• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Maadili Ya KiTaifa

Kasheshe

Kasheshe

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2007
Messages
4,699
Points
1,225
Kasheshe

Kasheshe

JF-Expert Member
Joined Jun 29, 2007
4,699 1,225
Asalaam Alaikum Wapenzi Watanzania Wazalendo;

Baada ya Malumbano ya muda mrefu ya Ufisadi/Mafisadi, Walarushwa/Rushwa, Watuhumiwa/Wahukumiwa, Mapambano ya Mtu na Mtu, Ukereketwa,Ufurukutwa,Ungangari,Ungunguri, haki sawa kwa wote, Mpaka Kieleweke, na Kila kitu ambacho kinaonyesha mmoja anajua zaidi au anamachungu na nchi yake zaidi ya Mwingine sasa ni wakati muafaka at least kwenye thread hii kuacha mapambano hayo... Kuacha personality issues,

  • sasa tujadili ni maadili gani ya kitaifa ambayo kiongozi yeyote, wa siasa, wa serikali, wa shirika la umma au wa umma kwa ujumla anatakiwa awe!
  • Ni mambo gani ni lazima yafuatwe na viongozi wote bila kujali vyama vyao?
  • Ni Mambo gani ya mwiko na kwa viongozi, kwa maana akifanya kosa na kuthibitika atengwe na jamii au kupewa adhabu kali?

Ninayo ya kwangu ninayoamini lakini nareserve ili kuacha uwanja mpana!

RULES:
Kwenye thread hii sitazamii malumbano ya mtu na mtu! Sitazamii matusi, sitazamii, wewe hujui, mimi najua!!! Kila maoni yana maana, huwezi jua maoni yenu yawaza kuwa ya maana kama Mh. Rais atatekeleza ahadi yake kuhusu kipengele hiki...


Karibuni
 
M

Mwakilishi

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2007
Messages
484
Points
195
M

Mwakilishi

JF-Expert Member
Joined Jan 31, 2007
484 195
Kilitime, heshima mbele mkuu,

Shukrani kwa kuja na mada hii, mojawapo ninalofikiria mimi ni kuwa kiongozi anapaswa kukumbuka siku zote kuwa anawatumikia wananchi au wale anaowaongoza badala ya kujiona mtawala bin sultani fulani, hili litapelekea viongozi kuwajibika ipasavyo na kutanguliza manufaa ya wanaowaongoza.
 
Kasheshe

Kasheshe

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2007
Messages
4,699
Points
1,225
Kasheshe

Kasheshe

JF-Expert Member
Joined Jun 29, 2007
4,699 1,225
mojawapo ninalofikiria mimi ni kuwa kiongozi anapaswa kukumbuka siku zote kuwa anawatumikia wananchi au wale anaowaongoza badala ya kujiona mtawala bin sultani fulani, hili litapelekea viongozi kuwajibika ipasavyo na kutanguliza manufaa ya wanaowaongoza.
Ahsante Mzalendo "Mwakilishi"

La muhimu hapa iweke kwa namna ambayo akiambiwa awe na sifa x, kama hiyo ulipendekeza hapo juu, wananchi tunahitaji tuiweze kuipima "measurable" ili tuweze kumhukumu yule ambaye is not adhered to maadili ya kitaifa "national code of conduct for public leaders as well as citizen" sijui kimombo chake ndio hicho!!!

Tuweke vizuri ili hatimaye tuje na summary nzuri!!! katika hili, hii ndio itakuwa njia yako yakulitumikia taifa hasa uwe ambaye sio kiongozi leo!!!
 
Field Marshall ES

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2006
Messages
12,659
Points
0
Field Marshall ES

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined Apr 27, 2006
12,659 0
Kiongozi ni lazima awe mwananchi halisi, aliyezaliwa na kukulia nchini Tanzania, awe na elimu ya kutosha ya angalau Degreee moja ya University inayoeleweka, asiwe na record ya uhalifu au wizi, awe na record ya uchapaji kazi na matokeo ya kazi hizo yawe open kwa public kabla hajapewa nafasi ya kuongoza, ni lazima awe na uelewo ambao ni above the average concerning position anayoitaka au atakayopewa, awe na heshima kwa wananchi na iwe clear kwake kuwa wananchi wamempa nfasi ya kuwaongoza na wana haki ya kumuondoa wakati wowote bila taarifa atakapo onekana kupwaya au kushindwa ku-live up to the expectations za wananchi au level ya nafasi aliyopewa kiuongozi, yaani aelewe kuwa cheo ni dahamana tu sio haki yake ya kuazaliwa nayo, kama viongozi wengi tulionao wanavyodhani. Pia mali zake ziorodheshwe kwa public kabla hajaingia kwenye nafasi hiyo.

