Maalim Seif awaponza viongozi wa Jeshi la Polisi Pemba, yaamriwa wavuliwe vyeo

Huo ni udhibitisho kuwa nguvu pekee ya ccm ni matumizi ya vyombo vya dola. Hizo hofu anazopandikiza huyo waziri, ndio huwafanya viongozi wengine wa jeshi la polisi kutii lolote wanaloogizwa dhidi ya haki za wapinzani, na wengine huenda mbali mpaka kufanya mauaji au kuleta vilema ili kulinda vyeo. Hivyo vyombo vya dola ndio pekee vinavyoendelea kulinda uwepo wa ccm hapa nchini.
Tindo, ambaye halijui ulilosema naamini atakuwa amejitoa ufahamu na kutegemea ubongo wa polepole kufikiria, namkumbuka Polepole alipokuwa mwanaharakati, ninayo clip yake moja alivyosema, "sanduku la kupigia Kura likiachwa Huru, ccm ijiandae kuondoka madarakani", leo hii amekuwa kama chizi fulani hivi.
 
Back
Top Bottom