Maajabu ya serikali ya CCM: Spika wa Bunge ana kinga na hashtakiwi, Wabunge wanatunga sheria lakini hawalipi kodi!

Ukiachilia mbali apo kwa wabunge wanaolipwa misharaa mikubwa ivyo kuna huu msururu wa viongozii ambao kama kweli tunataka kuijenga nchi lazima msururu huo ukatwee unakuta kuna Dc,Rc,Meya,wajumbe mbalimbali wa halmashauri, n.k wote hao wanapokea fedha ikiwa kuna miundo mbinu haijakaa sawa hizi sekta ambazo hazizalishi chochote zinazohudumiwa na serikali kuna haja yakuzipunguza siyo kuongeza tuu kodi
 
Kwa hiyo tuseme adui mkubwa wa maendeleo na uhuru wa taifa letu ni Bunge.
Bunge ni kupe,bunge limegeuka wanyonyaji,bunge ni kikwazo cha mwananchi wa kawaida,bunge ni kinyume cha Azimio la Arusha, Bunge ni fursa ya kula bila kunawa,ni bunge ni biashara kubwa isiohitaji mtaji mkubwa.
 
 
WANANCHI ndio WAJINGA
 
Maajabu ya Watanzania wanaowalinda hao wabunge waliopiba kura na kukimbia na maboksi ya kura,
Wabunge wapo sahihi maana wanaongoza malofa yanayohongwa kanga na kofia.
 

Kwanini tunaendelea kuwalea majambazi hawa yarabi?
 
WANANCHI ndio WAJINGA
Ni kweli kabisa na kwa kuwekeza katika mtaji wa ujinga CCM wameweza kufanikiwa kwa asilimia 100%! Tanzania kwa sasa iko miongoni mwa mataifa duniani yaliyosheheni idadi kubwa ya wajinga!

Hebu fikiria taifa ambalo kwa zaidi ya miaka 50 linaongozwa na chama kile kile, watu wale wale na akili zile zile huku imepiga kambi kwenye lindi la umasikini licha ya urithi wa mali asili lukuki.

Na bado wapo wananchi wanaamini tutafika...nashauri tuanze upya kwa kukiri ujinga wetu.
 
Kawaulize wabunge wako wastaafu wakina Mbowe ilikuwaje nawao walikuwa wanakuja hizo pesa bila kulipa kodi??
 
Wewe ndiyo mjinga na ukoo wako wote usituingize na sisi bhana!
 
Na ndiyo maana wataalamu wetu madaktari, mainjinia, maprofesa n.k. wameamua kuaibisha taaluma zao kuwahi huko kuvuna wasipopanda.
 
Huko ndipo wanapopoozwa wale wa kusifu na kulamba nyayo wakubwa.
 
Nimeamka ndo maana tumepandishiwa tozo kwenye miamala ya kutuma na kutoa pesa hii kitu inaumiza sana hasa sisi wa kipato kidogo
 
Hao jamaa wa mjengoni ndio wakwepa kulipa kodi wa kwanza Tanzania na ndio wanaoongoza kwa kutokua wazalendo..TRA wapo busy kukamata risiti kwenye mifuko ya mauzo ya elfu mbili huku wahuni wachache wakijilia keki ya Taifa peke yao...
 
Hao jamaa wa mjengoni ndio wakwepa kulipa kodi wa kwanza Tanzania na ndio wanaoongoza kwa kutokua wazalendo..TRA wapo busy kukamata risiti kwenye mifuko ya mauzo ya elfu mbili huku wahuni wachache wakijilia keki ya Taifa peke yao...
Fikiria mtu yuko bungeni akidai ni mwakilishi wako halafu huko anafanya nini? Badala ya kukutetea wewe anatetea maovu unayotendewa na taasisi ambayo alitakiwa aisimamie kulinda usalama na maslahi yako.

Kwa maana nyingine ni kuwa anaungana na watesi wako kufanya maisha yako yawe magumu zaidi na kuanza kutunga sheria mbovu kandamizi huku yeye akijiwekea kinga ya kutobanwa na sheria hiyo hiyo ya hovyo!

Je inaingia akilini kweli kwamba huyo mtu alichaguliwa kihalali kukuwakilisha? Kwa kweli bunge letu kwa sasa si la wawakilishi wetu bali ni la askari wa kukodi kulinda maslahi ya genge lililowasukumiza humo, CCM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…