Shukrani
 
Dua

Dua

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2006
Messages
3,117
Points
2,000
Dua

Dua

JF-Expert Member
Joined Nov 14, 2006
3,117 2,000
Waambie warudishe Azimio la Arusha lina kila kitu kwa viongozi. Yesu alimwambia mtoto wa tajiri nenda kauze mali alizokuachia baba yako unifuate na ufalme wa mbinguni utakuwa wako.
 
Kasheshe

Kasheshe

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2007
Messages
4,699
Points
1,225
Kasheshe

Kasheshe

JF-Expert Member
Joined Jun 29, 2007
4,699 1,225
na iwe clear kwake kuwa wananchi wamempa nfasi ya kuwaongoza na wana haki ya kumuondoa wakati wowote bila taarifa atakapo onekana kupwaya au kushindwa ku-live up to the expectations za wananchi au level ya nafasi aliyopewa kiuongozi, yaani aelewe kuwa cheo ni dahamana tu sio haki yake ya kuazaliwa nayo, kama viongozi wengi tulionao wanavyodhani.
Field Marshall ES;

Nitajaribu kuongezea kitu kwenye hoja yako,,, unaonaje kwa mfano mtu akipewa nafasi atapewa miezi sita (6) kujifunza nafasi yake mpya, then atatakiwa baada ya kujifunza kazi yake mpya na mazingira yake, atoe plan/objectives zake za vitu atakavyo-accompkish in 3 au 5 years, depending atakiwa awe madarakani kwenye cheo hicho kwa wakati gani, la muhimu kuwe na Performance Appraisal kwenye 1.5 years au 2.5 years respective kujua anaendelea vipi, kama dalili sio nzuri aondolewe immediately will this help, hii inakuwa hata kwa wabunge, madiwani etc....
 
Kasheshe

Kasheshe

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2007
Messages
4,699
Points
1,225
Kasheshe

Kasheshe

JF-Expert Member
Joined Jun 29, 2007
4,699 1,225
Waambie warudishe Azimio la Arusha lina kila kitu kwa viongozi. Yesu alimwambia mtoto wa tajiri nenda kauze mali alizokuachia baba yako unifuate na ufalme wa mbinguni utakuwa wako.
Ni Kweli,

But the best will be tuangalie ya kwetu as if we have never had Azimio la Arusha, thereafter tutaangalia yepi yakuchukua kutoka huko na yapi tuyaache...

Better always allow fresh ideas....
 
Dua

Dua

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2006
Messages
3,117
Points
2,000
Dua

Dua

JF-Expert Member
Joined Nov 14, 2006
3,117 2,000
Ni Kweli,

But the best will be tuangalie ya kwetu as if we have never had Azimio la Arusha, thereafter tutaangalia yepi yakuchukua kutoka huko na yapi tuyaache...

Better always allow fresh ideas....
Huwezi kufanya hivyo, niliwahi kusema nafikiri katika mada mojawapo hata USA, UK, Japan na nchi zilizoendelea kuliko sisi wana maazimio yao ya Arusha lakini kwa jina jingine. Leo hii unasikia viongozi wanajinyonga kwa sababu ya kuogopa kuhojiwa na kamati za bunge kwa ubadhirifu. marekani sheria zao ukiwa kiongozi au UK huwezi kufanya mambo ambayo yanatokea bongo halafu unasema ati unataka ushahidi wakati pesa haionekani. - UPUUZI GANI HUU?
 
Mwawado

Mwawado

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2006
Messages
998
Points
195
Mwawado

Mwawado

JF-Expert Member
Joined Nov 2, 2006
998 195
SIFA ZA KIONGOZI KWA MTAZAMO WANGU;

- Awe Raia wa Tanzania kwa kuzaliwa,na amewahi kuishi TANZANIA
kwa kipindi kichopungua miaka 10 mfululizo ktk uhai wake.

