Maalim Seif: Tunataka Zanzibar yetu!

Maalim Seif: Tunataka Zanzibar yetu!

Na kesho tunaambiwa yuko Buguruni, angeonyesha mfano kwa kuisusia Tanganyika.
 
Anafuata nini huku...............aichane passport ya Tanzania......asubiri ya Zanzibar
 
"Mimi sitafuni maneno kwamba ni muumini wa Zanzibar yenye mamlaka kamili kitaifa na kimataifa itakayofuatiwa na mashirikiano kati yake na Tanganyika kupitia Muungano wa Mkataba. Namshangaa leo anakuja kiongozi wa Zanzibar anasema tuna bendera na muhuri na wimbo wa taifa, hayo yanatosha. Hivi huyu anajua anachokisema au anatumikia maslahi ya waliomtuma? Una bendera gani hii ambayo mwisho wake Chumbe? Mimi nataka niione bendera ya Dola ya Zanzibar inapepea Umoja wa Mataifa, New York pale. Nataka tuwe na Paspoti ya Zanzibar, nikisafiri nitoe Paspoti ya nchi yangu. Nataka tuwe na Ofisi za Kibalozi za Zanzibar katika nchi za nje.


Leo hata mamlaka ya kiuchumi hatuna. Tumeamua rasilimali yetu ya mafuta na gesi asilia yasiwe mambo ya Muungano, mpaka leo Tanganyika wamekwamisha, wanatuzuia tusinufaike na rasilimali zetu tukajenga uchumi wetu. Wanasema tuna viwango na mfumo mmoja wa kodi lakini bidhaa zikitoka Zanzibar wanazitoza ushuru tena. Lengo ni kuua uchumi wetu ili hatimaye tudhoofike na tusalimu amri kwao. Yaguju! Wasahau hilo. Leo hata katika mikutano ya kimataifa, viongozi wetu wa Zanzibar hawapewi heshima ya uwakilishi wa nchi yetu.


Inafika mahala hata Naibu Waziri tu wa Bara anaongoza ujumbe wa Tanzania wakati kuna Waziri kamili kutoka Zanzibar lakini haheshimiwi. Tutarejesha mamlaka yetu kamili. Tuwe na Benki Kuu, tuwe na sarafu yetu ya Zanzibar, tupange uchumi wetu kwa maslahi ya watu wetu. Tunataka tuwe na uanachama katika jumuiya na mashirika yote ya kimataifa. Tuwe na Waziri wa Mambo ya Nje wa Zanzibar. Tuwe na uwezo wa kuingia mikataba na nchi za kigeni. Hayo ndiyo tunayoyataka. Tukisema hivi hatuna maana tunataka ugomvi na Tanganyika. Hapana! Tunataka tuwe majirani wema na Tanganyika kama tutakavyokuwa na ujirani mwema na Kenya. Hayo yatafikiwa kupitia Muungano wa Mkataba wa Madola mawili huru kamili."

Seif asema Tunataka Zanzibar yetu | Mzalendo.net
Aliyeanzisha ndoa kati ya CCM na CUF ni yeye.. Zanzibar yao wanayoitaka ni ipi? kwani si wanaishi huko Zanzibar?!!Zanzibar ipi tena?....mbona siwaelewi hawa jamaa?
 
Ipitishwe refurundum watu waseme kama wanataka muuungano ama la.Hivi kipindi tunaungana wananchi walishirikishwa?au ni julius na Abeid tu waliamua.Mbona waskotish wanataka uhuru wao why not zenji?
 
huyo ndo chanzo cha machafuko zanzibar shida yake ni uroho wa madaraka ndo unamsumbua na wakitaka kujitenga tuwape ila wenzao walioko huku bara hatutawataka kuwaona wakagombee ardhi kwao vizuri
 
Tatizo la Watanganyika kusahau. Hawataki kujiita hivo na hata baba wa taifa alishasema kuwa "CHAKE ni chake ila CHANGU ni CHETU", aliona mpasuko wa Muungano na kututahadharisha.
Na kesho tunaambiwa yuko Buguruni, angeonyesha mfano kwa kuisusia Tanganyika.
 
Huyu yawezekana ndo source ya uamsho...........kumbe wana support

enhe ndio hivyo huyo tulishamuelezela vizuri hapa jf. Inashangaza ccm znz wamerubunika kumuingiza jikoni smz. Lakini tutamngoa na kumaliza udhia once for all safari hii.
 
enhe ndio hivyo huyo tulishamuelezela vizuri hapa jf. Inashangaza ccm znz wamerubunika kumuingiza jikoni smz. Lakini tutamngoa na kumaliza udhia once for all safari hii.

again CDM minds ulitaka watu wauwane uje ufurahike humu???
 
