Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 4,783
- 14,975
Azimio hilo limefikiwa baada ya kukamilika kwa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi uliofanyika kwa siku tano katika shule ya Polisi Moshi mkoani Kilimanjaro.
Aidha, CP Mkumbo amesema kuwa, Jeshi la Polisi lina jukumu kubwa la kuhakikisha kuwa uchaguzi unafanyika katika mazingira ya usalama, amani na utulivu, Hivyo katika kufikia azma hiyo limeazimia kwa pamoja kusimamia sheria na kanuni zote za nchi, kulinda mikutano ya kisiasa ya vyama vyote na kuweka mazingira bora ya kushirikiana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, viongozi wa kisiasa na wananchi kwa ujumla.
Akigusia maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa 2025, Katibu Mkuu Gugu alilitaka Jeshi la Polisi kuendelea kusimamia kwa umakini utekelezaji wa mikakati ya kiusalama kuelekea uchaguzi huo.
Alisisitiza umuhimu wa kuhuisha mipangokazi ya uchaguzi, kutoa mafunzo kwa maafisa na askari, na kuhakikisha doria na ulinzi wa misafara ya kisiasa unafanyika kwa ufanisi ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika katika mazingira ya amani na usalama.