- Awe na umri wa Mtu mzima (Miaka 21)na kiwango cha Elimu angalau
Shahada moja (minimum).Awe Muumini wa Dini yoyote
Inayotambulika ktk Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Kwa mtazamo
wangu Masuala ya Imani yana nafasi ktk Uongozi na suala zima
la kutoa maamuzi ya Haki.

- Awe Mtu anayekubali kuilinda na kuitetea Katiba Ya Jamhuri ya
Muungano.***Mpya?...(Itakayokidhi matakwa ya muungano,na
inayokwendana na wakati).Awe Tayari kuilinda na kuitetea
Katiba hiyo Mahali/Wakati wowote.


- Awe Mwanachama wa Chama chochote Halali (Kilichosajiliwa) cha
siasa (Hiyo itasaidia kuwa na Viongozi wanaosimamia sera na
sio mawazo Binafsi ktk kutekeleza majukumu)

- Awe amechaguliwa na Wananchi kwa zaidi ya kura 50,na Mpinzani
wake awe amekubali matokeo ya kushindwa.Kama ni kiongozi wa
Kuteuliwa ni lazima athibitishwe ama Bunge ama Jopo la Majaji
au kuundwe Mfumo maalumu wa kuthibitisha Teuzi Mbalimbali,
Chombo hicho kiwe Huru!!

-Awe Tayari kutangaza MALI zake anapoingia na kutoka Madarakani.
Pia awe tayari kutetea Hoja au kujiuzulu punde kunapotokea
Kashfa katika Eneo lake la Uongozi.Awe Mchapakazi hodari na
mfuataji wa sheria na kanuni za kazi.
 
Kasheshe

Kasheshe

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2007
Messages
4,699
Points
1,225
Kasheshe

Kasheshe

JF-Expert Member
Joined Jun 29, 2007
4,699 1,225
Mwawado,

Nashukuru.

kwa potential contributors to this thread, mnaweza kutofautisha viongozi wa siasa kama wanasiasa na viongozi wateuliwa Technocrat, Mwawado amefanya vizuri lakini mnaofuata fanyeni vizuri zaidi kwa kutofautisha sifa zao, ingawa ni wazi kuna area wanakuwa wana sifa sawa!!!

Wakati huo huo, wananchi nao wanatakiwa wawe je?

viongozi wa serikali zao za chini/mitaa wawe je?

Wakati unajibu fikiria mawazo yatakayokuwa validy for the next 15-25 years


Tuendelee na mjadala!

Msivunjike moyo, mambo kama haya si watanzania wengi wanapenda kuyajadili, lakini haya ndio mambo yakuweza kuhakikisha utastaafu salama na wajukuu wako watakuwa salama


My Take;
Kiongozi wa Umma, Technorat lazima awe full time Employee kwa kazi yake,,, kwa maana anaweza miliki hisa kwenye kampuni anaweza kuwa non-active directors, lakini hawezi kuwa managing director wa kampuni wakati huo ni mfanyakazi wa Serikali... as atakuwa na conflict of interest... not only that like pia lazima atangaze shughuli ambazo zinawezakuwa na conflict of interest na majukumu yake na kwa hiyo kukataa kuchukua cheo ambacho kina conflict of interest au inapofikia sehemu ambayo kuna conflict of interest ana-declare ili wengine waangalie haki inafanyika, asipofanya hivyo na ikigundulika aundolewe mara moja...
 
Kisura

Kisura

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2007
Messages
364
Points
195
Kisura

Kisura

JF-Expert Member
Joined Jun 21, 2007
364 195
Kiongozi, first and foremost, needs to be a Leader, and not a Manager. Kiongozi anatakiwa awe na uhusiano wa karibu na watu wa chini yake, awe ni mtu anayesikiliza mawazo wa watu wa chini yake, kabla hawajaamua kutake action ndani ya kampuni ambayo ita-affect kila mfanyakazi chini yake. Asiwe ni mtu anayependa kufanya decision kubwa kubwa bila kusikiliza watu wengine, kwasabau ukweli ni kwamba, no matter how educated you are, what schools you went, or how much experiences you have, you sure don’t know EVERYTHING!