Naona kuna sababu ya kuipigia kura CHADEMA, si kwamba naipenda ila napenda muungano uvujinke. Maana kwa kutumia mlinganyo rahisi kabisa yani ya kwamba.
CHADEMA = D
CUF = U
CCM =C
Muungano = M

[TABLE="class: cms_table"]
[TR]
[TD]D[/TD]
[TD]U[/TD]
[TD]C[/TD]
[TD]M[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]1[/TD]
[TD]1[/TD]
[TD]1[/TD]
[TD]Not allowed[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]1[/TD]
[TD]1[/TD]
[TD]0[/TD]
[TD]0[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]1[/TD]
[TD]0[/TD]
[TD]1[/TD]
[TD]0[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]1[/TD]
[TD]0[/TD]
[TD]0[/TD]
[TD]1[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]0[/TD]
[TD]1[/TD]
[TD]1[/TD]
[TD]1[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]0[/TD]
[TD]1[/TD]
[TD]0[/TD]
[TD]1[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]0[/TD]
[TD]0[/TD]
[TD]1[/TD]
[TD]1[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]0[/TD]
[TD]0[/TD]
[TD]0[/TD]
[TD]Not allowed[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

0= False
1= True.
Hivyo wazanzibari mwaka 2015 kura za rais wa muungano waipigie CHADEMA.
 
Hebu someni kwa makini kwenye nyeusi hapo chini

Zanzibar clashes over missing cleric Sheik Farid Hadi


_63579861_sheikh-farid-hadi-564x272.jpg
Muslim cleric Sheik Farid Hadi has been missing since Tuesday

Continue reading the main storyRelated Stories



More than 50 people have been arrested followings two days of riots that have shut down businesses and schools on the Tanzanian island of Zanzibar.
The trouble began when supporters of Muslim cleric Sheik Farid Hadi, who campaigns for Zanzibar's autonomy, found out that he had gone missing.
There were running battles between the police and young men throwing stones and burning tyres.
One policeman was killed after being attacked on Wednesday evening.

The BBC's Aboubakar Famau in Zanzibar says police continued to use tear gas on Thursday to quell the situation and disperse any groups.
It is believed that criminal gangs took advantage of the situation and joined the riots.
Bars and shops have been looted in the violence, stones and burnt tyres litter the roads and national school exams that were due to be written on Thursday were postponed.

Mr Hadi, who leads a group called Uamsho, has not been seen since Tuesday.
His group has distanced itself from the violence and says it was not involved in the death of the policeman.
Our reporter says that at a joint media conference on Thursday both the police and Uamsho leaders called for calm.
The police said 51 people had been arrested and assured Uamsho supporters that they did not know why the Muslim cleric had gone missing and were still searching for him.
Zanzibar is a semi-autonomous territory that maintains a political union with Tanzania, but has its own parliament and president.
Tourism is Zanzibar's biggest industry, but most Zanzibaris have yet to benefit from it and the average wage is less than $1 (£0.60) per day.
Sheikh Hadi and his Uamsho movement are particularly popular with disillusioned and jobless youth.
 
Hivi sio uhaini hiyo statement yake?

Alipoapa hakuapa kutetea muungano wetu feki huyu mroho wa madaraka?

Alipounganisha CUF na CCM what the hell did he think he was doing?

Hivi lile figure head aka mwenyekiti jina Lipumba bado yupo Tanzania?
 
Amefikiria wapemba kama laki mbili hivi waliopo Bara na biashara zao na mali zao itakuaje?
 
huyo ndo chanzo cha machafuko zanzibar shida yake ni uroho wa madaraka ndo unamsumbua na wakitaka kujitenga tuwape ila wenzao walioko huku bara hatutawataka kuwaona wakagombee ardhi kwao vizuri

Huvi kuna nini kilichojificha katika Muungano huu ambacho hakitakiwi kijuilikane mpaka inafikia mtu akiamua kuuzungumzia anatiwa hatiani na kuonekana kama anatenda dhambi?! Inawezekana ile Dhana ya Sheikh Ilunga Hassan ya kwamba Zanzibar inatawaliwa na Watanganyika kwa 'MFUMO KRISTO' kupitia mgongo wa Muungano hapa ndio inajidhihirisha! Na ndio maana Wazanzibari hatuipendi CHADEMA, na itakua ni ndoto Chama hichi kua cha Kitaifa mpaka tutakapojitenga na Watanganyika.
 
Back
Top Bottom