Maajabu ya biashara ya uchimbaji wa madini ya dhahabu

Maajabu ya biashara ya uchimbaji wa madini ya dhahabu

Mleta uzi, kwa maelezo yako na picha zako unaongelea uchimbaji wa level ya chini sana huo sio hata uchimbaji mdogo ni artisanal mining.

Uchimbaji ni sayansi hakuna ndumba. Unaweza kuwa unaamini ushirikina ila haina maana kwamba unafanya kazi. Hizo ni imani za watu wajinga.
 
Kwa taarifa tu utafiti ni ghali kuliko hata kuchimba kwenyewe. Ila sisi tunawekeza kwenye kuchimba zaidi ya utafiti.

THIS. Watu hawajui hili.

NI-43-101 au the JORC report can easily cost you 1M USD. Easily.
 
Kwenye level ya kumiliki mgodi yaan toka eneo mpaka wafanyakazi

PML unaweza kata hata kwa laki1 TSH serikali kila siku inauza ila pana mzigo?

Kim Jong Jr kasema kufanya utafiti ni ghali kuliko hata uchimbaji wenyewe, I couldn't agree more.

Exploration survey can easily cost you 1M USD kufanya survey ya uhakika. Tafuta exploration report ya kampuni yeyote kubwa zipo online ujionee how comprehensive it is. Na exploration huwa ni endelevu sio kitu cha siku moja unaacha hata wakati unachimba exploration inaendelea.

However, unaweza chimba kienyeji kama wachimbaji wadogo wengine ila sio artisanal mining kama ya mleta uzi huo ni uchimbaji mdogo sana hauna tija.
 
Hapa ndio mimi nahitaji kupata darasa jinsi gani ya kuanza hii biashara,mtaji wa kuanzia ni kiasi gani,pa kununulia ni wapi,soko la kuuza ni wapi.
Na cha muhimu zaidi najilinda vipi na utapeli wa kwenye madini,pia nawezaje kuyajua madini feki na halisi.
Msaada hapa
Ngoja nianze kwa kukujibu kama ifuatavyo na kisha hesabu ya mtaji uraifanya mwenyewe.
Kwanza anza kufanya utafiti (exploration) baada ya kupata dondoo za eneo husika.
Baada ya hapo utaweza kutambua eneo husika lina kiasi gani cha dhahambu kwa kila tani moja. Napia itatambua kwamba aina gani ya uchimbaji (underground ama open pit mining) itakufaa ikiwa utapata dhahabu eneohilo.
Baada ya hapo utaanza uchimbaji na wakati huo ukijenga maabara kwaajili ya kupimia kifusi madini utakachokua unatoa kwenye mgodi wako.
Baada ya kujenga maabara huku ukiendelea kurundika kifusi madini (stock pile) ndipo utaanza kujenga plant iweya CLP ama CIL. Wakati unaendelea kujenga plant pia Tellings itakua ikiendelea kujengwa.
Lakini haya yote yataanza kufanyika baada ya kupata leseni ya kitalu husika.
 
Shukrani
 
Hi ni biashara pekee ambayo mtu au mchimbaji anaweza kukukopesa hata milioni 50 bila kuandikishana au kuwepo na shahidi yoyote.
View attachment 3282399

Ni biashara ambayo mtu anaweza kukuuzia udongo ambao hauna uhakika wa kilichomo ndani.
View attachment 3282400

Ni biashara ambayo pamoja na mtu anaweka pesa kubwa, ila wanaamini uchawi kwa asilimia 90

Biashara ya dhahabu ni biashara ambayo inaweza ikakufanya milionea kwa mwezi mmoja na ikachukua pesa zako zote ukawa maskini ndani ya miezi mitatu.

Ardhi ina siri nyingi sana na pesa ina siri nyingi sana.

Unaweza ukachimba shimo au duara ukaambulia udongo tu, ila mwenzako akachimba pembeni tu akapata utajiri.

Pamoja na pesa walizonazo wachimbaji wa dhahabu, hakuna mtu mwenye pesa za kuwekeza kwa kiwango kikubwa cha kutumia sayansi kama wazungu.

Dhahabu ambayo tayari imechimbwa ni kama asilimia 3 tu ya dhahabu ambayo haijaguswa Tanzania.

Nimefanya kazi kwenye uchimbaji miiaka nane hakuna kitu utanidanganya kwenye dhahabu.
Technology Vs Superstition Atakae Pata kura nyingi Ndio Njia yake Itafuatwa,,Case Closed.
 
Sio ushirikina ni mila na desturi za jamii za kiafrika,kabla hujawa brainwashed na dini za mashariki ya kati,bure wa head.