Kiongozi lazima awe ni mtu anayekubali mabadiliko(change), dunia inabadilika kila siku. Kiongozi anatakiwa awe na mtazamo huo. Badala ya kung’ang’ania kufanya mambo kimwaka 47, inabidi watu wa-adopt to change. Pamoja na kuwa hii ni sehemu iko obvious kwa kila mtu, but it remains to be the most resisted area. Please change before you have to.

Nakumbuka kuna wakati Tanzania wanachi walikuwa wanatumia simu za kutumia internet kupiga nchi za nje, na sijui ilikuwa ni TTCL, au ni tamko toka kwa waziri wa mawasiliano, kuwa hizo shughuli zisitishwe, na zikapigwa marufuku. Watu walikuwa hawatumii simu za TTCL kwasabu walipata simu za internet ambazo zilikuwa cheap. Hawa waheshimiwa wakaamua kupiga marufuku matumizi hayo kwa sababu kampuni ya simu ilikuwahaileti faida/ kupata hasara? This was/is absurd! Kiongozi mzuri atakuwa a-deal na hii challenge, kiongozi anahitaji ku-deal na change, instead of striving to stop people from adopting to change and technology(kwa sababu huwezi), he/she needs to concentrate on innovation. Hivyo kiongozi lazima awe Innovative.

Na mwisho, a good leader anatakiwa a-take responsibility of his failures, awe ready to step down aki-fail as a leader. Asituletee ubabe wa viongozi wetu wa kibongo, tena wanadiriki kwenda kwenye vyombo vya habari, na kusema "sing’atuki ng’oo,hata mfanyaje"!!!!
 
Gamba la Nyoka

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2007
Messages
6,919
Points
2,000
Gamba la Nyoka

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
Joined May 1, 2007
6,919 2,000
Ninataka kiongozi mwenye hekima na busara
Mwenye uwezo wa kutoa maamuzi ya muelekeo wa sera
Ambaye hana ubaguzi wa uzanzibari na uzanzibara
anayechukia wizi na wanaoitia nchi hasara

Alete mageuzi ya kuondoa ufukara
na akifanya uteuzi aunde serikali bora
huyu ndiye kiongozi ,kiongozi aliye imara

Mkweli na muwazi ,kwa wala rushwa hana masihara
Anayemuamini Mwenyezi Mungu, awe mtulivu asiwe na papara
Ambaye kwa hakika hawezi kuitoa nchi kafara
Huyu ndiye kiongozi, kiongozi alo bora
 
Masanja

Masanja

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2007
Messages
4,139
Points
2,000
Masanja

Masanja

JF-Expert Member
Joined Aug 1, 2007
4,139 2,000
Kanuni za mwana TANU za mwaka 1954 nadhani badi ziko very relevant sana kwa wote wanaotaka kutuongoza.
 
green29

green29

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2007
Messages
312
Points
225
green29

green29

JF-Expert Member
Joined Jul 4, 2007
312 225
Kama jina lake linavyojieleza, kazi ya kiongozi ni kuongoza. Pamoja na sifa nyingine, kazi hii inahitaji Kiongozi awe ni mtu anayejua muelekeo anapowaongoza watu wake... anawaongoza kuwapeleka wapi? Atatumia njia gani kufika huko? lazima awe na uhakika kwamba hiyo njia itawafikisha watu wake wanapotaka kufika.. Haitakuwa na maana kama baada ya kwenda kilometa 100 unawaambia watu wako "...samahani nafiri tumepotea, ngoja tujaribu njia nyingine". Hii ni sawa na kuwafanyia majaribio wananchi.
 
N

NakuliliaTanzania

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2007
Messages
560
Points
0
N

NakuliliaTanzania

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2007
560 0
nadhani tutakuwa pia makini tunapoestablish hizi criteria na indicators kufikiria pia temporal and spatial dimensions!
 
