Paspoti ya Zanzibar, nikisafiri nitoe Paspoti ya nchi yangu. Nataka tuwe na Ofisi za Kibalozi za Zanzibar katika nchi za nje. Leo hata mamlaka ya kiuchumi hatuna.

Tumeamua rasilimali yetu ya mafuta na gesi asilia yasiwe mambo ya Muungano, mpaka leo Tanganyika wamekwamisha, wanatuzuia tusinufaike na rasilimali zetu tukajenga uchumi wetu. Wanasema tuna viwango na mfumo mmoja wa kodi lakini bidhaa zikitoka Zanzibar wanazitoza ushuru tena. Lengo ni kuua uchumi wetu ili hatimaye tudhoofike na tusalimu amri kwao. Yaguju! Wasahau hilo.

Leo hata katika mikutano ya kimataifa, viongozi wetu wa Zanzibar hawapewi heshima ya uwakilishi wa nchi yetu. Inafika mahala hata Naibu Waziri tu wa Bara anaongoza ujumbe wa Tanzania wakati kuna Waziri kamili kutoka Zanzibar lakini haheshimiwi. Tutarejesha mamlaka yetu kamili.

Tuwe na Benki Kuu, tuwe na sarafu yetu ya Zanzibar, tupange uchumi wetu kwa maslahi ya watu wetu. Tunataka tuwe na uanachama katika jumuiya na mashirika yote ya kimataifa. Tuwe na Waziri wa Mambo ya Nje wa Zanzibar. Tuwe na uwezo wa kuingia mikataba na nchi za kigeni.

Hayo ndiyo tunayoyataka. Tukisema hivi hatuna maana tunataka ugomvi na Tanganyika. Hapana! Tunataka tuwe majirani wema na Tanganyika kama tutakavyokuwa na ujirani mwema na Kenya. Hayo yatafikiwa kupitia Muungano wa Mkataba wa Madola mawili huru kamili."


Kama utasoma kwa Umakini Speech hii utaona Dhulma wanayofanyiwa wazanzibar na CCM
 
Tangu asubuhi nimesema malengo ya maalim sefu na kijana wake jussa ni tofauti na ya Lipumba - CUF tanganyika

wanatumika kama mgongo na hakuna Lolote zaidi ya CUF- watanganyika kuwaandama Chadema.

CUF- Tanganyika sio CUF- zanzibar, watanganyika shitukeni msitumike kuinanga chadema kwa msala upitao......
 
Mambo ya ki-Pemba hayo. Naona ametumia sana "tuwe", "yetu", "tuna", "tusi...", n.k. Bora atumie "muwe", "yenu", "mna", "msi...", n.k. Hayo ndio mwafaka zaidi kwake.
 
Maskini ya Mungu Lipumba anatumiwa na hawa wanaodai nchi yao. Na Lipumba nae aanze kudai nchi yake ya Tanganyika
 
Kama kuna chama ambacho msajili anapaswa kukifuta haraka basi ni CUF. Haiwezekani mtendaji mkuu wa chama anahubiri waziwazi tena bila kificho utengano wa kitaifa halafu anatazamwa tu!

Tanzania ni moja na mipaka yake lazima ilindwe kwa gharama zote. Hoja zake alipaswa azitolee kama mwananchi wa kawaida kwenye Tume ya Katiba na sio majukwaani. Tendwa upo?
 
Nafuu Maalin umeamua KUYATAMKA badala ya KUYATAFUNA maneno yako! Kwa kuwa wewe utamkaye haya ni Kiongozi wa Juu katika SMK; itakuwa vizuri kwa WANA-NDOA wenzenu-CCM kukubai kwamba MUUNGANO umekwisha kuwa mzigo usiobebeka!

Kama katika mahusiano mengine ya kibinadamu; waliopendana na kuaminiana ikilazimika kuachana huuma; japo si mwisho wa maisha yao!
Tanganyika na Zanzibar (watakuja myambuana baadaye nani Unguja nani Pemba) tuuvunje Muungano kwa amani ili walau tubakize udugu wetu (ulioleta huo Muungano miaka ile)!

Hata kama ni PARTNER katika biashara kama kila siku anakilalamikia wamuibia; achana naye mapema ulinde heshima yako na uhusiano wenu!
 
tumeambiwa suala la kuvunja muungano haliwezi kujadiliwa kwenye mchakato wa katiba mpya..kitakachojadiliwa ni jinsi ya kuboresha muungano.
Tupime na kuamua juu ya kile anachokiongea maalim seif kiongozi wa SMZ hata kama kipo nje ya mjadala wa katiba mpya.
 
M aalim Seif ni Katibu Mkuu wa CUF, lakini pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar. Nataka kufahamu kama haya aliyazungumza kama kiongozi wa CUF au wa SMZ? Kama alizungumza kama kiongozi wa CUF, hivi msimamo huo unakubaliana na viongozi wenzake kwenye serikali ya umoja wa kitaifa? Kama alizungumza kama kiongozi wa SMZ, nadhani sasa Serikali ya Muungano inaweza kuanza kuelewa ni nini hasa Wazanzibari wanachokitaka.
 
Baada ya kujificha nyuma ya uamsho sasa inalazimu kujitokeza hadharani.

Zanzibar haingozwi na chama kimoja cha siasa, ni serikali ya umoja wa kitaifa na Maalim Seif ni mmoja wa viongozi watatu wa juu kabisa Zanzibar. Sasa kwa nini analalamika kuhusu muungano wakati huo huo anaruhusu wabunge wake waende kwenye bunge la muungano? Kwanini asiamuru muswada wa kumaliza haya mambo ukapelekwa haraka BLW?
 
Sasa anamlalamikia nani kwani nani anawazuia kujitenga kweli hawa watu bure kabisa
 
Huyu ni Mpemba na wapemba hawatakiwi Unguja na hawapendwi hili liko wazi so wauguja ndio hawataki kuvunja muungano ni wapemba tu... na wamanga..

Kumbe Watanganyika ndio wamezuia uchimbaji wa mafuta Zanzibar duh Sijalijua hili!!!!
 
Back
Top Bottom