Imani za ushirikina sio desturi za ki africa tu. Hata wazungu walikuwa na imani za kishirikina hasa karne ya 15 mpaka karne ya 20, wazungu wameacha kuamini ushirikina kwenye karne hii ya 21
 
Njoo huku kanda ya ziwa uone wachimbaji wanavyopendezesha mji
Wana ma gest ma hotel majumba ya kufa mtu

Gali zao pendwa za polini ni Kluger za kutembelea ni VXV8
Huko nilikuwepo pia, kimsingi wachimbaji wa Chunya na Kanda ya Ziwa pigo zao zinafanana

Gari pendwa Kluger, Ford Ranger, Toyota Hilux double cabin, Land Cruiser n.k

Wapo waliowekeza sio tu kwenye guest, hata hotel hata kuuza chemicals na vifaa vya uchimbaji, usafirishaji n.k

Pale nilikuwa nazungumzia hasa madogo wanaojipata baadhi ni wajinga hawana akili ya kujiongeza gari lao pendwa crown wakibongoa
​
 
Hapa ndio mimi nahitaji kupata darasa jinsi gani ya kuanza hii biashara,mtaji wa kuanzia ni kiasi gani,pa kununulia ni wapi,soko la kuuza ni wapi.
Na cha muhimu zaidi najilinda vipi na utapeli wa kwenye madini,pia nawezaje kuyajua madini feki na halisi.
Msaada hapa
Nakurudia
 
Hi ni biashara pekee ambayo mtu au mchimbaji anaweza kukukopesa hata milioni 50 bila kuandikishana au kuwepo na shahidi yoyote.
View attachment 3282399

Ni biashara ambayo mtu anaweza kukuuzia udongo ambao hauna uhakika wa kilichomo ndani.
View attachment 3282400

Ni biashara ambayo pamoja na mtu anaweka pesa kubwa, ila wanaamini uchawi kwa asilimia 90

Biashara ya dhahabu ni biashara ambayo inaweza ikakufanya milionea kwa mwezi mmoja na ikachukua pesa zako zote ukawa maskini ndani ya miezi mitatu.

Ardhi ina siri nyingi sana na pesa ina siri nyingi sana.

Unaweza ukachimba shimo au duara ukaambulia udongo tu, ila mwenzako akachimba pembeni tu akapata utajiri.

Pamoja na pesa walizonazo wachimbaji wa dhahabu, hakuna mtu mwenye pesa za kuwekeza kwa kiwango kikubwa cha kutumia sayansi kama wazungu.

Dhahabu ambayo tayari imechimbwa ni kama asilimia 3 tu ya dhahabu ambayo haijaguswa Tanzania.

Nimefanya kazi kwenye uchimbaji miiaka nane hakuna kitu utanidanganya kwenye dhahabu.
Hivi kumbe bado kuna watu wanatumia winch za kunyonga kwa mkono?.

Wachimbaji wanapaswa kwenda na technology aise kazi za nguvu siku hiz hazitakiwi. Winch ya mafuta(petrol) haizid hata mil3.

Kwa anaehitaji aniPM
 
Kama ukiifanya kisayansi na ukawa mvumilivu utafanikiwa...ila ina mazingaombwe mengi sana
 
Samahani nilikuwa nataka kujua naweza kuanza na mtaji wa shs kwenye hii biashara ya dhahabu? maana naipenda sana nataka nianze hii biashara maana naona unasema ni elimu tu hata mtaji mdogo unatosha?? naomba unisaidie

Awali ya yote itambulike kuwa mimi si mjuzi kiviile wa hiyo Biashara.
Pili, hakuna sehemu nimewahi kuandika kuwa unaweza kuifanya kwa Mtaji mdogo.

Ninachoweza kusema;
Uwanda wa Biashara hiyo ni mpana mno.
Unaposema unataka kuifanya ni kutokea pembe ipi:
Kuchimba?
Kuichuuza eneo inapochimbwa,?
Kuileta mjini tokea inapochimbwa?
Kuisafirisha Ng'ambo ama vipi?

Lolote utakalolichagua kati ya hayo,
Je, swali la msingi lingine, wewe unaifahamu hiyo
Dhahabu yenyewe hata ukiiona?
inafananaje, au zipo za tofautitofauti kiasi gani?
Wapi inapatikana?
Kwenye mazingira gani na kwa utaratibu gani?

Iwapo unayo majibu chanya ya maswali hayo upo pazuri.
Lakini kama huna majibu hayo nashauri uyatafute mwenyewe na utaratibu mzuri ufike maeneo mengi li ujiridhishe kuujua ugumu amn urahisi wa mazingira muhimu ya chanzo cha mzigo wako.
 
Hivi kumbe bado kuna watu wanatumia winch za kunyonga kwa mkono?.

Wachimbaji wanapaswa kwenda na technology aise kazi za nguvu siku hiz hazitakiwi. Winch ya mafuta(petrol) haizid hata mil3.

Kwa anaehitaji aniPM
Ebu nikuulize hivi....
Unazo winch za ainagani??
Winch ulizo nazo ninabeba tani ngapi??
Winch zenu zinatumia wire rope ya milimita ngapi??
Winch mlizo nazo zina break system za aina gani??
Winch zenu zinauwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi kwenye kina cha mita ngapi??
 
Back
Top Bottom