Kasheshe

Kasheshe

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2007
Messages
4,699
Points
1,225
Kasheshe

Kasheshe

JF-Expert Member
Joined Jun 29, 2007
4,699 1,225
Ili flow iende vizuri,,, hili hapa azimio la arusha,,,

Nimesoma kweli kama ni marekebisho yanahitajika machache,,, ama kweli wenzetu walikuwa wanafikiri,,, tofauti na sasa ambao mawazo mengi ni disposable, yanadumu kwa muda mfupi
 
M

Mr Rocky

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2007
Messages
15,196
Points
2,000
M

Mr Rocky

JF-Expert Member
Joined Oct 10, 2007
15,196 2,000
SIFA ZA KIONGOZI KWA MTAZAMO WANGU;

- Awe Raia wa Tanzania kwa kuzaliwa,na amewahi kuishi TANZANIA
kwa kipindi kichopungua miaka 10 mfululizo ktk uhai wake.

- Awe na umri wa Mtu mzima (Miaka 21)na kiwango cha Elimu angalau
Shahada moja (minimum).Awe Muumini wa Dini yoyote
Inayotambulika ktk Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Kwa mtazamo
wangu Masuala ya Imani yana nafasi ktk Uongozi na suala zima
la kutoa maamuzi ya Haki.

- Awe Mtu anayekubali kuilinda na kuitetea Katiba Ya Jamhuri ya
Muungano.***Mpya?...(Itakayokidhi matakwa ya muungano,na
inayokwendana na wakati).Awe Tayari kuilinda na kuitetea
Katiba hiyo Mahali/Wakati wowote.


- Awe Mwanachama wa Chama chochote Halali (Kilichosajiliwa) cha
siasa (Hiyo itasaidia kuwa na Viongozi wanaosimamia sera na
sio mawazo Binafsi ktk kutekeleza majukumu)

- Awe amechaguliwa na Wananchi kwa zaidi ya kura 50,na Mpinzani
wake awe amekubali matokeo ya kushindwa.Kama ni kiongozi wa
Kuteuliwa ni lazima athibitishwe ama Bunge ama Jopo la Majaji
au kuundwe Mfumo maalumu wa kuthibitisha Teuzi Mbalimbali,
Chombo hicho kiwe Huru!!

-Awe Tayari kutangaza MALI zake anapoingia na kutoka Madarakani.
Pia awe tayari kutetea Hoja au kujiuzulu punde kunapotokea
Kashfa katika Eneo lake la Uongozi.Awe Mchapakazi hodari na
mfuataji wa sheria na kanuni za kazi.

nimependa hiki cha hapa ambacho ni kutangaza mali binafsi wakati unaingia madarakani na wakati unatoka madarakani.

kifupi hii sheria ya maadili ya viongoi ni nzuri ila kuna loop hole mahali maana haisemi ikiwa kiongozi anayelipwa mshahara wa milioni moja kwa mwezi ukikata na kodi na makato mengine at least ana laki saba ukichanganya na posho kwa mfano anakuwa na kitu kama two million ila ukija kuangalia huyo mtu ana jumba kule masaki la million hamsini au hata five hundred Million hiyo amount ya ziada anaipata wapi ni for short period of time.

je na ile ya kuandika majina ya watu ambao hata hawapo humu duniani nayo unasemaje
 
Gamba la Nyoka

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2007
Messages
6,919
Points
2,000
Gamba la Nyoka

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
Joined May 1, 2007
6,919 2,000
Aisee kumbe hili ndo azimio la Arusha!
Kweli hili Azimio ndo ilikuwa Tochi ya Ukombozi kama lingetekelezwa kisayansi badala ya mitulinga.

Hili azimio lilikuwa zuri ila lilihitaji mabadiriko kidogo, mfano lingeruhusu wananchi wa kawaida wenye uwezo kuweza kuendesha biashara na miradi mikubwa mikubwa huku na serikali nayo ikiendelea na programme zake kama kawaida kama zilivyoainishwa na azimio hapo juu.

au mfano pale anapojitikeza mtanzania ana uwezo wa kufanya jambo fulani mathalani kujenga kiwanda cha kusindika nyama, serikali ingeweza kuingia ubia na mtu yule badala ya kuwatoa wananchi wasishiriki moja kwa moja kama mtu binafsi.

Na pia azimio liliwabana sana viongozi, kitu kama kiongozi kutokuwa na mishahara miwili nadhani ilizidi sana, chukulia mfano kiongozi ni profesa lecturer mwandamizi halafu at the same time ni mkuu wa kitengo fulani serikalini , kwa nini asile mishahara miwili?

Kumbe azimio halikukataza investment kutoka nje ila lilitaka watanzania wanufaike kikamilifu kutokana na investment hiyo siyo wageni wabebe faida kubwa halafu sisi tuambulie kiduchu.

Kiufupi ninadhani kuna wakati watanzania watajiuliza tunatoka wapi tunakwenda wapi, na siku wakilifunua azimio la Arusha watasema turekebishe baadhi ya vitu halafu ndo uje uwe mwongozo wetu kiuchumi.

Sijaona mle azimio likisema watu wasiwe na video, wasiendeshe magari ya gharama, nadhani kuna tatizo somewhere juu ya utekelezaji wake! something must be wrong somewhere!

halafu kitu kingine nilichokipendea hilo azimio la arusha ni wepesi wake, hata mtoto darasa la saba akilisoma ataelewa nini sera ya nchi na atajua nini wajibu wa raia katika juhudi nzima ya kuleta maendeleo. kuna haja ya viongozi wetu kuwaeleza wananchi kwa lugha nyepesi na iliyonyooka nini sera ya nchi kwa wakati huu, na tunafanya nini ili kufikia malengo tunayokusudia.
 
Idimi

Idimi

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2007
Messages
12,192
Points
2,000
Idimi

Idimi

JF-Expert Member
Joined Mar 18, 2007
12,192 2,000
Kiongozi wa Umma, Technorat lazima awe full time Employee kwa kazi yake,,, kwa maana anaweza miliki hisa kwenye kampuni anaweza kuwa non-active directors, lakini hawezi kuwa managing director wa kampuni wakati huo ni mfanyakazi wa Serikali... as atakuwa na conflict of interest... not only that like pia lazima atangaze shughuli ambazo zinawezakuwa na conflict of interest na majukumu yake na kwa hiyo kukataa kuchukua cheo ambacho kina conflict of interest au inapofikia sehemu ambayo kuna conflict of interest ana-declare ili wengine waangalie haki inafanyika, asipofanya hivyo na ikigundulika aundolewe mara moja...
__________________
Nawapongeza wana JF kwa makala hii moto. Kwa kujazia, naona hawa tunaowaita "technocrats", wapewe kazi za taaluma zao. Sio mhandisi anapewa utawala, daktari anapewa uongozi katika uchumi, msanifu anakuwa mtawala nk. Pamoja na maadili lazima taaluma ya mtu izingatiwe katika kumpa uongozi wa kitengo fulani, nadhani ataongoza kwa ufanisi sana akisaidiwa na 'technocrats' wengine waliopo hapo kazini.
 
Mwanamalundi

Mwanamalundi

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2007
Messages
3,130
Points
1,500
Mwanamalundi

Mwanamalundi

JF-Expert Member
Joined Aug 30, 2007
3,130 1,500
Hivi mnataka kuniambia kuwa tanzania hatuna maadili ya viongozi??? Mbona hata hayo, maadili machache yaliyopo hakuna anayeyatekeleza??? mnataka maadili yepi tena??? kwa kifupi hayo yote mnayoongelea hapo juu yapo kwenye makabrasha ya tume ya maadili ya viongozi wa umma na hakuna hata mmoja anayetekeleza.

OK, mtasema kuwa sasa hivi tunaongozwa na azimio la zanzibar. That is fine. Ni kikao kipi cha chama ama serikali kilichowahi kutangaza hadharani kuwa "Miiko ya viongozi" kama ilivyoanishwa kwenye Azimio la Arusha imefutwa??? Kwa kuwa hatujaelezwa, hatuoni haja ya kutafuta miiko mingine wakati hii tuliyo nayo imeshindwa hata kupika "bokoboko", achilia mbali hiyo pilau tunayoililia!!! Kwa kifupi, si kweli kuwa tanzania hatuna miiko ya viongozi. Tatizo ni kwamba kabla ya kuingia ikulu wanavunja hiyo miiko, wakiingia ikulu unadhani wana muda wa kuchonga mingine???
 

Forum statistics

Threads 1,402,998
Members 531,040
Posts 34,411,676
Top